Breaking

Saturday, May 5, 2018

8:35 AM

Watu wa Dodoma na mikoa jirani msikose kumsiliza Jeniberth Alberth kupitia radio maisha


Watu  wa  Dodoma na  mikoa  ya  jirani  msikose  kusikiliza kipindi cha   #USHIKWAPO SHIKAMANA Kipindi ambacho kinawalenga hasa vijana changamoto,fulsa,maendeleo,na mambo mengine wanayo kumbana nayo katika kuzifikia ndoto zao kinachoongozwa na mtangazaji mwenye kipaji Jeniberth Alberth 

  #USHIKWAPO SHIKAMANA  kipo  kwanzia  jumatatu  mpaka  Alhamisi  Muda  ni  saa  kumi jioni  mpaka saa  kumi mbili  jioni  
   #USHIKWAPO SHIKAMANA ni kipindi bora kinachoongozwa na Jeniberth Alberth mtangaji  mwenye  uwezo  mkubwa wa  kutanganza kupitia  radio  Maisha  Dodoma ...

Image may contain: 1 person
8:18 AM

Mbunge Aibua Sakata la Vifo vya Mtikila na Chacha wangwe Bungeni


Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Janeth Masaburi amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Mwigulu Nchemba kutoa taarifa bungeni juu ya vifo vya wanasiasa Chacha Wangwe aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila.

Wangwe ambaye alikuwa mbunge wa Tarime kwa tiketi ya Chadema alifariki dunia Julai 27 mwaka 2008 katika ajali ya gari iliyotokea Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma,  Mtikila alifariki katika ajali ya gari  Oktoba 4, 2015 Chalinze wilayani Bagamoyo.

Akichangia bajeti ya wizara hiyo  mwaka 2018/19, Masaburi amemtaka pia waziri huyo kutoa taarifa za kifo cha watalii waliomwagiwa tindikali na makanisa yaliyochomwa moto.

“Tunaomba taarifa, kifo cha Wangwe, Mtikila, watalii waliomwagiwa tindikali na makanisa yaliyochomwa moto Zanzibar,” amesema.

Kuhusu amani amesema Tanzania ipo mahali salama tangu kuasisiwa kwake enzi ya Hayati Mwalimu Nyerere na maraisi wastaafu Ali HassaMwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete.

“Hii nchi yetu sote, humu tupo zaidi ya 300 ila Watanzania wapo milioni 60, kila mtu ana haki hamasa ambazo zinatolewa kwa kutubagua zishindwe kwa jina la yesu.  Bila amani hatuwezi kulima hakuna kwenda shule, kustarehe wala kuzaliana,” amesema.

Amesema watu wasitanie amani kwa kutumia dini kwamba dini fulani inaonewa na kuhoji mbona wapo ndani ya Bunge.

“Tusitanie amani, ninaomba Serikali iongeze bajeti ya kutosha katika vyombo vya ulinzi na usalama pia makazi yao yaboreshwe na kujengwa nchi nzima,”amesema. 

