Breaking

Showing posts with label Kenya News. Show all posts
Showing posts with label Kenya News. Show all posts

Saturday, June 2, 2018

2:13 PM

Mdau asema Rais Kenyatta akili yake ni kama imeazimwa toka Ulaya au Amerika.


UJUMBE umeandikwa  na  Livino Haule

Kenyatta licha ya mapungufu kadhaa kama binadamu, ni kiongozi mweusi wenye fikra za kizungu.
Kenyatta ni Rais wa nchi iliyopo Afrika lakini akili yake ni kama imeazimwa toka Ulaya au Amerika.
Ni Rais wa nchi ya dunia ya 3 lakini upeo wake katika mambo ya maslahi ya Taifa umekuwa upeo wa viongozi wachache wa nchi za dunia ya kwanza.
Akili na upeo wa Kenyatta haulingaishwi hata nusu yake na Rais Trump. Kenyatta ni mstaarabu mwenye hulka ya kipekee ever in Afrika.
Ni akili yenye kipawa kuacha ushauri wa polisi, usalama, jeshi, Naibu wake, chama chake na hata marafiki; na kutazama malengo ya utangamano wa Taifa la Kenya
Mungu mwema amlinde Kenyatta na kumfanya mfano wa Ulimwengu mzima katika zama hizi za "militarised goverments"

Image may contain: Livino Haule, smiling, standing and suit
 Bw;Livino Haule  aliyeandika  ujumbe     hapo  juu  ambaye  ni  mchambuzi  wa  maswala  ya siasa  

Thursday, May 3, 2018

7:55 AM

Rais Uhuru ammiminia sifa tele aliyekuwa mpinzani wake mkuu, Raila Odinga

Mwandishi: Joshua Kithome 
Rais Uhuru amemsifu sana kiongozi wa upinzani, Raila Odinga katika hotuba yake - Uhuru alimpongeza Raila kwa kukubali kufanya kazi pamoja naye katika kuwaunganisha Wakenya Rais Uhuru Kenyatta kwa mara nyingine amemsifia sana kiongozi wa upinzani, Raila Odinga mbele ya naibu wake William Ruto kwa kutii mwito wake wa kuungana katika kufanyaka kazi pamoja. 
Akitoa hotuba yake ya Hali ya Taifa siku ya Jumatano, Mei 2, rais alisema kuwa nia yake ya kuwaleta Wakenya pamoja haikuwa rahisi kuafikiwa bila Raila. Rais Uhuru na Raila walikubaliana kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kuungana katika kuwafanyia Wakenya kazi hapo mwezi Machi 9, 2018.  
"Si mimi pekee niliyehisi haja ya kuleta umoja tena, Raila Odinga alifanya alikuwa na wazo hilo pia. Wacha nimsifu kwa uzalendo alioudhihirisha," Alisema Uhuru. Aliwasihi viongozi kuungana pamoja na kuwatumikia Wakenya, waombe msamaha kwa kuwafeli Wakenya mwaka uliopita wa siasa.  
Hii sio mara ya kwanza kiongozi huyo wa taifa kumsifu Raila Odinga. Alifanya hivyo pia katika ibada ya mazishi ya mwendazake Kenneth Matiba alipoonyesha nia ya kufanya kazi pamoja katika kurejesha umoja wa Wakenya 
7:49 AM

Hii ndio sababu Rais Uhuru Kenyatta amewaomba msamaha

Mwandishi: Tina Mutinda  
 Kiongozi huyo wa Jubilee anajutia matamshi aliyotoa wakati wa kampeni 2017 -Rais aliwaomba wananchi na wanasiasa kuimarisha amani na umoja nchini Rais Uhuru Kenyatta amewaomba wananchi kumsamehe kwa matamshi yoyote aliyotoa na yaliyowaumiza wakati wa uchaguzi mkuu wa 2017. Rais Uhuru alichukua fursa ya hotuba ya kitaifa kuwaomba wananchi msamaha Jumatano, Mei 2.  
"Ikiwa kuna chochote nilichosema mwaka jana kilichowaumiza, ikiwa niliharibu umoja wa taifa hili kwa njia yoyote, ninawaomba mnisamehe na muungane nami kurekebisha hali,” alisema Uhuru 
Alisema kuwa viongozi wanafaa kuishi maisha yanayoweza kuigwa, na ndio maana aliomba msamaha.  
Aliwataka viongozi kuongoza kampeni ya kuwaleta wananchi pamoja kwa kuwakumbusha kuwa ukali haulipi lakini ukosoaji kwa njia ya kujenga ni muhimu. Kiongozi huyo aliwataka viongozi na wananchi vile vile kuheshimiana kuambatana na tofauti zao na kubuni njia za kushirikiana. Uchaguzi wa 2017 ulikumbwa na machafuko na vita ambazo zilianzishwa na uhasama kati ya Uhuru na kiongozi wa upinzani Raila Odinga. 
Kabla ya salamu kati yao ambayo imekuwa maarufu sana, Raila alimkashifu Uhuru na wenzake kwa wizi wa kura za urais wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Uhuru kwa upande wake alishambulia majaji na mahakama hasa baada ya ushindi wake kubatilishwa na Mahakama ya Juu. Wakati huo, viongozi katika pande zote mbili walionekana kushambuliana na kuchochea wananchi, hali iliyowatenganisha zaidi wananchi 
Hii ndio sababu Rais Uhuru Kenyatta amewaomba msamaha
Rais Uhuru Kenyatta amewaomba Wakenya msamaha. Picha/Kwa Hisani  

