Breaking

Showing posts with label elimu. Show all posts
Showing posts with label elimu. Show all posts

Wednesday, April 5, 2017

5:44 PM

MARAIS WALIOUAWA KWA KUPIGWA RISASI WAKIWA MADARAKANI

  Image result for LAURENT Desire KabilaRelated image
Tunawaletea marais waliouawa kwa kupigwa risasi wakiwa madarakani. ABRAHAM Lincoln; alikuwa Rais wa 16 wa Marekani. Aliuawa mwaka 1865 jijini Washington kwa kupigwa risasi kichwani kwa nyuma na John Wilkes. Alikuwa amekaa na mkewe. Bastola iliyotumika inaitwa Deringer. 
Image result for INDIRA Priyadarshini Gandhi

INDIRA Priyadarshini Gandhi; Alikuwa Rais wa India. Aliuawa mwaka1984 kwa kupigwa risasi na walinzi wake, Satwant Singh na Beant Singh jijini New Delh, India. 
JOHN Francis Kennedy ‘JFK’; ni Rais wa 35 wa Marekani. Aliuawa mwaka 1963 mjini Dallas kwa kupigwa risasi na Lee Harvey akiwa kwenye gari la wazi barabarani.
Image result for LAURENT Desire Kabila
LAURENT Desire Kabila; alimng’oa madarakani Rais Mabotu Seseko wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, lakini mwaka 2001 akauawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa ni walinzi wake. 
Image result
THOMAS Isdor Noel Sankara; alikuwa Rais wa Burkina Faso Alitawala nchi kwa miaka 4 hadi 1984 alipouawa kwa kupigwa risasi inasemekana alihusika  kufanya mauaji  hayo ni  rafiki  yake  wa  kisiasa   Blaise Compaore ambaye  alikuja  kuwa  rais  wa nchi  hiyo  kwa  muda  mrefu  lakini  mwisho  wa siku  alikimbia nchi hiyo.
Image result
 WILLIAM Richard Tolbert Jr; Alipigwa risasi mwaka 1980 katika mapinduzi ya kijeshi akiwa Rais wa Liberia. Samuel Doe akiwa na cheo cha sajenti ndiye aliyetajwa kumuua.
Image result for Ghaddaf;

 MUHAMMAR Muhamad Abu Migar al Ghaddaf; Alikuwa Rais wa Libya kwa miaka 42. Aliuawa kwa kupigwa risasi ya kichwa kwenye vurugu za kisiasa mjini Sirte, Libya, Oktoba 20, 2011. 
Image result

ABEID Amani Karume; alikuwa Rais wa Zanzibar tangu mapinduzi ya mwaka 1964. Aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa anacheza bao mwaka 1972 na mtu ambaye hakuwahi kupatikana. Jean baptist ouedraogo; aliitawala Burkina Faso kwa mwaka mmoja tu, 1982-83. Aliuawa kwa kupigwa risasi na Thomas Sankara ambaye alichukua madaraka ya kuiongoza nchi hiyo kabla na yeye kupinduliwa.

10:39 AM

Hii ni Miji 10 ya Afrika yenye MABILIONEA wenye utajiri wa zaidi ya BILIONI 60

Hii ni Miji 10 ya Afrika yenye MABILIONEA wenye utajiri wa zaidi ya BILIONI 60
Image result for miji mikubwa afrika
10. Kano Nigeria,
9. Marrakesh Morocco
8. Addid Ababa Ethiopia
7. Abuja Nigeria
6. Dar es salaam Tanzania
5. Nairobi Kenya ambako kuna matajiri wa aina hiyo wapatao 69.
4. ni Capetown South Africa yenye matajiri 115
 3. Lagos Nigeria yenye 131
2. Cairo Egypt
1. Johannesburg South Africa yenye matajiri wa aina hiyo 238.
10:24 AM

Mfahamu Carlos the Jackal: Gaidi tishio zaidi kuwahi kutokea duniani

[​IMG]
Carlos The Jackal, kwa jina la kuzaliwa anaitwa Ilich Ramirez Sanchez,alizaliwa mwaka 1949 huko Venezuela.
Carlos alizaliwa katika familia inayojiweza kiuchumi,ambapo baba yake alikuwa ni mwanasheria mahiri mwenye itikadi za kikomunist,hata jina la Ilich alilompatia Carlos lilikuwa kwaajili ya kumuenzi mwanamapinduzi wa kikomusti wa Urusi aitwae Lenin,ambae Ilich lilikuwa ni jina lake la kati.

Duniani kuna magaidi wakubwa maarufu wawili ambao karibu kila mtu amepata kuwasikia,Carlos the Jackal na Osama bin Laden.

Tofauti kubwa ya Carlos na Osama ni kwamba Carlos yeye alikuwa gaidi wa kisiasa wa itikadi za kikomunist wakati Osama bin Laden yeye ni gaidi wa itikadi za kidini.

Pia tofauti kubwa zingine ni kuwa Carlos yeye alikuwa ni gaidi ambae anapanga mikakati na kwenda front mwenyewe kwenda kuitekeleza wakati Osama alikuwa yeye ni mpanga mikakati na mfadhili wa matukio ya kigaidi.
Kwa mukhtadha huo utaona kuwa Carlos the Jackal ndo gaidi mkubwa aliyepata kutokea duniani.
Image result for Carlos The Jackal

Carlos alianza kujiunga na movement za kisiasa za kikomunist tangu bado akiwa mdogo kutokana na msukumo wa baba yake, ambae alikuwa mkomunist muaminifu.

Alijiunga na chama cha National Communist Party cha nchini Venezuela mwaka 1959 kabla ya kwenda kujiunga na camp ya Matanzas huko Havana Cuba.
Mwaka 1968 alijiunga na chuo kikuu cha Patrice Lumumba cha huko Urusi ambacho kilikuwa maarufu kwa kuzalisha wanamapinduzi hodari duniani.

Lakini hakukaa sana akawa amefukuzwa hapo chuoni kwasababu mbalimbali ikiwemo kutokufaulu vizuri masomo yake na matatizo mengine na uongozi wa chuo hicho.

Baada ya kufukuzwa chuo alienda moja kwa moja mpaka Beirut Lebanon ambako alijiunga na kundi la PLPF na kujitolea kuwa mpiganaji kwa ajili ya kuwatetea wapalestina pamoja na kupinga uzayuni.

Mwaka huo wa 1970 ndo mwaka ambao Carlos alianza rasmi kuwa mpiganaji wa kigaidi,alipofika Beirut alipelekwa huko nje ya mji wa Amman- Jordan kwaajili ya mafunzo ya upiganaji kwa kutumia silaha.

Alipokamilisha mafunzo hayo alienda kujifua zaidi kwenye chuo cha mambo ya kijeshi kinachoitwa H4 ambacho walikuwa wanafundishwa na maafisa wa kijeshi wa Iraq mpakani mwa Iraq na Syria.

Baada ya kukamilisha mafunzo hayo,alienda kujiunga na wapiganaji wa Black September huko Jordan,ambao ni kundi la wapalestina waliokuwa wa PLPF na PLO chini ya Yasser Arafat ambao walikuwa wakipigana na serikali ya Jordan.
Akiwa na Black September ni huko ambako alijizolea umaarufu wa kuwa mpiganaji hodari na jasiri.

Baada ya vita ya Jordan kuisha Carlos alipelekwa jijini London ili aweze kuwa anakusanya taarifa za watu muhimu wenye itikadi kali ya kizayuni ambao wanatakiwa watekwe au wauawe.
Baada ya kukamilisha hii kazi alienda Ufaransa ambako alikutana na Mohamed Boudia ambae ni gaidi habari ingine wa kizazi chake.
Mohammed Boudia alikuwa na sifa ya kipekee ya kujibadili muonekano na hata kutokea kama mwanamke,mzee nk pale anapotaka kuwakwepa majasusi wa Mossad wa Israel.

Waziri mkuu wa Israel kipindi hicho mama Golda Meir alimuweka Boudia katika list ya watu 11 ambao lazima wauwe kwa sababu ya kushiriki kupanga na kutekeleza mauaji ya wana michezo wa Israel kwenye Olimpic ya Munich mwaka 1979 (Tafuta movie inayoitwa Munich).

Akiwa na Mohamed Boudia walifanya matukio mengi ya kigaidi kwa kushirikiana.

