Breaking

Showing posts with label News. Show all posts
Showing posts with label News. Show all posts

Tuesday, March 27, 2018

1:31 PM

Huu ndio undani wa aliyemuua Mkewe na kumficha MbuyuniUNDANI wa mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina Bernard Shumba mkazi wa Singida kugundulika na jeshi la polisi mkoani humo kuwa amemuua mke wake miaka minane iliyopita kisha kuufi cha mwili wa marehemu kwenye mbuyu, umeanikwa.

Habari kutoka chanzo cha kuaminika zinasema Shumba alikuwa mara kwa mara akiwa kwenye vilabu alikuwa akigombana na mtu anasema kwamba anaweza kumfanyizia kama alivyomfanya mkewe.

Kutokana na tambo zake hizo raia wema waliamua kuliarifu jeshi la polisi ambalo kwa weledi mkubwa walithibitisha kile alichokuwa akisema Shumba kwani alikwenda kuwaonesha polisi alikomfi cha  mkewe miaka minane iliyopita baada ya kumuua.

“Tuwapongeze polisi kwa kazi nzuri kwa sababu tambo za huyu bwana zimezaa matunda na kuonesha yalipo mabaki ya mkewe,” alisema mtoa taarifa wetu ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.“Nitoe wito kwa wananchi kwamba, watu wabaya wasifi chiwe siri kama bwana,” alisema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Deborah Magiligimba, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa baada ya kukamatwa alikiri kutenda kosa hilo na kwenda kuonyesha mwili wa marehemu aliokuwa ameuhifadhi ndani ya mbuyu ambapo jeshi hilo kwa kushirikiana na wananchi limefanikiwa kupata mabaki yake.

“Inadaiwa kuwa mnamo Julai 10, 2010 katika Kijiji “Baada ya 17, 2018 ambapo taarifa zilipopatikana zikidai kuwa alimuua.“Baada ya mtuhumiwa kukamatwa na kuhojiwa alikiri kufanya kitendo hicho na kuonyesha sehemu alipoufi cha mwili huo Machi 18, mwaka huu majira ya saa 10:00 jioni, “ alisema kamanda huyo wa polisi.

Mkuu wa polisi kituo cha Mkalama na timu yake ya makachero walifi ka eneo la tukio na kufanikiwa kupata mabaki ya mifupa yakiwa ndani ya mti huo. Baadhi ya mifupa imechukuliwa kwa ajili ya kupelekwa kwa mkemia wa serikali na iliyobakia ndugu wamekabidhiwa kwa ajili ya mazishi.


Image may contain: 4 people, including Mollel Hillary Mollel, people smiling, text

Monday, March 26, 2018

11:57 AM

Abdul Nondo aachiwa kwa dhamanaleo March 26, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa imemuachia kwa dhamana Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania Abdul Nondo ambaye alikuwa anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Iringa.

Nondo amepewa masharti ya dhamana  ni wadhamini wawili mmoja mtumishi wa Serikali wote wakazi wa Iringa na bondi ya kauli Tshs Milioni 5, atarudi Mahakamani April 10, 2018.

Image may contain: 4 people, including Mollel Hillary Mollel, people smiling, text
10:52 AM

Stormy Daniels: Mwigizaji video za utupu adai alitishiwa kuacha kutoa kashfa ngono za Rais TRUMPMwigizaji wa video za utupu Stormy Daniels, ambaye jina lake halisi ni Stephanie Clifford, amesema alitishiwa na kutakiwa kukaa kimywa kuhusu kufanya tendo la ndoa na Donald Trump mwaka 2006.

Ameambia kituo cha runinga cha CBS News kwamba mwanamume mmoja alifika kwake alipokuwa kwenye maegesho ya magari mjini Las Vegas mwaka 2011.

Mtu huyo ambaye hakumfahamu anadaiwa kumwambia "mwache Trump", kisha akamtazama binti mdogo wa mwigizaji huyo na kuongeza: "Itakuwa aibu sana iwapo jambo litamtendekea mamake."

Bw Trump amekanusha vikali kwamba aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji huyo.

Mawakili wa Bw Trump wanataka kulipwa fidia ya $20m (£14m) na mwanamke huyo, wakisema alikiuka makubaliano ya kuweka siri ambayo aliyatia saini katika ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.

Mwanamke huyo anasema madai hayo hayana msingi.

Bi Clifford anasema alifanya tendo la ngono na Bw Trump mara moja pekee, katika chumba cha hoteli wakati wa mashindano ya gofu ya watu mashuhuri Lake Tahoe, California, Julai 2006.