Sunday, April 29, 2018

12:50 PM

DP Ruto Smells Hell, Retreats Says No More 2022 Campaigns, To Focus As Uhuru Ordered

RUTO, NAKURU, APRIL 28, 2018, LEADERS

Deputy President William Ruto has asked leaders to heed the call by President Uhuru Kenyatta to stop engaging in politics and instead focus their energies on development.
Mr Ruto, at the same time, said Jubilee was united with a clear agenda of uniting the country, saying there were no groupings in the party.
“We have no political camps in our party. We are united and our aim is to bring the country together to eliminate tribalism, division and hatred as well as implement our development agenda for the people of Kenya,” said Mr Ruto.
Speaking during the launch of the Mavuno Daima Dairy cooperative society in Olenguruone, Nakuru County on Saturday, Mr Ruto said it was time leaders implemented what they promised the electorate prior to last year’s General Elections.
“The only debt we have as leaders for the people of Kenya is development. Kenyans elected Governors, MPs and MCAs during the last year’s General Election with the sole aim of serving them. This is the opportunity for us to serve them because time for politics is over,” said Mr Ruto.
“President Uhuru Kenyatta has told us to focus our energies on development and stop engaging in politics. We should therefore heed the call,” said Mr Ruto.
Present were Governor Lee Kinyanjui (Nakuru) and former Bomet Governor Isaac Ruto.
Others were MPs Moses Cheboi (Kuresoi North), Kuria Kimani (Molo), Liza Chelule (Women Rep, Nakuru), Charity Kathambi (Njoro), Beatrice Kones (Bomet East), Joyce Korir (Women Rep, Bomet), Gideon Keter (nominated), Joseph Tanui (Kuresoi South), Kipsengeret Koros (Sigowet/Soin)
The Deputy President urged leaders to work together and explore ways of solving the problems facing Kenyans.
“As leaders we need to unite and forge a common development agenda for our people. Let’s put behind issues to do with politics because there is time for everything,” said Mr Ruto.
The Deputy President also said the Government was committed to ensuring free primary and affordable secondary education for all Kenyans irrespective of their family backgrounds.
He warned of disciplinary action against the management of day secondary schools in the country found demanding fees from students.
The Deputy President said no one should demand for fees from students in day secondary schools as the Government has paid fees for them.
He thanked the people of Nakuru for supporting the Government since 2013, assuring them that Jubilee was focused on service delivery.
Governor Kinyanjui said the county was ready to help farmers form cooperative societies to market their produce.
He said investors from United States were ready to invest in the pyrethrum sector at a cost of Sh 400million, saying it will go a long way in addressing the challenges facing the sector.
“As county government we are ready to welcome and work with investors whose focus is to help improve the lives of the people through initiation of development projects,” said Mr Kinyanjui.
And while opening the Kiptagich Tea factory, Mr Ruto said the Government would improve all roads leading to major agricultural zones in the country to enable farmers transport their farm, produce to the markets and the factories.
He said tea farmers would from next year benefit from fertilizers to be supplied by the Government.
The Deputy President said the Government has lifted land caveat in Nakuru County but cases before courts were making it difficult for land transaction to take place.
He said once those cases were dropped, land transactions would take place, thus paving way for issuance of land title deeds.
The MPs said they would work together in implementing the Government’s development agenda.
“As leaders we will work together in implementing the Jubilee’s development agenda,” said Mr Cheboi.
Former Governor Isaac Ruto praised the efforts being made by the Government in addressing the challenges facing tea farmers.
“It is impressive that the Government is putting more emphasis in the development of the tea sector which is among the country’s top exchange earners,” said Mr Rutto.
The Deputy President also addressed wananchi during the opening of classrooms in Karao Secondary School.
END

Friday, April 20, 2018

2:05 PM

Raila and Kibaki meet as handshake gains momentum

By NANCY AGUTU @nancyagutu
A file photo of Opposition leader Raila Odinga with former President Mwai Kibaki.
Retired President Mwai Kibaki and Opposition leader Raila Odinga are meeting in Muthaiga, Nairobi, and will issue a statement at around 1pm.
It is not clear what they are discussing but Raila has met leaders such as former President Daniel arap Moi and discussed the state of the nation as well as the 2022 election with them.
The meetings followed his handshake with President Uhuru Kenyatta at Harambee House on March 9.
After the lengthy and deadly 2017 elections seasons, the two resolved to unite and push for peace, unity and development.
The truce between Uhuru and Raila and the meeting on April 12, between Raila and Moi, are shifting the political landscape. The country is in campaign mode four years too soon.
A suspected clandestine deal among the Kenyatta, Moi and Odinga families, if it takes shape, would be a powerful force in 2022, a juggernaut crushing competitors.
With Uhuru exiting and Raila indicating he might not run for State House, politicians are trying to sense which way the wind is blowing and positioning themselves as potential heirs.
The scheming and expected betrayal back-stabbing are reminiscent of the Jomo Kenyatta, Moi and Kibaki succession wars.

