Breaking

Showing posts with label mpira wa miguu. Show all posts
Showing posts with label mpira wa miguu. Show all posts

Sunday, June 3, 2018

9:21 AM

Video: Wachezaji wa Real Madrid wamlilia Zinedine Zidane kwa staili ya aina yake


Licha ya kuwa kocha pekee barani Ulaya kuisaidia timu yake ya Real Madrid kutwa taji la UEFA kwa nyakati tatu mfululizo Zidane amekuwa miongoni mwa makocha wanaoheshimika sana pia maarufu mwenye sifa nyingi nzuri.Mfaransa huyo ameamua kuikacha timu yake ya Real Madrid kama kocha na kukimbilia nchini Qatar huku wachezaji wake wakimuaga kwa majonzi ya aina yake kwa kutumia akaunti zao za mitandao ya kijamii.Saturday, June 2, 2018

1:20 PM

Tawi la Yanga Mwanza lamjia juu Mzee AkilimaliTawi moja la Yanga mkoani Mwanza limeibuka na kupiga kauli ya Mjumbe wa Baraza la Wazee Yanga baada ya kuibuka na kueleza kuwa anataka kugombea nafasi ya Uenyekiti ndani ya klabu hiyo.

Mzee huyo ameibuka hivi karibuni na kutangaza kuwa atagombea nafasi hiyo ili kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti, Yusuph Manji ambaye alijiuzulu ili kupumzika.

Kwa mujibu wa Radio One kupitia kipindi cha Spoti Leo, Kiongozi wa tawi hilo, Mhando Madega, amesema kuwa mzee huyo amekuwa mnafiki na mchochezi kwani amekuwa akiibuka pale Yanga inapokuwa haina wakati mzuri.

Aidha, Madega ameongeza kwa kueleza kuwa Akilimali hajawa na msaada wowote ndani ya Yanga zaidi ya kutupia lawama uongozi ambao umekuwa ukiipigania klabu katika nyakati zote ambazo inapitia.

Madega ameuomba uongozi wa Yanga uangalie namna ya kumsimamisha Akilimali ikiwezekana kumfuta kabisa uanachama ndani ya klabu kwani amekuwa akileta sintofahamu nyingi zisizokuwa na maana.

Thursday, May 3, 2018

7:35 AM

Huyu ndiye mchezaji bora wa mwaka Manchester UnitedKIPA Mspaniola, David de Gea ameshinda tuzo mbili katika sherehe za mwisho wa msimu za Manchester United usiku wa jana.

Mlinda mlango huyo ambaye amedaka kila mechi ya Ligi Kuu ya England kwa muda wote msimu huu hadi sasa.

Katika mechi 35 alizodaka hadi sasa, De Gea hakuruhusu bao hata moja katika mechi 17 kati ya hizo, hivyo kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kabla ya kubeba na tuzo ya Sir Matt Busby ya Mchezaji Bora wa Mwaka chaguo la mashabiki.

Katika sherehe za jana ilishuhudiwa wachezaji wakifika na wake na mahawara zao, maarufu kama WAG ukumbi wa Uwanja wa Old Trafford.

De Gea alifika na mpenzi wake, nyota wa Pop, Edurne Garcia, ambaye aliiwakilisha Hispania katika shindano la kuimba wimbo Ulaya, lililojulikana kama Eurovision Song Contest mwaka 2015.

Mspaniola mwenzake, Juan Mata alifika na mkewe Evelina Kamph, wakati Ander Herrera alikwenda na mpenzi wake, Isabel Collado na Marcos Rojo alifika na mpenzi wake, Eugenia Lusardo.

Nemanja Matic alisjhinda tuzo ya Bao Bora la msimu kutokana na bao lake la dakika za mwishoni alilofunga katika ushindi wa United wa 3-2 dhidi ya Crystal Palace mwezi Machi.

