Breaking

Showing posts with label BUSINESS. Show all posts
Showing posts with label BUSINESS. Show all posts

Sunday, March 4, 2018

8:58 PM

Jinsi ya kutafuta Masoko ya biashara yako


UTANGULIZI
Kuwafundisha washiriki kufikiri ki- masoko na kuelewa baadhi ya mbinu za masoko kitu ambacho kitawafanya waelewwe maana ya maneno “soko na masoko” pia utafiti wa soko na kuyafanyia kazi  katika biashara/miradi yao.

Soko ni nini?
Soko ni utaratibu au mtindo  uliowekwa kwa mujibu wa kanuni /sheria  kumwezesha mfanya biashara kuuza bidhaa zake kwa wateja/walaji. Husaidia kupanga nini uuze,nani umuuzie au jinsi gani watu wanavyoweza kujuakitu gani unauza,hivyo kukuwezesha kuzalisha kile ambacho kinahitajika  katika soko sahihi.

Mafanikio katika biashara hutokana na mwonekano wa kipekee  wa bidhaa au bidhaa unayozalisha kukidhi matakwa ya walaji au wateja pia, kuweza kutambua  aina fulani ya watu ambao wangependa kununua bidhaa yako na kuweza kueleza  bayana ni kitu gani, watu wategemee kunufaika kwa kunua bidhaa zako kati ya kundi hili la walengwa.

Kwa kifupi soko ni MTEJA Wa bidhaa na huduma uayozalisha

Soko lako ni;

 • Wateja wako ulionao kwasasa
 • Wateja uaotarajia kuwapata baadae
 • Wateja uliopoteza na untarajia watakurudia tena

Masoko ni nini?
Masoko ni shughuli yoyote ile anayofanya mfanyabiashara ili kuimarisha biashara yake.

Haitoshelezi tu kukaa kungojea oda.

Mfano wa shughuli hizo ni;

 • Kuelewa matakwa ya wateja wa bidhaa yako
 • Kupanga bei ambayo wateja  watakuwa tayari kulipa na itakupa faida
 • Usambazaji wa bidhaa au huduma kwa wateja wako
 • Kuwavutia wateja wanaume bidhaa au huduma yako

UTAFITI WA SOKO
1. Kwa nini tujifunze kuhusu soko?
a)  Mahitaji (demand)

Waswahili husema ‘unaweza kumlazimisha punda aende mtoni lakini huwezi kumlazimisha anywe maji’inamaana bidhaa zako kuwa wakati soko halihitaji bidhaa zako huwezi kulazimisha bidhaa yako inunuliwe

b)  Bidhaa sahihi – usijaribu kumuuzia kitana mtu mwenye kipara bali muuzie kofia

c)  Kufuata mkumbo-ni vema kutofautisha bidhaa za kuuza kwa wateja

2. Unahitaji kufahamu nini kutokana na soko lako?
Maswali yafuatayo ndio yakusaidia kufanya utafiti wa soko lako

Wateja wako ni akina nani?

 • Wako wapi
 • Mahitaji yao ni nini?
 • Wanapendelea nini kutokana na bidhaa zako
 • Ni mara ngapi na kiasi gani a wanacho nunua?
 • Wana nunua wakati gani?
 • Ni kiasi gani cha pesa wako tayari kutoa?
 • Ni jinsi gani bidhaa zitawafikia wateja
 • Washindani wako ni wapi?
 • Ubora wa bidhaa zao na bei zao vikoje

NB; kutafuta majibu ya maswali haya kunaitwa utafiti wa masoko

3. Jinsi ya kufanya utafiti a soko
Mbinu zifuatazo zinaeza kutumika kufanya utafiti wa soko la bidhaa au huduma unazozalisha:-

 • Kupitia Kwa wateja (kusikiliza maoni yao, kuachunguza na kuwauliza maswali).
 • Kuwauliza maswali watumiaji mbali mbali wa bidhaa zako ( nini wanachohitaji na wasicho kihitaji, mapendekezo na nini kiongezwe)
 • Kwa marafiki na ndugu
 • Kusoma kwenye vitabu, magazeti, kusikiliza radio na kuangalia televisheni
 • Kupeleka bidhaa zako katika maonesho ya biashara
 • Kuangalia biashara za washindani wako: bei, ubora, tofauti za bidhaa,, kuonesha bidhaa, na huduma zinazoambatana na bidhaa zako
 • Onesha sampuli ya bidhaaa au tembezasampuli ya bidhaa na waulize watu maoni juu ya bidhaa zako

4. Jumuisho la masuala ya masoko

B-Nne  katika masoko
 • Bidhaa
 • Bei
 • Banda
 • Bango

a)  BIDHAA- Bidhaa ni kitu chochote kinachozalishwa kwa ajili ya kuuza au kutumia.