Wednesday, April 18, 2018

10:12 AM

Raila akutana na Ruto kwa mara ya kwanza tangu walipoafikiana na Uhuru kufanya kazi kwa pamoja

Mwandishi: Lauryn Kusimba  
Raila akutana na Ruto kwa mara ya kwanza tangu walipoafikiana na Uhuru kufanya kazi kwa pamoja.Picha:  


Raila Odinga na naibu rais William Ruto walikutana kwa mara ya kwanza tangu Raila alipoamua kufanya kazi kwa pamoja na serikali ya Jubilee - Wawili hao walikuwa wameenda nyumbani kwa marehemu Kenneth Matiba kufariji familia yake -Raila aliiomba serikali kufidia familia ya Matiba kwa majukumu aliyoyatekeleza katika kupigania 
Image may contain: 9 people, people smiling, people standing and suit

demokrasia ya nchi ya  Kenya -Matiba alifariki akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kuugua kwa muda mrefu katika hospitali ya Karen jijini Nairobi 
Kinara wa muungano wa NASA, Raila Odinga na naibu rais William Ruto walikutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza tangu Raila alipoamua kuungana na serikali ya Jubilee ili wafanye kazi kwa pamoja. 
Vigogo hao wawili walikutana nyumbani kwa marehemu Matiba ambapo walikuwa wameenda kufariji familia yake.  
Akiwahutubia waombolezaji, Raila aliitaka serikali kuifidia familia ya marehemu kwa kazi aliyoifanyia nchi hasa ya kupigania demokrasia. Raila aliongezea kwamba biashara nyingi za Matiba zilianguka kwa ajili ya kupigania demokrasia ya nchi hii 
Image may contain: 3 people, people smiling, people sitting, table and indoor
" Serikali inapaswa kuifidia familia ya Marehemu kwa masaibu yote aliyoyapitia kwa niaba ya Wakenya," Raila alisema Akiomboleza kifo cha Matiba, Ruto alimtaja kuwa kiongozi shupavu na shujaa atakaye kumbukwa zaidi kwa kupigania demokrasia. 
Matiba atakumbukwa kwa kupinga vikali utawala wa chama kimoja ambapo alizuiliwa mwaka wa 1990 bila ya kufunguliwa mashtaka. Afya ya Matiba ilianza kudhoofika akiwa kuzuizini na amekuwa akiugua ugonjwa wa 'Stroke' tangu mwaka wa 1990. Matiba aliaga dunia Jumapilia Aprili 15 akiwa na umri wa miaka 85 katika hospitali ya Karen jijini Nairobi.  