Walitumia advantage moja kubwa ya kufanana,Carlos na Boudia walikuwa wanafanana wajihi hata kimo,na kwasababu Mohamed Boudia kipindi hicho tayari alikuwa ni gaidi anayewindwa na shirika la kijasusi la Mossad na lile la Ufaransa la DST,walikuwa wanahakikisha wanakuwa katika muonekano mmoja wa kufanana muda wote ambao ulikuwa unatumika kuwaingiza maboya majasusi waliokuwa wanawafatilia.

Kwa mfano kama Mohammed Boudia alikuwa anataka kwenda kufanya tukio,Carlos alikuwa ndio anaanza kutoka kwenye nyumba na kuondoka na gari..

hii ilikuwa inapelekea wale waliokuwa wanamfatilia wamfuate kwa nyuma kujua anaenda wapi,kuonana na nani na kufanya nini.
Kwa kutumia mwanya huo Carlos alikuwa anawazungusha mji mzima kupoteza muda na huko nyuma Muhammed Boudia alikuwa akitoka na kwenda kufanya matukio.

Hii haikuchukua muda sana kabla mamlaka za usalama za Mossad hazijashtukia mchezo na kumuua kwa bomu la kutega kwenye gari Mohammed Boudia mwaka 1973.(Tafuta kitabu cha Maisha ya Mohammed Boudia).

Baada ya kifo cha rafiki yake Mohammed Boudia,Carlos alifanya tukio la kulipa kisasi la kutaka kumuua Joseph Sieff alikuwa ni mfanyabiashara tajiri na kiongozi wa movement za kizayuni aliyekuwa anaishi ufaransa, ambapo alimpiga risasi ya chini ya pua,na alipotaka kummalizia bastola aliyokuwa anaitumia ilijam hivyo akakimbia.

Mwaka 1975, aliekuwa mtu wa kati wa mawasiliano (contact person) kati ya PLPF na Carlos,Michel Mourkharbal alikamatwa na shirika la kijasusi la DST la ufaransa na kubanwa ili akawaonyeshe Carlos (mpaka kipindi hicho hakuna shirika la kijasusi lilikuwa linamjua Carlos kwa sura), Michel pamoja na spy agents hao wa DST walimkuta Carlos katika house party na marafiki zake wakinywa.

Baada ya kutakiwa awaonyeshe Carlos ni nani,alipowaonyesha tu Carlos aliwashuti wote watatu na kuwauwa.Baada ya tukio hilo alitoroka ufaransa na kwenda Beirut.

Mwaka 1975 Carlos alitikisa dunia kwa kuongoza kundi la Black September na kuwateka mawaziri na maafisa wa ngazi za juu 60 wa nchi zinazoongoza kwa kutoa mafuta duniani OPEC, huko Vienna Austria.

Katika tukio hilo watu watatu waliuwa, Carlos alitoa sharti kwa serikali ya Austria kusoma kwenye TV na radio kila baada ya masaa mawili juu ya mateso ya watu wa Palestina ama sivyo ataendelea kuua mateka.

Kitu ambacho kilitekelezwa na serikali ya Austria. Baada ya siku mbili walipatiwa ndege ambayo iliwapeleka mpaka Libya ambako Ghadafi alikataa kuwapokea kwasababu kati ya hao watu watatu waliouawa alikuwemo afisa wa Libya.

Waliachia baadhi ya mateka na kuelekea Algeria ambako aliachia mateka waliobaki.Baada ya tukio hili Carlos alifukuzwa kutoka katika kundi la PLPF kwasababu ya kukiuka maelekezo ya mkuu wake Waddie Haddad kwa kutokuwaua mawaziri wa OPEC pale alipoona kuwa masharti waliyotoa hayakutekelezwa.

Katika tukio hili inasemekana Carlos alipokea mshiko wa nguvu kutoka serikali ya Saudia ili asiwadhuru mawaziri na maafisa wake, kati ya dola million 20-50,ambazo wenzake wanasema alizichikichia kwa matumizi yake binafsi na sio kwaajili ya mapambano ya kuikomboa Palestina.

Baada ya kufukuzwa ndani ya PLPF Carlos alielekea Ujerumani mashariki ambako walikuwa wanafata itikadi ya kikomunist,ambako alipewa support ya wafanyakazi 75 na aliweza kuunda kundi lake mwenyewe linaloitwa Organization of Armed Struggle,ambalo lilikuwa na wapiganaji wa kilebanon,Syria na waasi wa kijerumani.

Ambapo aliendesha harakati zake za kigaidi kwa kulipua sehemu mbalimbali za ujerumani magharibi.Inasemekana kipindi chote hiki Carlos alikuwa agent wa shirika la kijasusi la KGB la Urusi lililokuwa likimuunga mkono na kumtumia kwa siri.

Mwaka 1982, aliekuwa mke wa Carlos-Magdalena Kopp,alikamatwa nchini ufaransa akiwa na gaidi mwingine wa kikundi cha Carlos wakiwa wamebeba milipuko kwenye gari,baada ya kukamatwa Carlos alitoa sharti waachiwe ama atalipua sehemu mbalimbali za Ufaransa.
Serikali ya nchi hiyo ilikataa,kitu kilichosababisha kutokee balaa la milipuko ya mfululizo iliyojeruhi watu mamia na kuua zaidi ya watu kumi.

Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha,miaka ya mwisho wa vita baridi kati ya marekani na Urusi,Carlos alikuwa hapati support tena aliyokuwa ameizoea kutoka kwenye nchi zinazofata mrengo wa kikomunist.

Mataifa mengi yaliyokuwa yanamtumia yaliona hayana kazi nae tena na kuanza kumfukuza katika nchi zao.Mpaka kufikia mwaka 1985 Hungary walimfukuza ambapo alijaribu kwenda Iraq,Libya na Cuba ambako nako walimkataa.

Mwishoni alipokelewa na Syria ambao walimpa sharti la kutojihusisha na mambo ya kigaidi.
Ambapo alikaa bila kufanya matukio yoyote mpaka mwaka 1991 ambapo serikali ya Saddam Hussein walimfuata baada ya kuisha vita vya ghuba,ili akawafanyie kazi za kigaidi dhidi ya nchi za magharibi,jambo ambalo lilipelekea Syria kumtimua na akaelekea Jordan ambako aliishi kwa muda mfupi kabla ya kupewa hifadhi Sudan (Tafuta movie inayoitwa Carlos).

Mwaka 1994 mashirika ya kijasusi ya Marekani na Ufaransa yalipata fununu juu ya uwepo wa Carlos nchini Sudan na kuanza kumfuatilia.

Baada ya makubaliano na nchi ya Sudan ilitakiwa akabidhiwe kwa Ufaransa.Jambo ambalo lilitekelezwa kipindi ambacho Carlos alikuwa amefaniwa operesheni ya tezi dume.

Mlinzi wake alimsubiri akiwa amelala usiku akampa dawa ya kumlevya na kumfunga miguu na mikono kisha walimuhamisha hapo hospitali na kwenda kumficha mahali pengine,
baadae walimkabidhi kwa shirika la kijasusi la Ufaransa lililomsafirisha mpaka Paris kwaajili ya kwenda kujibu mashtaka ya kuwaua majasusi wawili wa ufaransa pamoja na informer wao.

Mwaka 1997 alikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela. Huyo ndo Carlos the Jackal, gaidi aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kujibadili ili asiweze kukamatwa na ambae aliisumbua sana dunia zaidi ya miaka 20...

