Breaking

Showing posts with label . burudani. Show all posts
Showing posts with label . burudani. Show all posts

Sunday, June 3, 2018

9:09 AM

Koffi Olomide akamatwa kwa Unyanyasaji wa KingonoMahakama nchini Ufaransa imetoa hati ya kukamatwa kwa Mfalme wa muziki aina ya Rumba raia wa DRC Koffi Olomide ambaye anadaiwa kushambulia kingono na kuwapiga wachezaji wake wanne wakiwa Paris kati ya mwaka 2002 na 2006.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 61 aliondolewa nchini Ufaransa mwishoni mwa mwezi Januari kufuatia madai ya unyanyasaji aliyotekeleza nchini Ufaransa.
Wachezaji wake wanne wameeleza kuwa walilazimishwa kufanya ngono mara kadhaa wakiwa Drc au ziarani huku wakitaja walipokuwa ufaransa walifungiwa chumbani kwa saa 24 chini ya ulinzi wa wanaume watatu katika kitongoji kimoja jijini Paris.
Wachezaji hao wameeleza mara kadhaa kulazimishwa kufanya ngono bila kutumia kinga hotelini lakini pia studio ambapo walipigwa pale walipokataa.
Kwa mujibu wa walalamika wamedai kufanya matakwa ya mwanamuziki huyo baada ya kutishiwa kukosa kibarua,madai ambayo yanadaiwa kusemwa na wachezaji wake wote wakike.

Saturday, June 2, 2018

1:26 PM

Nay wa Mitego aisifia ngoma mpya ya DiamondRapper Nay wa Mitego ametoa neno katika ngoma mpya ya Diamond Platnumz ya ‘Iyena’ amesema hata angetupa ngoma hiyo barabarani inge – hit tu.

Ney amesema kuwa licha ya kwamba ngoma kali yupo na mzazi mwenzie mwenye nyota na mafanikio, Zari The Bass Lady, amemtaka msanii huyo aendelee kupuyanga na wachafua nyota.

“Mzee Mwenzangu Diamond platnumz Hii Ngoma Iyena Ata Ungeenda Kuacha Tu Barabarani Ukajifanya Kama Umeitupa Inge Hit Tu. Licha Ya Kwamba Ngoma Kali Pia Upo Na Mkeo Original Mama Tee Mwenye Nyota Ya Hela Na Mafanikio. Sasa Wewe Endelea Kupuyanga Na Hao Mapugi Machafua Nyota. Nitaongea Na Mama Tee Yaishe Tu.(Yamoyoni) Haya Fanya Muende YouTube,” ameandika Nay wa Mitego kupitia mtandao wake wa Instagram.

Hata hivyo utakumbuka miaka mitano iliyopita Diamond na Nay wa Mtego walitoa hits iliyokwenda jina la Muziki gani, hata hivyo hawakuishia hapo baadaye walitoa nyimbo nyingine inaitwa ‘Mapenzi Pesa’.

Saturday, May 5, 2018

8:35 AM

Watu wa Dodoma na mikoa jirani msikose kumsiliza Jeniberth Alberth kupitia radio maisha


Watu  wa  Dodoma na  mikoa  ya  jirani  msikose  kusikiliza kipindi cha   #USHIKWAPO SHIKAMANA Kipindi ambacho kinawalenga hasa vijana changamoto,fulsa,maendeleo,na mambo mengine wanayo kumbana nayo katika kuzifikia ndoto zao kinachoongozwa na mtangazaji mwenye kipaji Jeniberth Alberth 

  #USHIKWAPO SHIKAMANA  kipo  kwanzia  jumatatu  mpaka  Alhamisi  Muda  ni  saa  kumi jioni  mpaka saa  kumi mbili  jioni  
   #USHIKWAPO SHIKAMANA ni kipindi bora kinachoongozwa na Jeniberth Alberth mtangaji  mwenye  uwezo  mkubwa wa  kutanganza kupitia  radio  Maisha  Dodoma ...

