Breaking

Showing posts with label MAKALA. Show all posts
Showing posts with label MAKALA. Show all posts

Monday, March 26, 2018

11:50 AM

MARAIS WALIOUAWA KWA KUPIGWA RISASI WAKIWA MADARAKANI


 Related image
Tunawaletea marais waliouawa kwa kupigwa risasi wakiwa madarakani. ABRAHAM Lincoln; alikuwa Rais wa 16 wa Marekani. Aliuawa mwaka 1865 jijini Washington kwa kupigwa risasi kichwani kwa nyuma na John Wilkes. Alikuwa amekaa na mkewe. Bastola iliyotumika inaitwa Deringer. 
Image result for INDIRA Priyadarshini Gandhi

INDIRA Priyadarshini Gandhi; Alikuwa Rais wa India. Aliuawa mwaka1984 kwa kupigwa risasi na walinzi wake, Satwant Singh na Beant Singh jijini New Delh, India. 
JOHN Francis Kennedy ‘JFK’; ni Rais wa 35 wa Marekani. Aliuawa mwaka 1963 mjini Dallas kwa kupigwa risasi na Lee Harvey akiwa kwenye gari la wazi barabarani.
Image result for LAURENT Desire Kabila
LAURENT Desire Kabila; alimng’oa madarakani Rais Mabotu Seseko wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, lakini mwaka 2001 akauawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa ni walinzi wake. 
Image result
THOMAS Isdor Noel Sankara; alikuwa Rais wa Burkina Faso Alitawala nchi kwa miaka 4 hadi 1984 alipouawa kwa kupigwa risasi inasemekana alihusika  kufanya mauaji  hayo ni  rafiki  yake  wa  kisiasa   Blaise Compaore ambaye  alikuja  kuwa  rais  wa nchi  hiyo  kwa  muda  mrefu  lakini  mwisho  wa siku  alikimbia nchi hiyo.
Image result
 WILLIAM Richard Tolbert Jr; Alipigwa risasi mwaka 1980 katika mapinduzi ya kijeshi akiwa Rais wa Liberia. Samuel Doe akiwa na cheo cha sajenti ndiye aliyetajwa kumuua.
Image result for Ghaddaf;

 MUHAMMAR Muhamad Abu Migar al Ghaddaf; Alikuwa Rais wa Libya kwa miaka 42. Aliuawa kwa kupigwa risasi ya kichwa kwenye vurugu za kisiasa mjini Sirte, Libya, Oktoba 20, 2011. 
Image result

ABEID Amani Karume; alikuwa Rais wa Zanzibar tangu mapinduzi ya mwaka 1964. Aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa anacheza bao mwaka 1972 na mtu ambaye hakuwahi kupatikana. Jean baptist ouedraogo; aliitawala Burkina Faso kwa mwaka mmoja tu, 1982-83. Aliuawa kwa kupigwa risasi na Thomas Sankara ambaye alichukua madaraka ya kuiongoza nchi hiyo kabla na yeye kupinduliwa.

11:06 AM

Historia ya Che Guevara, Je Wajua Aliwahi Kukimbilia Tanzania na Kujificha?


Kama kijana msomi wa shahada ya udaktari, che Guevara alisafiri nchi nyingi sana huko bara la Amerika ya kusini na rafiki yake, akawa ni mtu mwenye uchungu mkubwa kuona maisha ya dhiki,njaa, magonjwa nchi za America ya kusini, akawa na mwamko mkubwa kubadili hali ile kwa kuwa aliamini ya kuwa mfumo wa ubepari ndio chanzo kikubwa kilichokuwa kinaitafuna Latin America.

Miaka ya 50 akiwa anasoma udaktari huko Mexico Che Guevara alikutana na Fidel Castro na Raul Castro ambapo watatu hao walipanga mapinduzi ya kumg’oa raisi wa Cuba wakati huo Fulgencio batista ambaye alikuwa na huhusiano wa kimaslahi na America, Che akapata nguvu na uaminifu mkubwa kutoka kwa Fedel Castro na kupandishwa kuwa kiongozi wa wanamgambo (guerilla insurgents) Punde tu baada ya Fulgencio batista kukimbia CUBA,Che alihusika kama mtu muhimu katika serikali ya Cuba iliyoongozwa na Fidel Castro, akiwa kama Gavana wa benki kuu ya Cuba ambapo saini yake ilianza kutumika katika noti za CUBA , baadae kama waziri wa kilimo wa Cuba.