 SOURCE : JF-Expert Member


Sunday, April 2, 2017

6:36 PM

SOMA MAKALA NZITO KUTOKA KWA YERICKO NYERERE YENYE UJUMBE KWENDA RAIS MAGUFULI

Imeandikwa  na  Yericko Nyerere
Image may contain: 1 person, closeup
ZAWADI YA JUMAPILI KWA MH. RAIS JOHN POMBE MAGUFULI
Mh Rais, kwanza kabisa naomba nikusalimie SHIKAMOO... Mh rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pili naomba utambue Mh Rais mimi Yericko Nyerere mkulima wa Bamia Mbutu Kigamboni ninavichukia vitu viwili tu duniani, cha kwanza ni Shetani yule afahamikae na wakristu na waislamu, na cha pili naichukia CCM yani hicho chama ambacho kimekupa dhamana ya urais na ambacho wewe ni mwenyekiti wake. Hili nakuomba utambue wazi misimamo yangu kwa kuwa ni haki yangu inayolindwa kwa katiba ya nchi yangu na katiba ya ulimwengu.
Leo jumapili nataka nikupe zawadi yangu maalumu kwako Mh rais wangu kipenzi, ninatumia mitandao ya kijamii kama ukurasa wangu wa facebook, JamiiForums na twita kufikisha zawadi yangu ya jumapili kwako kwakuwa naamini wewe ni mmoja ya wasomaji wazuri wa habari za mitandaoni na ninahakika wewe ni mmoja ya "mashabiki wangu" katika kurasa zangu za mitandao kama JamiiForums, Instagram na Twita. Nilifurahi juzi uliposema unasoma haya tunayotaandika...
Naam, Mh Rais, tunapingana kwa mengi, tunakosoana kwa mengi japo wewe hupendi kupingwa wala kukosolewa, Lakini leo nakuomba ukubali kupingwa, kukosolewa na kusifiwa, yote hii nikwakuwa wote mimi na wewe na wale tunalipenda taifa na wote tunawajibika kwa taifa letu lifike kwenye ndoto ya taifa huru kiuchumi, kifikra, kisiasa na kitamaduni.
Naaam, Katika kujenga taifa letu ni lazima tuwe na kipaumbele, na katika taifa lililoparaganyika kama Tanzania linahitaji mbinu tofauti sana katika kufikia malengo ya taifa la uchumi wa kati na uchumi imara.
Hapo awali tulishauri serikali yako iwe na vipaumbele mhimu katika kujenga taifa, hili lilitokana na ukweli kwamba taifa na serikali yako Mh Rais John Pombe Magufuli haikuwa na dira wala kipaumbele kilichoonekana kwa umma, kila jambo tuliligusa kanakwamba hatuna malengo.
Baada ya hapo nilianza kusikia na kukuona mh Rais unasema Tanzania inapanga kununua ndege aina ya Boeing 787 Dash 8 Dreamliner yenye uwezo wa kuchukua abiria 262 ambayo inatarajiwa kuwasili nchini Juni 2018.
Ndege nyingine ambazo Tanzania itazinunua ni ndege moja aina Bombardier Q400 Dash 8 NextGen inayotarajiwa kuwasili Mwezi Juni 2017, ndege 2 aina ya Bombardier CS300 zenye uwezo wa kuchukua kati ya abiria 137 na 150 na zinazotarajiwa kuwasili nchini kati ya Mei na Juni, 2018. Malipo ya awali kwa ndege hizi yameshafanyika. Hii inamaana kwamba taifa litakuwa na ndege 6. Hapa nilianza kupata mwangaa wa kipaumbele chak, safi sana.
Nimefuatilia kwa miezi kadhaa tangu shirika la ndege kupitia pangaboi zake lianze kazi, nikiri kuna mabadiliko makubwa ya kimfumo, nimeona wanatumia mfumo ambao unatumiwa na Emirates, na Rwanda. Ni mfumo mzuri katika katika ulimwengu mpya wa biashara ya anga...
Pia udhibiti wa watumishi wa umma katika kusafiri kumeongeza faida kubwa kwa shirika hili, ifahamike kuwa mteja mkubwa wa biashara ya anga nchini tanzania ni serikali kupitia watumishi wake, Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2015 TASAF pekee ndio iliyovunja rekodi kwakulipa nauli ya ndege yenye thamani ya Shilingi bilioni 3 (safari za ndani).
Utaratibu mpya wa serikali hivi sasa watumishi wote wanaosafiri nchini (safari za ndani) wanatumia ATCL, na malipo ya nauli zao yanalipya kupitia bajeti ya wizara husika yaani mfano wizara ya Nishati Na Madini katika bajeti yao wameainisha kwamba watatumia 59 bilioni katika safari za ndani, basi upembuzi yakinifu unafanywa kuhusu safari zote zitakazotumia ndege, pesa inapelekwa kabisa ATCL...
Kinachofuata ni wizara muda wa watumishi wao kusafiri ukifika wanapeleka majina mapema wakahakikiwe na wakatiwe tiketi tu.
Kiongozi wa Ethiopia alipoamua kujenge shirika la ndege la Ethiopia aliamua kwa dhati kusimamisha baadhi ya mambo katika taifa kwa mwaka mzima ili ajenge shirika hilo bora barani Afrika, moja ya mambo yaliyosimamishwa ni Elumu na Afya,
Yaani wizara hizo hazikupewa pesa ya bajeti kwa mwaka huo na badala yake pesa ikanunulia ndege... Huko ni Ethiopia na tuombe kiongozi yeyote nchini asije kuiga staili hii kwani Ethiopia walikufa watu wengi kwakukosa huduma za Afya.
Msimamo wangu toka awali ni kwamba, ili taifa liendelee ni lazima tuwe na vipaumbele na kila kipaumbele tuhakikishe kinafika mwisho katika utekelezwaji, na hili bado naendelea kusimamia na kuamini kwamba hii ndio njia maridhawa ya kuongoza nchi duniani kote.
Tanzania ina vitu vitatu ambavyo vikipangwa kwenye vipaumbele vya taifa kimoja baada ya kingine taifa litapona na kuwa la mfano barani Afrika.
1. Nishati na Madini
2. Bandari/Maji
3. Anga
Nimefurahi zaidi kuona sasa "inawezekana" unaingia kwenye kipaumbele cha pili ambacho ni sekta ya madini. Kati ya hivi vipaumbele naamini taifa likiamua kutekeleza kimoja kimoja mpaka mwisho taifa litafanikiwa na kuwa taifa la mfano barani Afrika. Hoja ni namna ya kuvitekeleza vipaumbele hivi huku siasa za vyama zikilitafuna taifa bila ganzi wala lepe.
Leo nasimama wima KUKUPONGEZA kwa hatua yako ya kuthubutukuzuia makontena yaliyo na mchanga wa madini ambayo yanasafirishwa kwenda Ulaya kwa uchakataji zaidi.
Ninazo sababu nyingi za kukupongeza kwa hatua hii, Naomba ifahamike kwamba, Tangu mwanzoni mwa miaka ya 1998 taifa ndipo lilipoanza kuumizwa na mikataba ya kilaghai katika sekta hii ya madini, mikataba hii mingi wewe Rais wangu ulishiriki ukiwa ndani ya baraza la mawaziri wakati ikiingiwa, hivyo wewe ni mmoja ya wanaolitweza taifa hili leo kwa mikataba hii inayompa haki mwekezaji kubeba ule mchanga uliouzuia juzi. Nilitaraji uanze na mikataba yenyewe, vile viwanja vya ndege vilivyomigoni vinavyotumika kutoroshea madini bila kulipa kodi.
Migodi ya Buzwagi na Bulyankulu, inaelezwa kwamba 70% ya tani za mawe ya mchanga wa dhahabu unaku katika mwitikio sawa na mchakato wa mgodi wa geita. Hivyo taarifa za kuaminikazinasema 70% ya tani za mawe/mchanga ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyankulu wanapata dhahabu halisi 97% hapo hapo mgodini.
Kwahiyo hicho kinachosafirishwa kwa makontena kinachoitwa mchanga ni 30% ya tani za mawe/mchanga wa madini. Maana imechanganyikana na copper na silver. Kwa hiyo wanachofanya wanafanya nikusafirisha kwenda kuchakata ili kupata gold, copper na silver.
Migodi ya Geita na North Mara, dhahabu inasafishwa palepale. Yaani wanachimba, inapelekwa mashine ya kuchakata pale pale mgodini hadi wanapata gold bars (dhahabu halisi 98%). Migodi ya Buzwagi na Bulyankulu, mawe yake ni tofauti kidogo na yale ya Geita na North Mara, maweyake yana dhahabu, copper na silver.
Kwa hiyo Bulyankulu wanachimba takriban tani milioni moja kwa mwaka. Wakifanya hiyo uchakataji wanaiconcentrate hadi inabaki tani elfu ishirini na tano tu. Hii ndio yale Makontena ya kusafirisha nje yakachakatwe huko kupata dhabu halisi
Kwa Buzwagi, wanachimba tani milioni nne kwa mwaka, wakifanya hio uchakataji, wanabaki na tani elfu ishiri na tano pia. Hii ndio yale Makontena ya kusafirisha nje yakachakatwe huko kupata dhabu halisi
Sasa hizo tani elfu hamsini ndizo zinazosafirishwa kwenda nje kwa mwaka (tani elfu ishirini na tano za Bulya na tani elfu ishirini na tano kutoka Buzwagi)
In summary katika mapato yote ya Bulyankulu na Buzwagi, mapato asilimia 70 yanapatikana hapo hapo mgodini bila kupeleka kuchakata nje ya nchi. Na mapato yao asilimia 30 ndio yanatokana na michanga (concentrate) inayosafirishwa nje. Kati hiyo 30%, asilimia 25 ni mapato kutoka dhahabu na asilimia tano ni copper na silver.
Asilimia 95 mauzo ya makampuni haya yanatokana na dhahabu, asilimia tano ni copper na silver. Kati ya hizo 95%, asilimia 70 ya dhahabu inasafishwa mgodini, na asilimia 25 ya dhahabu ndio inasafirishwa nje kuchakatwa, pamoja na hiyo asilimia tano nyingine ambayo ni copper na silver. Mashine bora za kuchakata hiyo michanga zipo Germany, China na Japan.
Tanzania tunaweza kujenga kiwanda cha kuchakata hapahapa bila kusafirisha mchanga tena, ili hiyo asilimia 30 ya mapato ya Bulyankulu na Buzwagi yasafishwe hapa hapa Tanzania, muda mfupu nasi kama nchi tutakuwa na uwezo wa kushindana na wachina, wajapani na wajerumani. Maana kutegemea mzigo wa Buzwagi na Bulyankulu hautatosha kuendesha hiyo mitambo. Taarifa zinasema mgodi wa Buzwagi wamebakiza miezi 12 tu kumaliza hiyo michanga inayosafirishwa, Inamaana itabakia Bulyankulu tu ndio itakayokuwa inatoa hiyo michanga....tani elfu 25 kwa mwaka.
Japo kwa haraka haijafahamika kwenye tani 50,000 zinazikwenda nje kuchakatwa maduni hupatikana kiadi gani, lakini Kwahesabu za kawaida bei ya gram 1 dhahabu bei inasimamia (50,000/=) elfu 50,000/=
Hivyo kilo1 ya dhahabu sawa na gram 1000 ni (50,000,000/=) milioni 50.
Tweke kadirilio la chini makampuni haya hupata 1/4 ya madini toka kwenye mchanga wa tani 50,000, Tani 12.5 ya dhahabu sawa na kilo ngapi ya dhahabu? Zidisha mara bei ya gramu ya dhahabu ili ujue makapuni yanatuibia shingangapi kwenye mchanga huu tu.
Kuvunja mikataba hii au kuingilia chochote katika biashara hii ni ngumu sana, Taifa lilihitaji mtu anayeweza kutumia mwanya wa amri ya kirais (presidential decree) ili kuhakikisha mikataba hii inahuishwa. Nakupongeza rais Magufuli katika hili mamlaka yako ninashauri yatumike huku kwa nguvu zote bila kusikiliza kelele za watu, badala ya mamlaka yako kutumika kwa vitu visivyo na tija katika taifa "mfano" kumkamata Malisa GJBen-Rabiu Wa Saanane na Yericko Nyerere kwakuwa tu wanakukwaza huku mitandano, hayo yatakuwa matumizi mabaya ya madaraka. Lakini katika hili la madini rais una sapoti yangu kabisa.
Mh Rais, Mwaka majuzi nilifika katikmiji ya Berlin na Bremen nchini Ujerumani, nikapata fursa ya kuzuru sehemu ya uhifadhi wa kumbukumbu za makoloni ya ujerumani, moja ya makoloni hayo ni Tanganyika. Katika kumbukumbu zile ipo michoro ya madini ya Tanganyika ambapo inaonyesha kuna AINA 360 za madini katika ardhi ya Tanganyika ikiwa ni nchi ya kwanza barani Afrika kuwa na aina nyingi za madini.
Mtazamo wangu Rais Magufuli huhitaji kutumia amana ya pesa ya nchi taslimu katika kutekeleza vipaumbele vyaka vya taifa, bali tumia raslimali hizi katika kulijenga taifa, dunia imebadilika, ipo katika uhitaji, wewe unayo unahitaji kiwanda cha kuchakata mchanga wa madini hapahapa, ACCIA, Bulyankulu, Buzwagi na GGM wanahitaji madini, wambie wajenge hapa huo mtambo tutakatana kwenye mirahaba ya madini, Wewe una gesi, yule anao utalaamu, wewe unayo uranium, yule anavyo vinu vya nyuklia, wewe unayo Tanzania, yule ana kiwanda cha vito, wewe unacho chuma, yule ana kiwanda cha chuma anahitaji chuma,
Mfano, katika mazingira haya unatoaje pesa taslimu kununua ndege ikiwa wenye kiwanda cha ndege wanahitaji madini ya Zinki na wanaagiza Uchina ilihali Uchina hawa wanayapata Tanzania madini hayo? Kwanini usimwambie Boing alete ndege 40 kisha aje achukue mdini hayo Tanzania kwa miaka10.
Unatoaje pesa taslimu kujenga Reli ilihali wachina hawa wanahitaji madini ya safaya? Kwanini usimwambie mchina ajenge reli kisha avune madini ya safaya kwa miaka 10.
Unatoaje pesa kununua ndege za kivita ilihali Warusi wanahitaji Uranium kwaajili ya viwanda vyao vya kurutubishia silaha za kikemia? Kwanini usimwambie Mrusi aje avune madini ya uranium kwa miaka kumi?
Kwanini hatujifunzi kutoka kwa nchi zilizofanikiwa mfano Singapore, Malaysia, China nk?
Nchi zenye raslimali nyingi kama Tanzania haiwezi kutumia mfumo wa nchi zisizo na raslimali kama Kenya, Rwanda nk katika kufikia uchumi wa kisasa. Lazima tutumie raslimali zetu kujenga taifa lakini tukumbuke njia ya kuzitumia raslimal hizi sio lazima ziwe zile zinazopendekezwa na wazungu...
Tuamue sasa mfano Zambia, Uganda na nchi nyingine zikihitaji gas tutumie negotiator wazuri, Kenya wakihitaji Gesi tunapima kiasi cha gesi wanayohitaji kisha kinathaminishwa na kuwapa kazi ya kujenga mji wa Dodoma wenye thamani ya trilioni 12. Zambia wakihitaji vilevile tunawapa kazi ya kusambaza maji nchi nzima kulingana na mahitaji yao...
China vilevile wakihitaji makaa ya Mawe, tunawambia tunahitaji Reli ya kisasa kutoka Tanzania hadi Rwanda, hakuna kutumia pesa ya umma kufanya jambo ambalo lingefanywa na raslimali tulizozikalia.. Urais hauna chuo.
Dubai, China, Malaysia S.Korea, N.Korea, Singapore nk walifanikiwa kwakutumia mfumo huu, tun kila sababu ya kuchagua nani tushirikiane na nani tusishirikiane kwa maslahi ya Taifa...
Pamoja na kwamba kuna masharti na mikataba ya kimataifa inayoweza kutuzuia kufanya biashara ya namna hii, lakini lazima tujifunze kwa waliofanikiwa kupitia njia hii...
Katika hili la kuchagua kipaumbele na sasa kuingia kwenye sekta ya madini nakupongeza sana, mengine yaache yajiendee kama yayalivyo lakini tekeleza moja kwa vitendo na lifike mwisho kabisa, hakika matokeo chanya yatapatikana...ijapokuwa unaathiriwa na siasa za vyama.
Na Yericko Nyerere
 