Sifa za bidhaa
Bidhaa nzuri ni ile inayoridhisha na inakidhi matakwa ya soko. Kwa mfano:-

 • Ubora(muda, malighafi nzuri, iliyotengenezwa vizuri)
 • Yenye kuvutia ( rangi,mapambo,usafi, utengenezaji mzuri)
 • Mtindo (umbile zuri, inahusiana na thamani,saizi)
 • Ya kisasa (Inayoendana matumizi ya mtindo uliopo- fassion)
 • Tofauti na bidhaa za ashindani

b) BEI- Bei nithamani ya bidhaa au huduma ambayo mteja yuko tayari kumudu au kulipia. Kwa hiyo bei hujumuisha Gharama zote na faida au Bei huiumuisha gharama za ununuzi, gharama za uendeshaji na faida.

Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kupanga bei.
 • Ghrama zote ka jumla (gharama halisi)
 • Bei za wapinzani
 • Mahali ulipo 9 kiasi ambacho wwateja wwako radhi kulipia kwa kutegemea uezo wao kifedha)
 • Msimu (kwa mfano bei kubwa za vinyago msimu wa watalii au bei ndogo za feniture wakati wa mvua )
 • Kupata faida ya kutosha kuendesha shughuli bila matatizo

c) Banda au mahali pa kufanyia biashara
Banda ni mahali muhimu sana  katika kuuza bidhaa au huduma. Mahali pa kufanyia biashara  panatakiwa pae na sifa zifuatazo:-

 • Rahisi kufikiwa na wateja
 • Usalama, usafi
 • Sehemu ya maegesho
 • Kuwa karibu na huduma nyingine muhimu kama vile usafiri wa daladala, sehemu za vinywaji, vyakula,umeme n.k
 • Yenye mwanga wa kutosha
 • Rahisi kuonekana
 • Huduma hutolewa saa zote

5. Upangaji mzuri wa bidhaa mahali pa biashara.

 • Bidhaa zipangwe kwa seti
 • Mahali pa wazi panapoonekana kiurahisi
 • Weka bidhaa chache katika makundi madogo madogo
 • Weka bidhaa za aina mbalimbali
 • Panga sehemu yenye mwanga wa kutosha
 • Sehemu safi
 • Tumia picha au katalogi

6. BANGO AU UVUMISHAJI
Uvumishaji unajumuisha shughuli kadhaa  ikiwa ni pamoja na uvumishaji  wa mauzo,utangazaji,uhusiano wa jumuia na mbinu za kuuza. Shughuli hizo zinasaidia kuwavitia wateja, lakini hasahasa zinawapa wateja imani na bidhaa zako kuhakikisha kuwa hawanunui kwa mtu mwingine.Jambo muhimu la kuzingatia katika uvumishaji wa bidhaa ni lazima uwe mchangamfu na kuwa macho kuvutia wateja.

Kuvumisha mauzo (sales promotion)
 • Punguza bei yako kidogo ili wateja waone kuwa ni ndogo. Mfano:-  shs 999.00 badala ya 1000.00
 • Weka bei maalum wakati wa sikukuu mbalimbali
 • Panga bidhaa madirishani ilizionekane kwa nje (display)
 • Uza bidhaa zinazoendana. Mfano muuza maandazi anaweza kuuza chai au muuza sukari anaweza kuuza majani ya chai
 • Utangazaji

Radio, magazeti,tv,sinema,mabango,kadi za biashara za mwenye biashara9business card)na sifa zinazotolewa kwa njia yam domo na watu watu waliokwisha kutumia bidhaa hizo.

Mahusiano
Kuchangia huduma za jamii Kama vile elimu, afya mazingira n.k

Mbinu za uuzaji

 • Jinsi ya kutambulisha bidhaa, eleza faida za bidhaa na ubora ake
 • Kumthamini mteja
 • Eleza faida ya bidhaa yako kabla hujataja bei
 • Jaribu kuuliza juu ya mahitaji ya mteja ili uweze kumwelekeza kwenye bidhaa itakayomfaa.
 • Kama mteja akiuliza bidhaa ambayo huuzi , unamwekeza zinapoatikana.

MKAKATI WA MASOKO
Kuwa na mkakati wa soko utakusaidia kufiki malengo yako kupitia kuweka lengo kuu/kubuni bidhaa/huduma mchanganyiko na kuchukua SWOT ANALYSIS(maeneo tunayofanya vizuri,maeneo ambayo hatufanyi vizuri,fursa tulizonazo, na changamoto zinazotukabili) katika bidhaa /huduma.

MAELEZO YA MALENGO YAKO
Maelezo ya malengo ni nini? Ni maelezo ya jumla  juu ya kila unachotarajia kufikia,au lengo kuu la shirika. Hujulikana pia kama dira ya shirika . hivyo ni vema kuwa na wazo ambalo unaweza kuliweka kama kitovu cha kukuwezesha kuona unapoelekea  kibiashara. Kulingana na kukua kwa biashara yako waweza kuendeleza malengo yako kuipa nguvu dira yako

Lengo lako lazima liwe dhahiri / bayana
 • Ni nini unataka kutimiza?
 • Kwa nini/ sababu gani ya kutimiza?
 • Nani atafanya nini?
 • Ni wapi utafanyia kile unachotarajia?
 • Kipi kinatakiwa kufikia lengo lako?
Malengo yako lazima yaweze kupimika.