Stormy amesema nini hasa?
Ameambia kipindi hicho cha Dakika 60, ambacho kilipeperushwa hewani Jumapili jioni, kwamba mwanamume huyo alimjia baada yake kukubali kusimulia kisa chake kwa jarida moja.

"Nilikuwa kwenye maegesho ya magari, nilikuwa naelekea kwenye kikao cha mazoezi niliwa nimembeba binti wangu mchanga," alisema.

"Mwanamume alinijia na kuniambia, 'Mwache Trump. Sahau taarifa hiyo'. Kisha, aliinama na kumtazama binti wangu na kusema, 'Ni msichana mdogo mrembo sana. Itakuwa ni aibu sana iwapo jambo litamtendekea mamake'. Na hivyo tu, akaondoka."

Rais huyo alikuwa kituo chake cha gofu na hoteli cha Mar-a-Lago jimbo la Florida wikendi lakini alirejea White House kabla ya kipindi hicho kurushwa hewani.

Bi Trump hata hivyo alisalia Florida, msemaji mmoja wa White House alisema.

Nini kinadaiwa kutokea 2006?
Bi Clifford aliambia CBS kwamba mara pekee ambapo alifanya ngono na Bw Trump ni wakati alipomwalika kwa chakula cha jioni kwenye chumba chake cha hoteli.

Anasema Bw Trump alimuonesha jarida lililokuwa na picha yake kwenye jalada.

Anasema alilichukua jarida hilo na kumgonga Trump nalo makalioni kama utani.

"Aligeuka na kuteremsha suruali yake chini kidogo, unajua, alikuwa na suruali ya ndani na vitu vingine, na nilimgonga kidogo kidogo kwa utani," anasema.

Bw Clifford anasema ingawa hakuvutiwa kwa vyovyote vile na Bw Trump, alifanya mapenzi naye wakati huo, akisema: "Sikukataa. Mimi si mwathiriwa."

Bw Trump, anaongeza, alikuwa amedokeza kwamba kulikuwa na uwezekano angeshirikishwa kwenye kipindi chake cha runinga cha The Apprentice.

Anasema alichukulia mkutano wao kuwa sawa na "mkutano wa makubaliano ya kibiashara".

Na pesa je?
Bi Clifford ameambia CBS alipokeza "fedha za kukaa kimya" kutoka kwa wakili wa kibinafsi wa Trump kwa sababu alikuwa na wasiwasi kuhusu usalama wa familia yake.

Amewahi kusema awali kwamba alilipwa $130,000 na wakili huyo Michael Cohen kusalia kimya kuhusu uhusiano wao huo kabla ya uchaguzi mkuu wa 2016.

Bw Cohen alithibitisha Februari kwamba alimlipa mwanamke huyo lakini hakusema alimlipa kwa niaba ya nani.

Wakosoaji wa Bw Trump wamedokeza kwamba kuna uwezekano pesa hizo zilikuwa sehemu ya mchango wa pesa haramu za kampeni.

Bw Cohen alisema mwezi jana kwamba Bw Trump na kampuni yake ya Trump Organization hawakuhusika katika kulipwa kwa pesa hizo.

Aidha, amekanusha kumtishia Bi Clifford, CBS News wameripoti.

Madai ya Stormy ni tofauti?
Bi Clifford ni mmoja kati ya wanawake watatu ambao wameanza kesi dhidi ya Rais Trump kuhusu madai ya uhusiano wa kimapenzi au udhalilishaji.

Wakili wake Michael Avenatti ameambia BBC kwamba kesi ya mteja wake ni tofauti na wengine kwa sababu inahusu "visa vya kutolewa vitisho na mbinu ambazo zilitumiwa kumnyamazisha mteja wangu."

"Nafikiri ni kisa cha kustaajabisha na kinafaa kuwashangaza sio tu Wamarekani bali pia watu katika mataifa yaliyostaarabika ya magharibi," amesema.

Ameongeza: "Hivi sivyo watu walio madarakani wanavyofaa kuendesha shughuli zao."

