Breaking

Showing posts with label . POLITICS. Show all posts
Showing posts with label . POLITICS. Show all posts

Sunday, June 3, 2018

9:11 AM

Rais saini mswada Vijana kuwania uraisi ukiwa na miaka 35


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, ametia saini kuwa sheria mswada unaopunguza umri kwa wananchi wa taifa hilo wanaotaka kuwania nyadhifa mbalimbali za kisiasa.
Sasa ni rasmi kuwa, raia wa Nigeria mwenye umri wa miaka 35 anaweza kuwania urais kuanzia Uchaguzi Mkuu wa mwaka ujao, umri wa chini ulikuwa miaka40.
Wanaotaka kuwania ubunge, wanastahili kuwa na umri wa miaka 25 na kuendelea huku wale wanotaka kuwa Maseneta na Magawavana wanastahili kuwa na umri wa miaka 35.
Rais Buhari mwenye umri wa miaka 75, tayari amesema atatetea kiti chake kwa muhula wa pili.

Saturday, May 5, 2018

8:18 AM

Mbunge Aibua Sakata la Vifo vya Mtikila na Chacha wangwe Bungeni


Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Janeth Masaburi amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Mwigulu Nchemba kutoa taarifa bungeni juu ya vifo vya wanasiasa Chacha Wangwe aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila.

Wangwe ambaye alikuwa mbunge wa Tarime kwa tiketi ya Chadema alifariki dunia Julai 27 mwaka 2008 katika ajali ya gari iliyotokea Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma,  Mtikila alifariki katika ajali ya gari  Oktoba 4, 2015 Chalinze wilayani Bagamoyo.

Akichangia bajeti ya wizara hiyo  mwaka 2018/19, Masaburi amemtaka pia waziri huyo kutoa taarifa za kifo cha watalii waliomwagiwa tindikali na makanisa yaliyochomwa moto.

“Tunaomba taarifa, kifo cha Wangwe, Mtikila, watalii waliomwagiwa tindikali na makanisa yaliyochomwa moto Zanzibar,” amesema.

Kuhusu amani amesema Tanzania ipo mahali salama tangu kuasisiwa kwake enzi ya Hayati Mwalimu Nyerere na maraisi wastaafu Ali HassaMwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete.

“Hii nchi yetu sote, humu tupo zaidi ya 300 ila Watanzania wapo milioni 60, kila mtu ana haki hamasa ambazo zinatolewa kwa kutubagua zishindwe kwa jina la yesu.  Bila amani hatuwezi kulima hakuna kwenda shule, kustarehe wala kuzaliana,” amesema.

Amesema watu wasitanie amani kwa kutumia dini kwamba dini fulani inaonewa na kuhoji mbona wapo ndani ya Bunge.

“Tusitanie amani, ninaomba Serikali iongeze bajeti ya kutosha katika vyombo vya ulinzi na usalama pia makazi yao yaboreshwe na kujengwa nchi nzima,”amesema. 

Tuesday, May 1, 2018

Thursday, April 26, 2018

11:08 AM

Hapa Ndipo Atakapozikwa Obama?

Hapa Ndipo Atakapozikwa Obama?

Marais saba wa Marekani na wake zao wamezikwa katika maeneo ya maktaba na makumbusho zilizobeba kazi zao za tangu ujanani hadi katika uongozi wa Taifa hilo.

Pia marais wote wa Taifa hilo wana utamaduni wa kutaja eneo watakalozikwa, kwa kuwa utangazaji hufanyika mara tu waingiapo Ikulu au wawapo katika mbio za kuwania kuingia Ikulu.

Hatua hiyo hufanyika ili kutoliweka Taifa katika sintofahamu pindi wanapoondoka duniani ghafla. Kwa sasa Marekani haina sheria ya eneo maalumu la mazishi ya viongozi kama zilivyo baadhi ya nchi zilizoendelea kutokana na kila mmoja kuwa na wosia wake tangu anapoanza maisha ya kujitegemea.

Hata hivyo, wakati huo ukiwa utamaduni wa kawaida wa marais hao kuwa na mahala wanapochagua kuzikwa washindapo uchaguzi kwa mara ya kwanza, Rais wa 44 wa Taifa hilo, Barack Obama hakufanya na hajafanya hivyo hadi sasa.

Maeneo walikozikwa marais wa Marekani yapo katika majimbo 23 ikiwemo District of Columbia. Marais 45 wameitawala nchi hiyo tangu mwaka 1789. Kati yao, 38 wamefariki dunia.