Monday, April 16, 2018

8:32 PM

Raila akamilisha ziara ya kumwakilisha Uhuru Afrika Kusini

Na CHARLES WASONGA
  Kiongozi  wa upinzani nchini  Kenya  Raila  Odinga  akiwa  Naibu rais  wa  Afrika  kusini  David Mabuza
KIONGOZI wa Upinzani Raila Odinga anatarajiwa kurudi nchini KENYA  muda  wowote  baada ya ziara rasmi ya kumwakilisha Rais Uhuru Kenyatta kwenye mazishi ya Winnie Mandela Afrika Kusini.
Mbali na hafla hiyo ya mazishi, Bw Odinga jana alikuwa amepengiwa kuwa na mkutano wa kibinafsi na Rais Cyril Ramaphosa.
Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, mshauri wake Bw Silas Jakakimba, alisema mkutano huo ulikuwa wa kibinafsi.
“Mheshimiwa Raila Odinga atakutana na Rais Cyril Ramaphosa kabla ya kurejea Kenya. Mkutano huo utakuwa na kibinafsi,” akasema Bw Jakakimba ambaye alikuwa katika ujumbe wa kiongozi huyo.
Bw Odinga anatambuliwa kuwa na urafiki na viongozi kadhaa wa Afrika, akiwemo Bw Ramaphosa ambaye alichukua uongozi majuzi kutoka kwa aliyekuwa rais Jacob Zuma.
Alipowasili Afrika Kusini siku ya Ijumaa, kiongozi huyo wa chama cha ODM ambaye sasa anashirikiana na Rais Kenyatta, alilakiwa na Balozi wa Kenya nchini humo Bi Jean N Kamau na maafisa wa ngazi ya juu katika serikali ya Afrika Kusini.
Kiongozi huyo aliandamana na mkewe, Ida, bintiye Winnie Odinga na Seneta wa Kisii Profesa Sam Ongeri.
Winnie, ambaye alishiriki katika mapambano dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo, alikuwa mkewe Rais wa kwanza mweusi nchini humo shujaa Nelson Mandela. Alizikwa Jumamosi katika hafla iliyohudhuriwa na maelfu ya watu pamoja na wageni kutoka mataifa ya nje.
Katika risala yake ya rambirambi, Bw Odinga alisema daima marehemu Winnie atakumbukwa na wale ambao walishuhudia na kufaidi kutokana na juhudi zake na kupinga utawala dhalimu wa mbeberu.
“Alijitolea mhanga kwa ajili ya ukombozi wa Afrika Kusini na watu wake. Na akapoteza mengi kama mtu binafsi. Lakini nafasi yake katika historia ni thabiti kwa mashujaa na wahasiriwa ulimwenguni,” akasema Bw Odinga.
Wakati wa ibada ya ukumbusho iliyoandaliwa katika uwanja wa michezo wa Orlando mjini Soweto, Bw Odinga alikutana na Naibu Rais wa Afrika Kusini David Mabuza, Waziri wa Mahusiano ya Kimataifa Lindwe Sisulu, Rais wa zamani Thabo Mbeki, miongoni mwa viongozi wengine mashuhuri.
Bi Mandela aliyefariki Aprili 2 akiwa na umri wa miaka 81 alizikwa katika bustani ya Four Way Memorial jijini Johannesburg.
Hapo ndipo mjukuu wake, Zenani Mandela alizikwa mnamo 2010 alipofariki baada ya kugongwa na gari.
Kumwakilisha rais kwenye hafla hiyo muhimu ya kitaifa kunaonekana kuwa sehemu ya matunda ya ushirikiano wa Bw Odinga na Bw Kenyatta, ambaye alikuwa mpinzani wake mkuu kwenye Uchaguzi Mkuu wa Agosti 8 mwaka jana.
Lakini tangu wasalimiane hadharani Machi 9 mwaka huu, mambo yamebadilika.
8:25 PM

ODM: Ruto anavuruga muafaka wa Uhuru na Raila


VALENTINE OBARA


WABUNGE wa upinzani wamemkashifu Naibu Rais, Bw William Ruto, kwa kupinga pendekezo kuhusu marekebisho ya katiba, wakisema ndiye kikwazo kwa muafaka.

Wabunge sita wa chama cha ODM Jumapili walisema msimamo wa Bw Ruto kupinga uundaji wa nafasi zaidi za uongozi kama vile wadhifa wa waziri mkuu, ni ishara kuwa haungi mkono juhudi za upatanisho zinazoendelezwa na Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga.
Viongozi hao walisisitiza kuwa lazima marekebisho ya katiba yafanywe, Bw Ruto apende asipende.
Wakizungumza katika Kanisa la Church of God lililo katika mtaa wa South B, Kaunti ya Nairobi, wabunge hao walisema matamshi ya Naibu Rais yanaonyesha haungi mkono ushirikiano wa Rais Kenyatta na Bw Odinga.
“Wakati Wakenya wanapojitahidi kuungana, wengine wanatia bidii kuwatenganisha. Hii haifai. Bw Ruto anafaa ajue tutahamasisha Wakenya ili waunge mkono juhudi zozote za kubadilisha mfumo wa uongozi wakati huo utakapofika,” akasema Mbunge wa Alego Usonga, Bw Samuel Atandi.
Alikuwa ameandamana na Bw Anthony Oluoch (Mathare), Bw George Aladwa (Makadara), Bw Caleb Amisi (Saboti), Bi Florence Mutua (Mbunge Mwakilishi Mwanamke wa Busia) na Mbunge Maalumu, Bw Geoffrey Osotsi.
Marekebisho ya mfumo wa uongozi yanatarajiwa kuwa miongoni mwa mapendekezo yatakayotolewa kufuatia ushirikiano uliotangazwa mnamo Machi 9, kati ya Rais Kenyatta na Bw Odinga.
Wazo la kuunda nafasi ya waziri mkuu limekuwa likishinikizwa zaidi na viongozi wa kidini ambao wanaamini itakuwa njia ya kuleta uwiano wa kitaifa kwa kuwezesha jamii tofauti kushikilia nyadhifa za uongozi.