Thursday, March 16, 2017

9:55 AM

ELIMU#### Hatua 4 zitakazomaliza changamoto zako zote za kimaisha


Je, ni mara ngapi umewahi kusikia ule usemi usemao 'kisicho kuua kitakuimarisha kiaskari' je wewe unaamini vipi katika usemi huu? Sasa leo naomba nikwambie kuhusu changamoto zinavyoweza kukuimarisha katika maisha yako.

Kwenye hatua za maisha kuna changamoto nyingi sana na kama hauna msimamo unaweza kujikuta unakata tamaa kabisa kutokana na magumu unayopitia.

Tambua kuwa kila mtu katika maisha yake huwa na changamoto zake hivyo zinazokukuta wewe usidhani kuwa umeonewa kumbuka kuwa kila mtu anachangamoto zake na huenda nyingine ni kubwa kuliko zako.

Tofauti ya kupambana na changamoto mara nyingi hutofautiana kwenye jinsi gani wanakabiliana na yale yanayowatokea na ndio maana tatizo moja linaweza kuwatokea watu wawili, lakini wakapata matokeo tofauti.

Hizi hapa njia za kushinda changamoto zako katika maisha yako.

1. Siku zote unapaswa kuamini kuwa kila changamoto unayopitia  iko ndani ya uwezo wako na unauwezo wa kuishinda.

2. Tambua kuwa kila changamoto unazozipitia katika maisha yako sasa huweza kubadilika kuwa fursa endapo utakabiliana nayo vizuri.