Image may contain: 1 person

Thursday, May 3, 2018

7:29 AM

Wema Sepetu Afunguka Sababu Iliyomfanya Kutoudhuria Harusi ya Alikiba

Wema Sepetu Afunguka Sababu Iliyomfanya Kutoudhuria Harusi ya Alikiba

Msanii wa Filamu Bongo, Wema Sepetu amefunguka sababu ya kutohudhuria kwenye harusi ya msanii Alikiba.

Mrembo huyo amesema harusi ya Alikiba iligongana na birthday ya mdogo wake hivyo akashindwa kwenda kwani anaiweka familia yake mbele kwanza.

“That because ile ni siku ambayo nilimfanyia mdogo wangu birth day party, mdogo wangu alikuwa anatimiza miaka 20 mwaka huu. Kwa hiyo mwaka jana sikumfanyia chochote mwaka huu nikawa nimemuhaidi i will do the party,” amesema.

“So family first na Alikiba anajua mimi namsapoti mwisho wa siku sina kinyongo chochote namtakia kila la kheri kwenye maisha yake ya ndoa,” Wema ameiambia Bongo5.

Utakumbuka April 19, 2018 Msanii Alikiba alifunga ndoa na mpenzi wake mjini Mombasa nchini Kenya na April 29, 2018 walifanya sherehe ya pili Dar es Salaam. 

Sunday, April 29, 2018

12:34 PM

Mzee Majuto arudishwa Muhimbili, wiki ijayo kupelekwa India

Msanii wa Filamu nchini, Mzee Majuto amerudishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo awali alikuwa akipatiwa matibabu kabla ya kuhamishiwa hopitali ya binafsi, Tumai
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa serikali imeamua kumrudisha Hospitali ya Taifa ili kufanyiwa vipimo upya kujua kinachomsumbua.

“Wakati akisubiri kusafiri kwenda nje ya nchi (India) kati ya Jumatatu na Jumanne kwa ajili ya matibabu tumeamua tumuhamishie kwanza Muhimbili ili afanyiwe vipimo zaidi, lakini niwaambie mashabiki wake na Watanzania kwa ujumla kuwa Mzee Majuto anaendelea vizuri,” amesema Dkt. Mwakyembe.
Hapo jana April 27, 2018 Bungeni wakati ukiendelea mjadala wa bajeti ya
Wizari ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka 2018/19, Dkt. Mwakyembe alisema ameunda kamati ya wanasheria ili kupitia matangazo yote ya kibiashara aliyofanya msanii huyo ili kubaini iwapo anaibiwa kwani kwa sasa anategemea michango ili kufanikisha matibabu yake

Saturday, April 28, 2018

5:25 PM

Waziri Shonza Afunguka Kuhusu Kufungiwa kwa 'Mwanaume Mashine'

Waziri Shonza Afunguka Kuhusu Kufungiwa kwa 'Mwanaume Mashine'

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema wimbo wa Mwanaume Mashine haujafungiwa.

Ametoa kauli hiyo leo jioni Aprili 27, 2018 baada ya leo mchana Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu kuhoji sababu za kufungiwa kwa wimbo huo.

Shonza ametoa kauli hiyo wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha bajeti ya wizara hiyo mwaka 2018/19 baada ya Zungu kutaka kupewa jibu kuhusu ‘Mwanaume Mashine’ kutokana na maelezo ya Shonza na Waziri wa wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe wakati wanajibu hoja za wabunge kuhusu bajeti hiyo kutoeleza sababu za kufungiwa kwa wimbo huo.

Mchana Zungu alihoji kufungiwa kwa wimbo huo wakati unamtaja mchezaji mahiri wa Simba.

Bunge limepitisha Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mwaka 2018/19 

Thursday, April 26, 2018

11:12 AM

Steve Nyerere Kuwachangisha Wasanii Kumsafirisha Mzee Majuto Kwaajili ya Matibabu India

Steve Nyerere Kuwachangisha Wasanii Kumsafirisha Mzee Majuto Kwaajili ya Matibabu India

Wasanii wa filamu nchini Tanzania wakiwakilishwa na Steve Nyerere pamoja na Aunt Ezekiel Jumatano hii wamemtembela muigizaji mkongwe nchini, King Majuto, ambaye amelazwa katika Hospitali ya Tumaini iliyopo Upanga Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kumjulia hali hospitalini hapo Mwenyekiti wa Wasanii, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’, amesema kutakuwa hakuna haja ya wasanii hao kutoa michango mikubwa mara tu, mzee Majuto atakapopoteza maisha, kwahiyo wamejipanga na kumtafutia tiketi mbili ili aweze kwenda India kupata matibabu. 

