Breaking

Showing posts with label sport. Show all posts
Showing posts with label sport. Show all posts

Sunday, June 3, 2018

9:21 AM

Video: Wachezaji wa Real Madrid wamlilia Zinedine Zidane kwa staili ya aina yake


Licha ya kuwa kocha pekee barani Ulaya kuisaidia timu yake ya Real Madrid kutwa taji la UEFA kwa nyakati tatu mfululizo Zidane amekuwa miongoni mwa makocha wanaoheshimika sana pia maarufu mwenye sifa nyingi nzuri.Mfaransa huyo ameamua kuikacha timu yake ya Real Madrid kama kocha na kukimbilia nchini Qatar huku wachezaji wake wakimuaga kwa majonzi ya aina yake kwa kutumia akaunti zao za mitandao ya kijamii.Tuesday, May 1, 2018

2:41 PM

Samatta Awaonya Serengeti Boys " Tulizeni Vichwa Madogo Tusije Kusikia Mmeanza Kuoa"

Samatta Awaonya Serengeti Boys " Tulizeni Vichwa Madogo Tusije Kusikia Mmeanza Kuoa"
Nahodha wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Ally Samatta amewapongeza vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kwa kutwaa ubingwa wa CECAFA Challenge U-17 nchini Burundi.


Serengeti Boys Jumapili ilifanikitwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge U-17) kwa kuwafunga vijana wa Somalia, mabao 2-0 yaliyofungwa na Edson Jeremiah dakika ya 25 na Jaffar Mtoo dakika ya 66.

“Hongereni sana 'Serengeti' (U17) kwa ubingwa wa CECAFA kwa umri wa chini ya miaka 17. Tunaamini TFF ina mipango mikubwa juu yenu. Tulizeni vichwa madogo, tusianze kusikia mmeanza kuoa sasa (utani). Hongereni sana,”. Samatta ameandika kupitia 'Twitter'.Serengeti Boys imerejea nchini Alfajiri ya leo na kupokewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe ambaye amewapongeza vijana kwa ushindi huo.

Monday, April 23, 2018

11:53 AM

Salah ashinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka PFAMchezaji hatari wa klabu ya soka ya Liverpool, Mohamed Salah ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka inayotolewa na Chama cha Wachezaji wa kulipwa nchini England (PFA).

Salah ameshinda tuzo hiyo kwa kuwabwaga wachezaji wengine akiwemo Harry Kane (Tottenham Hotspur), David De Gea (Manchester United), Kevin De Bruyne, David Silva na Leroy Sane (Manchester City).

Wakati huo huo Leroy Sane ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa soka nchini Uingereza. Sane amewashinda Sterling (Manchester City), Ryan Sessegnon (Fulham), Harry Kane (Tottenham Hotspur) na Marcus Rashford (Manchester United).

Kwa upande wa soka la wanawake, Fran Kirby (24) wa klabu ya Chelsea amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa wanawake ya PFA.

Naye Lauren Hemp wa Bristol City na timu ya wanawake chini ya umri wa miaka 19, amshinda tuzo ya mchezaji chipukizi kwa upande wa wanawake.

Saturday, April 21, 2018

11:14 AM

Hawa ndio wanaotajwa kuchukua nafasi ya WengerPamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Arsenal Ivan Gazidis, kusema timu hiyo bado haijaanza mchakato wa kumpata mrithi wa kocha Arsene Wenger lakini tayari majina kadhaa yameanza kutajwa kuziba nafasi hiyo.

Gazidis ameweka wazi kuwa mchakato huo utakapoanza utaongozwa na yeye mwenyewe, mkuu wa mahusiano ya soka Raul Sanllehi na Afisa mwajiri wa klabu Sven Mislintat.

Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel, anatajwa zaidi kuchukua nafasi ya mzee Wenger ambaye amekaa klabuni hapo kwa miaka 22. Kocha mwingine ni Carlo Ancelotti pamoja na Massimiliano Allegri ambaye ni kocha wa Juventus.