Salamu si makubaliano
Hata hivyo, Bw Ruto Jumapili alisema ‘salamu’ za viongozi ambao walikuwa mahasimu wa kisiasa hazimaanishi kuna makubaliano ya kuunda nafasi mpya au kugawana mamlaka na watu fulani, huku akitaka viongozi wakome kupigia debe marekebisho ya katiba.
“Wakati wa siasa ulipita na uchaguzi mwingine utafanywa 2022, kwa hivyo inafaa tutumie nguvu zetu kuhudumia wananchi ambao walituchagua,” akasema.
Aliongeza kuwa Wakenya ndio wenye mamlaka ya kuchagua viongozi wanaotaka na jukumu hilo halifai kutolewa kwa watu wachache ikizingatiwa kuwa endapo kutakuwa na nafasi ya waziri mkuu, kuna uwezekano mkubwa atakuwa akichaguliwa na wabunge.
“Wakenya ndio wenye jukumu la kuchagua viongozi wanaotaka kwa msingi wa katiba. Hakuna vile watu wachache bungeni wanaweza kupewa jukumu la kuchagua watu kushikilia mamlaka makuu. Hiyo ni kazi ya wananchi,” akasema.
Alikuwa akizungumza katika Kaunti ya Turkana ambako aliandamana na Kiongozi wa Wachache katika Seneti, Bw Kipchumba Murkomen na magavana Josphat Nanok (Turkana), Stanley Kiptis (Baringo), Alex Tolgos (Elgeyo Marakwet) na Naibu Gavana wa Kaunti ya Uasin Gishu, Bw Daniel Chemno miongoni mwa wengine.
Hili linatokea siku mbili tu baada ya viongozi wa kanisa Katoliki kupendekeza kuwa katiba irekebishwe ili kuunda nafasi zaidi serikalini kwa nia ya kumaliza uhasama wa kisiasa nchini.

11:31 AM

“My Family Has Lost A Great Friend” – H.E. RAILA ODINGA Mourns His Brother-In-Struggle K. MATIBA


Johannesburg;
April 15, 2018
MOURNING KENNETH MATIBA:
Mama Ida and I have this evening learnt with deep shock of the passing of second liberation hero Hon. Kenneth Matiba.
Our country has lost one of the last living symbols of the pains our people have had to bear in order to get where we are.
Image may contain: 1 person, smiling, standing
It is hardly where we intended or ought to be, but certainly better than where we were at this time over 20 years ago, thanks to the sacrifices of Hon. Matiba and his team.
As a family, we have a very special bond with Hon. Kenneth Matiba and his family; one sealed by a shared vision and the scars of our shared struggles.
We pass deeply felt condolences to his Widow Edith and the family. We intend to speak more comprehensively about Hon. Matiba in the next few days.
May God grant strength to the family at this lonely and trying moment.
H.E. Raila Odinga
Mama Ida Odinga
April 15, 2018.

Saturday, April 14, 2018

10:38 PM

Railla Odinga kukutana na rais Afrika kusini Bw; Cyphril Ramaphosa kabla ya kurudi nchini Kenya

Bw;Railla Odinga kukutana na rais Afrika kusini Cyphril Ramaphosa kabla ya kurudi nchini Kenya 
Mshauri wa Odinga Bw;Jackson Jakakimba amesema kikao cha Odinga na Rais wa Afrika Kusini bw; Cyphril Ramaphosa kitakuwa cha siri [ private]
Inafahamika Odinga ana urafiki wa karibu na Cyphril Ramaphosa ata kabla hajakuwa rais wa Afrika kusini  hivi  karibuni,,, 
Raila Odinga ni kati ya viongozi wa upinzanii mwenye marafiki wengi ambao kwa  sasa wapo madarakani mfano mzuri ni rais wa GHANA Bw : Nana Akufo-Addo,Rais wa Ivory Coast Bw;Alassane Ouattara ,Rais wa msumbiji Bw; Filipe Nyusi ,Rais wa Tanzania John Magufuli

Thursday, April 12, 2018

7:41 AM

Masaibu ya Weta ni mwiba wa kujidunga – Raila

Huenda Raila akateuliwa Balozi Maalum barani Afrika, Kutengewa  ofisi  maalum  pamoja na  kulipwa   malipo yake ya uzeeni
Na VALENTINE OBARA
 KIONGOZI wa Chama cha Ford Kenya, Bw Moses Wetang’ula, ametakiwa akome kumlaumu mwenzake wa Chama cha ODM, Bw Raila Odinga, kwa masaibu ya kisiasa anayopitia
.
Maseneta wa Muungano wa NASA na Bw Dennis Onyango, ambaye ni msemaji wa Bw Odinga, Jumanne walipuuzilia mbali madai ya Seneta huyo wa Bungoma kwamba Bw Odinga ndiye alipanga njama na maseneta hao kumpokonya mamlaka ya kiongozi wa wachache katika seneti.
Kulingana na Bw Onyango, uamuzi wa kumg’oa Bw Wetang’ula ulifanywa na maseneta ambao hawakupendezwa na mitindo yake ya uongozi kwa hivyo anapaswa kujilaumu mwenyewe.
Mpaka leo, hakuna seneta wa NASA ambaye amejitokeza kumtetea Bw Wetang’ula. Hatujawahi kushuhudia kiongozi akikataliwa jinsi hii kwa hivyo ni ishara inayoonyesha kulikuwa na tatizo kubwa kati yake na wenzake,” akasema kwenye taarifa kwa vyumba vya habari.
Seneta wa Siaya, Bw James Orengo wa ODM, alichaguliwa kuchukua nafasi ya Bw Wetang’ula.
Bw Wetang’ula amekuwa akidai kuwa kinara mwenzake, Bw Odinga, alifahamu kuhusu mipango ya kung’olewa kwake kwani anaamini wanachama wa ODM hawawezi kuchukua hatua kubwa kama hiyo bila kiongozi wao kujua.