Mwaka 1964 akiwa kama mmoja ya msafara wa watu wa serikali ya Cuba umoja wa Mataifa New York MArekani, aliweza kupata “sifa” ya “mwanamapinduzi halisi wa kukumbukwa” pale alipotoa hotuba ndefu katika ukumbi wa UN akilaumu wazi ukimya wa Umoja huo juu ya kilichokuwa kinaendelea Afrika ya kusini (ubaguzi wa Rangi) alinukuliwa akisema

“wale wanaoua watoto wao na kuwabagua kila siku kwa sababu ya rangi ya ngozi zao, wazungu wanawaua watu weusi na hawakamatwi, serikali ya kikaburu inawalinda wauaji, na mbaya Zaidi inawaadhibu watu weusi kwa kuwa tu wanatataka haki zao na utu wao, vipi watu hawa (makaburu) wakaitwa watetezi na walinzi wa Amani?”

MGOGORO WA CONGO – DRC
miezi michache baada ya kutoa hotuba UN, Che alitoweka katika maisha ya kawaida “public life” na hakuna aliyejua alikwenda wapi mpaka baadae ilipokuja gundulika Che alikuwa akipigana sambamba na Laurent Kabila huko Congo dhidi ya wabeligiji na baadhi ya wapiganaji wa ki cuba waliokuwa Afrika, vita ambayo ilishindikana na akakimbilia Tanzania na kukaa maeneo ya karibu na ziwa Tanganyika na baadae Dar es salaam huku akiishi kwa kujificha


Image result for Che Guevara,
baadae mwaka 1966 alirejea Cuba kumuaga kwa Fudel castro na kusafiri kwenda Bolivia kuendeleza harakati zake za kuzikomboa nchi za America ya kusini kutoka kwenye makucha ya Ubepari…aliingia Bolivia akiwa kama mfanyabiashara hasiyejulikana baada ya kunyoa upara, kuweka mvi bandia na kuyoa ndevu zake zote, akaweka kambi na baadhi ya wapiganaji wenzake aliowakuta Bolivia maeneo ya milima ya montane dry fores

KUKAMTWA NA KUUWAWA
Mwaka 1967, makachero wa Bolivia wakisaidiwa na CIA amabye alikuwa akiwakilsha ndugu Felix Rodriguez waligundua maficho ya ache na kundi lake huko milimani Bolivia, asubuhi ya October 8 mwaka 1967 wanajeshi takribani 1,800 walizingira maeneo yoote ya milima walikokuwa wamejificha akina Che na ikapiganwa vita ya masaa kadhaa na Che akipigwa Risasi za miguu na kukamatwa na wenzake,

Yasemekana baada ya kuzidiwa katika mapigano yale alisema

“Usifyatue risasi, mi ni Che Guevara nina thamani kubwa kuwa hai kuliko kunikamata nimekufa”

Alifungwa kama na wenzake akakamatwa na kupelekwa kijiji cha La higuera ambapo baada ya raisi wa Bolivia ndugu René Barrientos kusikia amekamtwa alitoa amri auwawe haraka sana, wakati huo huo CIA walimtaka apelekwe Panama akahojiwe kwa kina na salama yake ili hasiuwawe alikuwa apelekwe America japo haikutokea.
Siku moja kabal ya kuuwawa alichukuliwa na baadhi ya wanajeshi na kupiga picha ya kumbukumbu na kesho yake akauliwa na askari mmoja aliyejitolea na kumpiga risasi sita za kifua na kufa palepale

Kabla hajapigwa risasi na muuaji wake haya ndio yalikuwa maneno yake ya mwisho
“Najua umekuja kuniua, shoot mtu mwoga wewe!!! na ufahamu utakua umeua mwanaume kamili”

Aliacha wake wawili na watoto watano

Image may contain: 4 people, including Mollel Hillary Mollel, people smiling, text

Saturday, May 27, 2017

7:18 PM

Ukweli Mchungu..Kwa Hili la Mchanga wa Madini..Rais Magufuli Umetuonyesha Sura Yako ya Pili Kuhusu Nafasi Yako ya Urais..!!!

Image result for magufuli
Rais John Magufuli angalau amefanya jambo la ujasiri,haya yalimshinda Rais wa awamu ya nne Mh Jakaya Kikwete ambaye pamoja na kuunda kamati mbili,ile ya Jaji Mark Bomani na ile ya Laurence Masha, baada ya kumaliza kazi ziliwekwa kabatini!.

Kuiweka wazi Ripoti ya Prof Mruma ili watanzania wajue angalau kinachoendelea kwenye mgodi wa Kahama,kumeibua angalau hasira kidogo kwa watanzania,moja ya madhaifu ya watanzania wengi huwa hawakasiriki hata pale wanaponyonywa,wanapoibiwa tena waziwazi!.