Thursday, May 3, 2018

7:55 AM

Rais Uhuru ammiminia sifa tele aliyekuwa mpinzani wake mkuu, Raila Odinga

Mwandishi: Joshua Kithome 
Rais Uhuru amemsifu sana kiongozi wa upinzani, Raila Odinga katika hotuba yake - Uhuru alimpongeza Raila kwa kukubali kufanya kazi pamoja naye katika kuwaunganisha Wakenya Rais Uhuru Kenyatta kwa mara nyingine amemsifia sana kiongozi wa upinzani, Raila Odinga mbele ya naibu wake William Ruto kwa kutii mwito wake wa kuungana katika kufanyaka kazi pamoja. 
Akitoa hotuba yake ya Hali ya Taifa siku ya Jumatano, Mei 2, rais alisema kuwa nia yake ya kuwaleta Wakenya pamoja haikuwa rahisi kuafikiwa bila Raila. Rais Uhuru na Raila walikubaliana kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kuungana katika kuwafanyia Wakenya kazi hapo mwezi Machi 9, 2018.  
"Si mimi pekee niliyehisi haja ya kuleta umoja tena, Raila Odinga alifanya alikuwa na wazo hilo pia. Wacha nimsifu kwa uzalendo alioudhihirisha," Alisema Uhuru. Aliwasihi viongozi kuungana pamoja na kuwatumikia Wakenya, waombe msamaha kwa kuwafeli Wakenya mwaka uliopita wa siasa.  
Hii sio mara ya kwanza kiongozi huyo wa taifa kumsifu Raila Odinga. Alifanya hivyo pia katika ibada ya mazishi ya mwendazake Kenneth Matiba alipoonyesha nia ya kufanya kazi pamoja katika kurejesha umoja wa Wakenya 
7:49 AM

Hii ndio sababu Rais Uhuru Kenyatta amewaomba msamaha

Mwandishi: Tina Mutinda  
 Kiongozi huyo wa Jubilee anajutia matamshi aliyotoa wakati wa kampeni 2017 -Rais aliwaomba wananchi na wanasiasa kuimarisha amani na umoja nchini Rais Uhuru Kenyatta amewaomba wananchi kumsamehe kwa matamshi yoyote aliyotoa na yaliyowaumiza wakati wa uchaguzi mkuu wa 2017. Rais Uhuru alichukua fursa ya hotuba ya kitaifa kuwaomba wananchi msamaha Jumatano, Mei 2.  
"Ikiwa kuna chochote nilichosema mwaka jana kilichowaumiza, ikiwa niliharibu umoja wa taifa hili kwa njia yoyote, ninawaomba mnisamehe na muungane nami kurekebisha hali,” alisema Uhuru 
Alisema kuwa viongozi wanafaa kuishi maisha yanayoweza kuigwa, na ndio maana aliomba msamaha.  
Aliwataka viongozi kuongoza kampeni ya kuwaleta wananchi pamoja kwa kuwakumbusha kuwa ukali haulipi lakini ukosoaji kwa njia ya kujenga ni muhimu. Kiongozi huyo aliwataka viongozi na wananchi vile vile kuheshimiana kuambatana na tofauti zao na kubuni njia za kushirikiana. Uchaguzi wa 2017 ulikumbwa na machafuko na vita ambazo zilianzishwa na uhasama kati ya Uhuru na kiongozi wa upinzani Raila Odinga. 
Kabla ya salamu kati yao ambayo imekuwa maarufu sana, Raila alimkashifu Uhuru na wenzake kwa wizi wa kura za urais wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Uhuru kwa upande wake alishambulia majaji na mahakama hasa baada ya ushindi wake kubatilishwa na Mahakama ya Juu. Wakati huo, viongozi katika pande zote mbili walionekana kushambuliana na kuchochea wananchi, hali iliyowatenganisha zaidi wananchi 
Hii ndio sababu Rais Uhuru Kenyatta amewaomba msamaha
Rais Uhuru Kenyatta amewaomba Wakenya msamaha. Picha/Kwa Hisani  
7:35 AM

Huyu ndiye mchezaji bora wa mwaka Manchester UnitedKIPA Mspaniola, David de Gea ameshinda tuzo mbili katika sherehe za mwisho wa msimu za Manchester United usiku wa jana.

Mlinda mlango huyo ambaye amedaka kila mechi ya Ligi Kuu ya England kwa muda wote msimu huu hadi sasa.

Katika mechi 35 alizodaka hadi sasa, De Gea hakuruhusu bao hata moja katika mechi 17 kati ya hizo, hivyo kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kabla ya kubeba na tuzo ya Sir Matt Busby ya Mchezaji Bora wa Mwaka chaguo la mashabiki.