3. Kumbuka kuwa hakuna tatizo jipya maishani kila unachopitia kuna mtu au watu waliwahi kupitia au wanapitia pia kwa sasa na bado walishinda. Hivyo na wewe unaweza kushinda.

4. Pamoja na changamoto ambazo unapitia sasa, lakini kumbuka kuwa hakuna changamoto ya milele kwani changamoto zote huwa ni za muda mfupi tu na zitapita.

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi

Saturday, February 4, 2017

4:56 PM

UNATAKA KUJUA?? Anaitwa kanali Patrick Karegeya mkuu wa idara ya ujasusi Rwanda,Aliuawa kwa kunyongwa huko Afrika kusini

imeandikwa kwa Respicius Francis


#SIASA NI HATARI SANA .
1-Kwenye picha mwenye suti nyeusii Anaitwa Kanali Patrick Karegeya alikuwa mkuu wa idara ya ujasusi ya Rwanda kabla ya kukimbilia uhamishoni Nchini Afrika Kusini.
-Karegeya aliuawa Mwaka 2014 katika Hotelini moja ,Afrika Kusini, ambako alikuwa akiishi kwa miaka kadhaa ambapo viongozi wa upinzani nchini Rwanda walimtuhumu rais wa nchi hiyo Paul Kagame kufuatia mauaji hayo.
-Kanali Karegeya alikuwa ni rafiki wa karibu na mshirika mkubwa wa rais Kagame wakati wa vita vilivyomweka madarakani rais huyo na baadaye kukosana, alikutwa amenyongwa katika Hoteli ya Michelangelo, mjini Johannesburg.
-Taarifa za polisi zilisema kuwa mwili wake ulipatikana kitandani ndani ya Hoteli hiyo, ambapo uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa shingo yake ilikuwa imevimba huku kukiwa na kitambaa chenye damu na kamba ndani ya chumba hicho,
-Theogene Rudasingwa ambaye ni kati ya viongozi wa upinzani anayeishi uhamishoni nchini Marekani alipozungumza na simu na waandishi wa habari alisema mauaji hayo yalifanyika yanafuatia amri iliyotolewa na rais Kagame lakini serikali ya rais ---Kagame ilikanusa kwa nguvu tuhuma hizo./
Marehemu Karegeya, alitumikia kama mkuu wa ujasusi nje ya nchi kwa karibu mwongo mmoja kabla ya kushushwa cheo na kuwa msemaji wa jeshi na baadaye akakamatwa na kufungwa.
Mwaka 2006 alivuliwa cheo cha kanali na mwaka mmoja baadaye alikimbilia uhamishoni.
-Yeye na wenzake bila uwepo wao mwaka 2011walihukumiwa kifungo cha muda mrefu nchini Rwanda kwa madai ya kuchochea mgawanyiko wa kikabila na kuhatarisha usalama wa nchi na uvamizi katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali. Rwanda ilitoa amri ya kukamatwa kwa viongozi hao.
-Karegeya aliyekuwa na umri wa miaka 53 kwa mujibu wa Polisi, ameacha mke na watoto watatu wanaoishi mjini Johannesburg, Afrika Kusini. 

Image may contain: 1 person
2 - Kwenye picha ya mtu mwenye nguo za kijeshi ni Faustin Kayumba Nyamwasa ambaye ni mpinzani mkubwa wa Rais Paul Kagame alinusurika kuuawa mara mbili mwaka 2010 alipokuwa, akiishi uhamishoni nchini Afrika Kusini
Bw: Nyamwasa Anasema marehemu Kanali Patrick Karegeya. alikwenda katika Hoteli hiyo kukutana na mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Apollo, ambaye alijifanya ni rafiki wa upinzani, ambapo chumba alichokutwa amekufa kiliandikishwa kwa jina na mtu huyo,


kwa  makala  za kusisimua hakikisha una mFollow  Respicius Francis kupitia ukurasa wake wa facebook

Wednesday, January 11, 2017

1:02 PM

USHUPAVU NI MSINGI WA KUYAMUDU MAZINGIRA NA KICHOCHEO CHA MAENDELEO YETU NA JAMII YETU.

Picha ya Fred Matuja
Eric Robert Greitens ni gavana wa 56 wa jimbo la Missouri nchi Marekani. Atakuwa anatimiza miaka 42 ifikapo April 10 mwaka huu.
Pamoja na kuingia katika shughuli za kisiasa na uongozi, pia Eric ni afisa wa kijeshi mwenye cheo (rank) cha luteni kamanda na kwa mfumo wa nchi za majeshi wa Commonwealth ambayo na Tanzania ni mwanachama, luteni kamanda ana cheo cha meja.
Gavana Eric Greitens alimshirikisha mwandishi wa kitabu aitwae Bill Murphy; Bill kaandika kitabu chenye dondoo kwa wazazi na walezi namna ya kutengeneza mfumo wa malezi ya watoto na vijana wenye mafanikio (How to Raise Successful Kids).
Katika kitabu hicho, Eric katoa mbinu kadhaa za kukuza akili ya mtoto au kijana ili afanikiwe maishani kwa kuwa na mchango wa maendeleo katika jamii yake pia. Binafsi kama Mtanzania niliepata kusoma taaluma ya elimu (au ualimu kama ambavyo watu wengi wamezoea kuita) nimeguswa na maarifa haya ni ninawiwa deni la kumshirikisha mtu yeyote kupitia ukurasa huu kwa lengo la kuchukua maarifa haya na kuyatumia yeye binafsi hali kadhalika kusaidia watoto na vijana walio nyumbani kwako na katika jamii inayotuzunguka kwa ujumla ili tuwe na Taifa lenye kuwajibika kupigana kwa lengo la kufanikiwa na kuambukiza mafanikio kwa wengine.
Pamoja na mfumo wa utandawazi na mabadiliko ya kimfumo hapa nchini, ila bado msingi wa ujamaa una sehemu kubwa sana Tanzania. Mfano, kama kuna msiba au harusi mfumo wa michango kufanikisha hafla hizi una misingi ya kijamaa. Katika mfumo wa kibepari hawana mifumo ya kusaidiana kama ilivyo hapa Tanzania ya leo. Hivyo kama wajamaa, tuna mengi ya kukumbatia na kuelimishana hususani, nyakati hizi zenye changamoto kubwa za kimtazamo. Pamoja na changamoto hizi za kifikra ambapo taarifa zinasafiri kutoka pande yoyote ya dunia kwa teknolojia ya mawasiliano, bado tuna jukumu la kuweka misingi ya kizalendo yenye kusudi jema la kutafsiri dhana ya kuwajibika ili kuijenga Tanzania yetu. Taifa hili ni letu, watu wa taifa hili ni ndugu zetu, tunawajibika kuwajenga kwa pamoja ili tuwe taifa lenye mafanikio yanayotufaidisha wote.
Luteni kamanda Eric anatufundisha, moja ya msingi wa mafanikio kwa mtoto, kijana na mtu yeyote maishani ni USTAHIMIVU (resiliance). Tafsiri rahisi ya ustahimivu ni uwezo wa kurejea kwa haraka kutoka katika changamoto za magumu; au hali ngumu na kuendelea kuwa na mzalishaji mwenye tija. (being productive and effective)
Ukisoma maisha ya yeyote aliefanikiwa na kuacha alama katika jamii yake, utakuta kila moja alikuwa na sifa hii. Eric amesisitiza, Inahitaji kuvumilia ili kufanikiwa hususani katika umahiri katika jeshi la Marekani. Nina hakika, nidhamu hii itakuwa inagusa na majeshi mengine yote hapa duniani. Hali kadhalika nidhamu kama hii inagusa watu waliofanikiwa iwe katika taaluma, biashara, harakati kama za kupigania uhuru walizofanya akina Mwl. Nyerere na kadhalika.
Luteni kamanda Eric anasisitiza umuhimu wa kuwasaidia watoto na vijana kwa kuwajengea mifumo ya kuwajibika ili kutimiza kusudi la wao kuwepo pale walipo. Ikiwa ni shule, chuoni au kazini, kuna ulazima kila mtu awe na fikra za kutimiza “mission” yay eye kuwa pale yenye mchango endelevu wka jamii yake.
Anasisitiza kuwa, watoto na vijana wanaweza kujifunza kupitia mbinu hizi hali kadhalika mtu yeyote vilevile anaweza kukuza au kuongeza ushupavu wa akili yake ili awe na ufanisi na tija katika shughuli zake za kila siku.
Kwa muhtasari, hizi ni dondoo chache zilizoainishwa na luteni kamanda Eric, ambazo sisi wazazi, walezi, viongozi katika maeneo ya kazi tunaweza kufanya ili kuleta kichocheo cha kuathiri watu walio tuzunguka,
1. Weka mfano mkuu wa kuigwa (Set a great example)
Kama ilivyo program yoyote ile yenye nia ya kuboresha maisha ya mtu, kuongeza ushupavu kunahitaji kuonesha hali ya kujitoa (demonstrating commitment). Mzazi, mlezi ambae una nafasi ya uongozi kwa watoto na vijana una wajibu wa kuwatia moyo watoto, vijana na watu wegine wanaokuzunguka kwa kujifunza kwa mfano kwa namna wewe unavyo ishi na kutenda kazi zako.
Kutoa tafsiri nzuri ili ieleweke, kumbuka msemo wa Ralph Waldo Emerson… “maisha yetu tunayoishi yanasema sauti kubwa sana kuliko yale tunayotamka”
"Watu wakiona jinsi unavyoweza kujinyanyua pale unapobamizwa chini, watajifunza tabia hiyo kwa kuiga toka ndani ya mioyo yao”
2. Wajibika/ Timiza wajibu wako (Take responsibility)
Kuwajibika maana yake ni unahusika kudhibiti maisha yako. Kuna mambo utatambua huwezi kuyadhibiti, na ukifahamu tofauti, utacheza nafasi yako kwa kufanya kila uwezalo kwa lile lililo ndani ya uwezo wako ili ufanikiwe.
Tunawajibika kuwafundisha watoto na vijana, hali kadhalika nasi kuishi maisha ya kutowalaumu au kutafuta sababu, ila kuwajibika kimatendo kwa mambo yanayotuhusu sisi, familia na jamii zetu.
3. Tafuta kuwatumikia wengine (Seek to serve others)
Pamoja na kutengeneza mfumo wa kuwajenga wengine ili kuwa na mchango kwao na dunia inayokuzunguka (kuwa na athari chanya kwa watu wengine). Toa huduma kwa wegine, maisha si kwa ajili wewe peke yako. Kila mmoja anawajibika kuwa rasimali na utambulike kama mtu wa kutegemewa na jamii yako kama suluhisho kwa changamoto zinazoizunguka jamii.’
Eric anasema "Watu tunatakiwa kujua tuna kitu cha kuwapa wengine” na tunawajibu wa kijifunza kutoa taswira ya kubadili mazingira yanayotuzunguka kuwa bora zaidi.
4. Tujifunze kushukuru kila siku (Practice daily gratitude)
Tabia ya kushukuru iko kwa watu wengi waliofanikiwa. Watu wanaotaka kufanikiwa na waliofanikiwa mara kwa mara hufanya majukumu yao bila kijali wanapitia changamoto gani. Hupenda kujenga tabia ya kuwashukuru wengine. Ili kunapanua uwezo wako wa kutenda kazi kama kiongozi (mzazi, mlezi una wajibu wa kuonesha uongozi) kwa kujenga akili yako kujikubali na kushukuru Mungu kwa vipawa, karama na uwezo ulio nao ambao umejaliwa kwa ajili ya kuwasaidia watu walio katika mzunguko wako wa ushawishi.
Tunawajibika kukabiliana na kila siku kwa shauku ya kufanikisha majukumu yetu; hata siku mbaya ya kukatisha tamaa na yenye hali ngumu, jione una kitu bora pengine kuliko wengine katika jamii iliyokuzunguka, na jiweke/jione una mchango kwa dunia inayokuzunguka.
Itaendelea
Fredrick Matuja
fmatuja@hotmail.com(P.T)