Image may contain: 4 people, including Mollel Hillary Mollel, people smiling, text

Tuesday, March 1, 2016

10:54 PM

Watafutaji kazi walazimishwa kuvua nguo India

Mamia ya vijana katika jimbo la Bihar nchini India wamelazimishwa kuvua nguo ili kusalia na suruali zao za ndani wakati wa mtihani wa kuajiriwa kwa wanajeshi ili kuzuia kufanyika kwa udanganyifu.
Picha zimeonyesha vijana wanaowania kuwa wanajeshi wakiwa wamekaa na kukunja miguu katika uwanja mmoja ulopo mji wa Muzaffar huku wakiwa wamevalia suruali zao za ndani pekee.
Jeshi limesema kuwa lilifanya hivyo ili kuhifadhi mda wa kuwachunguza makurutu wengi.
Kurutu mmoja aliliambia gazeti la India Express alihisi kwamba hawakupewa heshima.
Maafisa wanasema kuwa makurutu wapatao 1,159 walishiriki katika mtihani huo wa saa moja wa kujiunga na jeshi la India.
''Wakati tulipoingia katika eneo la Chakkar Maidan,tuliagizwa kuvua nguo zote isipokuwa suruali ya ndani.Hatukuweza kukataa bali kutimiza yaliohitajika licha ya kwamba halikuwa jambo la kawaida''.
Makurutu hao walitawanywa kwa urefu wa futi nane kila upande,Gazeti la India Express lilimnukuu kurutu mmoja akisema.
Gazeti hilo lilimnukuu afisa mmoja wa ngazi za juu katika jeshi akisema kuwa ni makosa kwa utawala kuwafanyia hivyo makurutu hao.
Bihar na maeneo mengine ya India Kaskazini ni maarufu kwa udanganyifu katika mitihani ,mwaka uliopita serikali ya jimbo hilo iliaibishwa baada ya wazazi na marafiki kupigwa picha wakipanda kuta za shule ili kuwapatia majibu ya mitihani wanafunzi.
10:14 PM

Polisi Walivalia Njuga Suala la Freemaso Dar es Salaam..Matapeli Wajipatia Mamilioni Kuuza Form Feki za Kujiunga Kwenye Mtandao huo

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro (pichani) amesema kuwa jeshi lake linafuatilia kwa karibu madai mawili, kwamba kuna watu wanajipati mamilioni ya shilingi kwa kuuza fomu wanazodai ni za kujiunga na taasisi maarufu duniani ya Freemaso

Pili kuwepo kwa madai kwamba eti watu wanaojiunga na taasisi hiyo wamekuwa wakitoa makafara watu wao wa karibu kama moja ya masharti ya kujiunga, Uwazi lina habari yote.

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jijini Dar hivi karibuni, Kamanda Sirro alisema kufuatia malalamiko hayo, amemwagiza Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ZCO Masawe kupeleka makachero kwenye jengo hilo ili kufanya uchunguzi wa kina wa kuwabaini wahusika na kuwanasa mpaka kwenye vyombo vya sheria.

Alama za Freemason.
“Nimewasikia kuhusu hao watu wanaowatapeli wananchi wakijifanya wanauza fomu ya kujiunga na Freemason, pia kama kweli kuna wanaojiunga wakiwatoa kafara watu, nimeshamwagiza ZCO Masawe apange timu aende kwenye eneo hilo ili kuwanasa watu wao.

“Watanzania wenyewe pia wanatakiwa kuwa makini sana na watu wa aina hiyo kwani kama mtu anataka kukutapeli anajulikana tu,” alisema Kamanda Sirro.

POLISI WAMEANZA
Taarifa zaidi kutoka ndani ya jeshi hilo zinadai kuwa, tayari polisi wameshafika eneo husika na kufanya uchunguzi wao na wanaendelea nao.

“Agizo la afande Sirro tayari polisi wanalifanyia kazi, wakati wowote ule utasikia watu wamekamatwa maana tumepewa ushirikiano mkubwa na walinzi wa eneo lile,” alisema mtoa taarifa mmoja ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe kwa sababu yeye si msemaji wa jeshi hilo.

WALINZI FREEMASON WAZUNGUMZA
 walinzi walikiri kuwepo kwa watu wanaosimama jirani kabisa na geti la kuingia ndani ya jengo hilo wakisema wanauza fomu za kujiunga na taasisi hiyo.

Lakini wakakanusha habari kwamba kuna wanaojiunga kwa kutoa kafara ndugu zao wakisema ni maneno ya mitaani ambayo yameenea duniani kote.

John Ngonyani ni mlinzi wa eneo hilo ambaye alisema Ofisi za Freemason zilifungwa tangu Novemba 15, mwaka jana na viongozi wote wapo likizo hadi Machi 15, mwaka huu.

“Siyo hapa tu kumefungwa bali hata ofisi zilizopo mikoani yaani Arusha, Mbeya, Mwanza na Kilimanjaro nazo zimefungwa hadi Machi 15,” alisema mlinzi huyo.