Madhaifu makubwa ya watanzania ni upole na unyonge hata pale wanapotendewa mambo ya hovyo,wanaoonyanyaswa,miaka yote wakazi wa Geita,Kahama,Nzega,Tarime,Biharamulo wameishia kitazama tu mali zao zikipanda ndege na kwenda Ulaya,Asia na Marekani!.

Angalau Mrehemu Chacha Wangwe aliyekuwa mbunge wa Tarime alivishinda kwa kiasi chake vita hivi,Wangwe alihakikisha wana wa Tarime wanapata angalau kiasi kidogo,alisimama kidete kuhakikisha kila mkazi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa North Mara wanapata karo ya shule/Chuo kama sehemu ya kufaidi utajiri wao!.

Angalau Tundu Lissu wakati hata akiwa hajawa mbunge alizunguka kuanzia Kahama mpaka Nyamongo akitoa msaada wa kisheria kwa walioitwa wavamizi wa mgodini,nakumbuka akiwa na shirika la wanasheria watetezi wa masuala ya mazingira walitoa masaada wa bure kwa waliokamatwa kwa kudaiwa kuvamia mgodi!.

Nakumbuka jinsi Lissu alivyokumbana na kesi ya uchochezi pale alipopaza sauti baada ya kuwepo kwa taarifa za watu kufukiwa huko kwenye mgozi wa dhahabu wa Bulyanhulu!.

Angalau wewe Lissu uliuweka uwoga pembeni ukaandika kitabu kwa kushirikiana na Mark Curtus mlichokipa jina la "The golden opportunity"kitabu mlichokiandika kwa lugha ya kiswahili na kingereza,kitabu hiki kimeleza kinagaubaga jinsi tunavyoibiwa!.Kama serikali ingeamua kukifanyia kazi kitabu hiki,tusingefika hapa leo!.

Angalau Comrade/wakunyumba Hamis Kigwangala wakati fulani alisimama kidete kupinga wana wa Nzega kuishi maisha ya ufukara wakati Mungu kawajalia dhahabu,ndugu yangu huyu nakumbuka alivyojikuta mikononi mwa polisi!.

Niliwahi msikia Augustino Mrema akizunguka nchi nzima akiwatuhumu Ashanti Gold mine kuwa walimhonga kiongozi wa juu wa serikali ya awamu ya tatu,angalau ulipaza sauti kulikemea hili!.

Angalau Zitto Kabwe ulisimama kidete kuusaka ukweli ndani ya bunge mwaka 2007,juu ya waziri wa kipindi hicho Nazir Karamagi kwenda Uingereza na kusaini mkataba kati ya Tanzania na Barrick ili wachimbe madini Buzwagi!

Angalau Marehemu Dr Sengondo Mvungi ulipinga bila woga kwenye maandiko na hata ulipoalikwa kwenye vyombo vya habari kiongozi mkuu wa nchi kujiuzia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwila tena kwa bei ya kaptula!

Angalau aliyepata kuwa mbunge Mh Kimaro yeye alipambana bungenu na Mzee Sitta kupaza sauti kupinga kiongozi wa juu kabisa kujiuzia mgodi,kelele hizi zilioazwa sana na Dr Wilbroad Slaa kila akisimama bungeni alikuwa mwiba kuhusu mgodi wa Kiwila,nakumbuka sauti zenu zilizaa matunda mpaka serikali ikatangaza kuurejesha mgodi ule serikalini!.

Angalau kamati ya viongozi wa dini ya haki na amani,mlitimiza wajibu wenu,amlizunguka nchi nzima mkiongozwa na akina Askofu Mkuu Paul Ruzoka,Shehe Fereji na maaskofu wengine na mashehe,nakumbuka jinsi mlivyozuiliwa kuingia kwenye mgodi wa Geita bila kujali nafasi zenu kwenye jamii,jinsi mlivyotafuta ukweli wa kilichoitwa sumu za mto Tigithe huko Mkoani Mara.

Ripoti yenu ambayo hata mimi mlinioatia imethibitisha kuwa majinya mto tigite yalikuwa na sumu kutoka mgodini,watu waliyatumia wakafa,wakababuka,lakini mgodi ukaishia kuwaita wavamizi,watumishi wa Mungu mmeacha alama kwenye utetezi wenu dhidi ya wizi huu!.

Mh Rais Magufuli akiongea kwa uchungu mara baada ya kukabidhiwa ripoti na Prof Mruma,na alichukua hatua pale pale!.