Jimbo lenye makaburi mengi walikozikwa marais ni Virginia walikozikwa saba. Tangu 1789, Wamarekani 49 wamehudumu kama makamu wa rais, kati yao 41 walishafariki dunia. Jimbo lenye makaburi mengi ya makamu wa rais ni New York walipozikwa 10.

Kizungumkuti cha Obama

Kwa upande wa Obama, inaelezwa kwamba hadi mwisho wa utawala wake ulioanza 2009 hadi 2017 hakueleza atazikwa wapi, iwe kwa maandishi au mdomo kwa wasaidizi wake.

Kwa wasaidizi na watu wake wa karibu ilibaki kuwa iwapo ingetokea akafariki dunia ghafla, basi angezikwa katika Jimbo la Chicago mahali ambako nyota yake ya kisiasa ilianzia kung’ara.

Hata hivyo, ikiwa ni zaidi ya miaka miwili sasa tangu astaafu, Obama yuko ‘bize’ na ujenzi wa makumbusho ya kazi zake ambayo pia itatumika kama maktaba katika eneo la Jackson Park, Chicago, mahala ambapo pia wengi wanadhani kaburi lake litajengwa hata kabla hajafa. Pia ni katika eneo hilo anapojenga makumbusho panatajwa kuwa ndipo mkewe, Michelle atakapozikwa. Marais saba wa Marekani na wake zao wamezikwa kwenye makumbusho au maktaba walizoanzisha, utaratibu ulioasisiwa mwaka 1945 baada ya kifo cha rais wa 32, Franklin Roosevelt.

Roosevelt alizikwa katika Makumbusho ya Taifa ya Historia ya Franklin Roosevelt iliyopo Hyde Park, New York.

Swali lililopo vichwani mwa wengi na ni Obama pekee mwenye jibu,

INAENDELEA UK 18

INATOKA UK 17

ni lile la mwanasiasa huyo aliyeondoka madarakani akiwa na miaka 55 atazikwa katika Jackson Park au wapi?

Taarifa za ndani zinadai makumbusho hiyo inayojengwa katika eneo la kati ya eka 23 hadi 24 haionyeshi kuwapo ramani ya kaburi au makaburi ya familia yake, ingawa kwa thamani ya ‘mjengo’ na ardhi vinavyofikia zaidi ya Dola 300 milioni za Marekani (zaidi ya Sh700 bilioni) lolote linaweza kufanyika iwe sasa au baadaye.

Baadhi ya wadadisi wa mambo wanasema utamaduni wa viongozi wa Taifa hilo kuzikwa katika makumbusho au maktaba zao umepitwa na wakati na kwamba, ni vyema kukawa na eneo maalumu la kihistoria litakalotumika kama sehemu ya makaburi ya marais walioitawala Marekani.

Hata hivyo, wanaopinga wana hoja kuwa makumbusho au maktaba zao kutengewa maeneo ya makaburi ni jambo jema na linavutia makumi kwa maelfu ya watu kuzitembelea ili kujionea vitu mbalimbali vilivyotunzwa.

“Palipo na kaburi kwenye maktaba ya rais, hilo ni jambo jema maana linavuta hisia za watu kufika na kujionea vitu vilivyomo,” anasema Benjamin Hufbauer, Profesa wa Chuo Kikuu cha Louisville ambaye pia ni mwandishi wa kitabu cha Presidential Temples: How Memorials and Libraries Shape Public Memory.

Profesa Hufbauer anasema, hata hivyo ni vyema Obama na familia yake wakazingatia kwamba kuweka eneo watakapozikwa katika maktaba hiyo ni jambo muhimu kwa sababu ya sifa tofauti alizonazo.

“Kwanza Obama alikuwa rais mweusi wa kwanza na pili, kizazi chake kina mchanganyiko wa uhamiaji na ukazi (wa Marekani) hivyo itakuwa vizuri zaidi akiwa na eneo hilo ambalo pia litawavuta mamilioni ya Waafrika na Wazungu kulitembelea,” anasema.

Marekani kuna maktaba na makumbusho 13 za marais, lakini ile ya Obama itakuwa chini ya Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka cha Taifa, ingawa kutokana na baadhi ya nyaraka alizotumia kama rais kuhifadhiwa maeneo tofauti haitapata fungu la fedha la kujiendesha kutoka kituo hicho. Kituo hicho ni idara ya Serikali.