Thursday, December 29, 2016

10:10 AM

MAKALA MZITO!!! KAMA WEWE NI KIJANA UNATAFUTA AJIRA USIPITE BILA KUSOMA UJUMBE HUU KUTOKA KWA {Respicius Francis}Image may contain: 1 person, standing
  Respicius Francis mwaandishi  wa  makala  hii  kupitia  ukurasa  wake  wa facebook
, AJIRA ,AJIRA,
-Ajira imekuwa ni kilio sugu kwa vijana wengi hasa wale wanaomaliza elimu ya juu ,Na bahati mbaya sana serikali za kiafrika zimeshidwa kutatua tatizo hili
 Ukiangalia hapa Tanzania hili tatizo limekuwa sugu sana kila kijana analilia ajira ata zile fani ambazo ulikuwa unamaliza unaajiriwa moja kwa moja mfano kama ualimu mambo yamegeuka kwasabubu mitaani kuna vijana wengi ambao wamemaliza ualimu wakisubiri ,
-Ajira umekuwa ni wimbo kwenye mitandao ya kijamii hasa whatsapp,facebook maana haiwezi kupita siku bila kuona aandishi la kulalamikia ukosefu wa ajira,, Kwa upande wa serikali imekuwa inatoa majibu kwa vijana wajiajirii wasisubiri kuajiariwa na serikali, lakini serikali inasahau kuwa elimu ambao wamekuwa wanatoa kwa vijana kwanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu ni ile ambayo inamjenga kijana kusubiri kuajiriwa kwahiyo inawezekana hawa vijana wanaouliza ajira kwa serikali wana haki kabisa kwasababu tokea wanaanzaa shule ya msingi mpaka chuo kikuu waliambiwa kuwa wanasoma kwa ajiri ya kuajiriwa siyo kujiajiri kama serikali inavyotaka, Ata masomo ambayo tunafundishwa huko shuleni vyuoni yanamjenga kijana katika mazingira ya kuajiriwa siyo kujiajiri kwahiyo ukimwambia kijana kujiajiri ni vigumu kukuelewa na mwingine anaona unamshushaa thamani au unadharau elimu yake...
-Ajira limekuwa tatizo sugu Tanzania kwasababu unakuta shirika au kampuni linahitaji wafanyakazi 17 lakini wanaoenda kufanyiwa interview ni watu 1000 yan utafikiri watu wanaenda kutazama Mechi ya simba na yanga kumbe masikini wanaenda kupigana kupata ajira, Hii ni ishara kuwa tatizo ajira katika nchi ya Tanzania ni sugu lakini licha ya hivyo bado serikali inaendelea kutoa msisitizo kwa vijana wajiajiri siyo kutegemea kuajiriwa na serikali ..
UFUMBUZI
Vijana ni kweli ajira za kuajiriwa hakuna je tufanye nini??
-Hivi kuendelea kulalamika kwenye facebook kutatusaidia?
-Hivi kuendelea kulalamika kwenye makundi ya whatsapp kutatusaidia??
-Hivi kuendelea kuwalilia wanasiasa wakati wameisha twambia ajira hakuna njia pekee ni kujiajiri kutatusaiidia??
-Hivi kuendelea kushiriki interview zenye waombaji wa kazi 1000 zitatusaidia??
Hivi kuendelea kulalamika mikopo hakuna itatusaidia ?
UKWELI NI KWAMBA HAIWEZI KUTUSAIDIA KABISA CHA MUHIMU NI SISI VIJANA KUCHUKUA MAAMUZI MAGUMU YA KISAIKOLOJIA KUTAMBUA KUWA KUPATA AJIRA KWA KARNE HII NI BAHATI NASIBU, SASA VIJANA TUTAENDELEA KUSUBIRI BAHATI NASIBU HII MPAKA LINI??
USHAURI WANGU KWA VIJANA
Tunapomaliza vyuo vikuu tusitupane na tusitengane cha muhimu tuhakikishe tunaendelea kuwa wa moja ili kuweza kupambana na changamoto ya ukosefu wa ajira maana siku zote umoja ni nguvu..Tatizo ambalo kwa sisi vijana tunapomaliza vyuo vikuu mambo yanaishia hapo yule ...
-Hivi tukiwa watu kumi ambao tumesomea ualimu katika chuo ualimu hatuwezi tukaa chini na kubuni kitu ambacho kitatupunguiza uchungu wa kukosa ajira? mfano tukianzisha tution center au kituo kwa ajiri ya watu wanaorudi mtihani wa FORM 4 na SIX ??
-Hivi tukiwa madkatari kumi mbao tumeliza chuo kimoja hatuwezi kubuni kitu ambacho kinaweza kutupatia ajira ? mfano kwa kuanzisha huduma ya jamii katika maeneo ambapo kuna upungufu sana huduma afya kwa kutoa afya majumbani kwa watu ambapo wananchi wanaweza kuwa wanachangia huduma hiyo gharama nafuu sana??
-Hivi tukiwa watu 10 ambao tumesomea masoko hatuwezi kukaa chini tukabuni namna gani shule za msingi na sekondary private zinaweza zikawa zinawapata wanafunzi kirahisi badala ya kutumia gharama nyingi kutangaza kwe nye radio na tvi???
Hivi tukiwa watu kumi ambao tumesomea IT katika chuo kimoja hatuwez kukaa chini tukabuni namna shule au sekondary za msingi zinaweza kuwa zinatuma ripoti ya mwanafuzi kwa njia simu badala ya kuandika kwenye karatasi??
HAYA NI MAWAZO AMBAYO TUNAWEZA KUYAFANYA KAMA TUTAMUA KWA MOYO MOJA KUYATEKELEZA lakini lazima tukubali mpaka ufanikiwe lazima uwe tayari kupambana,Uwe tayari kuwa mvumilivu. uwe, tayari kuthubutu,Uwe tayari kutoka jasho,Uwe tayari kukutana na maumivu vinginevyo utaishia njiani..
VIJANA WATAULIZA MTAJI UNAPATIKANA WAPI WAKATI TUMEMALIZA CHUO??
JIBU
-vijana kama tuliweza kununua simu Smartphone na laptop wakati tunasoma chuo, hivi watu kumi tutashindwa kujifunga mkanda kupata mtaji kidogo??
-Vijana kama tuliweza kushiriki kuchangia harusi wakati tunasoma chuo ,hivi watu kumi tutashindwa kutafuta mtaji?
-vijana kama tuliweza kwenda Club,Kwenda bar kupiga moja baridi moja wakati tunasoma chupo, hivi watu kumi tutashindwa kupambana kutafuta mtaji>>??
Vijana kama tumeweza kufanya party kubwa wakati wa kumaliza masomo yetu ya chuo,Hivi watu kumi tutashindwa kupata mtaji wa kufanya biashara.??.
-Wakati vijana tunatumia mitandao ya kijamii kuchati hasa kupitia mtandao wa whatsapp ebu tumia muda kidogo na wenzako uliomaliza nao chuo kupitia mitandao hiyo hiyo kujadili ni namna gani ya kupambana na tatizo la ajira ??
-Vijana ambao mmeliza chuo kikuu na kubahatika kupata ajira au nafasi ebu nzuri rudini nyuma na kuwashika wenzenu mkono ambao hawajapata ajira pale wanapowaomba ushirikiano siyo kuendekeza ubinafsi na umimi maana kumekuwepo na tabia chafu mtu anapomaliz chuo na kupata ajira uwaona wenzeka wasiyo kuwa na ajira ni wajinga au hawana bahati...
-Vijana ambao hamna ajira mnatakiwa kuwa wabunifu kwa kukaa chini kuandika miradi ya biashara au wazo la biashara kupeleka kuwashawishi vijana wenzenu ambao wanaweza kutoa mitaji na kuwapa mitaja hasa hao wenye ajira,kwa kuonyesha ni jinsi gani huyo aliyekupa mtaji atafaidika vipi na wewe utafaidika vipi???
imeandikwa na Respicius Francis
simu 0755515906 au 0655515906
whatsapp 0755515906
Facebook .    Respicius Francis