TUZO ZA MAN UNITED MSIMU WA 2017-18 
Sir Matt Busby Mchezaji Bora wa Mwaka (chaguo la mashabiki) — David de Gea

Mchezaji Bora wa Mwaka — David de Gea 

Meneja wa Wachezaji wa Mwaka — Scott McTominay

Bao Bora la Msimu — Nemanja Matic (vs Crystal Palace)

Mchezaji wa Timu ya Wachezaji wa Akiba ya Denzil Haroun wa Mwaka— Demetri Mitchell

Mchezaji Bora wa Timu ya Vijana ya Jimmy Murphy wa Mwaka — Tahith Chong

Tuzo Maalum— Michael Carrick

Tuesday, May 1, 2018

2:41 PM

Samatta Awaonya Serengeti Boys " Tulizeni Vichwa Madogo Tusije Kusikia Mmeanza Kuoa"

Samatta Awaonya Serengeti Boys " Tulizeni Vichwa Madogo Tusije Kusikia Mmeanza Kuoa"
Nahodha wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Ally Samatta amewapongeza vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kwa kutwaa ubingwa wa CECAFA Challenge U-17 nchini Burundi.


Serengeti Boys Jumapili ilifanikitwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge U-17) kwa kuwafunga vijana wa Somalia, mabao 2-0 yaliyofungwa na Edson Jeremiah dakika ya 25 na Jaffar Mtoo dakika ya 66.

“Hongereni sana 'Serengeti' (U17) kwa ubingwa wa CECAFA kwa umri wa chini ya miaka 17. Tunaamini TFF ina mipango mikubwa juu yenu. Tulizeni vichwa madogo, tusianze kusikia mmeanza kuoa sasa (utani). Hongereni sana,”. Samatta ameandika kupitia 'Twitter'.Serengeti Boys imerejea nchini Alfajiri ya leo na kupokewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe ambaye amewapongeza vijana kwa ushindi huo.

Monday, April 23, 2018

11:53 AM

Salah ashinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka PFAMchezaji hatari wa klabu ya soka ya Liverpool, Mohamed Salah ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka inayotolewa na Chama cha Wachezaji wa kulipwa nchini England (PFA).

Salah ameshinda tuzo hiyo kwa kuwabwaga wachezaji wengine akiwemo Harry Kane (Tottenham Hotspur), David De Gea (Manchester United), Kevin De Bruyne, David Silva na Leroy Sane (Manchester City).

Wakati huo huo Leroy Sane ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa soka nchini Uingereza. Sane amewashinda Sterling (Manchester City), Ryan Sessegnon (Fulham), Harry Kane (Tottenham Hotspur) na Marcus Rashford (Manchester United).

Kwa upande wa soka la wanawake, Fran Kirby (24) wa klabu ya Chelsea amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa wanawake ya PFA.

Naye Lauren Hemp wa Bristol City na timu ya wanawake chini ya umri wa miaka 19, amshinda tuzo ya mchezaji chipukizi kwa upande wa wanawake.

Saturday, April 21, 2018

11:14 AM

Hawa ndio wanaotajwa kuchukua nafasi ya WengerPamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Arsenal Ivan Gazidis, kusema timu hiyo bado haijaanza mchakato wa kumpata mrithi wa kocha Arsene Wenger lakini tayari majina kadhaa yameanza kutajwa kuziba nafasi hiyo.

Gazidis ameweka wazi kuwa mchakato huo utakapoanza utaongozwa na yeye mwenyewe, mkuu wa mahusiano ya soka Raul Sanllehi na Afisa mwajiri wa klabu Sven Mislintat.

Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel, anatajwa zaidi kuchukua nafasi ya mzee Wenger ambaye amekaa klabuni hapo kwa miaka 22. Kocha mwingine ni Carlo Ancelotti pamoja na Massimiliano Allegri ambaye ni kocha wa Juventus.