Mbali na hao imeelezwa kuwa Mkurugenzi  Gazidis ana uhusiano wa karibu na nahodha wa zamani wa timu hiyo Mikel Arteta ambaye kwasasa ni msaidizi wa Pep Guardiola kwenye kikosi cha Manchester City.

Orodha hiyo haijakamilika bila jina la nyota wa zamani wa timu hiyo Thierry Henry ambaye naye anatajwa miongoni mwa wanaoweza kuchukua nafasi ya Wenger. Makocha wengine ni kocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique na kocha wa Hoffenheim Julian Nagelsmann.

Friday, April 20, 2018

7:39 AM

Wachezaji hawa uwenda wakaondoka Man United mwisho wa msimu huuMtandao wa Squawka.com moja kati ya stori kubwa walioiripoti leo Alhamisi ya April 19 2018 ni pamoja na hii ya wachezaji wa Man United ambao wanatazamiwa kuwa wataondoka mwisho wa msimu kwa sababu mbalimbali ikiwemo kukosa nafasi ya kucheza.

1- Anthony Martial ametajwa kuwa ataondoka Man United baada ya kugoma kusaini mkataba mpya wa miaka mitano kutokana na kocha Jose Mourinho kutomchezesha mara kwa mara, hivyo vilabu vya Juventus na Inter Milan vimekuwa vikihusishwa nae kwa karibu, Martial ameanza katika game 16 tu za Man United msimu huu na nafasi yake amekuwa akipewa Rashford.

2- Paul Pogba pamoja na kuwa amenunuliwa kwa pesa nyingi kutoka Juventus na kujiunga na Man United na amefanikiwa kutoa assist nyingi zaidi ya mchezaji yoyote wa Man United katika EPL lakini amekuwa anafanya vizuri kiasi chini ya Jose Mourinho na kuna wakati watu walihoji namna ya Mourinho anavyomtumia kiungo huyo.

3- Marouane Fellaini huyu alikuwa moja kati ya wachezaji wanaopendwa sana na Jose Mourinho msimu uliyoisha lakini maisha yake Man United yanadaiwa kama kukaribia mwisho baada ya kufanikiwa kucheza katika game 19 pekee za mashindano yote msimu huu huku akianza katika game tano pekee na amecheza kwa jumla ya dakika 694.

4- Ander Herrera baada ya ujio wa Nemanja Matic ndani ya Man United Herrera ameonekana kuanza kukosa nafasi ya kucheza na amepata kuanza katika game 10 za Man United, hivyo uwepo wa wachezaji wanatajwa kumzidi uwezo kunaweza kumfanya akakimbia Man United na kwenda timu ambayo atapata nafasi ya kucheza.

5- Luke Shaw anatajwa kuwa yeye mwenyewe ameanza kuhisi kuwa hana nafasi tena ndani ya kikosi cha Man United kutokana na nafasi  yake kuwa kuna kiungo kama Ashley Young wameanza kucheza hiyo inatokana na jeraha lake la muda mrefu alilolipata msimu uliyopita hivyo anakosa nafasi pia kutokana na kukosa fitness.

Wednesday, April 18, 2018

4:05 PM

PFA yataja kikosi bora cha EPL 2017/18, Man City yaongoza kutoa wachezaji wengi

Chama cha Wachezaji wa kulipwa nchini Uingereza (PFA), kimetaja orodha ya kikosi bora cha wachezaji wa ligi hiyo kwa msimu wa 2017/2018.


Katika kikosi hicho klabu ya soka ya Manchester United imefanikiwa kutoa wachezaji watano. Wakati huo huo Tottenham Hotspur imetoa wachezaji watatu kwenye kikosi hicho.

Kikosi cha wachezaji waliochaguliwa na PFA kwa msimu wa 2017/2018
Wachezaji waliotajwa kwenye kikosi hicho ni David De Gea, Kyle Walker, Jan Vertonghen, Nicolás Otamendi, Marcos Alonso, David Silva, Kevin De Bruyne na Christian Eriksen.
Wengine waliotajwa kwenye orodha hiyo ni Harry Kane, Mohamed Salah na Sergio Agüero.