Tuesday, April 24, 2018

3:42 PM

Yul Edochie atangaza kugombea Urais 2019muigizaji wa filamu wa Nigeria Yul Edochie ambaye pia ni mtoto wa muigizaji maarufu na mkongwe wa nchini humo Pete Edochie, ametangaza kugombea urais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi ujao mwaka 2019.

Yul ametangaza uamuzi huo leo hii kupitia ukurasa wake wa twitter, akisema kwamba umefika wakati sasa wa kusitisha uongozi mbaya wa viongozi waliopo kwenye nchi hiyo.

“Leo natangaza malengo yangu ya kugombea Urais wa nchi hii bora zaidi duniani Nigeria, nchi iliyobarikiwa iliyoumizwa kwa miongo kadhaa na viongozi wabaya. Inatosha!! Wanaigeria wenzangu, simameni na mimi, tufikishe matatizo yetu kwenye kituo cha mwisho cha basi”, ameandika Yul Edochie.

Azimio lake limeonekana kuvutia sana vijana ambao walihukumu taarifa ya Rais Muhammadu Buhari katika Mkutano wa Biashara wa Jumuiya ya Madola, akisema vijana wengi wa nchi hiyo ni wavivu.

Yul alishawahi kugombea ugavana wa jimbo la Anambra mwaka 2017, lakini alishindwa na safari hii kutangaza nia kwenye nafasi hiyo kubwa ya uongozi wa nchi.

Nigeria inatarajia kufanya uchaguzi mkuu wa Urais mwaka 2019 huku Rais wa sasa wa nchi hiyo Muhammadu Buhari akitarajiwa kugombea, licha ya misukosuko mingi na lawana anazopewa na Wanaigeria kwa kuyumbisha uchumi wa nchi hiyo\

Monday, April 23, 2018

11:55 AM

Mzee Gelard: Agness aliniaga kabla ya kifo chakeMZEE Gerald Waya, ambaye ni baba mzazi wa aliyekuwa Msanii wa Bongo Movies na Model, Agness Gerald  ‘Masogange’, amesema mwanaye alikuwa nguzo kubwa katika maisha yake, hivyo kifo chake ni pigo kubwa kwake na familia nzima.

Akizungumza nyumbani kwake Mbalizi II wilayani Mbeya, leo Aprili 22, 2018 Mzee Waya amesema Masogange ni mtoto wanne katika familia yake ya watoto sita, wa kike wakiwa watano. Amesema Masogange alisoma Shule ya Msingi Utengule-Mbalizi na sekondari ya Sangu alikoishia kidato cha pili.

Waya amesema Masogange alipata matatizo hivyo akalazimika kuacha shule. Hata hivyo amesema hataki kuzungumzia mambo mabaya wakati huu anapoomboleza kifo cha mwanaye.

 “Aliishia form two (kidato cha pili), akapata matatizo ikabidi aache shule. Tulikosana kidogo lakini tukayamaliza yeye akaenda Dar es Salaam,” amesema.

Waya amesema, “Mwanangu alikuwa nguvu kwangu, alikarabati nyumba hii ninayoishi kwa sasa na nilikuwa nafarijika sana, lakini leo kusikia msiba huu kwa kweli inaniuma sana.”

Amesema Masogange alimpigia simu, “Tukaongea naye akaniambia ‘mimi baba ninaumwa’. Nikamuuliza nini tatizo akasema, “aah!   baba niombee tu kwa Mungu’. Na Jumamosi iliyopita nilimpigia simu wakati yupo hospitali kujua maendeleo yake lakini akaniambia ‘baba byee’.  Nikaanza kulia, na hapo sikuwasiliana naye tena hadi nilipopata taarifa za kifo chake,” amesema.