Ingawa hadi sasa atakapozikwa Obama hapajafahamika, marais wanaoondoka madarakani wanatakiwa kiutaratibu kueleza watakapozikwa kwa mkuu majeshi kupitia kitengo cha huduma za wastaafu na zaidi ya hilo wanapaswa kupata ushauri wa kitalaamu, na hasa inapotokea kuwa sehemu hizo zinakuwa na masilahi mengi ya nchi.

Familia itaamua atakapozikwa

Kigingi kingine kinachoweza kuikabili makumbusho ya Obama ni kile cha iwapo ataamua kuwa eneo la makaburi liwepo ndani yake, sheria za Illinois zinataka kibali mpaka kitolewe baada ya usanifu mpya kuwasilishwa. Kwa sasa si Obama, taasisi yake wala makumbusho anayoijenga iliyowasilisha ombi hilo.

Licha ya kwamba rais huyo mstaafu hajafanya lolote mpaka sasa, na ukweli kwamba kifo hakipigi hodi, wanafamilia wataamua wapi watamfanyia maziko iwapo atafariki dunia kabla hajaamua atakapozikwa lakini vyovyote iwavyo mwili wake hautazikwa nje ya Chicago mahali ambako alikulia na kupatia umaarufu wake kisiasa.

Kwa mujibu wa watu wa karibu wa Obama, makumbusho yake inayotarajiwa kuzinduliwa miaka minne ijayo, itakuwa ya kisasa na yenye hadhi ya juu zaidi ikizingatiwa kwamba ndiye rais wa saba bora zaidi nchini humo (kwa mujibu wa utafiti wa mashirika makubwa matano ya habari nchini Marekani).

Marais 10 bora wa Marekani na ubora wao kwa mujibu wa mashirika hayo kwa kufuatia mtiririko ni Abraham Lincoln, George Washington, Franklin Roosevelt, Theodore Roosevelt, Thomas Jefferson, Harry Truman, Dwight Eisenhower, Obama, Ronald Reagan na Lyndon Johnson.

“Kama kutakuwa na eneo la makaburi nadhani litakuwa linatembelewa na watu wengi wakiwamo watalii kuona atapokuwa ‘amelala’ mmoja wa viongozi bora zaidi wa Marekani,” anasema mmoja wa wasaidizi wa Obama.

Mtendaji mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Makumbusho Afrika na Marekani iliyopo Charleston, Michael Boulware anasema utembeleaji wa maeneo ya kihistoria unamfanya mtu aguswe na historia husika.

“Unaweza kusikia hadithi popote, unaweza kuisoma kwenye vitabu viwili au vitatu, lakini kuwa katika eneo husika kunaongeza uwezo wa akili kujihisi ni sehemu ya historia,” anasema.

“Sidhani kama kuna swali kwamba Rais Obama hatakufa, lakini kama rais mwenye rekodi (zilizotukuka) na historia ya aina yake, anastahili kuenziwa na kadri muda unavyokwenda ataendelea kuonekana bora zaidi kihistoria.”

Obama pia anaweza kuamua kuzikwa katika Jimbo la Hawaii, huko ndiko alikozaliwa na kutumia muda mwingi wa ujana akilelewa na mama yake, Ann Dunham. Pia, Hawaii ndilo eneo maarufu kwa familia yake analolitembelea kila mara na pia Obama anaweza kuwa rais wa kwanza wa Marekani kwa mabaki ya mwili wake kuchomwa moto, utamaduni ambao unafanywa na jamii kubwa ya Kiasia nchini humo.

Walivyozikwa baadhi ya marais

Harry Truman alizikwa kwenye maktaba na makumbusho yake iliyopo eneo la Independence, Mo; Ronald Reagan alizikwa katika maktaba na makumbusho yake, Simi Valley, California; Herbert Hoover alizikwa kwenye maktaba na makumbusho yake West Branch na Dwight Eisenhower kwenye eneo la shughuli zake la Abilene lililopo Kansas.

Wengine ni Richard Nixon aliyezikwa kwenye viwanja vya maktaba ya rais vya Yorba Linda huko California na Gerald Ford aliyezikwa kwenye makumbusho yake ya Grand Rapids iliyopo Michigan.

Hata hivyo, John F. Kennedy na Lyndon Johnson hawakuzikwa kwenye maktaba na makumbusho zao zilizopo Boston na Austin. Kennedy aliyeuawa kwa risasi jijini Dallas, Texas, Novemba 22, 1963 alizikwa katika makaburi ya Arlington, ilhali Lyndon alizikwa kwenye ranchi ya familia iliyopo Texas.