Suala la kikabila 
Lakini Bw Orengo alisema inasikitisha jinsi suala hilo limegeuzwa kuwa la kikabila ilhali uamuzi ulifanywa kidemokrasia.
“Raila Amolo Odinga hafai kuhusishwa kwa suala hilo kwa kuwa hakuna seneta yeyote kutoka kwa vyama tanzu ambaye alipinga mabadiliko ya uongozi katika seneti,” akasema.
Bw Onyango alifichua kuwa wakati wa mkutano ulioitishwa na Bw Odinga kumpatanisha seneta huyo na wenzake, maseneta walimlaumu kwa “kutofahamu mambo, kuwa mbinafsi, mjeuri na mwenye uzoefu wa kuwalazimishia maamuzi kwa kudai yalikuwa maagizo ya wakuu wa NASA ilhali wakati mwingi huo ulikuwa ni uongo”.
Bw Wetang’ula jana alinukuliwa kusema Bw Odinga alikutana kisiri na maseneta wa ODM ambapo mpango wa kumng’atua ulifanywa.

Wednesday, April 11, 2018

4:55 PM

Rais Kenyatta asaini sheria ya pedi bure kwa wanafunziwa Kenya Uhuru Kenyatta amesaini muswada wa sheria ambao sasa utakuwa kamili, inayoitaka serikali kugawa pedi bure kwa wanafunzi wa kike nchini humo.

Rais Kenyatta amesaini sheria hiyo jana Aprili 10, ambayo pia inaitaka serikali kuweka mazingira salama kwa wanafunzi hao kuweza kuhifadhi pedi zao.

“Sheria ya Marekebisho ya Elimu ya Msingi, kuweka wajibu wa kutoa taulo za usafi (pedi) za kutosha na za ubora kwa kila mtoto msichana aliyesajiliwa na kujiandikisha katika taasisi ya elimu ya msingi ya umma na kufikia ujira, kwa serikali”, imesema taarifa iliyotolewa na serikali ya Kenya kwa vyombo vya habari.

Ripoti ya UNESCO ya mwaka 2016 imeeleza kwamba binti mmoja kati ya 10 kwenye nchi zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara, anakosekana shuleni kwa siku ambazo yupo kwenye hedhi, kutokana na kukosa pedi za kujistiri.

Saturday, April 7, 2018

10:10 PM

Dangote Awakosoa Maofisa Kenya kwa kuendekeza ufisadi, Asema Kenya ina ufisadi kuliko Nigeria


Dangote awakosoa maofisa Kenya
Mfanyabiashara anayeshika nafasi ya kwanza kwa utajiri barani Afrika, Aliko Dangote amekosoa utawala wa Kenya kwa ubinafsi wao na kuendelea kushindwa kuweka mbele masuala yenye maslahi kwa taifa linapokuja suala la maendeleo.

Akizungumza katika mahojiano na mwandishi mashuhuri wa Kenya Jeff Koinange, Dangote alisema alifuta mipango ya kujenga kiwanda kikubwa cha saruji baada ya kukatishwa tamaa na watoa maamuzi ambao aliwaita ni “mafisadi kuliko Wanigeria.”

Akizungumza katika kipindi cha alfajiri cha studio za redio FM, Jeff alielezea mazungumzo binafsi aliyofanya na Dangote alipohudhuria hafla iliyoandaliwa na bilionea huyo kwa ajili ya kumuaga binti yake mwezi uliopita nchini Nigeria.

“Nilimuuliza, ‘Al Hajj lini utakuja tena Kenya?’ na yeye alisema ‘Jeff, kuna watu wako kule (Kenya) ambao wametanguliza ubinafsi wao na maslahi binafsi kuliko ya taifa. Sikuwahi kufikiria Kenya ingekuwa imekubuhu kwa rushwa kuliko Nigeria,’” alielezea Koinange.

Dangote, anayekadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Shilingi za Kenya 1.5 trilioni kwa utafiti wa jarida la Forbes, alitembelea Kenya Septemba 2013 katika msafara wa wafanyabiashara matajiri 50 kutoka Nigeria walioongozana na rais wa wakati huo Goodluck Jonathan.

Tajiri huyo wa Nigeria hivi karibuni alisogeza hadi mwaka 2021 kuleta kiwanda chake nchini baadala ya mwaka ujao.

Dangote anafahamika kwa kupanga bei ya chini ili kudhibiti soko jipya na hatua ya kusogeza mbele itawapa nafuu wafanyabiashara wengine katika soko hilo ambalo linashuhudia ushindani mkali.