Mbali na hao imeelezwa kuwa Mkurugenzi  Gazidis ana uhusiano wa karibu na nahodha wa zamani wa timu hiyo Mikel Arteta ambaye kwasasa ni msaidizi wa Pep Guardiola kwenye kikosi cha Manchester City.

Orodha hiyo haijakamilika bila jina la nyota wa zamani wa timu hiyo Thierry Henry ambaye naye anatajwa miongoni mwa wanaoweza kuchukua nafasi ya Wenger. Makocha wengine ni kocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique na kocha wa Hoffenheim Julian Nagelsmann.

Friday, April 20, 2018

7:39 AM

Wachezaji hawa uwenda wakaondoka Man United mwisho wa msimu huuMtandao wa Squawka.com moja kati ya stori kubwa walioiripoti leo Alhamisi ya April 19 2018 ni pamoja na hii ya wachezaji wa Man United ambao wanatazamiwa kuwa wataondoka mwisho wa msimu kwa sababu mbalimbali ikiwemo kukosa nafasi ya kucheza.

1- Anthony Martial ametajwa kuwa ataondoka Man United baada ya kugoma kusaini mkataba mpya wa miaka mitano kutokana na kocha Jose Mourinho kutomchezesha mara kwa mara, hivyo vilabu vya Juventus na Inter Milan vimekuwa vikihusishwa nae kwa karibu, Martial ameanza katika game 16 tu za Man United msimu huu na nafasi yake amekuwa akipewa Rashford.

2- Paul Pogba pamoja na kuwa amenunuliwa kwa pesa nyingi kutoka Juventus na kujiunga na Man United na amefanikiwa kutoa assist nyingi zaidi ya mchezaji yoyote wa Man United katika EPL lakini amekuwa anafanya vizuri kiasi chini ya Jose Mourinho na kuna wakati watu walihoji namna ya Mourinho anavyomtumia kiungo huyo.

3- Marouane Fellaini huyu alikuwa moja kati ya wachezaji wanaopendwa sana na Jose Mourinho msimu uliyoisha lakini maisha yake Man United yanadaiwa kama kukaribia mwisho baada ya kufanikiwa kucheza katika game 19 pekee za mashindano yote msimu huu huku akianza katika game tano pekee na amecheza kwa jumla ya dakika 694.

4- Ander Herrera baada ya ujio wa Nemanja Matic ndani ya Man United Herrera ameonekana kuanza kukosa nafasi ya kucheza na amepata kuanza katika game 10 za Man United, hivyo uwepo wa wachezaji wanatajwa kumzidi uwezo kunaweza kumfanya akakimbia Man United na kwenda timu ambayo atapata nafasi ya kucheza.

5- Luke Shaw anatajwa kuwa yeye mwenyewe ameanza kuhisi kuwa hana nafasi tena ndani ya kikosi cha Man United kutokana na nafasi  yake kuwa kuna kiungo kama Ashley Young wameanza kucheza hiyo inatokana na jeraha lake la muda mrefu alilolipata msimu uliyopita hivyo anakosa nafasi pia kutokana na kukosa fitness.

Wednesday, April 18, 2018

4:05 PM

PFA yataja kikosi bora cha EPL 2017/18, Man City yaongoza kutoa wachezaji wengi

Chama cha Wachezaji wa kulipwa nchini Uingereza (PFA), kimetaja orodha ya kikosi bora cha wachezaji wa ligi hiyo kwa msimu wa 2017/2018.


Katika kikosi hicho klabu ya soka ya Manchester United imefanikiwa kutoa wachezaji watano. Wakati huo huo Tottenham Hotspur imetoa wachezaji watatu kwenye kikosi hicho.

Kikosi cha wachezaji waliochaguliwa na PFA kwa msimu wa 2017/2018
Wachezaji waliotajwa kwenye kikosi hicho ni David De Gea, Kyle Walker, Jan Vertonghen, Nicolás Otamendi, Marcos Alonso, David Silva, Kevin De Bruyne na Christian Eriksen.
Wengine waliotajwa kwenye orodha hiyo ni Harry Kane, Mohamed Salah na Sergio Agüero.