2:01 PM

Barcelona yaipa rekodi hii Celta VigoLicha ya kwenda sare ya mabao 2-2 ikiwa ugenini katika Ligi Kuu Spain, FC. Barcelona imeendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kuwa na alama zake 83 kati ya michezo 33 iliyocheza.

Barcelona ililazimisha sare hiyo huku mabao yake yakifungwa na wacheze, Dembele dakika ya 36 na la pili likitiwa kimiani na Alcacer mnamo dakika ya 64.

Kikosi hicho kilicheza kikiwa pungufu kuanzia dakika ya 71 baada ya Sergi Roberto kulimwa kadi nyekundu.

Celta Vigo imekuwa timu pekee ambayo imeshindwa kupoteza mbele ya Barcelona msimu huu baada ya kuilazimisha Barcelona kupata matokeo ya sare katika michezo yote miwili ya ligi.

Hiyo imekuwa ni rekodi kwa Celta ukiangalia baadhi ya vigogo wengine kama Atletico na Real Madrid tayari wameshapokea vichapo kutoka kwa vinara hao wa ligi msimu huu.

Monday, April 16, 2018

8:06 PM

Majeruhi Neymar atuma pongezi kwa wenzake


Nyota wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Brazil Neymar Jr, ameipongeza klabu yake hiyo kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Ufaransa (Ligue 1) huku akiweka wazi kuwa alitamani sana kuwepo wakati wanatwaa ubingwa.

Neymar hayupo na timu yake tangu mwezi Februari kufuatia kuumia mguu na kulazimika kusafirishwa kwenda nchini kwao Brazil kwaajili ya matibabu ambayo yalitazamiwa kutumia miezi mitatu hadi minne.

Baada ya jana PSG kutwaa ubingwa huo Neymar aliwapongeza wachezaji wenzake kupitia mitandao yake ya kijamii ambapo aliandika ''Nilitamani sana kuwa pamoja na nyie, hongereni kwa ubingwa''.

PSG usiku wa jana waliibuka na ushindi mnono wa mabao 7-1 dhidi ya Mabingwa watetezi Monaco. Baada ya ushindi huo PSG wamefikisha alama 87 ambazo haziwezi kufikiwa na Monaco yenye alama 70 huku zikiwa zimebaki mechi 5 pekee.

Ubingwa huu ni wa 7 kwa PSG ikiwa imetwaa katika misimu ya 1985–86, 1993–94, 2012–13, 2013–14, 2014–15, 2015–16 na 2017–18.

Friday, April 13, 2018

8:39 AM

Kenya yashinda medali ya dhahabu ya kwanzaWycliffe Kinyamal ameishindia Kenya medali ya dhahabu ya kwanza katika mbio za fainali za wanaume za mita 800, katika mashindano ya Jumuiya ya madola.

Aliyekuwa bingwa Nijel Amos wa Botswana, aliyemshinda David Rudisha miaka minne iliyopita, aliishia kuwa wa mwisho katika mchuano huo.

Mwenzake Kinyamal, kutoka Kenya, Jonathan Kitilit alishika nafasi ya sita, wakati Joseph Deng, wa Australia, aliyezaliwa kwenye kambi ya wakimbizi baada ya mama yake kukimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe Sudan, alishika nafasi ya saba.

Mwanariadha kutoka Afrika Kusini, Caster Semenya, anatarajiwa kupata medali ya pili ya dhahabu, baada ya kumaliza wa kwanza katika raundi ya kuingia katika fainali za mita 800.