Thursday, April 5, 2018

6:17 PM

Viongozi wajuta kumuunga mkono Raila kwenye uchaguzi


Huenda Raila akateuliwa Balozi Maalum barani Afrika, Kutengewa  ofisi  maalum  pamoja na  kulipwa   malipo yake ya uzeeni
Na GERALD BWISA
VIONGOZI wa Ford Kenya kutoka Kaunti ya Trans Nzoia Jumanne walieleza majuto yao kwa kumuunga mkono Kinara wa ODM, Raila Odinga kwenye chaguzi za 2013 na 2017.
Wakiongozwa na Mbunge wa Kwanza, Bw Ferdinand Wanyonyi, viongozi hao walikashifu kuvuliwa majuzi kwa kiongozi wao Moses Wetang’ula wadhifa wake wa kiongozi wa wachache katika Seneti.
“Tumejifunza kutokana na usaliti wa ODM na Raila atakuwa na kibarua kigumu kupata uungwaji mkono kutoka eneo hili siku zijazo,” akasema Bw Wanyonyi alipohutubia wanahabari mjini kitale.
Naye Diwani wa Motosiet, Bernard Muganda alisema watabuni mbinu ya kushirikiana na viongozi kutoka maeneo mengine na kuwataka wafuasi wao kutokata tamaa.
“Si lazima tushirikiane na watu kutoka Nyanza. Tunaweza kuunda miungano na watu kutoka maeneo mengine kama Bonde la Ufa na Kati,” akasema.
Bw Wanyonyi alisema mkutano walioandaa majuzi na Naibu Rais haimanishi wameanzisha ushirikiano wa kisiasai

Saturday, March 31, 2018

7:27 AM

Miguna Awaandikia Waraka Wakenya "Mipo Hai Lakini Nina Maumivu Makali"


Miguna Awaandikia Waraka Wakenya "Mipo Hai Lakini Nina Maumivu Makali"
Habari za asubuhi, mchana na jioni wazalendo wa Kenya na marafiki wa Kenya popote mlipo. Mimi niko hai. Namshukuru Mungu kwa hilo.

Lakini nina maumivu makali, msongo wa mawazo na usumbufu. Mkono wangu wa kushoto bado umevimba vibaya. Naamini majambazi ya Jubilee yalinidunga sindano ya IV kunifanya nisiwe na fahamu katika kipindi chote cha safari nikiwa kwenye ndege kati ya Nairobi na Dubai.

Upande wa kushoto wote unaniuma sana. Bado sijafanyiwa vipimo ili kubaini kemikali ambayo majambazi haya yalinidunga kwa nguvu na kinyume cha sheria Jumanne jioni.

Napenda kuwafahamisha mke wangu, watoto, familia, ndugu, marafiki, wafuasi wangu, wanaotutakia mema na wanachama wa vuguvugu la kundi la NRM kwamba nimetelekezwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai.

Nawasubiri wanasheria wangu wawasiliane nami kuhusu amri za hivi karibuni zilizotolewa na mahakama na hatua gani wameshachukua au wanatarajia kuchukua ili kukazia hukumu.

Narudia kusema kwamba ni lazima tuhakikishe kwamba kila mtu, bila kujali ana mabavu au dhaifu kiasi gani, anaheshimu, anazingatia na kutii amri za mahakama na atende kazi kwa kuzingatia utawala wa sheria.

Hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria!

Pili, mahakama zenye mamlaka zimetoa amri kwa serikali isiyohalali kunirejeshea au kunipa hati halali ya kusafiria ya Kenya. Nataka na ninatarajia amri hizo zitaheshimiwa kikamilifu.

Nasisitiza kwamba haki zangu za kikatiba za kuwa pasipoti ya Kenya ziheshimiwe na zizingatiwe.

Dk Miguna Miguna ashangaa amefikaje Dubai

Haki yangu ya kusafiri ndani na nje ya nchi kwa uhuru pia lazima iheshimiwe na izingatiwe wakati wote, katika namna ileile haki hizi zinavyotumika kwa Wakenya wengine.

Nasubiri kuruhusiwa na mamlaka za Shirika la Ndege la Emirates na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na kupewa tiketi ya kurudi Nairobi.

Natarajia kurejea Nairobi kwa ndege mapema iwezekanavyo. Ni haki yangu ya kuzaliwa, kikatiba na kisheria pia. Sitaacha kudai haki zangu kwa sababu ya utawala wa kiimla na matakwa ya waliotwaa mamlaka kwa mabavu.

Nawataka wote tubaki imara, tuzingatie malengo na tusiogope. Hiyo ndiyo njia pekee kwetu sisi kujikomboa na kuikomboa Kenya kutoka kwenye makucha ya madikteta Jubilee pamoja na wasaidizi wao na washirika wao. Dk Miguna Miguna 

Thursday, March 29, 2018

7:24 AM

Miguna afukuzwa nchini Kenya kwa mara ya pili,Apandishwa Kwenye ndege kwa nguvuMiguna Miguna amefukuzwa nchini  Kenya  kwa mara ya pili
 Miguna anasemekana kupandishwa ndege yenye nambari ya usajili EK 722 iliyokuwa ikielekea Dubai - Haya yamejiri hata baada ya korti kutoa amri ya kumuachilia huru na kumruhusu aingie nchini  lakini  serikali  ya  Kenya  imekataa  kutii  na  kuheshimu  amri  ya  mahakama .