2:01 PM

Barcelona yaipa rekodi hii Celta VigoLicha ya kwenda sare ya mabao 2-2 ikiwa ugenini katika Ligi Kuu Spain, FC. Barcelona imeendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kuwa na alama zake 83 kati ya michezo 33 iliyocheza.

Barcelona ililazimisha sare hiyo huku mabao yake yakifungwa na wacheze, Dembele dakika ya 36 na la pili likitiwa kimiani na Alcacer mnamo dakika ya 64.

Kikosi hicho kilicheza kikiwa pungufu kuanzia dakika ya 71 baada ya Sergi Roberto kulimwa kadi nyekundu.

Celta Vigo imekuwa timu pekee ambayo imeshindwa kupoteza mbele ya Barcelona msimu huu baada ya kuilazimisha Barcelona kupata matokeo ya sare katika michezo yote miwili ya ligi.

Hiyo imekuwa ni rekodi kwa Celta ukiangalia baadhi ya vigogo wengine kama Atletico na Real Madrid tayari wameshapokea vichapo kutoka kwa vinara hao wa ligi msimu huu.

Monday, April 16, 2018

8:06 PM

Majeruhi Neymar atuma pongezi kwa wenzake


Nyota wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Brazil Neymar Jr, ameipongeza klabu yake hiyo kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Ufaransa (Ligue 1) huku akiweka wazi kuwa alitamani sana kuwepo wakati wanatwaa ubingwa.

Neymar hayupo na timu yake tangu mwezi Februari kufuatia kuumia mguu na kulazimika kusafirishwa kwenda nchini kwao Brazil kwaajili ya matibabu ambayo yalitazamiwa kutumia miezi mitatu hadi minne.

Baada ya jana PSG kutwaa ubingwa huo Neymar aliwapongeza wachezaji wenzake kupitia mitandao yake ya kijamii ambapo aliandika ''Nilitamani sana kuwa pamoja na nyie, hongereni kwa ubingwa''.

PSG usiku wa jana waliibuka na ushindi mnono wa mabao 7-1 dhidi ya Mabingwa watetezi Monaco. Baada ya ushindi huo PSG wamefikisha alama 87 ambazo haziwezi kufikiwa na Monaco yenye alama 70 huku zikiwa zimebaki mechi 5 pekee.

Ubingwa huu ni wa 7 kwa PSG ikiwa imetwaa katika misimu ya 1985–86, 1993–94, 2012–13, 2013–14, 2014–15, 2015–16 na 2017–18.

Friday, April 13, 2018

8:39 AM

Kenya yashinda medali ya dhahabu ya kwanzaWycliffe Kinyamal ameishindia Kenya medali ya dhahabu ya kwanza katika mbio za fainali za wanaume za mita 800, katika mashindano ya Jumuiya ya madola.

Aliyekuwa bingwa Nijel Amos wa Botswana, aliyemshinda David Rudisha miaka minne iliyopita, aliishia kuwa wa mwisho katika mchuano huo.

Mwenzake Kinyamal, kutoka Kenya, Jonathan Kitilit alishika nafasi ya sita, wakati Joseph Deng, wa Australia, aliyezaliwa kwenye kambi ya wakimbizi baada ya mama yake kukimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe Sudan, alishika nafasi ya saba.

Mwanariadha kutoka Afrika Kusini, Caster Semenya, anatarajiwa kupata medali ya pili ya dhahabu, baada ya kumaliza wa kwanza katika raundi ya kuingia katika fainali za mita 800.