Mh Rais geukia sasa upande wa sheria zako,hawa wakezaji muda wote huo wamekuwa wanafanya biashara halali ya kinyonyaji,serikali ya awamu ya tatu iliasisi huu ukwapuaji wa madini yetu!.

Tarehe 26.3.1997,serikali ilipeleka mapendekezo ya miswada miwili ya sheria,ile ya kodi na ile ya uwekezaji,ikiwa ni kipindi kifupi toka sera ya madini itungwe mwaka 1997.

Serikali ya Mkapa ilikuja na sera za kuwakaribisha wawekezaji na kuvutia mitaji kutoka nje(FDI),ikatunga sheria laini kwa wawekezaji,ikiwapa kipindi kirefu cha kuchota bila kulipa kodi,na hata walipoanza kulipa kodi walilipa kiduchu!.

Haya unayoyalilia Mhe Rais Magufuli ni matokeo ya watanzania kuwa na tabia za kutokasirika hata wanaponyonywa,haya ni matokeo ya wataalamu wa serikali ya awamu ya tatu ya mzee mkala,wabunge wa bunge ya Mzee Msekwa,baraza ka mawaziri la Mzee Mkapa kutuletea na kupitisha kwa hati ya dharua sheria mbili za kodi na ile ya uwekezaji!.

Mh Rais sasa badili sheria,waandae wataalamu wako wa sheria,zungumza nao ujue katika hili taifa litanasuka vipi na unyonyaji huu uliotengenezwa na sheria zetu wenyewe!.

Mh Rais bunge ambalo na wewe ulikuwa sehemu yake,miaka kumi iliyopita liliitaka serikali iipeleke bungeni ripoti ya ukaguzi kwenye sekta ya madini kutoka kutoka kampuni kutoka Marekani ya Alex Stewart Assayers(ASA report).

Nakumbuka ASA baada ya kukamilisha ukaguzi wao,walizungukza na waandishi wa habari,mbaya zaidi hawakusema jambo,walipoambiwa waseme wamebaini nini?jibu likawa,"Kazi tukiyotumwa na serikali imekamilika,hatuwezi sema chochote kwa sababu tunafungwa na sheria za ukaguzi za kimataifa",alisema Alex mbele ya waandishi wa habari jijiji Dsm!

Mh Rais mwaka 2007,Kuliibuka sakata la mkataba wa serikali na kampuni ya madini ya Barrick kutoka Canada juu ya uchimbaji wa madini huko Buzwagi,nakumbuka wewe ulikuwa naibu waziri,waziri wa nishati na madini Ndugu Nazir Karamagi alituhumiwa kusaini mkataba mbovu tena hotelini,bunge lilipoudai mkataba huo,liliambiwa mkataba ni siri,si media wala wabunge wamewahi uona mkataba huo,ni mkataba wa Buzwagi pekee ndiyo baadhi nasikia waliwahi uona baada ya kuvuja!.

Mh Rais badili sheria,ondoa kipengere cha usiri kwenye mikataba hii ya madini na maeneo mengine,ruhusi wananchi kupitia bunge wajadili mikataba hii inayowahusu!.

Na ndiyo maana ya utawala bora wenye dhana kama,uwajibikaji,utawala wa sheria,uwazi,haki za binadamu,n.k.

Ripoti ya Prof Mruma imetupa picha kiduchu cha tatizo kwenye sekta ya madini,hatujajua tunachopoteza Geita,kwenye mgodi mkubwa barabj Afrika,ripoti ya Prof Mruma haijagusa Geita,ripoti hii imepapasa tu kuhusu uhalisia kwenye sekta ya madini!.

Rais badili sheria ili unasuke katika mapambano haya,tunapambana na wizi ,kilio cha muda mrefu,ni sisi hawa hawa tuliojigunga kupitia sheria ya kodi na na ile ya uwekezaji zilizopitishwa kwa mbwembwe kwa hati ya dharura na kutusababishia umasikini,badili sheria Mh Rais tuwabane wawekezaji,ruhusu uwazi,hii ni biashara halali ya kinyama,iliyoruhusiwa na serikali na bunge letu huko nyuma!.

Katika vita hii dhidi ya mali zetu wenyewe,tujilaumu wenyewe,tulitunga sheria mbovu wenyewe,tukazipigia debe wenyewe,zimetifanya masikini,ni wakati wa wanasheria wetu kutuonesha tunapita wapi ili tutoke salama!.

Kumbuka hii ni vita na mabeberu,ukitaka kujua nguvu ya hawa mabwana,fanya utafiti juunya akina nani wanaunda Geopolitics department ya kampuni la GGM!.

