Breaking

Showing posts with label . News. Show all posts
Showing posts with label . News. Show all posts

Tuesday, April 17, 2018

9:44 PM

Mtoto aliyedai kutelekezwa na Lowasa akamatwa na Polisi


Wiki moja mara baada ya Fatuma Chikawe kujitokeza kwenye vyombo vya habari na kudai ametelekezwa na  Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowasa kwenye zoezi linaloendeshwa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, binti huyo amekamatwa na jeshi la Polisi Kanda maalumu.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.... 


Monday, April 16, 2018

8:16 PM

Mkuu wa zamani wa FBI Asema Trump Hana 'Maadili ya Uongozi

Mkuu wa zamani wa FBI  Asema Trump Hana 'Maadili ya Uongozi

Aliyekuwa mkuu wa shirika la upelelezi Marekani FBI James Comey amesema Donald Trump 'hana maadili ya uongozi kushikilia wadhifa wa rais' na ambaye anawachukulia wanawake kama 'kiteweo cha nyama'.

Bwana Comey alikuwa akihojiwa kwa mara ya kwanza kwenye televisheni tangu afutwe kazi na rais Trump mwaka jana.

Ameliambia shirika la habari la ABC kwamba Trump huzusha urongo kila saa na huenda amezuia haki itetendeke.

Saa chache kabla ya mahojiano hayo yapeperushwe, rais Trump alimshambulia Bwana Comey kwa kile anasema ni kusema 'urongo mwingi'.

Comey amekiambia kipindi cha ABC Jumapili usiku: 'Siamini madai yaliopo kumhusu kwamba ana matatizo ya kiakili au katika hatua za kwanza kuugua ugonjwa wa kusahau.'

'Sidhani kwamba ana mapungufu ya kiafya kumuwezesha kuwa rais. Nadhani hana maadili ya kuwa rais'.

"Rais wetu ni lazima aheshimu na afuate maadili ambayo ndio mzizi wa nchi hii. La muhimu zaidi ikiwa ni ukweli. Rais huyu hana uwezo wa kufanya hivyo," Comey amesema.

Baada ya mahojiano kupeperushwa, chama cha Trump - kupitia kamati ya kitaifa ya Republican - kilitoa taarifa ikisema kuwa hatua ya Comey kujitokeza mbele ya umma kunadi kitabu chake imeonyesha kwamba, "utiifu wake wa juu ni kwake mwenyewe".

Trump amuonya mkuu wa FBI aliyefutwa James Comey
Rais Trump achukizwa na tuhuma za Comey
Trump atetea hatua ya kumfuta Comey
"Kitu kibaya zaidi kushinda historia ya ukosefu wa nidhamu wa Comey ni kukubali kwake kusema chochote ili aweze kuuza vitabu," taarifa hiyo ilisema.

Je tumefikaje hapa?
Hadithi hii inaanzia wakati wa uchaguzi wa urais mnamo 2016, wakati Bwana Comey alikuwa mkurugenzi wa FBI director, na uchunguzi kuhusu namna mgombea wa urais wa chama cha Democrat Hillary Clinton alivyozishughulikia barua pepe za siri katika kompyuta binafsi wakati akiwa waziri wa mambo ya nje.

Mnamo Julai 2016, Comey alisema kwamba hakuwa na umakini katika namna alivyozishughulikia barua pepe hizo, lakini FBI haitomshtaki.

Hatahivyo mnamo Oktoba, sikukadhaa kabla ya uchaguzi, alituma barua bungeni akiliarifu kwamba FBI linaanzisha upya uchunguzi baada ya kugundua barua pepe zaidi.

Barua hiyo ilifichuliwa kwa umma - na Hillary Clinton akasema hatua hiyo ndiyo iliompa Trump ushindi.

Mnamo November, FBI lilisema limekamilisha ukaguzi wa barua pepe hizo mpya zilizogunduliwa na kwa mara nyingine likasema halitomshtaki.

Na bwana Trump alipopata urais, Bwana Comey alisema kuwa alijaribu kumshurutisha aape kumtii - Jambo ambalo rais analikana pakubwa.