Bara la Afrika linatarajia kupata medali zaidi baada ya wanamichezo watano:


  • Eglay Nalyanya - Kenya
  • Margaret Wambui - Kenya
  • Emily Tuei - Kenya
  • Docus Ajok - Uganda
  • Winnie Nanyondo- Uganda

Thursday, April 12, 2018

8:05 AM

Pep Guardiola na Liverpool kukutana na rungu la UEFA

Shirikisho la soka Barani Ulaya, UEFA limetoa adhabu kwa meneja wa Manchester City, Pep Guardiola kufuatia kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu wakati wa mchezo wao dhidi ya Liverpool uliyomalizika kwa kufungwa jumla ya mabao 2 – 1 hapo jana usiku.

 Wakati huo huo UEFA imeipatia adhabu Liverpool kwa kitendo cha mashabiki wake kufanya vurugu kwa kuwasha moto na kulishambulia basi la wachezaji wa Man City wakati wa mchezo wao wa kwanza wa klabu bingwa uliyopigwa Anfield.Guardiola ataadhibiwa kwa makosa mawili lakwanza ikiwa ni kupingana na maamuzi ya waamuzi baada ya kukataliwa bao lao la kuotea  ‘Offiside’ kitendo kilichopelekea akijikuta anavuka mstari na kuingia uwanjani na hivyo kutolewa kwenye benchi.


Kosa lapili likiwa ni kufanya mawasiliano na benchi la ufundi wakati yeye ametolewa eneo hilo hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 69 cha sheria ya UEFA.
Guardiola aliingia ndani ya uwanja wakati wa mapumziko akienda kumlalamikia mwaamuzi kwa kitendo cha kukataa bao lao ambalo lingeifanya City kuongoza kwa jumla mabao 2 – 0 kipindi cha kwanza.
Kesi hiyo itashughulikiwa na bodi inayosimamia maswala ya maadili na nidhamu ya UEFA Mei 31 mwaka 2018.

Tuesday, April 10, 2018

2:52 PM

RANALDO: ANATAJWA BORA ZAIDI UEFA KIHISTORIA


MADRID, Hispania: MIEZI kadhaa iliyopita, kuna wengi waliombe­za Cristiano Ronaldo wakati akipitia kipindi kigumu cha ukame. Ni Ronaldo huyo­huyo ambaye aliibuka ghafla na kwenda kuipa Real Madrid ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na La Liga.
Msimu huu pia, Ronaldo, 33, aliuanza kwa tabu, wengi wakaanza kuibua mas­wali tena juu ya kiwango chake, la­kini baada ya muda hakuna anaye­hoji tena.

Lakini ukweli ni kwamba huenda kizazi hiki tunamshuhudia mcheza­ji bora zaidi wa wakati wote katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mashabiki Jumanne iliyopita kwenye Uwanja wa Juventus, wal­ishuhudia kila kitu kwa uwazi zaidi. Baada ya Ronaldo kupiga bao la pili kali (Real ilishinda 0-3 ugenini), i l i b i d i mashabiki wa upinzani wasimame tu kumpa heshima kutoka­na na jinsi bao hilo lilivy­okuwa.

“Sikuamini. Nalazimi­ka kusema asante kwa mashabiki wote wa Ju­ventus. Walichokifanya kwangu kinashangaza. Hii haijawahi kutokea katika maisha yangu,” alisema Ro­naldo, baada ya mashabiki wa Juventus kusimama na kumpongeza kufuatia bao kali aliloifunga timu yao.
Suala la mchezaji bora za­idi litaendelea kuwa mjadala milele kwa kuwa ni mtazamo wa mtu. Kila mtu huwa na chaguo lake; mweupe au mweusi? Chapati au mandazi? Vitumbua au sambusa? Kunyoa au kufuga rasta?
Lakini kwa kile ambacho alikifan­ya Ronaldo Jumanne, inawezeka­na wengi wakaanza kukubali kuwa huyu ni mchezaji mkali zaidi kihistoria katika michuano hii.
Takwimu zinambeba: Yeye bin­afsi tangu aondoke kwenye Premier, amefunga mabao mengi kwenye michuano hiyo kuliko jumla ya ma­bao yaliyofungwa na timu mbili za Manchester United na Manches­ter City.