Kati ya marais watano wa zamani wanaoishi, Jimmy Carter amekuwa akizungumza mara kwa mara juu ya mahala atakapozikwa akisisitiza kuwa lazima iwe katika mji aliozaliwa wa Plains uliopo Georgia. Maktaba na makumbusho yake ya kirais ipo Atlanta, mji ambao upo mbali na Georgia.

Oktoba, 2017 mtangulizi wa Obama, George W. Bush alitangaza kuwa yeye na mkewe Laura watazikwa kwenye makaburi ya Taifa ya Texas yaliyopo Austin. Baba yake, George H.W. Bush na mkewe Barbara wana eneo lao ndani ya maktaba na makumbusho ya kirais iliyopo Texas A&M University na tayari mkewe Barbara amezikwa katika eneo hilo Aprili 21 mwaka huu.

Kwa upande wa Bill Clinton na mkewe Hillary pia hawajatangaza watakapozikwa, lakini zipo fununu juu ya Washington kuwa ndio mji watakapozikwa na hawajakanusha taarifa hiyo.

Kauli za mabosi wa makumbusho

Mkurugenzi mtendaji wa maktaba na makumbusho ya Harry Truman, Kurt Graham anasema ukweli kwamba eneo hilo lina kumbukumbu nyingi za rais huyo wa zamani, lakini pia kuzikwa kwake hapo kunaamsha hisia zaidi za wageni wanaopatembelea, linaongeza umakini na tafakuri ambayo huwezi kuipata katika maonyesho yoyote duniani.

Truman alizikwa pembeni mwa kaburi la mkewe, Bess ndani ya maktaba hiyo na bintiye na mjukuu wake waliozikwa kando kidogo ya wawili hao.

Katika maktaba na makumbusho za akina Nixon na Reagan, wageni huyachukulia makaburi yao kama maeneo fulani ya matambiko, kukiwa na ukimya mkubwa wawapo sehemu hizo.

Msemaji wa Taasisi ya Reagan, Melissa Giller anasema: “ Sidhani kama wageni hawahisi hisia za ajabu kwa kuwa Rais Reagan na mkewe walizikwa hapa. Hapa wageni siku zote wako kwenye makaburi yao wakitoa heshima na baadhi yao pia huja na maua na kuyaacha juu ya makaburi haya.

Imekusanywa na Kulwa Magwa kwa msaada wa taarifa mbalimbali

Tuesday, April 24, 2018

3:35 PM

Rais Magufuli Awataka Wastaafu Kuiga Mfano wa Mizengo Pinda

 Rais Magufuli Awataka Wastaafu Kuiga Mfano wa Mizengo Pinda
Rais John Magufuli jana alimmwagia sifa Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda kwa kumwelezea ni kiongozi mkimya na asiyependa kuzungumza ovyo ovyo.

Rais Magufuli alisema Pinda, maarufu kama Mtoto wa Mkulima, ni kiongozi anayefaa kuigwa na viongozi wengine, na kwamba hata yeye siku akistaafu atamfuata ili kujifunza.

Aliyasema hayo jana mjini Dodoma wakati akifungua Tawi la Benki ya NMB la Kambarage na Jengo la Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).

“Mzee Pinda anaishi maisha ya kawaida sana, hapigi kelele, hazungumzi chochote, Mzee Pinda ‘you are too special’ (wewe ni mtu wa kipeke),” alisema Rais Magufuli.

“Watu watakukumbuka (Pinda) kwa ukarimu wako, wewe ni mtu wa kawaida sana. Sasa hivi hatujui thamani yako lakini ipo siku tutaijua.

“Ndiyo maana bado unaonekana kijana, hujipi ‘pressure’ (hofu), unaamini kile unachofanya, na mimi nikistaafu nitakuja kuchukua ‘course’ (mafunzo) kwako.”

Sifa kwa Pinda zinakuja miezi saba tangu alipokosoa viongozi wastaafu wa "maeneo mengine" wanaosemasema kila wakati kuhusu uendeshaji wa serikali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Septemba 11, mwaka jana Rais Magufuli alitoa mfano wa majaji wastaafu ambao alisema ni tofauti na wastaafu wengine na kwamba huenda kujua sheria ndiko kunakowasaidia kutokuwa waropokaji.

Rais Magufuli alisema hayo wakati wa kumuapisha Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma.