Alisema: “Kwamba sasa shughuli zote za kiofisi hapa zimesitishwa hadi hapo viongozi watakaporudi, Machi 15. Hamna mambo ya kafara, hayo ni maneno ya watu mitaani tu. Hii ni taasisi ya kusaidia jamii, ipo duniani kote.”

Mlinzi huyo alisema, Jumatatu hadi Ijumaa ndiyo watu wengi wanaotaka kujiunga hufika hapo lakini Jumamosi na Jumapili ni wachache huku akisisitiza kuwa, hakuna mambo ya kafara zaidi ya watu kusaidiana.

ILIWAHI KUANDIKWA
Hivi karibuni kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers kilipokea malalamiko kutoka kwa watu ‘waliopigwa’ kutokana na tamaa ya utajiri kwa kuuziwa fomu feki za kujiunga na Freemason.

Baada ya malalamiko kutoka, OFM waliingia mzigoni kuchunguza ili kubaini ukweli wa malalamiko hayo na kuandikwa na gazeti ndugu na hili, Amani linalotoka kila Alhamisi.

Makamanda wa OFM walifunga safari hadi kwenye jengo hilo na kumfuatilia kila mmoja aliyekuwa akipita ambapo waliweza kugundua kuwepo kwa jambo hilo lakini kwa siri.

Kamanda mmoja wa OFM alishika bahasha yenye fomu ndani na kuweka maelezo kuwa ni za Freemason ambapo katika watu watano waliopita eneo hilo, wanne walitaka kununua kwa kuulizia bei. Wengine walifika na kuuliza jinsi ya kuingia kwenye ofisi hizo ili wakapewe maelekezo ya  kujiunga.

Mlinzi mmoja wa jengo hilo alishangaa Watanzania wanaokubali kuuziwa fomu nje ya jengo hilo.
 “Mimi nawashangaa sana Watanzania. Kama kweli kuna  fomu kwa nini mtu akuuzie nje. Viongozi wenyewe wakishaingia ndani hatujui wanachofanya. Kama ni fomu si tungekuwa tunaona watu wakiingia na kutoka nazo,” alisema mlinzi mmoja.

Sunday, February 28, 2016

1:49 PM

NENO LA LEO: KUNA WALIOAMUA KUTETEA UVIVU WAO KWA KUSINGIZIA FREEMASONS!