Bara la Afrika linatarajia kupata medali zaidi baada ya wanamichezo watano:


  • Eglay Nalyanya - Kenya
  • Margaret Wambui - Kenya
  • Emily Tuei - Kenya
  • Docus Ajok - Uganda
  • Winnie Nanyondo- Uganda

Thursday, April 12, 2018

8:05 AM

Pep Guardiola na Liverpool kukutana na rungu la UEFA

Shirikisho la soka Barani Ulaya, UEFA limetoa adhabu kwa meneja wa Manchester City, Pep Guardiola kufuatia kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu wakati wa mchezo wao dhidi ya Liverpool uliyomalizika kwa kufungwa jumla ya mabao 2 – 1 hapo jana usiku.

 Wakati huo huo UEFA imeipatia adhabu Liverpool kwa kitendo cha mashabiki wake kufanya vurugu kwa kuwasha moto na kulishambulia basi la wachezaji wa Man City wakati wa mchezo wao wa kwanza wa klabu bingwa uliyopigwa Anfield.Guardiola ataadhibiwa kwa makosa mawili lakwanza ikiwa ni kupingana na maamuzi ya waamuzi baada ya kukataliwa bao lao la kuotea  ‘Offiside’ kitendo kilichopelekea akijikuta anavuka mstari na kuingia uwanjani na hivyo kutolewa kwenye benchi.


Kosa lapili likiwa ni kufanya mawasiliano na benchi la ufundi wakati yeye ametolewa eneo hilo hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 69 cha sheria ya UEFA.
Guardiola aliingia ndani ya uwanja wakati wa mapumziko akienda kumlalamikia mwaamuzi kwa kitendo cha kukataa bao lao ambalo lingeifanya City kuongoza kwa jumla mabao 2 – 0 kipindi cha kwanza.
Kesi hiyo itashughulikiwa na bodi inayosimamia maswala ya maadili na nidhamu ya UEFA Mei 31 mwaka 2018.

Tuesday, April 10, 2018

2:52 PM

RANALDO: ANATAJWA BORA ZAIDI UEFA KIHISTORIA


MADRID, Hispania: MIEZI kadhaa iliyopita, kuna wengi waliombe­za Cristiano Ronaldo wakati akipitia kipindi kigumu cha ukame. Ni Ronaldo huyo­huyo ambaye aliibuka ghafla na kwenda kuipa Real Madrid ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na La Liga.
Msimu huu pia, Ronaldo, 33, aliuanza kwa tabu, wengi wakaanza kuibua mas­wali tena juu ya kiwango chake, la­kini baada ya muda hakuna anaye­hoji tena.

Lakini ukweli ni kwamba huenda kizazi hiki tunamshuhudia mcheza­ji bora zaidi wa wakati wote katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mashabiki Jumanne iliyopita kwenye Uwanja wa Juventus, wal­ishuhudia kila kitu kwa uwazi zaidi. Baada ya Ronaldo kupiga bao la pili kali (Real ilishinda 0-3 ugenini), i l i b i d i mashabiki wa upinzani wasimame tu kumpa heshima kutoka­na na jinsi bao hilo lilivy­okuwa.

“Sikuamini. Nalazimi­ka kusema asante kwa mashabiki wote wa Ju­ventus. Walichokifanya kwangu kinashangaza. Hii haijawahi kutokea katika maisha yangu,” alisema Ro­naldo, baada ya mashabiki wa Juventus kusimama na kumpongeza kufuatia bao kali aliloifunga timu yao.
Suala la mchezaji bora za­idi litaendelea kuwa mjadala milele kwa kuwa ni mtazamo wa mtu. Kila mtu huwa na chaguo lake; mweupe au mweusi? Chapati au mandazi? Vitumbua au sambusa? Kunyoa au kufuga rasta?
Lakini kwa kile ambacho alikifan­ya Ronaldo Jumanne, inawezeka­na wengi wakaanza kukubali kuwa huyu ni mchezaji mkali zaidi kihistoria katika michuano hii.
Takwimu zinambeba: Yeye bin­afsi tangu aondoke kwenye Premier, amefunga mabao mengi kwenye michuano hiyo kuliko jumla ya ma­bao yaliyofungwa na timu mbili za Manchester United na Manches­ter City.