“Nawashuruku majaji wakuu wastaafu, Barnabas Samatta na Augustino Ramadhani, walifanya kazi kubwa ya kujenga misingi ya mahakama nchini," alisema.

“Bahati nzuri majaji hawa ni waadilifu sana huwezi kumsikia Jaji (Mkuu mstaafu Othman) Chande, (Barnabas) Samatta, Augustino (Ramadhani), (Damian) Lubuva au majaji walioko hapa... ukiangalia wastaafu wa maeneo mengine hawachoki kusema, wanawashwawashwa.

“Ndiyo maana nawapongeza sana mahakama...Ni safi mno, nina uhakika wanapotaka kutoa ‘advice’ (ushauri) yoyote (wowote) lazima wanakushirikisha (Jaji Mkuu); ndiyo faida ya kujua sheria.

“Sisi wengine huku ambao hatujajua sheria mahali popote, chochote unaweza ukazungumza.

Monday, April 23, 2018

11:56 AM

Wabunge watakiwa kuchukua hatua stahiki


Wabunge wa wametakiwa kuchukua hatua stahiki kudhibiti vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vinavyofanywa dhidi ya wanawake na watoto wenye ulemavu katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

Ushauri huo umetolewa mara baada ya kufanyika utafiti uliofanywa na shirika la 'Action On Disability and Development' kwa kushirikiana na shirikisho la watu wenye ulemavu Tanzania kubaini kuwepo kwa vitendo vya udhalilishaji wanawake na watoto wenye ulemavu.

Akiongea na Wabunge katika semina iliyoandaliwa na Shirika la ADD, Mjini Dodoma, Mkurugenzi wa Shirika hilo Bi. Rose Tesha amesema kuwa baadhi ya ndugu na jamaa wamekuwa wakishiriki vitendo hivyo hususani kwa watoto wenye ulemavu wa kusikia na akili.

Wakitoa maoni yao katika Semina hiyo baadhi ya wabunge wametaka sheria iweze kurekebishwa ili mfuko wa jimbo pia uweze kuwahudumia watu wenye ulemavu huku wengine wakitaka uboreshaji wa miundombinu kwa watu wenye ulemavu.

Friday, April 20, 2018

1:22 PM

Comey: Hakuna Kiongozi anayeweza kumbadili tabia Rais TrumpAliyekuwa mkuu wa FBI nchini Marekani, James Comey ameiambia BBC kuwa haamini kuna kiongozi yoyote wa karibu na Rais wa Marekani Donald Trump anaweza kumbadilisha tabia yake,
Anasema tabia zake zinahatarisha hadhi ya nchi.

Kabla ya kufukuzwa na Trump Comey aliongoza uchunguzi dhidi ya kuhusika kwa Urusi katika uchaguzi wa Marekani.

Akizungumza katika kipindi cha Newsnight Comey anasema tabia za Trump zinaathiri wale wanaomzunguka.

"Nadhani tabia yake inaathiri hasa hasa kwenye suala la ukweli na jambo la msingi ni jinsi tabia hizo zinavyoathiri taasisi na watu wa karibu wake.Ana tabia a kuongea uongo na kuwa lazimisha wale wanamuunga mkono kukubalina naye na kuamini"

Trump alimshutumu Comey kuwa anayoyazungumza na uongo na siasa zake za ubaguzi.
1:13 PM

Serikali Yamjibu Zitto Kabwe Upotevu wa Trilioni 1.5 Zilizotajwa na CAGSerikali kupitia Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashantu Kijaju, imetolea ufafanuzi tuhuma za upotevu wa pesa takriban trilioni 1.5 zilizotajwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali. (CAG) kwenye ripoti yake.


Akisoma taarifa rasmi Bungeni Dkt, Kijaju amesema kwamba serikali sasa hivi inatumia mfumo mpya wa mahesabu wa kimataifa 'epses acrual', ambao unaweka uwazi mahesabu yote, na umeleta mafanikio makubwa kwa serikali.

Dkt. Kijaju ameendelea kwa kusema kwamba pesa hiyo ilikuwa haijajumuishwa matumizi yake wakati CAG anafanya na kukamilisha mahesabu yake, hivyo hakuna pesa ambayo imepotea bila matumizi yenye taarifa.

“Matokeo ya utekelezaji wa mpango mkakati wa uandaaji wa mfumo wa epses acrual excess accruals umeiwezesha serikali na taasisi zake kutoa taarifa za kina, na zinazoonyesha uwazi na uwajibikaji wa taasisi husika, hususani katika usimamizi wa mali, na madeni ya taasisi, kuongezeka kwa uwazi kumewawezesha watumiaji wa hesabu kupata taarifa zinazowasaidia kufanya maamuzi sahihi, na kwa wakati”, amesikika Dkt. Kijau kwenye taarifa hiyo.