Ndugu zangu.,
Ndio, kuna walioamua kutetea uvivu wao kwa kusingizia Freemasons.
Nimekisoma kitabu cha Sir Andy Chande kiitwacho ' A Knight In Africa'. Huko nyuma nilimsikia tu mtu anayeitwa Andy Chande, lakini, kupitia kitabu chake nimemfahamu zaidi alikotokea.
Kupitia simulizi ya maisha yake unaona jinsi Sir Andy alivyo mchapakazi. Anatoa mifano mingi ya kazi alizofanya; kwenye biashara na hata utumishi wa taifa hili. Ajabu ya Sir Andy, ameitumikia Serikali bila hata kuwa Mbunge au Waziri.
Na jioni moja nilipomwona pale kwenye ghafla fupi nyumbani kwa Balozi wa Sweden nikashawishika kuongea naye. Ucheshi niliouona kwenye maandiko yake upo pia kwa Andy unapozungumza naye. Kitabu chake kinasimulia pia historia ya nchi yetu. Kinatusaidia kuelewa tulikotoka, tulipo sasa na kuweza kufikiri juu ya wapi tuendako. Unaposikia leo sakata la sukari, au shirika la ndege ATC au la reli na mengineyo kuhusu mashirika ya umma na viwanda vyetu, basi, kitabu cha Sir Andy Chande ni kama ' kamusi' ya kukusaidia kupata tafsiri.
Andy alikuwa pia rafiki wa Julius Nyerere tangu enzi za kudai uhuru wa nchi hii. Andy na Julius walikuwa ni marafiki wa karibu, waligombana wakapatana, maana, kila mmoja alimuheshimu mwenzake. Nitasimulia mahala pengine juu ya urafiki wa wawili hawa. Julkius alimpenda na kumheshimu Andy kwa kuwa alikuwa ni rafiki aliyekuwa akimwambia ukweli, hata kama Julius atachukia kwa kuambiwa ukweli huo.
Mfano, Andy aliwahi kumkatalia Julius alipoombwa akagombee Ubunge Tabora kwenye uchaguzi wa kura tatu. Andy akatamka; " I would save better as a business man rather than a politician".
Famlia yake, kuanzia babu yake ni ya wafanyabiashara. Pale Bukene, Shinyanga, walianza na biashara ya kuuza magunia. Wakafanya pia biashara ya vinu vya kusaga na kukoboa. Baadae Andy na familia yake wakahamia Dar. Mbele ya Stesheni Kuu ya Tazara iliko sasa kampuni ya Azam ndipo kilipokuwa kiunga cha akina Chande. Walianza kwa kufyeka mapori. Hapo wakaweka vinu vya kukoboa na kusaga.
Asubuhi moja enzi za Azimio la Arusha, mwaka 1967, Andy anasimulia kwenye kitabu chake, kuwa aliamka asubuhi moja kwenda kiwandani kwao. Yeye alikuwa meneja wa kiwanda hicho. Getini akawakuta askari wa FFU. Akaambiwa kuwa kuanzia siku hiyo kiwanda kimetaifishwa. Kikaitwa National Milling Cooperation. Akaingizwa ofisini kwake akabidhi ofisi kwa Meneja mpya ambaye hakuwahi hata kukutana naye mitaani. Kukabidhi mali ya familia kwa mtu usiyemjua!
Alipomaliza kufanya shughuli ya kukabidhi, Andy akumuuliza Meneja Mpya kama angependa aongozane naye akamtambulishe kwa wafanyakazi wengine. Andy akaambiwa imetosha, aende zake tu.
Siku hiyo hiyo Andy akaitwa na rafiki yake Julius aende Ikulu. Hata alipoingia Ikulu, Andy alimwona Julius mwingine. Hakuwa mcheshi kama ilivyokuwa kawaida yake. Julius akamwambia Andy akae kitako na hapo hapo akamfahamisha maamuzi ya kutaifisha kiwanda chao na kuwa Shirika la Umma.
Na cha ajabu, Julius akamwomba rafiki yake Andy awe Mwenyekiti wa Kwanza wa Bodi ya National Milling Cooperation!
Andy akakubali! Na akaifanya kazi ile kwa nguvu zake zote.
Inasikitisha kuona leo Andy anaanikwa kwenye magazeti ya udaku na kutolewa taswira hasi. Tena ni Andy huyu huyu ambaye aliwahi kuwa mmoja wa wajumbe wa Tume iliyokuwa ikipitia filamu zote zinazoingizwa Tanzania kuziangalia kabla umma haujaonyeshwa. Lengo lilikuwa kuhakikisha kuwa filamu hizo za kigeni haziathiri maadili, mila na utamaduni wetu.
Leo Andy amekuwa mhanga wa baadhi ya vyombo vya habari vinavyokiuka maadili, mila na utamaduni wetu, kwa kumuanika hadharani, tena kwa kuweka picha zake, bila ridhaa yake, kuwa ni mwanachama wa jumuiya ya Freemasons, jumuiya ambayo, kwa kupotosha umma, media inadai wanachama wake wanaamudu mashetani!
Naam, kuna waliamua kutetea uvivu wao kwa kusingizia Freemasons!
Na hilo ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
Dar es Salaam(P.T)
Bw   Chande  akiwa  na rais  mstaafu  Mwinyi
Bw  Chande  akiwa  na rais  mstaafu Kikwete
12:51 PM

Siri ya Shule 10 Bora Tanzania Matokeo ya Kidato Cha Nne Hadharani


Usione vyaelea vimeundwa”, huo ni msemo wa wahenga ukimaanisha kila mafanikio yana maandalizi.

Msemo huo unaendana na kilichotokea katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne yaliyotangazwa wiki iliyopita, ambapo katika shule 10 zilizofanya vizuri hakuna hata moja yenye maandalizi hafifu. Shule nyingi kati ya hizo ada zake ni kuanzia Sh8 milioni hadi tisa kwa mwaka.

Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa shule hizo zote ni zenye majengo mazuri, walimu wazuri na wenye motisha, maabara zilizokamilika sehemu nzuri za kulala na zinazotoza ada zaidi ya Sh2.5 milioni, mbali ya gharama nyingine za chakula, malazi na vitabu.

Shule 10 zenye watahiniwa zaidi ya 40 zilizoshika nafasi za kwanza ni Kaizirege ya mkoani Kagera, Alliance Girls ya Mwanza, St. Francis Girls (Mbeya), Alliance Boys ya Mwanza, Canossa (Dar es Salaam), Marian Boys (Pwani), Alliance Rock Army (Mwanza), Feza Girls na Feza Boys (Dar es Salaam) pamoja na Uru Seminary (Kilimanjaro) ambayo ada yake imetajwa kati Sh1.5 milioni au Sh1.6 milioni kwa mwaka .