Tuwaruhusu wanasheria waoneshe njia,wataalam wa miamba wameshaonesha udhaifu,wasikilizeni sasa magwiji wa sheria,tupo katika kipindi kigumu!.

Wasalaaam!.

Monday, May 22, 2017

5:36 PM

Kama wewe ni mpenda demokrasia alafu unasifia utawala wa rais Vladimir Putin,Tambua unafanya makosa#Imeandikwa na Respicius Francis ambaye ni mmiliki wa mtandao wa www.tanzaniaclassic.com.
Image result for putin photo
#Utamkuta mtu kutoka chama cha upinzani ambaye anajiita mpiganaji wa demokrasia,Mpenda haki ,Mpenda huru hapo hapo anatamani uongozi wa Rais Putin...
#Unamkuta mtu kama huyu ambaye hapa Tanzania anajiita mpiganaji wa Demokrasia anatamani kuwa na Rais kama Putin ,,,
#Ndio yale yale ya enzi za Kikwete baadhi ya wapinzani walikuwa wanatumia muda wao kumsifia Kagame sana wakisema ni kiongozi mzuri,wakisema ni kiongozi shupavu lakini wanashindwa kutumia ata dakika 10 kuchunguza siasa ya Rwandaa...
#Sasa wapo watu humu wanajiita wapiganaji wa Demokrasia,wapiganaji wa haki,wapiganaji wa mawazo huru uwa wanamuona Rais Putin kama malaika wao huku wakishindwa kutumia muda kidogo kuchunguza 
uongozi wa rais Putin,
#Kule Urusi kiongozi wa upinzani kumkosoa rais Putini kosa kubwa tena ni haramu kabisa... adhabu yake ni kifo tu hakuna cha kufungwaaa....
#Wale ambao wanajiita wanademokrasia hasa kupitia upinzani ambao mmekuwa mnatamani kumpata kiongozi kama Putin naomba mtazame Orodha hii ya mauaji ya wapinzani wa rais Putin 
1-Boris Nemtsov huyu alikuwa ni mwanaisa wa upinzani nchini Urusi aliuawa kwa kupigwa risasi mwaka 2015...
2-Boris Berezovsky Huyu alikuwa bilionea mkubwa nchini Urusi na alikuwa mkosoaji wa Serikali ya Putin mpaka kufikia hatua ya kukimbilia uhamishoni nchini Uingereza lakini mwaka 2013 alikutwa ameuwa nyumbni kwake akiwa amefungiwa chooni ,Taarifa zinasema waliohusika na mauaji hayo ni majasusi wa Putin
3-Stanislav Markelov na Anastasia Baburova hawa waliuawa kwa siku moja mwaka 2009, Mwandishi wa habari 
4 -Anastasia Baburova alikuwa ameendika makala ya kumkosoa Rais Putin kupitia gazeti lakini siku chache akiwa anatembea na mwenzake Stanislav Markelov ambaye alikuwa ni mwanasheria wa shirika la kutetea haki za binadamu alipigwa risasi, Alipondoka chini ngudu 
Stanislav Markelov alijaribu kumsaidia lakini kwa bahati mbaya na yeye alitwangwa risasi wote wakapoteza maisha
5- Natalia Estemirova mwandishii wa habari ambaye alikuwa anafanya kazi na mwandishi wa habari Anna Politkovskaya aliyeuawa kwa kupigwa risasi , 
Natalia Estemirova kabla alikuwa ni mwanaharakati ambaye alitumia taaluma yake ya habari kuelezea udikteta wa rais Putin lakini hakuchukua muda alipigwa risasi ya kichwa akiwa nje ya nyumba yake ...
6-Anna Politkovskaya Huyu alikuwa mwandishi wa habari ambaye alitumia taaluma yake kukosoa serkali ya Rais Putin lakini adhabu yake ilikuwa ni kupigwa risasi mwaka 2006 na kupoteza maisha ,
7- Alexander Litvinenko Huyu alikuwa ni jasusi nchini Urusi alifariki dunia baada kunywa chai yenye sumu nchinii Uingereza mwaka 2006 ,Mr Litvinenko ndiye aliyetoa siri kuwa Putin ndiye aliyehusika kutoa amri ya kuawa mwandishi wa habari Anna Politkovskaya ambaye alikuwa anakasoa serikali yaken
8.Paul Klebnikov Huyu alikuwa ni mwandishi wa habari za uchunguzi nchini Urusi ,Pia alikuwa ni mhariri wa jarida la Forbes,Kabla ya kifo chake aliandika makala juu ya rushwa katika serikali ya Rais Putin ndio maana huyo rais ni bilionea wa kutisha sana hapa dunia,kilichotekea ni kupigwa risasi akiwa nje ya ofisini kwake mwaka 2004
9.Sergei Yushenkov Huyu alikuwa ni mwanasiasa wa upinzani ambaye alikuwa anakosoa utawala wa Rais Putin kilchotokea ni kupigwa risasii mwaka 2003
#SWALI KWA WAPIGANAJI WA DEMOKRASA bado mnaendelea kutamani rais Putin awe rais wenu???? Hivi bado mnaendelea kusiifia uongozi wa Putin>>?
Image may contain: 1 person, sitting
Kwenye pcha ni baadhi ya marehemu ambao wameuawa  