Kumbuka huyu ndiye mfungaji bora wa wakati wote wa michua­no hii, akiwa na mabao 120.
Bao lake la ‘tiki taka’ Ju­manne, linasadikika kuwa ni bao bora zaidi lililowahi kufungwa katika historia ya mtoano wa Ligi ya Mab­ingwa. Lilifungwa dhidi ya mmoja wa makipa bora zaidi wa wakati wote duniani, na lilifungwa li­cha ya jitihada za uhakika kutoka kwa safu ya ulinzi inayosadikika kuwa moja ya safu bora zaidi duniani, lakini jamaa akatupia tu.

Mtu aliyeshuhudia kwa uka­ribu zaidi bao hilo ambaye alikuwa golini aliishia kumsifia tu. “Akiwa ka­tika ubora wake? Nadhani hakuna aliyewahi kuwa kama Ronaldo. Mes­si na yeye (Ronaldo) wanaweza kul­inganishwa na Maradona na Pele,” anasema Gianluigi Buffon, kipa wa Juve.
Hakika Ronaldo inaoneka­na alizaliwa kwa ajili ya kuja kufanya maa­jabu kwenye Ligi ya Mab­ingwa Ulaya. Hata wakati akiwa na ukame kwenye La Liga, a l i e n ­delea kuwa hatari Ulaya msimu huu wa 2017-18.

Kwa mwendo wake huu wa kutu­pia mabao bila kuhurumia wapinza­ni wake, Ronaldo anaelekea kuvunja rekodi yake mwenyewe ya kufunga mabao 17 katika msimu mmoja, na kuna kila dalili kwamba atatwaa tuzo yake ya sita ya Ballon d’Or (Mchezaji Bora wa Dunia) kama Real Madrid itatwaa taji la Ligi ya Mabingwa kwa mwaka wa tatu mfululizo.

Pia msimu huu ameweka rekodi mbili mpya: Jumanne alifanikiwa kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao kwenye mechi 10 mfululizo za Ligi ya Mabingwa Ulaya, na alifunga katika kila mechi kwenye hatua ya makundi, suala ambalo halikuwahi kufanyika kabla.

Ronaldo inawezekana akapata tena Tuzo ya Puskas, ambayo ni ya bao bora zaidi duniani, aliwahi kui­pata mwaka 2009 baada ya kufunga bonge la bao katika Ligi ya Mab­ingwa dhidi ya Porto.
Ronaldo anaelekea kubeba taji lake la nne la Ligi ya Mabingwa aki­wa na Real Madrid, na la tano kwake kiujumla.

“Unyenyekevu ukizidi siyo vizuri,” alisema Ronaldo kabla ya fainali ya msimu uliopita. “Tunatakiwa kuthibi­tisha sifa yetu na tuwaonyeshe nani ni bora zaidi. Tunaweza kupata mataji mawili, kutetea ubingwa (wa La Liga) na kuingia katika historia ya Ligi ya Mabingwa. Kuna kichocheo kikubwa na tumebakiza hatua moja.”
Kuna hatua mbili na nusu zime­baki kwa ajili ya Madrid kugeuza mataji mawili mfululizo ya Uefa kuwa matatu mfululizo, lakini ugwiji wa Ronaldo katika mi­chuano hii, umeshathibitishwa hata kama hawatatwaa taji hili.

2:34 PM

Bodigadi wa Mayweather Anusurika Kifo Baada ya Kupigwa RisasiVyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kuwa mtu mmoja anaedaiwa kuwa mmoja wa walinzi wa karibu wa bondia wa Marekani, Floyd Mayweather amepigwa risasi nje ya Hoteli ya Atlanta hapo jana asubuhi siku ya Jumatatu.Mtandao wa habari za michezo wa TMZ Sports umeripoti kuwa kwamujibu wa taarifa za Polisi, risasi imetoka kwa mtu ambaye alikuwa kati ya moja ya magari matatu yaliyokuwa yamewasili nyuma ya hoteli ya InterContinental Buckhead majira ya saa 3 a.m. asubuhi siku ya Jumatatu.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha CNN kimeripoti kuwa mlinzi huyo ambaye jina lake halija fahamika amefikishwa kwenye Hospitali ya Grady Memorial kwaajili ya kupatiwa matibabu kufuatia risasi hiyo kumjeruhi mguuni na hali yake inaendelea vizuri.