 • Kwa kiasi gani?
 • Vingapi?
Malengo yako lazimayawe ya kufikiwa.
 • Ya juu Sana kisi cha kushindwa kufikia malengo yako?
 • Ya chini Sana kisi kwamba malengo yako hayaleti maana?
 • Ni muhimu kuweka malengo yanayokubalika lakini yenye kutamanisha.
Malengo yako yawe na uhusiano na kile unachotaka kufanya

 • Tuzo nitakayoipata baada ya kufikia malengo itazidi gharama (faida)
 • Tuzo nitakaipata baada ya kufikia malengo itafikia maezo ya malengo yako ya awaliKufikiwa kwa malengo yako kutakusaidia  kufikia mipango yako?

Malengo yako lazima yaende na wakati

Ni lini litaanza?
Itachua muda gani kufikia malengo yako?Naweza kufanya nini kila juma,Mwezi juu ya bidhaa nyingine iliyopo ambayo ina matumizi sawa na ile anayohitaji, mteja

Saturday, March 3, 2018

8:20 PM

Hii Ndiyo Sababu Kwa Nini Utangaze Biashara YakoWatu wengi wamekuwa wakijiuliza maswali mbalimbali ambayo yanahusiana na masuala ya kibiashara. Na miongoni mwa maswali ambayo wamekuwa wakiniuliza ni kuhusu ni nini faida ya kutangaza biashara kwa sehemu kubwa?

Swali hili ndilo limenifanya nishike kalamu yangu ili niweze kulijibu. Nakusihi twende sambamba ili niweze kueleza kwa kinagaubaga, kwa nini unapaswa kuitangaza biashara yako tena kwa nguvu zote.
Matangazo ni usambazaji wa taarifa  sahihi  kuhusu bidhaa au huduma kutoka kwa mfanyabiashara kwenda kwa mteja. Matangazo ndiyo roho ya biashara, kwani bila kufanya biashara yako bila matangazo ni sawa na bure.

Nafikiri pia utakubaliana nami ya kuwa ili uweze kufanya biashara  yenye tija ni lazima uitangaze biashara yako, kwani " biashara ni matangazo".  Matangazo ndiyo yatakuyokufanya uweze kuongeza mauzo ya kibiashara kila wakati.

Kwa kuzingatia hilo unaweza kuitangaza biashara yako kwa njia ambayo itakuwa ni rahisi kwako. Na sababu kubwa ya kuitangaza biashara yako ni kuongeza wateja wapya.

Leo na dhumuni kubwa la kutangaza biashara yako ni kukutana na na watu wapya,  ukiona umetangaza biashara yako na hakuna mteja mpya hata mmoja ujue fika kuna mahala ambapo umekosea.

Hivyo fanya tathimni upya na ujipange upya na kuona ni jinsi gani unaweza kuitangaza biashara hiyo. Vile vile katika upangaji wa malengo ya kibiashara hakikisha ya kwamba unapanga na mbinu za kukutana na watu wapya kila siku.

Nasisitiza juu ya kukutana na watu wapya, kwa sababu nimegundua ya biashara nyingi zimekuwa hazifanyi vizuri kwa sababu zimekuwa na watu ambao wanaizunguka biashara ile ni wale wale kila siku. Hivyo kila siku fanya tathimini juu wateja wapya ambao wamekuja katika biashara yako.

Asante kwa kutembelea mtandao huu wa dira ya mafanikio,  usisite kumshirikisha na mwingine ili aweze kujifunza

Sunday, November 26, 2017

Friday, November 24, 2017

12:08 PM

Do you love to have adventure or unique safari in Tanzania??

Do you love to have adventure or unique safari in Tanzania??
We like to take you there because we are offering options for every budget and luxury safari without any customization fees and we have best guides and drivers who know all the ins and outs of the safaris.Our specialty will always be groups and private escorted tours to incredible destinations.
Book now any wildlife Safaris (migration safaris, standard safaris and special safaris), Mountain Trekking (Mountain Kilimanjaro, Mountain Meru and Mountain Ol Doinyo Lengai), Zanzibar Holiday (Dolphin Hunting, city tours, Island tours, Coffee and spice tours,cultural tours, sunset Dhow Cruise and other tours in Island), Day Trip (Bicycle Riding, Waterfalls, National Parks and City Tour) and Cycling for the year 2018 and save 10% as Discount.
Website www.desiresafaris.com
E-mail: Booking@desiresafaris.com
WhatsApp 24 hrs : +255 686 303 302
Facebook Page: Desire Safaris Tanzania