Image may contain: 1 person, standing
Mwandishi  wa ujumbe huu   Respicius Francis ambaye ni mmiliki wa mtandao wawww.tanzaniaclassic.com

Saturday, May 20, 2017

10:02 PM

Mrisho Gambo aandikiwa ujumbe mzito, Usome hapa

Image result for mrisho gambo

#Imeandikwa na Respicius Francis ambaye ni mmiliki wa mtandao wa www.tanzaniaclassic.com.
Mrisho Gambo Naomba niulize hiyo sheria ya MTU kutoa rambirambi mpaka kupitia kwako imeanza lini? Nachukua nafasi kukwambia kama kijana ni muhimu sana utambue nafasi za viongozi wenzako katika jamiii, kitengo cha kuwakamata Meya na viongozi wa Dini na kuwaweka ndani kisa wameenda kutoa rambirambi hakikubaliki ata kidogo, 
Gambo nilikuwa nakuunga mkono tokea ukiwa Korogwe mkoani Tanga lakini hili la kuwakamata Meya na viongozi wa dini siwezi kukuunga mkono kwasababu nitakuwa nafanya dhambi kubwa mbele ya mwenyezi Mungu,
Gambo naomba ufanye maamuzi yako ya uongozi kwa Kumfurahisha Mungu lakini siyo kufanya maamuzi kwa kumfurahisha mtu binafsi maana hivi vyeo vinapita na hapa duniani kunapita sasa kuna sababu gani ya kunyanyasana?? Gambo kwenye uongozi hekima na busara ni kitu muhimu sana maana sikuona sababu ya msingi Mtu kama Meya na viongozi wa Dini kukamatwa na kulala mahabusu eti kisa ameenda kutoa rambirambi?? Hivi tunatengeneza taifa la aina gani? Tunafundisha nini kizazi hiki kinachokuja??
Hivi ndugu Gambo mbona mikoa mingine  yenye wapinzani imetulia na wakuu mikoa wanashirikina na wapinzan kuleta maendeleo ila kwako ndio kuna kuna tatizo?? Mfano mzuri kijana mwenzako Anthony Mtaka alikuwa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro alishirikiana vizur sana Mbowe na kuna kupindi kulitokea mafuriko hapo Kilimanjaro tuliona Mtaka alivyoshirikiana Mbowe kuhakikisha   wananchi wanapata msaada? Ila ndugu Gambo kila siku ni mapambano na wapinzani ,
Gambo naamini wewe una una mamlaka ya kumweka mtu ndani lakni lazima uwe makini kutumia mamlaka yako kwa kuzingatia haki na utu wa binadamu,Na hakikisha unatumia mamlaka yako kwa hofu Mungu .
Gambo lazima utambue hawa viongozi kama Meya,Mbunge ,Diwani ni viongozi ambao wametokana na wananchi na nyuma yao wapo maelfu ya wananchi kwahiyo pale wanapoona viongoz wao wananyanyaswa wana jenga chuki ambayo ni hatari ndani ya jamiii ,,

Gambo  

Image may contain: 1 person, standing
Mwandishi  wa ujumbe huu   Respicius Francis ambaye ni mmiliki wa mtandao wawww.tanzaniaclassic.com.