Saturday, April 21, 2018

11:19 AM

Tumependekeza Masogange Aagwe Leaders, Azikwe Mbeya- Steve Nyerere

Tumependekeza Masogange Aagwe Leaders, Azikwe Mbeya- Steve Nyerere
KIONGOZI wa Chama cha Wasanii Nchini, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ametoa taarifa rasmi ya chama hicho yenye mapendekezo kwa familia kuhusu taratibu za msiba wa msanii mwenzao, Agnes Gerard Masogange ambaye alifariki dunia jana jioni katika Kituo cha Huduma za Afya cha Mama Ngoma kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam.Akizungumza na wanahabari mara baada ya kikao cha wasanii uliofanyika Leaders Club jana usiku, Steve alisema wao kama wasanii wameridhia kila mmoja kutoa mchango wake wa pesa kwa ajili ya kufanikisha shughuli ya msiba na mazishi ya Masogange.Pia, amesema wameridhia na kupendekeza mwili wa Masogange uagwe katika Viwanja vya Leaders kesho Jumapili, Aprili 22, 2018 na kuzikwa nyumbani kwao mkoani Mbeya ili wasanii, mashabiki na Watanzania wapate fursa ya kumsindikiza katika safari yake ya mwisho.Aidha, Nyerere alisema mapendekezo hayo watayafikisha kwenye familia ya marehemu huku akiwashukuru wote waliojitoa kuchangia na kuwapa pole wasanii wakiwemo viongozi wa Serikali na Watanzania kwa ujumla. 
11:16 AM

Rammy Galis afunguka haya kuhusu kifo cha Masogange


Muigizaji Rammy Galis ni moja kati ya mastaa wa Bongo walionyesha kuguswa na kifo cha Agnes Masogange ambaye ni mpenzi wake wa zamani, Rammy Galis ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika ujumbe ambao umemuumiza kutokana na taarifa hizi.

“Mkono umekuwa mzitoo hata kuandika maumivu niliyonayoo naona nashindwa . Dunia tambara mbovu , unadeki salama mchana usiku unakua mmbovu umenifunza mengi niliyokua siyajui , ulisema nishkuru mungu watu wakikupenda kwani adui haumjui”

“Miezi 11 tumeishi nashkuru ulinipeleka kupima ( Palestina ) , Nilitokwa na jasho ukanicheka ukaniambia huwez nipenda kama nikikataa kupima magazeti ya udaku walipotaka sababu sikuweza kuweka tofauti zetu hadharani kwani bado moyoni niliamini ipo siku Tungeweza Kumuepusha shetani . Tulikesha Usiku Na Mchana ili Ucheze Filamu Yetu Kwa hisia ” Ukasema Hii Iwe Kumbukumbu Yako Kama Niliwahii Hata Kwenye Kazi Zako Kukusaidia”

“Sasa kwanini filamu yetu tulitunga jina liitwe #HUKUMU ? Ilikuwaje Story ya filamu mwisho unafariki ? kwani tulikua tunatungia iwe kweli Hukumu yako ???? Mungu ndio hakimu wa viumbe vyote katika dunia , umeondoka ghafla sanaa , Na hii pia ni funzo umeniachia #PumzikaSalama #MileleNakuombea#RIPLOVE😢”

Marehemu Agness Masogange enzi za uhai wake aliwahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na muigizaji Rammy Galis kwa kipindi kifupi kinachotajwa kufikia miezi 11 lakini baadae walachana na kutotaja sababu ya kuachana kwao.

Friday, April 20, 2018

10:56 PM

Diamond, Wema Sepetu, Steve Nyerere wamlilia AGNESS MASOGANGELeo April 20,2018 simanzi kubwa imetawala kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva kupoteza video vixen maarufu Agnes Gerald “Masogange” na kwa upande wa mastaa ambao wameonyesha kuguswa na msiba huu ni pamoja na wanamuziki na waigizaji akiwemo Wema Sepetu, Diamond Platnumz,  Steve Nyerere, na wengine.

Aslay Isihaka ameweka picha ya Masongange na kuandika, “Dah mbele yako nyuma yetu sister, safari yetu moja innalillah wainnailah raajiun,”

Huku Naseeb Abdul maarufu ‘Diamond Platnum’ akiweka picha ya mishumaa na maneno, “Rest in paradise Agnes.”