Uchunguzi huo umebaini shule tano kati ya 10, zilizoongoza ada zake ni kuanzia Sh8 milioni hadi tisa kwa mwaka.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kaizirege iliyoshika nafasi ya kwanza, kila mmoja analipa Sh2.5 milioni za ada. Malipo yote hayo kwa shule zote 10 ni tofauti na gharama za malazi, chakula na vitabu ambavyo malipo yake yanajitegemea.

Kwa makadirio ya ada pekee, mwanafunzi atakayesoma shule hii kwa miaka minne endapo ada hiyo haitaongezeka, atapata elimu hiyo bora katika mazingira mazuri ya kufundishia, lakini lazima awe na Sh10 milioni.

Meneja wa shule hiyo, Eulogius Katiti alisema wanafunzi wanasoma katika mazingira bora, sehemu nzuri ya kulala, chakula bora, vifaa vyote vya kufundishia na hakuna somo linalosomwa kwa nadharia, yote husomwa kwa vitendo kama inahitajika kufanya hivyo.

“Angalia kwenye mtandao, utaona ubora wa mazingira ya shule, mabweni, jumlisha na matokeo ya mwisho ndiyo utaona ni kwa jinsi gani fedha yao inafanya kazi na kuwapa kilicho bora,” alisema Katiti.

Shule ya wasichana ya St. Francis iliyopo mkoani Mbeya, iliyoshika namba tatu, ili mwanafunzi ajiunge na shule hiyo, anatakiwa alipe ada ya Sh2.2 milioni kwa mwaka, huku akitakiwa kulipa katika mikupuo minne.

Mwanafunzi anayesoma katika shule hiyo, anatakiwa kulipa kiasi cha Sh8.8 milioni kwa miaka minne (endapo ada itabaki palepale) mbali ya kulipia bweni, vitabu, chakula na malazi.

Katika Shule ya Sekondari ya wasichana Canossa ya Dar es Salaam, mzazi anahitaji kuwa na Sh3 milioni, ili mwanaye asome mwaka mmoja shuleni hapo, zikiwamo gharama za malazi, chakula, vifaa vya kusomea na ada.

Kwa maana hiyo kwa miaka minne anatakiwa kuwa na kiasi cha Sh12 milioni ili aweze kusoma shule ya Canossa.

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Feza Boys ada ni Sh2.9 milioni, lakini ikijumlishwa na gharama za chakula, malazi na vifaa vya masomo, jumla inafika Sh8 milioni na ushehe, ikiwa ni chini kidogo ya Sekondari ya Feza Girls ambazo gharama yake inafikia Sh9 milioni kwa mwaka.

Mkuu wa taaluma wa shule hiyo, Zakia Irembe alitetea gharama hizo, akisema zinaendana na kiwango cha elimu anachopata mwanafunzi na utulivu anaokuwa nao awapo shuleni hapo.

Alisema hakuna kitu kigumu katika masomo kama kusoma huku mwanafunzi anawaza atakula nini, hana uhakika wa kulala, lakini kwao chakula bora, malazi ya kuvutia, uhakika wa kufanya vizuri kutokana na weledi wa walimu katika kufundisha ndiyo siri pekee ya mafanikio yao.

Irembe alisema katika mlo wa wanafunzi kila wakati lazima kuwe na matunda, huku wanafunzi hao wakiwa hawali ugali na kufua nguo ni uamuzi wa mwanafunzi ama atumie mikono au mashine, uhakika wa umeme, kamera za CCTV kwa ajili ya usalama na kila bweni lina eneo la kupumzikia kutizama taarifa ya habari.

“Mzazi analipa fedha anabaki anatudai elimu, jukumu la kusimamia chakula, malazi ni letu, ndiyo maana vitu vyote kwetu ni bora ili kupata elimu bora pia. Elimu inahitaji uwekezaji mkubwa, kusoma siyo kila mtu anaweza, kunahitajika vitu vya ziada kuhakikisha akili ya msomaji inawaza masomo pekee,” alisema Irembe.

Mwanafunzi aliyeshika namba moja katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu, Butogwa Shija aliyekuwa akisoma katika Shule ya Wasichana Canossa, alisema kuwa licha ya kupenda kusoma, mazingira mazuri ya kusomea, uhakika wa kupata kila anachotaka katika kujifunza ndiyo chachu ya mafanikio yake.