Unaweza  kumfollow kupitia  Respicius Francis  katika  mtandao wa  facebook  

Tuesday, May 9, 2017

8:50 PM

HUU NI UJUMBE MZITO KWENDA WA WAPINZANI NCHINI TANZANIA WANAO TAMANI RAILA ODINGA ASHINDWE URAIS

imeandikwa  na Respicius Francis  Kupitia  ukurasa  wake wa facebook

Image result for raila odinga
Kwenye uchaguzi wa wakenya wapinzani nchini Tanzania wamegawanyika makundi 3
1.wapo wapinzani walikuwa wanamuuga mkono Uhuru Kenyatta mwanzo kabisa kabla ya hajakuwa rais na wameendelea kufanya hivyo 
2.Wapo wapinzani walikuwa wanamuuga mkono Raila Odinga tokea mwanzo na mpka muda huu wameendelea kumuunga mkono,Ata baada ya rais Magufuli kuingia madarakani....
3.wapo wapinzani ambao wamebadirisha maamuzi na kuancha kumuunga mkono Raila Odinga kutokana na sababu mbalmbali
-wengi wameacha kumuunga Raila Odinga kutokana ana urafiki na rais Magufuli 
 -Wengi wameacha kumuunga mkono Raila Odinga kutokana na kauli ya Lowassa kumuunga mkono Uhuru Kenyatta,
-wengi wameacha kumuunga mkono Raila Odinga wanaona matatizo wanayopata Tanzani mfano mikutano ya vyama siasa kupigwa marufuku wanaona Raila Odinga ni sehemu tatizo lao
-kundi hili tatu wanaona kumkomoa Raila Odinga ni kuhakikisaha anakosa urais tu 
#Mimi binafsi sina tatizo na kundi la kwanza na kundi la pili isipokuwa tatizo langu ni kundi la tatu ambalo linaamini matatizo wanayopata Raila Odingani sehemu ya tatizo lao kisa anaongea na adui yao namba moja
#Mimi nataka niwashauri kundi hili la tatu wakati wanaomba Mungu Raila Odinga Ashindwe urais watumie muda huo huo kuomba Mungu awape ujasiri ,uwezo,Uthubutu wa kuleta mabadilik katika nchi yao jambo ambalo wenyewe wameshindwa tokea wapate uhuru lakini @Odinga amefanikiwa kwa Asilimia kubwa wakati akiwa mpinzani 
#Naomba kundi tatu wajiulize Raila Odinga alitumia mbinu gani kuondoa chama tawala cha Kanu Madarakani akishirikiana na wenzake wao wameshindwa nini mpaka muda huu CCM imeendelea kukaa madarakani?? 
#Nataka Kundi hili tatu kwenye maaombi yao kwa Mungu ili Raila Odinga ashindwe rais watumie muda huo kuomba Mungu kuwapa ujasiri wakupigania katiba mpya Nchini mwao ambapo Raila Odinga amefanikiwa kupigania katiba mpaka ikapatikana lakini wao wameendelea kulia mpaka muda huu.
#Nataka kundi hili tatu wakati watakapokuwa wanasharekehea kwa nguvu Raila Odinga kushindwa urais baada ya uchaguzi ,wakati wanakwenda kumkushukuru Mungu kuwa maombi yao yamesikika watumie muda huo kuomba Mungu awape ujasiri,uwezo na maarifa ya kupigania tume uhuru ya uchaguzi ambapo wamekuwa wanalia kila siku waipate lakini kwa Raila Odinga huko Kenya amefanikiwa 
 #Naomba kundi la tatu wakati watakapo kuwa wamekaa kwenye viti vyao vya kuzunguka huku wanakunywa moja baridi na moja moto wakifurahia adui yao kushindwa rais watumie muda huo kuomba ujasiri kwa Mungu uliyosaidia Raila Odinga kuingiza wabunge wengi wa upinzani wakati kwenye nchi yao haijawahi kutokea zaidi ya chama kimoja kuendelea kulimiliki Bunge???
#Kundi hili la tatu wakati wakiendelea kuomba Mungu Raila Odinga ashindwa urais watumie muda mchache kutafakari hivi inakuwaje @Odinga anaweza kuunganisha wapinzani wenye nguvu kuungana na kupambana na chama tawala kwenye uchaguzi wakati hapa Tanzania tumeona wakina Lipumba na DK Slaa wakikimbia siku za mwisho kabla ya kufanyika uchaguzi ?
#Ukweli ni kwamba kushindwa Raila Odinga kuwa rais hakuwezi kusaidia lolote kufanikiwa kwao kisiasa hili kundi la tatu kama wataendelea kuendekeza unyonge,unafiki ,,mipango uchwara ..Mikakati uchwara,kuendekeza maneno mengi badala ya vitendo 
#mimi niwashauri kundi la tatu badala ya kutumia muda wenu kutoa vitamko uchwara vya kumuunga mkono Uhuru Kenyatta lengo likiwa kumkomoa Raila Odinga tumie muda huo kujifunza kutoka kwa Raila Odinga ni njia gani ametumia kupambana nchini Kenya mpaka mifumo ya mahakama nchini Kenya ipo uhuru kuliko nchini mwenu, 
 #kundi hili la tatu watumie muda kujiuliza hivi wameweza kuleta mabadiliko katika nchi yao kama alivyofanya Raila Odinga??
Image may contain: 1 person, standing
KWA  MAKALA   ENDELEA  KUMFOLLOW   
    Respicius Francis   kupitia  ukurasa  wake wa  facebook