Mnamo Machi 2017, wakati uchunguzi ulipokuwa unafanywa na FBI kuhusu tuhuma za ushirikiano kati ya timu ya kampeni ya Trump na Urusi inatuhumiwa kwamba Trump alimshinikiza Comey kutangaza wazi kwamba rais hatochunguzwa kibinafsi - jambo ambalo mkurugenzi huyo wa zamani wa FBI alikataa kufanya hivyo.

Baadhi ya wanasiasa wa Democrats walimlaumu Comey kwa kumfanya Bi Clinton apoteze kura katika uchaguzi , huku wafuasi wa Trump walihisi kwamba anamlenga rais katika uchunguzi huo.

Alifutwa kazi na rais Trump mwezi Mei, na alipata taarifa kuhusu kutimuliwa kwake katika vyombo vya habari nchini.

Comey alihojiwa bungeni kuhusu uchunguzi huo wa uwezekano kuwepo uhusiano kati ya kampeni ya Trump na Urusi na kutimuliwa kwake, na alimthumu rais kwa kusema urongo na kumchafulia jina. 
10:58 AM

Watu saba wafariki kutokana na Mvua Dar


watu saba wamefariki dunia kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam.

Kamanda wa polisi kanda maalum jiini Dar es salaam Lazaro Mambosasa amethibitisha vifo hivyo, na kueleza kwamba mwili mmoja umekutwa ukielea kuelekea maeneo ya Jangwani jijini Dar es salaam.

Sambamba na hilo Kamanda Mambosasa amesema maeneo mengi jijini Dar es salaam yamejaa maji, na kuwataka watu kuwa makini wanapotumia barabara hasa sehemu zenye makorongo, na kuwaangalia zaidi watoto ambao wanapita mara kwa mara wakienda shule au wakiwa wanarudi kutoka shule.


“Watu wasijaribu maji, ukijaribu maji ujue utaondoka nayo, kwa hiyo watoto wetu wanapokwenda shuleni tuwasindikize, sehemu nyingi zenye makorongo kwa mfano kule Kinyerezi, kule Goba kule Makongo, zile shortcut zote maji yamejaa, watu wajiepushe kutumia njia hizo, watapoteza watoto wakiwa wanaenda au kutoka shule”, amesema Kamanda Mambosasa.

Jeshi la Polisi limesema litaendelea kutoa taarifa za sehemu mbali mbali kuhusu hali ya mvua, ambayo inaendelea kuathiri sehemu kubwa ya nchi.

Saturday, April 14, 2018

5:23 PM

Zitto Kabwe Amlilia Mama Mzazi wa Mrisho Gambo

Zitto Kabwe Amlilia Mama Mzazi wa Mrisho Gambo

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ametoa salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo baada ya kufiwa ya mama yake mzazi usiku wa kuamkia jana.Zitto amesema kuwa anajua uchungu wa kupotelewa na mama huku akieleza kuwa hakuna faraja kama kumuuguza na kumsitiri mzazi.

Pole sana kwa Msiba huu mkubwa ndugu Mrisho Gambo. Najua uchungu wa kupotelewa na mama. Hakuna faraja kama kumuuguza na kumsitiri mzazi. Mola akupe subira wewe na ndugu zako. Inna lilah waina ilaih raajiun ameandika Zitto kwenye mitandao yake ya kijamii. 

Friday, April 13, 2018

8:38 AM

Rais Magufuli ambadilisha mpambe wake na awapandisha Vyeo Maofisa 28RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ameridhia na kuwapandisha vyeo maofisa 28 wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kuanzia leo Aprili 12, 2018 huku akimbadilisha Msaidizi wake Kanali Mbaraka Mkeremy ambaye amempandisha cheo na atapangiwa kazi nyingine jeshini.

Aidha, Rais pia amekukubali kumpandisha cheo kutoka Luteni Kanali kuwa kanali D.P.M Murunga na kuwa mpambe wa Rais akichukua nafasi ya Kanali Mkeremy.