Dkt. Kijaju ameendelea kwa kufafanua kwamba ..”Kutokana na matumizi ya mfumo wa huu viwango vya kimataifa vya uhasibu katika sekta ya umma, napenda kuliarifu Bunge lako tukufu na Watanzania kwa ujumla kwamba hakuna fedha taslim ya shilingi trilioni 1.51 iliyopotea, au kutumika kwa matumizi ambayo hayakuidhinishwa na Bunge, hivyo basi madai ya baadhi ya watu wasioitakia mema taifa letu na serikali yetu ya awamu ya tano, hayana msingi wowote wenye mantiki”.

Taarifa hiyo iliyosomwa na Dkt. Kijaju imesema kwamba taarifa ya CAG imeeleza jumla ya mapato yote ya serikali, kwa mwaka 2016/17, yalikuwa shilingi trilioni 25.3 ambapo fedha hizi zinajumuisha mapato ya kodi, mapato yasiyo ya kodi, mikopo ya ndani na nje, pamoja na misaada na mikopo nafuu kwa mashirika ya maendeleo. Kati ya mapato haya ya 25.3 yalikuwepo pia mapato tarajiwa, kama mapato ya kodi, jumla ya shilingi bilioni 687.3 pamoja na mapato yaliyokusanywa kwa niaba ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya jumla ya shilingi bilioni 203.92.

“Katika uandishi wa taarifa za ukaguzi CAG alitumia taarifa za hesabu na nyaraka mbali mbali ikiwa ni pamoja na taarifa za utekelezaji wa bajeti ambapo hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2017, mapato yalikuwa jumla ya shilingi trilioni 25.3 na matumizi yalikuwa shilingi trilioni 23.79, matumizi haya hayakujumuisha shilingi bilioni 697.85 zilizotumika kulipa dhamana za hati fungani za serikali zilioiva,. Matumizi haya yalikuwa hayajafanyiwa uhamisho wakati ukaguzi unaofanyika, hivyo basi, baada ya kufanya uhamisho jumla ya matumizi yote kwa kutumia ridhaa za matumizi yalikuwa shilingi trilioni 24. 4, kutokana na ufafanuzi huo shilingi trilioni 1.51 zilizodaiwa kutoonekana kwenye matumizi ya serikali yalitokana na mchanganuo ufuatao (angalia katika picha) ”, alisikika Dkt. Kijaju akilielezea Bunge.

Dkt. Kijaju alihitimisha tarifa hiyo akisema kwamba “Napenda kuhitimisha kwamba serikali kupitia wizara ya fedha na mipango imepata mafanikio makubwa sana kwa kutumia mfumo huu wa kimataifa, napenda kulitaarifu Bunge lako na wananchi kuwa serikali ya awamu ya tano ipo makini na haiwezi kuruhusu kwa namna yoyote ile upotevu wa fedha za umma”.

Wednesday, April 18, 2018

4:01 PM

Mh. Zitto Kabwe amjibu Polepole


Humprey Polepole Amshukia Zitto Kabwe Ripoti ya CAG..Adai Hakuna Hela yoyote Iliyopotea, Amtaka Arudi Shule
Baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole kumtuhumu Mhe. Zitto Kabwe kupotosha taarifa za CAG kuhusu kupotea kwa shilingi trilioni 1.5, kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo ameibuka na kujibu mapigo.
Zitto ametumia mtandao wa Twitter kujibu tuhuma hizo za Polepole kwa kumwambia amekuwa Mwenyekiti wa PAC/POAC kwa miaka nane hivyo anafahamu kile anachokisema.
“Serikali ya CCM ilidhani Watanzania ni mandondocha,wanapelekwa pelekwa tu. Nimekuwa Mwenyekiti wa PAC/POAC kwa miaka 8. Ninajua ninachosema.” ameandika Zitto.
“Jumla ya TZS trilioni 1.5 hazina maelezo ya matumizi yake Katika mwaka 2016/17. Sitajibishana na Mwenezi wa CCM, yeye size yake @AdoShaibu,” ameongeza
2:10 PM

Humprey Polepole Amshukia Zitto Kabwe Ripoti ya CAG..Adai Hakuna Hela yoyote Iliyopotea, Amtaka Arudi Shule