Mwanaharakati wa kundi la vugu vugu la NRM, Miguna Miguna ameripotiwa kufukuzwa  nchini  Kenya   i baada ya kuzuiliwa katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta kwa siku tatu tangu aliporejea nchini kutoka Canada. 

Taarifa  zinaema   kuwa Miguna Miguna alipandishwa ndege yenye nambari ya usajili ya EK 722 iliyokuwa ikielekea Dubai Jumatano Machi 28 licha ya korti kutoa amri ya kumuachilia huru.  
Mawakili wake wakiongozwa na James Orengo, Nelson Havi na Cliff Ombeta walifika katika uwanja huo wakitaka Miguna aachiliwe huru lakini walifurushwa na maafisa wa polisi. Kupitia ukurasa wake wa Twitter wakili na mbunge wa Rarieda Amollo Otieno alionyesha kughadhabishwa na serikali baada ya Miguna kufurushwa nchini kwa mara ya pili. 
Inasemekana Miguna alisindikishwa na maafisa wawili wa polisi. 

Image may contain: 4 people, including Mollel Hillary Mollel, people smiling, text7:02 AM

“They Despots Drugged, Assaulted And Forcefully Dragged Me To Dubai” MIGUNA Speaks From Exile

  :
Message from Dr. Miguna Miguna
I was dragged, assaulted, drugged and forcefully into Dubai. I woke up in Dubai and the despots are here insisting that I must travel on to London. I’m sick. I need medical treatment. A Mr. Njihia is threatening me. I need urgent help here. I want to take a flight only to Nairobi. Nowhere else! Disseminate it elsewhere!!

Image may contain: 4 people, including Mollel Hillary Mollel, people smiling, text


Wednesday, March 28, 2018

11:18 PM

· Kimya cha Raila kuhusu Miguna chakera wafuasi wake

 Na BENSON MATHEKA

KINARA wa NASA, Raila Odinga ameshangaza wengi kwa kimya chake kuhusu masaibu ya wakili Miguna Miguna, ambaye alimuapisha kama “rais wa wananchi” Januari 30.
Kimya cha Bw Odinga kimefanya Wakenya na hasa wafuasi wake kutia kwenye mizani mwafaka wake na Rais Uhuru Kenyatta hasa kwa kushindwa kumsaidia Bw Miguna kuingia nchini kutoka Canada.
Japo Odinga alifika katika uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA), ambako Bw Miguna alizuiliwa tangu Jumatatu alasiri, hakusema chochote kuhusu hatua ya serikali kumhangaisha.
Bw Miguna alirejea Kenya mnamo Jumatatu, wiki nne baada ya kutimuliwa kwa kumuapisha Bw Odinga kuwa rais wa wananchi, na ilitarajiwa kuwa mwafaka wa wake na Rais Kenyatta ungemsaidia kurejea Kenya na kurudishiwa paspoti yake bila mushkil.
Juhudi za mawakili kushawishi maafisa wa uhamiaji kumruhusu kuingia Kenya hazikufua dafu japo walikuwa na agizo la mahakama.
Bw Odinga alifika katika uwanja huo mwendo wa saa tatu usiku mnamo Jumatatu. Muda mfupi baadaye Bw Miguna alikamatwa machoni pake na maafisa zaidi ya 40 wa polisi waliokuwa na maagizo ya kumwingiza katika ndege ya Emirates iliyokuwa tayari kuelekea Dubai. Bw Odinga hakusema chochote.
“Miguna alinyanyuliwa na maafisa wapatao 40 wa polisi mbele ya Bw Odinga na mawakili wake, kisha akaingizwa katika chumba kilichokuwa chini ya ulinzi mkali kabla ya kulazimishwa kupanda ndege ya kuelekea Dubai. Bw Odinga alitazama tu!” alisema aliyeshuhudia matukio JKIA.
Kiongozi huyo wa chama cha ODM aliondoka uwanja huo punde tu Bw Miguna alipokamatwa bila kuzungumza na wanahabari, tofauti kabisa na ilivyokuwa mfanyabiashara Jimi Wanjigi na mwanamikakati wa NASA David Ndii walipokamatwa.
Hadi wakati wa kuchapisha taarifa hii, Bw Odinga hakuwa ametoa taarifa kuhusu masaibu ya Bw Miguna.
Kufuatia ushirika wake mpya na Rais Kenyatta, wengi walitarajia kuwa angechukua hatua za kumuomba Rais Kenyatta aagize maafisa wa uhamiaji na usalama wa kumruhusu Bw Miguna kuingia nchini na kurejeshewa paspoti yake ili kuepuka kizaazaa kilichoshuhudiwa katika uwanja wa JKIA.
Wadadisi wanasema kwa kukubali kushirikiana na Rais Kenyatta Bw Odinga alijifunga hivi kwamba hawezi kukosoa vitendo dhidi ya washirika wake wa kisiasa.

Image may contain: 4 people, including Mollel Hillary Mollel, people smiling, text