Rajab Kahali ‘Harmonize’ ameweka picha ya Masongange na kusema, “God’s plan  R.I.P. Aggy.

Naye Steven Mengere 'Steve Nyerere’ ameweka picha tatu tofauti za Masogange na kuzungumzia kifo hicho akianza kwa kusema;

“Nimepokea taarifa ya kifo chako kwa mshtuko mkubwa sana. Masogange amka mama Masogange. Staki kuamini.”

Mcheza filamu, Wema Sepetu ameweka picha ya Masongange ikiambatana na maneno, “Innah lillah wa innah illah rajiun... Dah...! 
7:38 AM

Diamond: Mpeni salamu zangu King KibaTarehe April 19, 2018 msanii Alikiba ameoa, mshindani wake kimuziki Diamond Platnumz hajakaa kimya kwenye hilo.

Diamond amefunguka kuwa amepewa taarifa za Alikiba kuoa siku ya leo, hivyo amemtumia salamu na kumtakia maisha mema ya ndoa. Kupitia ukurasa wake wa Intagram tumegulia kile alichogusia kuhusiana na ndoa ya Alikiba;

“Wadau Nimeambiwa King Kiba kaoa leo, mpeni Salam zangu za ndoa njema na Maisha yanye Furaha, Amani na Baraka tele,” amesema Diamond.

Msanii Alikiba amefunga ndoa na mpenzi wake  Aminah Rekish asubuhi ya leo mjini Mombasa nchini Kenya. Pia Utakumbuka Diamond alishaweka wazi mipango yake ya kuoa mwaka huu  

Wednesday, April 18, 2018

3:51 PM

Daimond Alikologa Basata Nao Wamwita .... Aripoti na Mameneja WakeMsanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz leo, April 18, 2018 amefika ofisi za Baraza la Sanaa Taifa (BASATA).

Muimbaji huyo wa ngoma ‘African Beaut’ amefika ofisi za Basata akiongoza na mameneja wake, Sallam SK, Mkubwa Fella pamoja na msanii Harmonize.

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa Diamond ameitwa na Baraza hilo kwa lengo la kukumbushwa masuala mbalimbali kuhusiana na muziki wake.

Wiki tatu zilizopita March 23, 2018 Diamond pamoja na meneja wake walifika Basata hata hivyo pande zote mbili hazikuweka wazi kile kilichojadiliwa baina yao. Hata hivyo safari hiyo ilijiri katika kipindi ambacho nyimbo mbili za Diamond ‘Waka na Hallelujah’ zilipofungiwa. 
2:08 PM

Ndoa ya Alikiba Yapanda Moto Ndugu na Rafiki wa Karibu Waanza Kutua Mombasa

Ndoa ya Alikiba Yapanda Moto Ndugu na Rafiki wa Karibu Waanza Kutua Mombasa
Ujio wa ndoa ya Alikiba kwa sasa ndio imeteka vichwa vya habari mjini.

Tayari maandalizi muhimu yameonekana kuanza kukamilika huku watu wa karibu wa msanii huyo wameonekana kuanza kutua mjini Mombasa, Kenya kwa ajili ya kuhudhuria ndoa hiyo.

Baadhi ya picha tayari zimeanza kusambaa mitandaoni zikiwaonyesha watu hao akiwemo msanii wa filamu Bongo, Esha Buheti na dada yake Alikiba, Zabibu na wengine.


Wakati huo huo Abdu Kiba ameweka moja ya picha hizo kwenye mtandao wa Instagram na kuandika ujumbe unaosomeka, “MY TEAM 💣💣💣💣 Mombasa kitaelewekaa tu.”

Alikiba anatarajiwa kufunga ndoa na mrembo Aminah Rikesh April 26, 2018 katika ukumbi wa Diamond Jubilee uliopo mjini Mombasa. 
1:59 PM

Ratiba ya ndoa ya Alikiba yaanikwa


Muimbaji nguli wa nchini Tanzania, Alikiba amesafiri pamoja na familia yake Jumanne hii (April 17, 2018) kuelekea mjini Mombasa nchini Kenya kwaajili ya kufunga ndoa na mpenzi wake, Aminah Rikesh itayofanyika April 26, 2018 katika ukumbi wa Diamond Jubilee wa nchini humo.