Kumbuka huyu ndiye mfungaji bora wa wakati wote wa michua­no hii, akiwa na mabao 120.
Bao lake la ‘tiki taka’ Ju­manne, linasadikika kuwa ni bao bora zaidi lililowahi kufungwa katika historia ya mtoano wa Ligi ya Mab­ingwa. Lilifungwa dhidi ya mmoja wa makipa bora zaidi wa wakati wote duniani, na lilifungwa li­cha ya jitihada za uhakika kutoka kwa safu ya ulinzi inayosadikika kuwa moja ya safu bora zaidi duniani, lakini jamaa akatupia tu.

Mtu aliyeshuhudia kwa uka­ribu zaidi bao hilo ambaye alikuwa golini aliishia kumsifia tu. “Akiwa ka­tika ubora wake? Nadhani hakuna aliyewahi kuwa kama Ronaldo. Mes­si na yeye (Ronaldo) wanaweza kul­inganishwa na Maradona na Pele,” anasema Gianluigi Buffon, kipa wa Juve.
Hakika Ronaldo inaoneka­na alizaliwa kwa ajili ya kuja kufanya maa­jabu kwenye Ligi ya Mab­ingwa Ulaya. Hata wakati akiwa na ukame kwenye La Liga, a l i e n ­delea kuwa hatari Ulaya msimu huu wa 2017-18.

Kwa mwendo wake huu wa kutu­pia mabao bila kuhurumia wapinza­ni wake, Ronaldo anaelekea kuvunja rekodi yake mwenyewe ya kufunga mabao 17 katika msimu mmoja, na kuna kila dalili kwamba atatwaa tuzo yake ya sita ya Ballon d’Or (Mchezaji Bora wa Dunia) kama Real Madrid itatwaa taji la Ligi ya Mabingwa kwa mwaka wa tatu mfululizo.

Pia msimu huu ameweka rekodi mbili mpya: Jumanne alifanikiwa kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao kwenye mechi 10 mfululizo za Ligi ya Mabingwa Ulaya, na alifunga katika kila mechi kwenye hatua ya makundi, suala ambalo halikuwahi kufanyika kabla.

Ronaldo inawezekana akapata tena Tuzo ya Puskas, ambayo ni ya bao bora zaidi duniani, aliwahi kui­pata mwaka 2009 baada ya kufunga bonge la bao katika Ligi ya Mab­ingwa dhidi ya Porto.
Ronaldo anaelekea kubeba taji lake la nne la Ligi ya Mabingwa aki­wa na Real Madrid, na la tano kwake kiujumla.

“Unyenyekevu ukizidi siyo vizuri,” alisema Ronaldo kabla ya fainali ya msimu uliopita. “Tunatakiwa kuthibi­tisha sifa yetu na tuwaonyeshe nani ni bora zaidi. Tunaweza kupata mataji mawili, kutetea ubingwa (wa La Liga) na kuingia katika historia ya Ligi ya Mabingwa. Kuna kichocheo kikubwa na tumebakiza hatua moja.”
Kuna hatua mbili na nusu zime­baki kwa ajili ya Madrid kugeuza mataji mawili mfululizo ya Uefa kuwa matatu mfululizo, lakini ugwiji wa Ronaldo katika mi­chuano hii, umeshathibitishwa hata kama hawatatwaa taji hili.

Sunday, April 8, 2018

2:32 PM

Kocha wa Juventus: Unajua Ronaldo yaani ni sawa na mvinyoCristiano Ronaldo

KOCHA wa Juventus, Massimiliano Allegri amemfananisha Cristiano Ronaldo na kinywaji cha mvinyo akisema kuwa kadiri umri unavyokwenda ndio anazidi kuwa mkali zaidi. Allegri alimkubali Ronaldo baada ya kuiongoza Real Madrid kuirarua Juventus 3-0 mbele ya mashabiki wao kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wiki iliyopita.