Akitoa taarifa ya uteuzi huo, Mkuu wa Majeshi, Jenelari Venancy Mabeyo amesema maofisa walioteuliwa wanakwenda kuimarisha safu za utendaji kazi kijeshi na kwamba maofisa wote hao watavalishwa vyeo vyao Ijumaa hii katika makamo makuu ya Jeshi Upanga Jijini Dar es salaam.

Katika uteuzi huo Rais Magufuli amewapandisha vyeo maofisa wa ngazi mbalimbali Jeshini ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma Kanali M E Gaguti ambaye sasa anapanda cheo na kuwa Brigedia Jenelari na kurejeshwa Jeshini.

Wednesday, April 11, 2018

8:24 PM

Msako wa Wanaume Waliotelekeza Watoto Kuanza Kesho Idadi ya Vigogo Yafikia 107

Msako wa Wanaume Waliotelekeza Watoto Kuanza Kesho Idadi ya Vigogo Yafikia 107

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa kuanzia kesho Alhamis wanaume wote ambao tayari wametajwa kutelekeza watoto wataanza kupelekewa barua za wito.Akizungumza na baadhi ya wanawake waliojitokeza kupeleka malalamiko yao, Makonda, amesema kuwa hakutakuwa na kigogo yoyote atakayehitaji kuonana naye kwa siri kama ambavyo wengi wamekuwa wakiomba kufanya hivyo na kueleza kuwa nafasi hiyo haipo.Amesema kuwa vigogo 107 tayari wametajwa kutelekeza watoto na amewaomba mara wapatapo wito wa barua yake wafike ofisini kwake mara moja kwani watakaokaidi watachukuliwa hatua kali za kesheria. Mbali na zoezi hilo Makonda amesema kuwa wadau mbalimbali wamejitokeza kusaidia kuwalipia watoto hao Bima za afya ili waweze kumudu gharama za matibabu kwa kipindi cha mwaka mmoja. 
5:24 PM

Tundu Lissu kufanyiwa upasuaji mwingine leo
Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mwingine siku yao.

Tundu Lissu yupo katika matibabu nchini Ubelgiji mara baada ya kushumbaliwa kwa kupingwa risasi na watu wasiojulikana September mwaka jana mjini Dodoma.
“Kama nilivyowataarifu siku za nyuma, mguu wa kulia bado una shida kutokana na risasi nyingi nilizopigwa na ‘watu wasiojulikana, operesheni ya leo ni sehemu ya tiba ya mguu huo. Napenda wote mfahamu kwamba niko kwenye mikono salama ya kitabibu. Mungu wetu amekuwa mwema sana kwangu tangu tarehe 7 September ya mwaka jana,” amesema Tundu Lissu.
Kabla ya kupelekwa Ubelgiji kwa ajili ya matibu zaidi, Lissu alikuwa akipokea matibabu Nairobi nchini Kenya ambapo December 26 aliweza kusimama kwa mara ya kwanza tangu aliposhambuliwa. January 07, 2018 ndipo aliwasili Ubelgiji.
4:53 PM

Vigogo waliotelekeza Watoto watakiwa kwa Makonda

 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa kuanzia kesho Alhamis wanaume wote ambao tayari wametajwa kutelekeza watoto wataanza kupelekewa barua za wito.

Akizungumza na baadhi ya wanawake waliojitokeza kupeleka malalamiko yao, Makonda, amesema kuwa hakutakuwa na kigogo yoyote atakayehitaji kuonana naye kwa siri kama ambavyo wengi wamekuwa wakiomba kufanya hivyo na kueleza kuwa nafasi hiyo haipo.

Amesema kuwa vigogo 107 tayari wametajwa kutelekeza watoto na amewaomba mara wapatapo wito wa barua yake wafike ofisini kwake mara moja kwani watakaokaidi watachukuliwa hatua kali za kesheria.