Thursday, December 8, 2016

7:54 AM

BAADA YA KUPOTEA BEN SAANANE HAYA NDIYO MASWALI MAZITO KWENDA MAKAO MAKUU CHADEMA

imeandikwa  na  Respicius Francis kupitia  ukurasa  wake  wa facebook

1.Leo nataka nitoe dukuduku kwa chama cha chadema juu ya kupotea Ben-Rabiu Wa Saanane,
2.Lazima tutambue Ben saanane ni mfanyakazi pale makao makuu chadema,
3.Lazima tutambue Ben Saanane siyo mfanyakzi tu bali ni kiongozi kwasababu amekuwa naongoza program mbalimbali Chadema pale makao makuu,
4.Ukitaja vijana 20 mashauri wa chadema uwezi kukosa kutaja jina la Ben saanane, 
5.Ben wa saanane kafanya kazi nyingi chadema hakuna kiongozi mkubwa wa Chadema hasiye mjua BEN ,
MALALAMIKO YANGU.
1.kama mfanyakazi wenu kutoka makao makuu anapotea kwa wiki mbili alafu taasisi kubwa kama Chadema mnakosa kutoa taarifa mpaka watu kutoka facebook ndio wanaoanza kuhoji Ben Saanane yupo wapi?? baada ya kuona page yake facebook ipo kimya bila kuandikwa chochote hivi kweli kitengo cha usalama cha chadema kinafanya kazi??
2.Mtu Kama Ben saanane mfanyakazi kutoka makao makuu anapotea zaidi ya wiki mbili alafu taasisi kubwa kama Chadema inashindwa kutoa taarifa rasmi kwa vyombo habari mpaka muda huu,Ni waulize nyinyi wadau hali hii inatupa picha gani??
3. Mimi najiuliza pia kama Ben saanane anapotea zaidi ya wiki mbili alafu mpaka sasa Sijaona Taarifa yoyote kutoka kwa BAVICHA ,NI waulize nyinyi wadau hali hii inawapa picha gani??,,
4.Mimi nawaulizamaswali nyie watu wa makao makuu chadema siku ya tatu imepita mnapiga simu ya Ben Saanane haipatikani umekaa kimya??, Siku ya saba imepita mnapiga simu ya ben saanane umekaa kimya tu?? wiki pili imepita mnapiga simu ya Ben haipatikani umekaa kimya tu, wiki tatu simu ya ben haipatikan bado mmekaa kimya mpaka watu wa pembeni ndio wanajitkeza na kuanza kuuliza Ben yupo wapi??,,,,Ni waulize nyie wadau hii kitu imekaaje??
                          MY TAKE
1.Nilitegemea ofisi kuu chadema kama taasisi watupe taarifa kamili juu ya kupotea kwa Ben saanane ,Haiwezikani mfanyakzi wao kutoka makao makuu anapotea zaidi ya wiki tatu alafu hakuna taarifa yoyote kutoka makao makuu chadema mpaka muda huu.. Hivi vijana wengine kama Ben wanaotetea chama na kukipenda chama wanajifunza nini kwa jambo hili???,,,Tangazo muhimu.
  Kama wewe   ni  mwanafunzi au kiongozi  wa serikali ya wanafunzi kati ya vyuo  hivi ambavyo  tumevitaja  hapa Chini   Au  una ndugu  yako  anasoma  kati  ya  vyuo  hivi Tafadhari  wasiliana na  mtandao wa Tanzania classic kupitia namba     
   hizi,  
simu  065515906 au
  0754519588
Whatsap  0755515906.

1.CHUO  CHA  UNITED AFRIKA.
2.CHUO KIKUU  CHA IFM MWANZA
3.CHUO  KIKUU ARUSHA
4.CHUO KIKUU  ZUSA   [Zanzibar]
5.CHUO KIKUU MUM [Morogoro]
6.CHUO KIKUU CHA  MAJI {Ubungo}
7.CHU KIKUU  SEKOMU
8.CHUO KIKUU ST JOHN [ DODOMA]
9.CHUO KIKUU TEOFILI-TEKU
10.CHUO  KIKUU IRINGA
11.CHUO KIKUU MKWAWA [IRINGA]
12.CHUO KIKUU MARIAN
13 .CHUO  KIKUU  TUMAIN {MBEYA]
14.CHUO KIKUU STELLA  MARIS
15.CHUO KIKUU SEBASTIAN [LUSHOTO]


Wednesday, December 7, 2016

6:58 AM

SIMULIZI ZA KUSISIMUA.. JE, NI KWELI GENERAL IDD AMIN ALIMUUA MKEWE?