Kuna mtu mmoja anaongoza kwa upotoshaji juu ya ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Chama chake kina mbunge mmoja tu wa ACT Wazalendo. Sijui kasoma shule gani huyu. Kaja anasoma juu juu tu eti trillion 1.5! Ana bahati ndugu Magufuli ni mpole ila tushamwambia mwaka 2020 akatafute kazi ya kufanya. Pia arudi shule akasome kwani hakuna hata shilingi moja iliyopotea - Humprey Polepole
9:41 AM

Jecha Salim Jecha Ang'atuka Tume ya Uchaguzi Zanzibar


Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha amemaliza muda wake wa majukumu ya tume hiyo kwa kipindi cha miaka mitano kilichoanzia Aprili 30,2 013 hadi Aprili 29, 2018 ambapo yeye na wajumbe wa tume hiyo wamekabidhi ripoti yao ya kazi.

Akitoa taarifa yake kwa Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Jecha amesema kuwa tume inaamini kwamba, mafanikio yaliyopatikana wakati wa utekelezaji wa majukumu yake hasa ya kiuchaguzi yalitokana na ushirikiano wa wadau mbalimbali na wananchi kwa jumla.

"Ndani ya miaka mitano tume imeweza kuendesha jumla ya chaguzi ndogo nne, zikiwemo chaguzi ndogo tatu za Udiwani na chaguzi moja ya uwakilishi pamoja na kusimamia uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25,2015 na ule wa marudio yake Machi 20, 2016. Tume imefanya mapitio ya majimbo ya uchaguzi na kubadilisha mipaka ya majimbo ya uchaguzi, majina ya majimbo na kuongeza idadi ya majimbo kutoka 50 hadi 54", ameeleza Jecha.

Pamoja na hayo, Jecha ameendelea kwa kusema "Tume imeweza kufanya uandikishaji wa wapiga kura kwa awamu mbili na kuliendeleza daftari la kudumu la wapiga kura sambamba na kuendesha programu mbalimbali za elimu ya wapiga kura kupitia vyombo vya habari, mikutano ya wadau, uchapishaji wa vipeperushi, majarida na makala mbalimbali".

Aidha, Mwenyekiti huyo amemueleza Dkt. Shein kuwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imechaguliwa kuwa kiongozi wa Uchaguzi Mkuu wa nchini Congo utakaofanyika mwezi Disemba mwaka huu.

Kwa upande wake, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein ameipongeza Tume hiyo kwa kutekeleza vyema majukumu yake ndani ya miaka mitano kwa kuendesha chaguzi zote .

"Tume hii inastahiki pongezi kwa kuifanikisha vyema kazi waliyopewa ikiwa ni pamoja na kuendesha chaguzi zote ukiwemo uchaguzi Mkuu, chaguzi ndogo na ule uchaguzi wa marudio ambazo zote hizo zilifanywa kwa ufanisi mkubwa", amesema Dkt. Shein.

Wajumbe wa tume hiyo ambao wamemaliza muda wao ni Mwenyekiti mwenyewe Jecha Salim Jecha, Jaji Abdul-hakim Ameir Issa, Balozi Omar Ramadhan Mapuri, Nassor Khamis Mohammed, Ayoub Bakari Hamad, Haji Ramadhan Haji na Salmin Senga Salmin ambao wote hao waliapishwa rasmi  Mei,4, 2013. 
9:39 AM

Dada Aliyedai nini Mtoto wa Mzee Edward Lowassa na Kuwa Ametelekezwa Akamatwa na PolisiKamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema wanamshikilia Fatuma Chikawe kwa tuhuma za kudanganya kuwa ni mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa.

 Hii ni wiki moja baada ya Fatuma kujitokeza kwenye vyombo vya habari na kudai ametelekezwa na Lowassa kwenye zoezi la kusikiliza malalamiko ya wanawake waliotelekezewa watoto linaloendeshwa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ambaye alisisitiza wahusika watoe taarifa za ukweli. 

Monday, April 16, 2018

Friday, April 13, 2018

8:59 AM

VIDEO## MSIGWA: Prof Kitila Kakazana Kujibu Maaskofu, Kasahau Kazi Yake


MSIGWA BUNGENI: "Prof Kitila Mkumbo Kakazana Kujibu Maaskofu, Kasahau Kazi Yake" Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, amesema tukitaka kujenga taifa lenye nguvu ni lazima kuwepo na hoja zinazokinzana. Aidha, Mch Msigwa, amedai kuwa , Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo, ni kama amesahau kazi yake na badala yake kutumia muda mwingi kuwajibu maaskofu. lnstal GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpubli..
  