Katika sherehe za jana ilishuhudiwa wachezaji wakifika na wake na mahawara zao, maarufu kama WAG ukumbi wa Uwanja wa Old Trafford.

De Gea alifika na mpenzi wake, nyota wa Pop, Edurne Garcia, ambaye aliiwakilisha Hispania katika shindano la kuimba wimbo Ulaya, lililojulikana kama Eurovision Song Contest mwaka 2015.

Mspaniola mwenzake, Juan Mata alifika na mkewe Evelina Kamph, wakati Ander Herrera alikwenda na mpenzi wake, Isabel Collado na Marcos Rojo alifika na mpenzi wake, Eugenia Lusardo.

Nemanja Matic alisjhinda tuzo ya Bao Bora la msimu kutokana na bao lake la dakika za mwishoni alilofunga katika ushindi wa United wa 3-2 dhidi ya Crystal Palace mwezi Machi.

TUZO ZA MAN UNITED MSIMU WA 2017-18 
Sir Matt Busby Mchezaji Bora wa Mwaka (chaguo la mashabiki) — David de Gea

Mchezaji Bora wa Mwaka — David de Gea 

Meneja wa Wachezaji wa Mwaka — Scott McTominay

Bao Bora la Msimu — Nemanja Matic (vs Crystal Palace)

Mchezaji wa Timu ya Wachezaji wa Akiba ya Denzil Haroun wa Mwaka— Demetri Mitchell

Mchezaji Bora wa Timu ya Vijana ya Jimmy Murphy wa Mwaka — Tahith Chong

Tuzo Maalum— Michael Carrick

7:32 AM

Mbinu 3 Za Kugundua Fursa Za Kibiashara Mahali UlipoKila kitu ambacho unakiona mbele ya macho yako ni lazima ukitafakari katika ubongo usiokuwa wa kawaida, yaani ni lazima uwaze kitakupaje pesa.

Aangalia njia ya kuzitambua fursa katika eneo lako unaloishi.

1. Tafuta mahitaji ya watu.
Kila mahali unapoishi kwa namna moja ama nyingine watu huwa wanahitaji huduma au bidhaa fulani. Hivyo ni vyema ukaa chini na kutafakari ni vitu gani unadhani watu wanahitaji nini zaidi ? Baada ya kupata majibu ni wakati wako muafaka wa kuweza kuvisogeza kwa watu hao na wao wakanunua. Kufanya hivyo ni njia nzuri ya wewe kupata pesa. Pia watu wengi hupenda Huduma ambayo inapatikana kwa rahisi hivyo fanya uchunguzi wa kutosha na kuona watu wanapenda nini zaidi kuzisogeza huduma hizo kwa watu.

2. Toa majibu ya changamoto za watu.
Kuna swali la msingi sana la kuujiuliza juu ya maisha yako. Swali lenyewe ni kama lifuatavyo hivi ni kwa nini huna pesa? Ukipata majibu ya swali hilo ni nusu ya kupata mafanikio.

Moja ya tafiti ambazo ziliwahi kufanywa ni kwamba watu wengi hawana pesa kwa sababu kuu mbili, mosi kwa sababu hawatatui matatizo za watu. Sababu ya pili, watu wengi hawana pesa kwa sababu wanatatua matatizo machache, hivyo siri ya kubwa ya mafanikio yako ipo katika kutatua matatizo ya watu wengi katika njia ya tofauti na walivyozoea wengine.

3. Rahisisha majibu ya kazi
Watu wengi hupenda vitu ambavyo havina ugumu katika kufanya kazi, wetu wengi tunapenda kufanya kazi kwa kutumia njia rahisi na kupata majibu kamili tunayoyatarajia. Hebu angalia moja ya tajiri mkubwa dunia bwana Steve Job ambaye ni mmliki wa kampuni ya Apple, yeye alitazama jinsi watu ambavyo walikuwa wanatumia vifaa vya kietroniki kama simu za butani, desktop computer ambazo kimsingi zilikuwa ni vigumu hata kutembea nazo.