Ndugu zangu,
AMA kwa hakika, wanawake ni moja ya sura za Idd Amin ambazo hazikujulikana sana nje ya mipaka ya Uganda.
Inasemwa, kuwa General Amin alikuwa anahusudu sana wanawake. Kwamba alikuwa tayari kuua kwa sababu ya mwanamke.
Ikafika wakati, General Idd Amin alikatisha ziara au shughuli ya Kiserikali ili apate fursa ya kwenda kufanya ngono na mwanamke.
Walinzi wake wa karibu walifanya kazi pia ya kwenda kuwachukua wanawake aliowatamani bosi wao.
Walinzi hao walikuwa na kibarua pia cha kukariri ni nani bibi wa bosi wao, maana vimada wa Idi Amin walikuwa wengi.
Walinzi hao walifanya kazi pia ya kukariri ni nani mtoto wa Amin , maana, idadi ya watoto wa Amin waliotambulishwa kwa watu wa usalama wa Amin ilikuwa kubwa.
Inasemwa pia, kuwa kifo cha mmoja wa wake wa General Amin aitwaye Kay, kilitokana na ajali ya gari, ni ajali ya kushangaza. Ni ya kupangwa.
Hadi hii leo kuna wanaoamini ajali hiyo haikuwa kazi ya Mungu bali kazi ya General Idd Amin aliyoipanga vema kwa kushirikiana na watu wake wa usalama.
Hata hivyo, hakuna aliyeweza kuthibitisha ukweli mzima juu ya jambo hilo.
Tukio lingine la kushangaza katika mauhusiano ya General Idd Amin na wake zake ni pale alipotoa talaka kwa mpigo kwa wake zake watatu.
Wake zake hao ni Malyamu , Nora na Kay. Amin aliwatuhumu Malyamu na Nora kwa kujihusisha na masuala ya biashara wakiwa ndani ya ndoa. Kay naye alipewa talaka kwa kile ambacho Idi Amin alidai ni binamu yake!
Lakini, ukweli juu ya kuharibika kwa mahusiano hayo ya ndoa kati ya General Idd Amin na wake zake hao ni kwa Amin mwenyewe kuendekeza zaidi wanawake wa nje na kuwasahau wake zake wa ndoa.
Jambo hilo linathibitishwa pia na mwandishi Henry Kyemba ambaye nimebahatika kusoma kitabu chake kiitwacho; ' State Of Blood'.
Inasemwa, kuwa kitendo cha General Idd Amin kuwaacha wake zake hao na kutumia muda mwingi kulala na wanawake wa nje kuliwafanya wake zake hao, nao kujisikia kutotimiziwa mahitaji yao ya ndani ya ndoa. Nao walianza kutafuta mabwana wa nje.
Na hakika, siku ile ya wake hao kupewa talaka zao walifurahia sana. Walijisikia wako huru kufanya mambo yao nje ya nyumba ya General Idd Amin.
Ndoa yao na Amin ilikuwa ni kama kifungo.
Hawakupenda kuwa na mahusiano ya siri na mabwana wa nje.
Siku hiyo ya kupewa talaka kwa mpigo, Malyamu, Nora na Kay walifanya sherehe kubwa.
Kusheherekea kuachwa na General Idd Amin. Katika sherehe hiyo waliwakaribisha mabwana zao. General Idd Amin hakupewa mwaliko! Walimwambia abaki na mkewe kipenzi , Madina.
Hata hivyo, Malyamu, Nora na Kay walijikuta katika wakati mgumu nje ya ndoa ya Amin. Mikasa gani iliwafika?
Maggid,
Iringa.

Monday, November 28, 2016

8:13 PM

Makala nzito!!! Njama 638 za mauaji alizoepuka Fidel Castro

Fidel Castro akivuta sigara yake
Njama ya kutumia sigara kumuua Fidel Castro ambayo ilitibuka inajulikana sana, lakini njama nyengine 637 dhidi ya maisha yake ni zipi?
Shirika la kijasusi nchini Marekani CIA na watu waliotoroka Cuba wakati wa uongozi wa Castro walitumia nusu ya karne moja kufanya njama za kumuua kiongozi ambaye taifa lake lina athari kubwa kwa Marekani, kulingana na balozi wa Marekani nchini Cuba Wayne Smith.
Wakati mmoja kiongozi huyo wa Cuba alinukuliwa akisema, iwapo kuepuka majaribio ya mauaji kungekuwa miongoni mwa michezo ya Olimpiki ningejishindia medali ya dhahabu.
Hatahivyo baadhi ya njama hizo hazikutekelezwa ,kulingana na aliyekuwa mlinzi wa zamani wa Fidel Castro, Fabian Escalante.
Stakhabadhi zilizofichuliwa wakati wa utawala wa Bill Clinton zilionyesha kuwa CIA wakati mmoja walianza kuwafanyia utafiti konokono wa eneo la Carebean.
Njama, ilikuwa kutafuta konokono mmoja ambaye angemvutia Castro anayependa sana kuogelea na kumjaza vilipuzi ndani yake kabla ya kumlipua Castro atakapomshika
Mpango mwengine ulikuwa ule wa kutengeza boya la kuogelea ambalo huvaliwa kama shati na ambalo lingetiwa ugonjwa mbaya wa ngozi ili kumuathiri kiongozi huyo.
Mipango yote hiyo ilitupiliwa mbali.
Ajenti huyo alisikitika na akataka mpango mwengine ambao sio rahisi kuugundua,ripoti hiyo ilisema.
Mpenzi wa zamani wa Castro, Marita Lorenz alipewa dawa za sumu kumwekea katika kinywaji chake
Image caption
Mpenzi wa zamani wa Castro, Marita Lorenz alipewa dawa za sumu kumwekea katika kinywaji chake
Mmoja ya wapenzi wa Castro wa zamani ,Marita Lorenz alisajiliwa.
Alipewa dawa zenye sumu ili kuweka katika kinywaji cha Castro.Lakini Castro aligundua jaribio hilo na anadaiwa kumpatia bunduki yake badala yake atumie kumuua.
''Huwezi kuniua. Hakuna anayeweza kuniua,"Bbi Lorenzo alisema Bw Castro alimwambia, alipokuwa anahojiwa na gazeti la New York daily
Castro alidaiwa kutabasamu na kuendelea kuvuta sigara yake.''Nilijihisi nimetolewa pumzi kwa sababu alikuwa na uhakika juu yangu.Alinikumbatia na tukafanya mapenzi''.
Jaribio jingine lililokuwa maarufu dhidi ya maisha ya Castro ni lile la 2000, wakati ambapo mpango uliwekwa kuweka vilipuzi vingi katika jukwaa ambalo alitarajiwa kuhutubia nchini Panama.
Castro na wananchi wa Cuba walikuwa dhiki kubwa kwa MarekaniImage copyrightAFP/GETTTY IMAGES
Image caption
Castro na wananchi wa Cuba walikuwa dhiki kubwa kwa Marekani
Mpango huo ulitibuliwa na vikosi vya usalama vya Castro.
Watu wanne ikiwemo mtoro mmoja wa Cuba pamoja na ajenti wa CIA kwa jina Luis Posada walifungwa lakini baadaye wakaachiliwa.
Pia kulikuwa na mipango ya kumfanya Castro ambaye pia anajulikana '' The Beared'' aonekana kama chombo cha kukejeliwa badala ya kumuua.
Mpango mmoja ulikuwa kumwagia viatu vyake chumvi ya thallium wakati wa ziara yake ya ughaibuni kwa lengo kwamba anaposhika ndevu zake zingeweza kukatika.
Lakini mpango huo ulitibuliwa baada ya Castro kuahirisha ziara hiyo.Castro alichukua tahadhari ya hali ya juu ili kuwakwepa watu waliopanga mauaji yake.
Mwaka 1979 alipokuwa akielekea mjini New York ili kuhutubia mkutano wa Umoja wa Mataifa hakuweza kuwazuia wanahabari waliomuuliza iwapo alikuwa amevaa fulana ya ndani ambayo ina kinga dhidi ya risasi, alivua shati lake na kuwaonyesha kifua chake.
Ajenti wa CIA na mtoro wa Cuba kulia Luis PosadaImage copyrightAP
Image caption
Ajenti wa CIA na mtoro wa Cuba kulia Luis Posada
''Nimevaa fulana ya kawaida'',alisema.
Miongo kadhaa awali mwaka 1975, tume ya bunge la seneti nchini Marekani ilifichua maelezo ya njama nane dhidi ya maisha ya Castro kwa kutumia vifaa ambavyo tume hiyo inasema ''vinachosha akili''.
Njama moja iliopangwa na ambayo karibu ifaulu mara mbili ilikuwa ile ya kutuma dawa za sumu Cuba na kuwapeleka watu kumuua kiongozi huyo.
Ndevu za Fidel Castro pia zililengwa katika njama hizo za mauajiImage copyrightKEYSTONE
Image caption
Ndevu za Fidel Castro pia zililengwa katika njama hizo za mauaji
Ulikuwa wakati kama huo ambapo rais Kennedy, ambaye aliruhusu uvamizi wa kumuondoa madarakani rais Castro mwaka 1961 aliuawa, ambapo ajenti wa CIA alikuwa anatoa kalamu yenye sumu ilio na sindano kwa ajenti mmoja wa Cuba ili kumuua kiongozi huyo.
chanzo":bbc