Monday, May 8, 2017

10:01 AM

Kama umezoea kuandika makala za kumkosoa Rais Paul Kagame ,Soma ujumbe huu unahusu sana

imeandikwa  na Respicius Francis  kupitia  ukurasa  wake  wa  facebook
Image may contain: 1 person, eyeglasses
#Kuna wakati nilikuwa naandika makala juu ya wafungwa wa kisiasa ambao wamefungwa Rwanda
#Pia nikaandika juu ya wapinzani Kageme ambao wameuawa katika mazingira ya utata tena wakiwa nje ya RWANDA ///
#Baada ya kuadika makala zile na kuzipost kwenye mtandao wa www.tanzaniaclassic.com nilizishare kwenye makundi 40 ya Rwanda hapa facebook 
 #Baada ya dakika 30 nimepost makala zile nilipkea ujumbe mtu ambaye alikuwa kwenye profile yake ameweka picha mbuzi akiniomba niache kuandika makala zile kwasababbu rais Kagame ana uwezo wa kumfikia mtu yoyote popote pale hasa hapa Afrika 
#Siku hiyo hiyo nikapokea Reques za watu wasipongua 50 kwa mpingo lakini cha kushangaza hao watu walikuwa wamejiunga facebook mwezi mmoja, mwaka mmoja na kwenye wall zao hajawahi kupost chochote,Alafu kwenye list ya marafiki zao wana idadi marafiki wasiyozidi 25 jambo ambalo siyo la kawaida,,,, huku kati ya watu waliyonitumia Reques kwenye profile zao wakiwa wameweka picha za warembo wazuri ...
#Baada siku tatu nilipokea simu kwa mtu kutoka Rwanda ambaye alijitamburisha kama mwanafunzi wa chuo kikuu kutoka Rwanda ambapo alinisifia sana kwa makala zile huku akitamani siku moja tuonane..
-Niliendelea kuwasiliana na mtu yule kwa wiki moja lakini maswali ya kijanja ambayo alikuwa anauliza alitaka kunijua mimi zadi huku yeye anakuwa mgumu kuweka mambo yake hadharani,,,
#Wakati naendelea kuwasiliana na huyu Mrwanda ambaye alikuwa anajifanya kuwa rafiki huku niliendelea kuandika makala zile huku nikishare kwenye makundi mengi ya Kirwanda hapa facebook ambapo aliendelea kunipongeza kwa kujua siasa ya RWANDA ,huku yeye akiniambia kuwa anajua lugha zaidi ya 30 ambazo zinaongelewa na makabila mbalimbali ukanda wa maziwa makuu mfano kikuyu,kihaya,kiganda,Kizaramo,kirwanda nk
#Alafu cha kushangaza yule kijana anajua siasa ya kila nchi hapa Afrika mashariki mpaka nashangaa,,
#Tulipokushindana na yeye kuanza kuongopa nilimwambia anipe jina analotumia facebook lakini ilikuwa ni ngumu ila mwisho wa siku akanipa akaunti facebook
#Nilimwambia anipe namba anayotumia whatsapp alinipa lakini cha kushangaza akitumiwaa ujumbe na mtu mwingine anabaki kimya lakini akitumiwa na mimi anakuwa mkalimu na kujibu haraka hapo nikajua huyu mtu siyo mtu wa kawaida ,,
#Baada ya marafiki zangu kuanza kumchunguza aliwablock na mimi aliniblok pia ,Mpaka muda huu namba zake hazipatikani hewani
#Yule jamaa ambaye alikuwa ameweka picha ya mbuzi kwenye profile yake ya facebook huku kwenye list yake ya marafiki akiwa na idadi ya marafiki 10 tu aliniambia kuwa ni bora ukaandika makala zinazohusu Rais wako Magufuli   lakini siyo Kagame huku akinitajia majina kama Charles Ingabire mwandishi wa habari kupitia mtandao Inyenyeri News alikuwa akiandika makala nyingi za kumkosoa Kagame baada ya hapo alikimbilia uhamishoni Uganda lakini alipiigwa risasi huko huko Uganda..
          
# SWALI
rais Kagame ana kitu gani mpaka awe na uwezo kwa kufatilia mtu yeyote mahali popote ??

                 KWA  MAKALA   ENDELEA  KUMFOLLOW   
    Respicius Francis   kupitia  ukurasa  wake wa  facebook