Mzazi wa mwanafunzi Innocent Lawrence aliyeshika nafasi ya tatu katika mtihani huo kutoka Feza Boys, Lawrence Nyakabunda alisema kuwa ada anayolipa katika shule hiyo inalingana na elimu anayopata mwanaye.

Alisema anakubaliana na ada kuwa kubwa, lakini anaridhishwa na kiwango cha elimu kijana wake anachopata.

Wakati wenye shule na wazazi wakisema hayo, Msomi wa masuala ya elimu, Profesa Kitila Mkumbo alisema sababu kubwa ya shule hizo kufanya vizuri ni aina ya wanafunzi wanaochukua, wanakuwa wamechujwa hadi wanapofika katika mtihani wa mwisho wote wanakuwa bora.

Alisema shule hizo pia zina walimu wa kutosha, wenye weledi wa ufundishaji, huku wakipewa motisha ya kufanya kazi hiyo.
12:47 PM

Soma Ripoti nzima Kuhusu Tukio la Ujambazi Mbagala: Waliofariki Dunia ni Watu 7........Kati Yao Majambazi ni 3, Askari 2 na Raia 2


Ujambazi wa kutumia vifaa vya kivita umeibuka jijini Dar es Salaam, ukiwemo uliofanyika katika uporaji wa Benki ya Access juzi, ambako majambazi walitumia bunduki za kivita aina ya SMG na mabomu ya kurusha kwa mkono.

Akizungumza jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, alisema mbali na uvamizi huo, pia Polisi imebaini na kukamata askari bandia, waliokuwa na sare rasmi za Jeshi la Polisi zenye vyeo na redio call, zenye uwezo wa kuingilia mawasiliano ya askari Polisi.

Akizungumzia matukio hayo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga alisema atakutana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi, ili Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Polisi, waanzishe msako wa pamoja dhidi ya wahalifu hao.

Uvamizi, mauaji Mbagala
Akisimulia ujambazi uliofanyika katika Benki ya Access Tawi la Mbagala, Kamanda Sirro alisema majambazi hao walikuwa 12, wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki sita na walifika kwenye benki hiyo saa 8:30 mchana.

Baada ya kufika, moja kwa moja waliingia kwenye chumba cha askari wanaolinda benki na kumpiga risasi kichwani askari mwenye namba H7739 Konstebo Harid na kufa papo hapo.

Mbali na mauaji hayo, Kamanda Sirro alisema walimshambulia askari mwingine, Konstebo Shaban miguuni na kupora silaha zao na kuingia nazo ndani ya benki, ambako walimshambulia mlinzi wa kampuni binafsi ya ulinzi na raia wengine wawili na kufa papo hapo, huku wengine watano wakijeruhiwa.

Baada ya hapo kwa mujibu wa Kamanda Sirro, majambazi hao walikimbilia chumba kinachohifadhi fedha nyingi (strong room) na kukipiga risasi katika jitihada ya kutaka kuingia ndani, lakini hawakuweza kuvunja.

Kutokana na ugumu wa kuvunja chumba hicho, Kamanda Sirro alisema haraka haraka wakahamia katika kaunta za watoa fedha na kupora fedha zilizokuwepo kati ya Sh milioni 20 mpaka Sh milioni 30 na kuondoka na silaha za polisi aina ya SMG mbili na ile yao moja pamoja na pikipiki zao.

Polisi waua watatu
Kamanda Sirro alisema taarifa zilisambazwa katika vikosi vya ulinzi, ambavyo vilijiimarisha.

Alitaja Kikosi cha Mbwa na Farasi eneo la Mkuranga, ambao walijiandaa na majambazi hao walipofika kijiji cha Chui wilayani Mkuranga mkoani Pwani, walipambana na polisi na askari wakafanikiwa kuua majambazi watatu.

Mbali na kuua watatu, silaha tatu zilikamatwa ambazo ndio zile SMG mbili za Polisi, walizochukua pamoja na ile yao moja, lakini wakakutwa pia na mabomu matatu ya kutupa kwa mkono yaliyotengenezwa Urusi.

“Hawa majambazi walikuwa wamejiandaa, kwa maana walikuwa na mabomu ya kutupwa kwa mkono matatu aina ya RGD 01 ambayo ni mbinu ya kujilinda wanaposhambulia,” alisema Kamanda Sirro.