“ Unajua Ronaldo yaani ni sawa na mvinyo kadiri muda unavyokwenda ndio anazidi kuwabora,” alisema Allegri baada ya mchezo huo, ambao Ronaldo aliacha mashabiki wa soka mdomo wazi baada ya kufunga bao maridadi la ‘tik tak’. Allegri alisema kuwa Ronaldo amekuwa straika bora wa dunia kwa miaka miwili sasa.

Alisema kuwa pamoja na fowadi huyo kuwa na umri wa miaka 33 lakini bado ana kiwango cha kutisha. Nyota ya Ronaldo bado ipo juu Real Madrid wakati wenzake waliounda kombinesheni ya BBC yaani Gareth Bale na Karim Benzema wakiwa wamechuja siku za karibuni.

Katika miaka ya nyuma, Ronaldo alikuwa anasifika kwa mbio na chenga lakini kutokana na umri kumtupa mkono siku hizi anahakikisha anakuwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga kila mara.

Saturday, April 7, 2018

10:00 PM

Bayern Munich yaichapa Augsburg, yabeba taji la BundesligaKlabu ya soka ya Bayern Munich imetwaa taji la Bundesliga msimu wa 2018/19 baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Augsburg kwenye mchezo uliomalizika jioni hii.

 Bayern sasa imeweka rekodi ya kutwaa taji hilo mara 6 mfululizo huku msimu huu wakiwa wamechukua zikiwa zimebaki mechi 5 kabla ya ligi hiyo kumalizika. Baada ya ushindi wa leo wamefikisha alama 72 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine.

Bayern ambayo i[po chini ya kocha wa muda na aliyewahi kuipa mataji matatu (Trebble)  Jupp Heynckes, ilianza vibaya msimu chini ya kocha Carlo Ancelotti ambaye baadae alitimuliwa na kurejeshwa kwa Jupp na kila kitu kilibadilika kuanzia hapo.


Mabingwa hao wapya wa Bundesliga leo waliwapumzisha nyota wao Robert Lewandowski, Thomas Muller, Thiago Alcantala, Franck Ribery, Mats Hummels na Javi Martinez ambao wote walianzia kwenye benchi ikiwa ni sehemu ya mipango ya mechi ya UEFA jumanne ijayo dhidi ya Sevilla.

Tangu msimu wa 2012/13 Bayern haijapoteza taji hilo na imekuwa ikichukua bila ushindani mkubwa haswa baada ya mpinzani wake Borussia Dortmund kutokuwa kwenye kiwango kizuri misimu ya hivi karibuni.
12:37 PM

Raiola Asema Guardiola ni Muongo

Raiola asema Guardiola ni muongo

Wakala wa kiungo wa Manchester United Paul Pogba Mino Raiola amesema alichosema kocha wa Manchester City Pep Guardiola kuwa Pogba alitaka kuuzwa kwenye usajili wa Januari si kweli.


''Sijawahi kuzungumza na Guardiola kuhusu mchezaji yeyote aliyechini yangu, si Pogba wala Mkhitaryan, hata Man City kama klabu sijawahi kuongea nayo lakini naiheshimu ni timu bora na ina kocha bora'', amesema.

Jana kwenye mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wa 'Derby' ya jiji la Manchester, Guardiola alisema kuwa Pogba alitaka kuuzwa Manchester City kwenye dirisha dogo la janauri kitu ambacho kimepingwa vikali na nyota huyo wa Ufaransa.Kwa upande wake Pogba kupitia ukurasa wake wa mtandao wa 'Twitter' ameeleza kushangazwa na alichosema Guardiola kwani hajawahi kuongelea suala hilo hata siku moja.