Wednesday, April 11, 2018

5:07 PM

Msigwa Amvaa Jerry Murro Sakata la Kutelekeza Mtoto "Ni Tuhuma Alizotengeneeza Jerry Murro"

 .
Mbunge wa Iringa mjini kupitia tiketi ya Chadema, Mch. Peter Msigwa amezidi kukana madai ya kumtelekeza mtoto na kueleza kuwa taarifa hizo zinaenezwa na Jerry Muro.

Akizungumza na EATV, Mch. Msigwa amesema kuwa madai hayo hayana ukweli wowote na kueleza iwapo lisemwalo lipo basi muhusika amtafute katika namba aliyoitoa na ikishindikana amfuate Bungeni.

“Mimi nitamtambuaje huyo mtoto, hiyo picha wameweka tu, ilipoanzia ni kwa Jerry Muro ndio ameanza kusambaza hizo habari kwamba mimi ni mwanamke aliyeenda kwa Makonda amejieleza ndio nimemuacha,” amesema Mch. Msigwa.

“Ninachokijibu pale, nakijibu kitu ambacho ameanzisha Jerry Muro, kwamba kuna mtu nimemtelekeza amekuwa akinitafauta na nimekuwa nikimzuia, nimejibu kwamba kama huyo mtu huyo yupo nimekuwa nikitoa namba zangu za simu na kama sipatikani aje hapa Bungeni,” amesisitiza.

Kuanzia mwanzo mwa wiki hii mamia ya wanawake walijitokeza ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ili kupata msaada wa kisheria baada ya kutelekezwa na wazazi wenzio. Pia RC Makonda ametoa nafasi ya kuwasikiliza wanaume waliotelekezwa na wake zao ambapo watapatiwa msaada wa kisheria. 

Saturday, April 7, 2018

12:33 PM

Rais Magufuli Atoboa Siri Alipokutana na Mkewe "Nyumba za Kota za Polisi Zimenipa Mke Janeth’'

Rais Magufuli Atoboa Siri Alipokutana na Mkewe "Nyumba za Kota za Polisi Zimenipa Mke Janeth̢۪'

“Nyumba za polisi ndizo zimenipa mke kwa hiyo nyumba za polisi ninazifahamu, huyu mke wangu niliye naye alikuwa mtoto wa polisi, marehemu baba yake hakuwa na cheo kikubwa alifariki akiwa sajenti,” ni maneno ya Rais Magufuli akizindua nyumba za askari Arusha nakukiri kuwa Janeth alimpata kwenye nyumba za kota.

Ameyazungumza hayo leo April 7, 2018 wakati wa uzinduzi wa nyumba 31 za polisi na kusema baba mkwe wake alikuwa sajenti wa polisi.

“Nyumba za polisi ndizo zimenipa mke kwa hiyo nyumba za polisi ninazifahamu, huyu mke wangu niliye naye alikuwa mtoto wa polisi, marehemu baba yake hakuwa na cheo kikubwa alifariki akiwa sajenti,” -Rais Magufuli

 “Ingekuwa nazindua Moshi, angenionyesha nyumba walizokaa lakini za Oysterbay alizoishi alishanionyesha na za Ukonga na za sehemu nyingine. Kwa hiyo maisha ya polisi ninayafahamu.” -Rais Magufuli 

Friday, April 6, 2018

9:23 PM

Rais akataa kujisalimisha kwa PolisiAliyekuwa Rais wa Brazil Luis Inácio Lula da Silva amegoma kujisalimisha kwa polisi kama alivyotakiwa na mahakama ya nchi hiyo hii leo, ili aanze kutumikia hukumu yake.

Rais huyo ambaye alishtakiwa kwa makosa ya rushwa na kuhukumiwa kwenda jela miaka 12, alikuwa nje kwa dhamana, na mahakama ilimtaka aende mwenyewe kwani sio busara kwenda kumkamata Rais Mstaafu.

Rais Da Silva amesema mahakama hiyo ina lengo la kumuharibia mipango yake ya kugombea urais hapo Oktoba mwaka huu, huku akiwa na matumaini makubwa ya kushinda uchaguzi kutokana na kutajwa kuwa kipenzi cha watu.

Mamia ya watu wamezunguka eneo la umoja wa wafanyakazi, ambalo lipo karibu na eneo analoishi kiongozi huyo.