Taarifa za ndoa yake ziligubikwa na usiri mkubwa hali ambayo ilivifanya vyombo vingi vya habari nchini Tanzania na Uganda kuandika tetesi za ndoa hiyo huku vingine vikienda mbali zaidi kwa kudai ndoa hiyo ilishafungwa.

Bongo5 iliamua kulivalia njuga suala hili ili kutafuta ukweli wa ndoa hiyo ndipo ukweli ulipobainika kwamba muimbaji huyo anafunga ndoa April 26, 2018 na siku ya jana amesafiri pamoja na familia yake kwenda Mombasa Kenya.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha uhakika, ndoa hiyo itarushwa live na kituo cha runinga cha Azam TV baada ya kukunua hali ya kurusha ndoa hiyo kwa kiasi kinachodaiwa ni zaidii ya milioni 100 za Tanzania.

Baada ya kumaliza kwa ndoa hiyo nchini Kenya, Muimbaji huyo atafanya sherehe nyingine nchini Tanzania wiki moja baada ya ndoa ya awali.

Chanzo hicho kimedai ndoa hiyo itagharimu mamilioni ya hela kutokana na maandalizi pamoja na deal hilo la Azam.
9:59 AM

Diamond kuhojiwa tena Polisi

Baada ya hapo jana April 16, 2018 msanii Diamond kuhojiwa na Polisi kufuatia kusambaza video zisizo na maadili mtandaoni, msanii huyo anatarajiwa kuhojiwa tena.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kushikiliwa kwa Diamond hapo jana kwa ajili ya mahojiano ila sasa ameachiwa kwa dhamana wakati uchunguzi zaidi unaendelea na utakapokamilika ataitwa tena polisi kwa mahojiano.
Taarifa za kuhojiwa Diamond na Polisi simesikika kwa mara ya kwanza leo Bungeni ambapo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe alisema Polisi walimkamata Diamond hapo jana, pia aliangiza msanii Nandy nae ahojiwe.
Hapo Juzi April 15, 2018 Diamond aliweka video mbili mtandaoni zisizo na maadili akiwa na wanawake wawili tofauti. Kabla ya hilo ilivuja video mtandaoni ikimuonyesha msanii Nandy akiwa faragha na msanii mwenzie, Bill Nass.

Tuesday, April 17, 2018

10:20 AM

Msanii Naseeb Abdul (Diamond) akamatwa na Polisi kwa kusambaza picha za faragha, Nandy naye ahojiwa

Mwakyembe amesema kuna baadhi ya wasanii ambao walianza kufanya uhuni ndani ya mitandao akiwemo mwanamuziki nyota wa muziki, Diamond ambae tayari amekamatwa na Jeshi la Polisi na anahojiwa kutokana na picha alizozungusha.

Pia Mwakyembe amesema pia imebidi binti Nandy naye akamatwe kisha kuhojiwa na wanaangalia namna ya kuwapeleka mahakamani.

Mwakyembe ametoa wito kwa vijana kuwa mitandao sio kokoro la kupeleka uchafu wote ambao umezuiwa na sheria zingine na nchi ina utamaduni wake ambapo inahitajika kulindwa kizazi cha sasa na cha kesho cha Taifa hili.

Saturday, April 14, 2018

5:36 PM

Koffi Olomide aalikwa tena KenyaMwanamuziki wa Dansi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Koffi Olomide anatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha nchini Kenya hivi karibuni ikiwa ni mara ya kwanza tangu afukuzwe nchini humo mwaka 2016.

Mnamo July 2016, Olomide alikamatwa na polisi wa Kenya na kurudishwa nchini DRC baada ya kusambaa kwa video iliyoonesha mwanamuziki huyo akimpiga mchezaji wa bendi yake wa kike kipindi akiwa jukwaani.

Jana April 13, 2018 alitangaza kualikwa nchini Kenya kufanya show kwenye mkutano mkubwa wa viongozi 47 wa majimbo ya nchi hiyo utakaofanyika Kakamega.