Mchezo wa leo ambao utapigwa kwenye uwanja wa Etihad nyumbani kwa Man City, unaweza kuamua bingwa endapo wenyeji watashinda basi wataibuka mabingwa wapya wa EPL msimu wa 2018/1 

Monday, March 26, 2018

7:01 PM

Elneny aongeza mkataba mpya kucheza Arsenal

Kiungo wa Misri Mohamed Elneny amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea Arsenal kwa kipindi kirefu.
Elneny alisajiliwa akitokea Basle mwezi January maka 2016 na ameshaichezea Arsenal michezo 65.

Baada ya kusaini mkataba huo, Elneny ameandika kwenye mitandao yake ya kijamii ujumbe unaosomeka, “Officially we will be together for a longer time, in order to reach what we started, and to put arsenal in it’s deserved spot In Europe and the whole world.”
Hata hivyo bado haijafahamika ni mkataba wa muda gani ambao ameongeza kuiheza timu hiyo.
Image may contain: 4 people, including Mollel Hillary Mollel, people smiling, text

6:06 PM

Samuel Umtiti kuelekea Manchester United

 

Mchezaji wa  wa klabu ya Barcelona  na  timu ya taifa ya Ufaransa, Samuel Umtiti huwenda akaondoka Nou Camp na kuelekea Manchester United  kwa dau la pauni milioni 50.

Umtiti huwenda akatimkia kwa mashetani hao wekundu kufuatia kukwama kwa mazungumzo ya mkataba wake na mabosi zake wa Barcelona.

Mchezaji huyo raia wa Ufaransa mara kadhaa amehusishwa kuamia Old Trafford na mpango huo kuonekana kukamilika baada ya Barcelona kukataa kumlipa anachohitaji.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya michezo nchini Hisania, mchezaji huyo wazamani wa Lyon anahitaji kuwa wapili katika viwango vya mshahara ndani ya kikosi cha Barca nyuma ya Andres Iniesta na Luis Suarez.

Image may contain: 4 people, including Mollel Hillary Mollel, people smiling, text

Sunday, March 4, 2018

5:22 PM

Tanzia: Nahodha wa klabu ya Fiorentina afariki dunia

 

Nahodha wa klabu ya Fiorentina inayoshiriki Ligi Kuu Italy, Serie A, Davide Astori (31) amefariki dunia, uongozi wa klabu umethibitisha.

Astori amefariki akiwa na wachezaji wenzake katika hoteli moja nchini Italy, wakati wakijiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Udinese FC.

Mchezaji huyo ametwaa mataji 14 katika maisha yake ya mchezo wa soka ambapo alianzia AC Milan na baadaye kuuzwa kwenda Cagliari.

Kifo hiki ambacho hakijajulikana sababu ni nini, kimepelekea mchezo ulipaswa kupigwa leo kati ya Fiorentina na Udinese kuahirishwa na utapangiwa tarehe nyingine, Nahodha ambaye aliwahi kuichezea pia timu ya taifa ya Italy nafasi ya ulinzi, namba 5.

Wednesday, February 28, 2018

12:22 PM

Klabu ya soka ya Real Madrid imezidi kujiweka katika nafasi mbaya ya kushinda taji la ligi kuu ya Hispania (La Liga) baada ya usiku wa jana kukubali kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa Espanyol.

Madrid ambao walikuwa katika uwanja wa ugenini wa RCD Espanyol, walifungwa goli hilo na Gerard Moreno katika dakika ya 90 ya mchezo.

Hata hivyo Cristiano Ronaldo wa Madrid hakuwepo katika mcheo huo.

Kutokana na matokeo hayo, Real inabakia katika nafasi yake ya tatu kwenye msimamo wa ligi akiwa na alama zao 51 huku akiwa mbele kwa mchezo mmoja, wakati huo huo Barcelona ndio anaongoza msimamo huo akiwa katika nafasi yake ya kwanza na alama 65.