 Mbali na zoezi hilo Makonda amesema kuwa wadau mbalimbali wamejitokeza kusaidia kuwalipia watoto hao Bima za afya ili waweze kumudu gharama za matibabu kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Monday, April 9, 2018

9:36 PM

Rais wa Zamani wa Brazil Ajisalimisha Gerezani Kutumikia Kifungo cha Miaka 12 Tarehe  April 9, 2018 stori ninayokusogezea ni kuhusu Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva amejisalimisha katika gereza la Curitiba tayari kuanza kutumikia kifungo cha miaka 12 baada ya awali kukwepa kufanya hivyo.

Ijumaa Mahakama ilimhukumu kwa mashtaka ya ufisadi, lakini alikimbilia katika makao makuu ya muungano wa wafanyakazi mjini Sao Paolo, ambako wafuasi wake walitaka asijisalimishe.

Televisheni nyingi nchini Brazil zimeonesha alivyowasili kwa helikopta katika Makao Makuu ya Polisi katika mji wa Curibita.

Lula alitoa hotuba katika mji wa Sao Bernardo do Campo kabla ya kujisalimisha, Lula amejitaja kuwa raia aliyekasirishwa na mashtaka ya kutungwa ya ufisadi. 
9:33 PM

Shule Yatangaza Kuruhusu Wanafunzi wa Kiume Kuvaa Sketi
shule moja ya bweni nchini Uingereza ijulikanayo kama Uppingham School imetangaza kuruhusu wanafunzi wa kiume wa shule hiyo kuvaa sketi.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Richard Maloney ameeleza kuwa mwanafunzi yeyote wa kiume atakayeomba ruhusa ya kuvaa sketi ataruhusiwa kwani anaamini uhuru na uchaguzi wa mtu ni lazima viheshimiwe.

Inaelezwa kuwa suala hili la kuvaa uniform ya aina yoyote kutasaidia sana katika kuondoa ubaguzi wa kijinsia baina ya wanafunzi. 

Saturday, April 7, 2018

9:57 PM

'Watakaoandamana kitakachowapata wasije kulaumu" IGP SirroMkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro amesema Jeshi lake liko imara kweli kweli katika kupambana na watu wanaotaka kuleta uvunjifu wa amani nchini, huku akiwasii wanaotaka kuandamana kuacha mara moja kwani kitakachowapata wasije kulaumiana

 IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo (Aprili 7, 2018) wakati akitoa salamu zake kwa Rais Dkt. Magufuli katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo mjini Arusha baada ya uzinduzi wa nyumba za askari na kushuhudia maonesho ya utayari ya jeshi hilo katika kukabiliana na uhalifu.

"Mhe. Rais Magufuli Jeshi lako Polisi liko imara tena imara kweli kweli, kwa kupambana na watu wote wanaotaka kuleta uvunjifu wa amani hapa nchini na kwa bahati nzuri wananchi wapo pamoja na wewe Rais na Jeshi lako. ila naomba nitoe ushauri wa bure kwa wale wote wenye nia ya kuchafua amani ya nchi yetu , ni wasii waache mara moja na kama wataona ushauri huo hauna maana basi baadae tusilaumiane", amesema IGP Sirro.

Pamoja na hayo, IGP Sirro ameendelea kwa kusema "upo uhamasishaji kwenye mitandao, na hili niseme  naamini wameshaandamana kwenye mitandao na wameshamaliza maandamano yao. Kwa hiyo la msingi sana tujenge nchi yetu".

Kwa upande mwingine, IGP Sirro amesema katika kipindi cha mwezi Januari hadi Februari mwaka 2018 kuna jumla ya matukio ya jinai yaliyoripotiwa ni 96,363 ikilinganishwa na matukio 104,073 yaliyoripotiwa kipindi kama hicho mwaka 2017
12:30 PM

Rais Magufuli aombwa kuwanyonga washtakiwa wa mauaji ya AlbinoNa James Timber, Mwanza
Mwenyekiti wa Watu wenye Ulemavu Ngozi (Ualbino) jijini Mwanza Alfred Kapole, amemuomba Rais Dk.John Magufuli kuwanyonga watu wanaoshikiliwa kwa makosa ya mauaji ya watu wenye ualbino.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na mtandao  wa Muungwana  amesema kuwa, wale waliohukumiwa kunyongwa wanyongwe mpaka kufa ili haki itendeke sawa na iwe fundisho kwa wengine ambao wanampango wa kufanya vitendo hivyo waogope kutokana na makali ya sheria.