Tisa watoroka
Pamoja na kujiimarisha kwa polisi, majambazi tisa walikimbia wakaacha pikipiki zote sita za aina tofauti, ambazo ni Haojue mbili zenye namba MC 560 AED na MC 207 BAN, San LG yenye namba MC 784 BDJ, Boxer yenye namba MC 248 AXE na King Lion mbili zenye namba MC 653 BDQ na MC 853 BDR.

Kamanda Siro alisema baada ya hapo, waliendelea kuwakimbiza majambazi hao hadi wakatokomea katika Msitu wa Kongowe, ambako juhudi za kuwatafuta zilianza mara moja.

“Nawahakikishia wananchi mtandao wote wa ujambazi kwenye mabenki na maeneo mengine, tutausafisha wote kwa maana hawa wanafanya uhalifu maeneo ya Dar es Salaam na Pwani na wana ndugu zao, tutawakamata wote,” alisisitiza Kamanda Sirro.

Alisema hawawezi kuona Watanzania wakiumia na kufa kwa tamaa za wachache, wenye kupenda utajiri wa haraka.

JWTZ kazini
Akizungumza kuhusu ujambazi huo, Waziri Kitwanga alisema Polisi inajipanga upya na atazungumza na Waziri mwenzake, Dk Mwinyi kuangalia jinsi ya majeshi hayo mawili, Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), watakavyofanya kazi pamoja ya msako katika misitu yote inayozunguka mikoa ya Pwani, kuanzia Bagamoyo hadi Kisarawe.

Alionya kama kuna kambi za uhalifu ndani ya misitu hiyo, zitasambaratishwa na kuomba raia wema watoe taarifa za uhalifu.

“Tutafanya operesheni kubwa na tutaifanya haraka, tunaomba wananchi watoe ushirikiano hasa waendesha bodaboda kwa maana zinatumika sana kwenye matukio haya. Mtandao wa majambazi ufahamu kwamba vyombo vya usalama havijalala, tutawamaliza wote, tutatumia nguvu zetu zote kuwamaliza na tutafanikiwa,” alisisitiza Kitwanga.

Kuhusu waendesha bodaboda, Kitwanga alisema ukaguzi wa kina unafanywa na kuwataka waendesha bodaboda hao wanaposimamishwa, wakubali na kutoa ushirikiano na wasione kama wanabughudhiwa, bali ni kuwakagua kwa sababu wahalifu hutumia vyombo hivyo zaidi kufanya matukio mabaya.

Polisi feki
Katika tukio jingine, Kamanda Sirro alisema polisi feki wanne wamekamatwa na wanashikilia kwa mahojiano, ili kubaini mtandao huo ambao unatumia sare za Polisi, redio za upepo na pingu kufanya matukio ya uhalifu.

Alisema walipata taarifa kutoka kwa raia wema ya kuwepo kwa mtandao wa askari bandia, ambao hutumia sare za jeshi hilo kufanya matukio ya uhalifu, ndipo walipowakamata hao wanne.

Kwa mujibu wa Kamanda Sirro, polisi feki watatu walikamatwa Februari 24, asubuhi saa mbili eneo la Upanga karibu na Daraja la Selander.

Alisema watuhumiwa hao baada ya kuhojiwa, walikiri kufanya matukio ya ujambazi kwa kutumia silaha na kumtaja mtuhumiwa mwenzao mmoja anayeishi Kinyerezi.

Kamanda Siro alisema Polisi walimfuata mtuhumiwa huyo nyumbani kwake Kinyerezi na walipofanya upekuzi, walimkuta na sare halisi ya Polisi, redio ya upepo na pingu.

Kamanda Sirro alisema baada ya uchunguzi, imebainika kwamba watuhumiwa hao wamekuwa wakitumia sare na vifaa hivyo vya Polisi, kufanya matukio mbalimbali ya ujambazi kwa kujiaminisha kuwa wao ni askari Polisi.

Alisema watuhumiwa hao wamekiri kufanya matukio mbalimbali, ikiwemo kuweka vizuizi katika barabara za mikoani na kufanya uporaji.

“Watuhumiwa hao wote wanahojiwa ili waeleze jinsi walivyopata sare na vifaa hivyo ya Polisi, wamekiri kufanya uhalifu maeneo mbalimbali, lakini wakati mwingine tunashindwa kukamata wahalifu kwa sababu redio call wanayotumia zinaingiliana na zetu, hivyo wanakuwa wamepata taarifa,” alisema Kamanda Sirro.

Katika tukio lingine, Februari 18 mwaka huu, watuhumiwa watatu wa ujambazi, walikamatwa eneo la Kiwalani Kwa Mkude jijini Dar es Salaam wakiwa na bastola moja