Taarifa kutoka Polisi zinaeleza kuwa wanaamini bondia, Mayweather alikuwa sehemu ya msafara huo uliyoshambuliwa licha ya kutokuwa na uhakika kama yeye ndiye alikuwa mlengwa wa tukio hilo. 

Monday, April 9, 2018

10:00 PM

Lionel Messi apata dili nonoMshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi amesaini dili nono na shirika la ‘World Tourism Organisation’ (UNWTO) linalojishughulisha na masuala  ya utalii ambalo linafanya kazi chini ya Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo {www.fcbarcelona.com} Messi amesaini dili hilo Jumamosi iliyopita baada ya mchezo wa La Liga kati ya FC Barcelona na Leganes kwenye mchezo ambao Messi alitupia magoli matatu.

Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab Pololokashvili wakati akimtambulisha Messi leo Aprili 09, 2018 amesema kuwa ni heshima kubwa kwa shirika hilo kufanya kazi na Messi.

“Messi ni moja ya wachezaji wakubwa duniani ni heshima kwa shirika letu kufanya naye tunajua ni mtu mwenye mitazamo chanya na anajituma sana uwanjani, bila shaka hii heshima kwetu,“amesema Zurab Pololokashvili.

Kwa upande wake Messi yeye amesema ni mafanikio makubwa kufanya kazi na shirika hilo na anaamini kuwa atafanya nao kazi vizuri kutangaza utalii.

Messi ameungana na mastaa wengine kama Fernando Hierro na kocha wa zamani wa Real Madrid na timu ya Hispania, Vicente del Bosque.

Sunday, April 8, 2018

2:32 PM

Kocha wa Juventus: Unajua Ronaldo yaani ni sawa na mvinyoCristiano Ronaldo

KOCHA wa Juventus, Massimiliano Allegri amemfananisha Cristiano Ronaldo na kinywaji cha mvinyo akisema kuwa kadiri umri unavyokwenda ndio anazidi kuwa mkali zaidi. Allegri alimkubali Ronaldo baada ya kuiongoza Real Madrid kuirarua Juventus 3-0 mbele ya mashabiki wao kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wiki iliyopita.

“ Unajua Ronaldo yaani ni sawa na mvinyo kadiri muda unavyokwenda ndio anazidi kuwabora,” alisema Allegri baada ya mchezo huo, ambao Ronaldo aliacha mashabiki wa soka mdomo wazi baada ya kufunga bao maridadi la ‘tik tak’. Allegri alisema kuwa Ronaldo amekuwa straika bora wa dunia kwa miaka miwili sasa.

Alisema kuwa pamoja na fowadi huyo kuwa na umri wa miaka 33 lakini bado ana kiwango cha kutisha. Nyota ya Ronaldo bado ipo juu Real Madrid wakati wenzake waliounda kombinesheni ya BBC yaani Gareth Bale na Karim Benzema wakiwa wamechuja siku za karibuni.

Katika miaka ya nyuma, Ronaldo alikuwa anasifika kwa mbio na chenga lakini kutokana na umri kumtupa mkono siku hizi anahakikisha anakuwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga kila mara.
2:31 PM

Pogba: Kuitazama Man City ilikuwa kama kifoKiungo wa Manchester United Paul Pogba amesema kitendo cha kuwatazama wapinzani wao Manchester City wakibeba ubingwa mbele yao ilikuwa ni sawa na kufa ndio maana walijitahidi kuhakikisha hilo halitokei.