Hivyo Steve Job akaamua kutengeneza vitu hivyo hivyo kwa kuongeza thamani leo hii tunafurahia simu za apple na laptop za apple ambazo zina mambo mengi pia zinasaidia kurahisisha kazi na kuifanya dunia kama kijiji.

Kwa hiyo kama alivyofanya tajiri huyo ni wakati mwafaka kufikiri ni zipi kazi ngumu ambazo zinawakabili watu na kuweza kuzipa majibu ya ugumu huo.
7:29 AM

Wema Sepetu Afunguka Sababu Iliyomfanya Kutoudhuria Harusi ya Alikiba

Wema Sepetu Afunguka Sababu Iliyomfanya Kutoudhuria Harusi ya Alikiba

Msanii wa Filamu Bongo, Wema Sepetu amefunguka sababu ya kutohudhuria kwenye harusi ya msanii Alikiba.

Mrembo huyo amesema harusi ya Alikiba iligongana na birthday ya mdogo wake hivyo akashindwa kwenda kwani anaiweka familia yake mbele kwanza.

“That because ile ni siku ambayo nilimfanyia mdogo wangu birth day party, mdogo wangu alikuwa anatimiza miaka 20 mwaka huu. Kwa hiyo mwaka jana sikumfanyia chochote mwaka huu nikawa nimemuhaidi i will do the party,” amesema.

“So family first na Alikiba anajua mimi namsapoti mwisho wa siku sina kinyongo chochote namtakia kila la kheri kwenye maisha yake ya ndoa,” Wema ameiambia Bongo5.

Utakumbuka April 19, 2018 Msanii Alikiba alifunga ndoa na mpenzi wake mjini Mombasa nchini Kenya na April 29, 2018 walifanya sherehe ya pili Dar es Salaam. 
7:28 AM

Aliyewatumbua Wenye Elimu ya Darasa la saba Naye Atumbuliwa

Aliyewatumbua Wenye Elimu ya Darasa la saba Naye Atumbuliwa

Mkurugenzi mtendaji  wa halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto mkoani Tanga Peter Nyalali  amemsimamisha kazi kaimu afisa utumishi wa halmashauri hiyo Protas Dibogo kwa kosa la kukaidi kuwarudisha kazini watendaji wa vijiji 41 baada ya serikali kuagiza warejeshwe.


Nyalali ametoa kauli hiyo wakati wa kikao chake na watumishi wa halmashauri hiyo ambapo, pamoja na mambo mengine amesisitiza watendaji hao kwenda kufanya kazi kwa bidii kwenye maeneo yao mara tu watakaporejea kazini.

Hivi karibuni serikali iliagiza kurudishwa kazini kwa watumishi wote walioajiriwa 01/05/2004, ambapo  Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Bumbuli Peter Nyalali  alimwagiza kaimu afisa utumishi wa halmashauri hiyo awarudishe kazini watendaji wa vijiji 41.

Pamoja na kutolewa agizo hilo Kaimu Afisa Utumishi Protas Dibogo hakutekeleza agizo hilo jambo lililosababisha  Mkurugenzi Nyalali kumsimamisha kazi.

"Masharti yanaonyesha kwamba nyie mmeanza tarehe 1 mwezi 5. Yeye anapotosha hapa anasema kwamba mmeanza mwezi wa 6. Ninamsimamisha kazi na nafasi yake atakaa Bi Asha Majid" Nyalali.

Tarehe 01/05/2004 serikali iliwaajiri watumishi waliokuwa wakijitolea katika maeneo mbalimbali nchini,ambapo  tarehe 20/05/2004 serikali ilitoa kibali cha kuajiri watumishi wapya wenye elimu ya darasa la saba huku ikiwataka kujiendeleza wawapo kazini 
7:26 AM

Serikali Gabon Yajiuzulu kwa Amri ya Mahakama

Serikali Gabon Yajiuzulu kwa Amri ya Mahakama
Serikali ya Gabon imejiuzulu siku moja baada ya Mahakama Kuu ya Katiba kuamuru Bunge livunjwe na kuagiza uongozi wa nchi ujiuzulu kutokana na kuchelewa kuitisha uchaguzi mkuu.