"Katiba yetu inatuongoza lakini cha ajabu hatujaona lolote kuhusu kuwanyonga watu wanaoua wenzao kwa makusudi tunaumia kuona mtu aliyeua kuendelea kula chakula cha nchi hii ambacho sisi wahanga ndio tunakatwa kodi inayochangia ununuzi wa chakula hicho," alisema Kapole.

Kapole amesema hofu imetanda kwa walemavu wa ngozi wanaishi kwa wasiwasi tangu itokee tukio la mtoto mwenye ualbino katika Wilaya ya Tarime aliponyolewa nywele kisha kukatwa kucha.

Pia amesema kuwa baada ya Sikukuu ya Pasaka alihisi watu wabaya waliofika nyumbani kwake wilayani nyakati za usiku kilichomsadia ni kupiga yowe ambapo watu hao walimkimbilia kusikojulikana.

Aidha ameiomba jamii inayowazunguka kuwa karibu na watu wenye ualbino, kwani  itapunguza changamoto hizo wanazokumbana nazo mara kwa mara.

Friday, April 6, 2018

8:20 PM

Zuma apandishwa kizimbani, kesi yaahirishwaKesi ya rushwa ya aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ya anayekabiliwa na tuhuma 16 zikiwemo za udanganyifu, ufisadi na kutakatisha fedha haramu wakati akiwa madarakani, imehairishwa hadi Juni 8, 2018, itakaposomwa tena.

Zuma alifika Mahakama Kuu ya Durban leo asubuhi Aprili 6, 2018 kwa ajili ya kusikiliza kesi yake hiyo ambayo huku wafuasi wake walijikusanya maeneo ya karibu ya mahakama hiyo huku wakiimba nyimbo za kumsifu, wakisema hawatamuacha mpaka mwisho, na wengine wakikikesha kumuombea.

Rais huyo wa tatu mweusi nchini Afrika Kusini alifunguliwa mashtaka na kesi yake kusikilizwa kisha kufutwa mwaka 2009 na sasa imeanza kusikilizwa tena baada ya kuondolewa madarakani na kumuachia Cyril Ramaphosa ambaye aliahidi kukomesha vitendo vya rushwa na ufisadi nchini humo.
12:10 PM

Rais Magufuli kuzindua Nyumba za Polisi Arusha ,April 7Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pohn Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa nyumba za polisi na vituo vya polisi Jijini Arusha.

Akizungumza na waandishi wahabari Kamanda wa polisi jijini hapa DCP Charles Mkumbo amesema kuwa kutakuwa na uzinduzi wa vituo viwili cha Utalii na Diplomasia na kingine ni Kituo cha daraja la kati kilichopo Murieti Jijini Arusha.

Kamanda Mkumbo amesema kuwa kutakuwepo pia na maonyesho mbalimbali ya jinsi Jeshi la Polisi linavyofanya kazi za kuwahudumia wananchi ambapo maonyesho hayo yatafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid .

Amewataka wananchi kutokuwa na hofu kwani hali ya usalama Jijini hapa umeimarishwa na amewaomba wajitokeze  kwa wingi katika sherehe hizo. 

Thursday, April 5, 2018

6:06 PM

Mtanzania Aliyemuua Mkewe Apandishwa Kizimbani Uingereza

Mtanzania Aliyemuua Mkewe  Apandishwa Mahakamani

Stori kutokea Uingereza leo April 5, 2018 ni kumhusu Kema Salum ambae ni Mtanzania amepandishwa kwa mara ya kwanza Mahakamani katika Mahakama ya Crown kwa tuhuma za kumuua mke wake, Leyla Mtumwa.

Salum mwenye miaka 38 anadaiwa kumuua mke wake, Leyla, siku ya Ijumaa kuu kwa kumchoma visu mara shingoni na kifuani. Mauaji hayo yalifanyika nyumbani kwa wanandoa hao, Kirkstall Avenue, Haringey, Uingereza.