"Sikutaka kupoteza dhidi ya Man City kwasababu walipotufunga msimu uliopita maumivu yake bado nayakumbuka hivyo sikutaka kuona tunapoteza tena, pia wao kuchukua taji mbele yetu ingekuwa ni kama adhabu ya kifo kwa mashabiki wetu," amesema.

Pogba pia ameweka wazi siri iliyowafanya wakarejea mchezoni kipindi cha pili kuwa wakati wa mapumziko katika vyumba vya kubadilishia nguo waliambiana hawana cha kupoteza hivyo ni lazima watoke wakatafute ushindi na wakafanikiwa.

Pogba alifunga mabao mawili ya haraka haraka katika dakika za 53 na 55 na kusawazisha mabao mawili ya Man City yaliyofungwa kipindi cha kwanza na nahodha Vicent Kompany dakika ya 25 na Ilkay Gundogan dakika ya 30.

Kama Man City wangeshinda jana wangeshangilia ubingwa mbele ya mashabiki na wachezaji wa Man United lakini mlinzi Chris Smalling alizima ndoto hiyo dakika ya 69 baada ya kufunga bao la tatu ambalo lilifanya mchezo huo kumalizika kwa 2-3.
2:17 PM

Mourinho atoa tamko hili kuhusu Man UBaada ya kuitwanga Manchester City kwa jumla ya mabao 3-2 katika mchezo wa Ligi Kuu England jana Jumamosi, Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, amesema timu yake inastahili kupewa heshima.

United ilikuwa nyuma kwa mabao 2-0 kabla ya kusawazisha na kuongeza jingine ambalo lilidumu mpaka dakika ya mwisho ya mchezo.

Kutokana na matokeo hayo ya ugenini, Mourinho amesema kuwa hakika wachezaji wake walipambana wakiwa ugenini kwa kupindua matokeo baada ya kuwa nyuma kwa bao hizo mbili.

"Nadhani tunastahili kupewa heshima, wachezaji wako vizuri nami niko vizuri kuliko watu wanavyofikiria" alisema Mourinho.

Katika mchezo huo, Manchester City ilijipatia mabao yake kupitia Vincent Kompany na Gundogan huku United wakifunga kupitia Pogba aliyetia kambani mabao mawili na jingine likifungwa na Smalling.

Saturday, April 7, 2018

10:00 PM

Bayern Munich yaichapa Augsburg, yabeba taji la BundesligaKlabu ya soka ya Bayern Munich imetwaa taji la Bundesliga msimu wa 2018/19 baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Augsburg kwenye mchezo uliomalizika jioni hii.

 Bayern sasa imeweka rekodi ya kutwaa taji hilo mara 6 mfululizo huku msimu huu wakiwa wamechukua zikiwa zimebaki mechi 5 kabla ya ligi hiyo kumalizika. Baada ya ushindi wa leo wamefikisha alama 72 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine.

Bayern ambayo i[po chini ya kocha wa muda na aliyewahi kuipa mataji matatu (Trebble)  Jupp Heynckes, ilianza vibaya msimu chini ya kocha Carlo Ancelotti ambaye baadae alitimuliwa na kurejeshwa kwa Jupp na kila kitu kilibadilika kuanzia hapo.


Mabingwa hao wapya wa Bundesliga leo waliwapumzisha nyota wao Robert Lewandowski, Thomas Muller, Thiago Alcantala, Franck Ribery, Mats Hummels na Javi Martinez ambao wote walianzia kwenye benchi ikiwa ni sehemu ya mipango ya mechi ya UEFA jumanne ijayo dhidi ya Sevilla.

Tangu msimu wa 2012/13 Bayern haijapoteza taji hilo na imekuwa ikichukua bila ushindani mkubwa haswa baada ya mpinzani wake Borussia Dortmund kutokuwa kwenye kiwango kizuri misimu ya hivi karibuni.
12:37 PM

Raiola Asema Guardiola ni Muongo

Raiola asema Guardiola ni muongo

Wakala wa kiungo wa Manchester United Paul Pogba Mino Raiola amesema alichosema kocha wa Manchester City Pep Guardiola kuwa Pogba alitaka kuuzwa kwenye usajili wa Januari si kweli.