Taarifa ya Serikali inasema Waziri Mkuu Emmanuel Issoze Ngondet "aliwasilisha barua ya kujiuzulu kutoka nafasi yake serikalini baada ya uamuzi wa Mahakama ya Katiba kuamuru shughuli za Bunge zisimame hatua iliyolazimisha Serikali kujiuzulu."

Kwa mujibu wa Mahakama Serikali ilipaswa kuandaa uchaguzi lakini uliahirishwa mara mbili kufikia Aprili 30.

Mahakama imesema shughuli za Bunge lililovunjwa sasa zitahamishiwa kwenye Baraza la Seneti hadi uchaguzi mpya ufanyike. Tarehe ya uchaguzi haijatangazwa.

Uchaguzi mkuu ulifanyika mwaka 2016 ambao Rais Ali Bongo alitangazwa kuwa mshindi matokeo yaliyopingwa na upinzani.

Ghasia zilizuka siku chache baada ya uchaguzi na wapinzani wanasema watu zaidi ya 50 waliuawa katika mapigano. Taarifa rasmi ya vifo ni watu watatu.

Bongo alitwaa mamlaka kutoka kwa baba yake Omar Bongo, ambaye alitawala kwa miaka 41 hadi alipofariki dunia mwaka 2009.

Tuesday, May 1, 2018

2:42 PM

Maelfu Waandamana rais wa Malawi AjiuzuluMaelfu ya raia wa Malawi mwishoni mwa wiki wameandamana kuipinga serikali katika maandamano ya kwanza tangu mwaka 2011.


Maandamo hayo yaliyoandaliwa na mashirika ya kiraia yamefanyika katika miji sita nchini humo kupinga vitendo vya ufisadi na utawala mbovu chini ya Rais Peter Mutharika, ambaye ameiongoza nchi hiyo tangu 2014.

Katika maandamano ya July 2011 dhidi ya serikali, polisi walifyatua risasi na kuwaua raia 20, mauaji yaliyoishtua nchi hiyo na kusababisha nchi wafadhili kusitisha misaada yao.

Rais wa zamani wa Malawi, Joyce Banda, alirejea nchini humo, Jumamosi iliyopita baada ya kuishi uhamishoni kwa miaka minne, licha kitisho cha kukamatwa kwa tuhuma za Rushwa. 
2:41 PM

Samatta Awaonya Serengeti Boys " Tulizeni Vichwa Madogo Tusije Kusikia Mmeanza Kuoa"

Samatta Awaonya Serengeti Boys " Tulizeni Vichwa Madogo Tusije Kusikia Mmeanza Kuoa"
Nahodha wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Ally Samatta amewapongeza vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kwa kutwaa ubingwa wa CECAFA Challenge U-17 nchini Burundi.


Serengeti Boys Jumapili ilifanikitwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge U-17) kwa kuwafunga vijana wa Somalia, mabao 2-0 yaliyofungwa na Edson Jeremiah dakika ya 25 na Jaffar Mtoo dakika ya 66.

“Hongereni sana 'Serengeti' (U17) kwa ubingwa wa CECAFA kwa umri wa chini ya miaka 17. Tunaamini TFF ina mipango mikubwa juu yenu. Tulizeni vichwa madogo, tusianze kusikia mmeanza kuoa sasa (utani). Hongereni sana,”. Samatta ameandika kupitia 'Twitter'.Serengeti Boys imerejea nchini Alfajiri ya leo na kupokewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe ambaye amewapongeza vijana kwa ushindi huo.