Kesi hiyo ya Salum haikuweza kusikilizwa baada ya kuwepo kwa mgomo wa wanasheria wa ngazi za juu nchini humo ulioanza tangu April 1, 2018.

Wakili anayemtetea Seona White amesema amewasiliana na vitengo zaidi ya 20 vya wanasheria, lakini hakuna aliyekubali kumtetea Salum kutokana na mgomo wa Wanasheria unaoendelea,

Jaji wa mahakama hiyo, Anuja Dhir amesema kesi hiyo itasikilizwa tena June 20 na akaamuru mtuhumiwa arudishwe mahabusu. 


Wednesday, March 28, 2018

1:37 PM

Mahakama Yaamuru mmiliki wa IPTL Akatibiwe MuhimbiliMahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru mmiliki wa IPTL, Harbinder  Sethi akatibiwe katika Hospital ya Taifa Muhimbili baada ya mshtakiwa huyo kulalamika afya yake imearibika sana.

Mbali ya Sethi, mshtakiwa mwingine ni mfanyabiashara James Rugemarila ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Bilioni 309.

Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi leo March 28, 2018 kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na pia wanafatilia vielelezo vya upelelezi nje ya nchi.

Baada ya kueleza hayo, Seth alisimama na kumueleza Hakimu Shaidi kuwa; 'Afya yangu imearibika sana, nahitaji kupelekwa hospitali.'

Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Shaidi amesema ni dhahiri afya ya mshtakiwa ikiangaliwa hata kwa macho inaonekana ni dhahifu.

“Naamuru mshtakiwa akatibiwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ili afya yake iwe njema,” amesema Hakimu Shaidi na kuahirisha kesi hiyo hadi April 11,2018.

Washtakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, kutakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya Dola za kimarekani 22, 198,544.60 na Sh, bilion 309.

Image may contain: 4 people, including Mollel Hillary Mollel, people smiling, text

8:22 AM

RC Makonda Awakalia Kooni Wanaume Wanaotelekeza Watoto "Ukimpa Mimba Mwanamke Dar Ujipange kwa Matunzo"


RC Makonda Awakalia Kooni Wanaotelekeza Watoto "Ukimpa Mimba Mwanamke Dar Ujipange kwa Matunzo"
Jopo la Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Maafisa Ustawi wa Jamii, Wanasheria pamoja na Askari Polisi kutoka Dawati la Jinsia  wamemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kuwa wamejidhatiti vyema kuwasikiliza kinamama waliotelekezwa na hawapatiwi pesa ya matunzo ya mtoto kwenye zoezi la siku tano za kuwapatia msaada wa kisheria kinamama hao linalotaraji kuanza April 09 Mwaka huu.
Akizungumza na wataalamu hao RC Makonda amesema tatizo la wamama waliotelekezwa ni kubwa na limekuwa likisababisha kinamama na watoto kuishi maisha ya tabu na kusababisha ongezeko la watoto wa mitaani na vizazi vya watoto wenye chuki na Baba zao.
RC Makonda amesema lengo la Zoezi hilo sio ugomvi bali ni kumwezesha Mtoto kupata mahitaji ili aweze kuitumia vyema fursa ya elimu bure chini ya serikali ya awamu ya tano.
Aidha RC Makonda amewahimiza wataalamu hao kuhakikisha wanawasikiliza kinamama kwa umakini na kusimamia haki pasipo upendeleo.
Pamoja na hayo RC Makonda amesema wapo kinababa ambao wameanza kutoa fedha ya matunzo ya Mtoto baana ya kusikia tangazo ambapo amewasihi kinamama hao kufika April 09 kwaajili ya kuonana na wataalamu ili waweke makubaliano kwenye mfumo rasmi wa kimaandishi.
IFIKE HATUA MWANAUME UKIMPA MWANAMKE UJAUZITO BILA MPANGILIO AOGOPE KAMA ILIVYO KWENYE UBAKAJI 


Image may contain: 4 people, including Mollel Hillary Mollel, people smiling, text