''Sijawahi kuzungumza na Guardiola kuhusu mchezaji yeyote aliyechini yangu, si Pogba wala Mkhitaryan, hata Man City kama klabu sijawahi kuongea nayo lakini naiheshimu ni timu bora na ina kocha bora'', amesema.

Jana kwenye mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wa 'Derby' ya jiji la Manchester, Guardiola alisema kuwa Pogba alitaka kuuzwa Manchester City kwenye dirisha dogo la janauri kitu ambacho kimepingwa vikali na nyota huyo wa Ufaransa.Kwa upande wake Pogba kupitia ukurasa wake wa mtandao wa 'Twitter' ameeleza kushangazwa na alichosema Guardiola kwani hajawahi kuongelea suala hilo hata siku moja.

Mchezo wa leo ambao utapigwa kwenye uwanja wa Etihad nyumbani kwa Man City, unaweza kuamua bingwa endapo wenyeji watashinda basi wataibuka mabingwa wapya wa EPL msimu wa 2018/1 

Saturday, March 31, 2018

2:11 PM

Anthony Joshua na Joseph Parker nani mbabeLeo Wales na dunia nzima itasimama kwa muda kuangalia pambano la wanamasumbwi wawili mahiri wa uzito wa juu duniani (heavyweight), Anthony Joshua wa Uingereza na Joseph Parker wa New Zealand.

Pambano hilo la kuwania ubingwa wa Dunia wa uzito wa juu katika mikanda minne ya WBA ,IBF, IBO na WBO , litapigwa uwanja wa Principality Cardiff nchini Wales, uwanja mbao Joshua mwaka jana alitetea mikanda yake dhidi ya Carlos Takam,

Wakali hao wa ndonga wameunganisha mikanda yao Joshua akiweka mezani mikanda yake ya ubingwa wa dunia wa WBA,IBF na IBO huku Parker akiweka mezani mkanda wake wa dunia wa WBO.

Mabondia hao wote ni mabingwa wa dunia na wote  hawajapigwa hata pambano moja, Joshua akiwa na rekodi ya 20-0 akishinda yote kwa KO huku Parker akiwa na rekodi ya 24-0 akishinda 18 kwa KO na 6 kwa pointi.

Pambano litaanza majira saa 4:30 usiku kwa saa za Wales (Saa 6 usiku kwa saa za Afrika mashariki) na bingwa ataondoka na mikanda yote minne.

Friday, March 30, 2018

8:54 PM

Kenya kuweka rekodi kombe la DuniaAden Marwa ni miongoni mwa waamuzi wasaidizi 10 kutoka Afrika watakaosimamia mechi za kombe la dunia.

Mwamuzi huyo mwenye uzoefu wa miaka 7 akifanya kazi na shirika la FIFA,alifanikiwa kuorodheshwa kwenye orodha ya mwisho kwa ajili ya kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil. Hata hivyo hakufanikiwa kusimamia mechi yeyote.

FIFA imechagua maafisa 6 kutoka barani Afrika kusimamia mechi za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Urusi.

Pamoja na hao waamuzi wasaidizi 10 wametoka barani Afrika, kwa ujumla maafisa 99 wamechaguliawa kusimamia michuano hiyo.

Aden Marwa ana uzoefu wa kuwa mwamuzi msaidizi katika michuano ya kombe la dunia la vilabu 2016 nchini Japan.

Alitajwa kuwa mwamuzi msaidizi wa CAF katika shirikisho la kombe la FIFA 2017 na alishiriki pia mwaka 2012,2013, na 2015 kwenye kombe la mataifa ya Afrika pamoja , kombe la dunia la walio chini ya miaka 17 , michuano ya CAF ya chini ya miaka 23 na kombe la dunia la vilabu la FIFA


Image may contain: 4 people, including Mollel Hillary Mollel, people smiling, text