Breaking

Showing posts with label . NEWS. Show all posts
Showing posts with label . NEWS. Show all posts

Saturday, April 21, 2018

11:20 AM

Kamata Kamata ya Makonda Kwa Wanaume Waliotelekeza Watoto Kufanyika Jumatatu

Kamata Kamata ya Makonda Kwa Wanaume Waliotelekeza Watoto Kufanyika Jumatatu

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema wanaume wote waliokaidi wito wa kufika ofsini kwake baada ya kupigiwa simu na kutumiwa barua za wito watakamatwa na Jeshi la Polisi kuanzia siku ya jumatatu ya April 23.

RC Makonda amesema ifikapo siku ya Jumapili majina ya wanaume waliokaidi wito yatafikishwa kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Lazaro Benedict Mambosasa kwaajili ya utekelezaji.

Aidha RC Makonda ameongeza siku nyingine tano kwaajili ya kusikiliza kesi zilizowasilishwa ofisini kwake na kufanya idadi ya kufikia siku 15.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema ataunda kamati ya wanasheria na maafisa ustawi wa jamii kutoka serikalini na taasisi binafsi kwaajili ya kufanya uchambuzi wa ukubwa wa tatizo na mapendekezo ya kisheria kisha kuwasilishwa wizara husika kisha kuwasilishwa Bungeni.

Hata hivyo RC Makonda amesema ifikapo April 25 na 26 atatoa ripoti ya mwelekeo dhidi ya mateso waliyokuwa wakipata kinamama na watoto waliotelwkezwa.

RC Makonda amesema Zoezi la kusikiliza kinamama waliotelekezwa limekuwa na mafanikio makubwa ambapo zaidi ya wananchi 17,000 walifika ofsini kwake ambapo hadi sasa kinamama 7,000 wamesikilizwa na wanaume 1,200 wamekubali kwa maandishi kutunza watoto wao na wengine wamepimwa DNA. 

Friday, April 20, 2018

1:25 PM

Meneja TPA kortini kwa tuhuma za umiliki wa nyumba 23MENEJA Uhasibu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Prosper Kimaro, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akikabiliwa na mashtaka ya kuwa na mali zisizolingana na kipato chake.

Akisomewa mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo. Kimaro  anadaiwa kumiliki nyumba 23,  viwanja vitatu na magari saba vyote vikiwa na thamani ya Sh. bilioni 1.4.

Mawakili wa Serikali, Vitalis Peter akisaidiana na Lilian Wiliam, walidai kuwa katika tarehe tofauti kati ya mwaka 2012 na 2016, wilayani Temeke, Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa mtumishi wa umma katika nafasi ya Meneja Uhasibu wa TPA, alikutwa na mali zisizoelezeka.

Mali hizo, kwa mujibu wa mawakili hao, ni nyumba mbili zilizoko mtaa wa Uwazi, Temeke zenye thamani ya Sh, 123,273,253 na nyumba moja iliyopo Yombo Vituka yenye thamani ya Sh. 12,956,000.

Peter alidai kuwa mshtakiwa alikutwa akimiliki nyumba 23 na viwanja vitatu vyote vikiwa na thamani ya Sh. 1,178,370,324.

"Mheshimiwa Hakimu mshtakiwa alikuwa na magari saba yakiwamo Toyota LandCruiser yenye namba za usajili T 395 DEJ lenye thamani ya Sh. 180,131,815, Mitsubishi  yenye namba za usajili, T 506 CMT ya Sh. 38,464,861, Massey Ferguson yenye namba za usajili T 838 CHH ya Sh. 24,469,060.50, Trela lenye namba za usajili T 383 CNZ la Sh. milioni 4.5, Toyota Harrier yenye namba za usajili T 338 CVX ya Sh. 35,860,617.30, Trela lenye namba za usajili T 938 CVB  la Sh. milioni 4.8 na Massey Ferguson yenye thamani ya Sh.19, 138,324.44." alidai Peter wakati akimsomea mashtaka kigogo huyo.

Alidai kuwa mali zote alizokutwa nazo mshtakiwa hazilingani na kipato chake cha zamani na cha sasa.Mshtakiwa alikana mashtaka hayo.

Upande wa Jamhuti ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na haukuwa na pingamizi la dhamana.

Hakimu Simba alisema mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa kuwa na wadhamani wawili watakaowasilisha hati za mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh. milioni 200 kila mmoja na pia awasilishe hati zake za kusafiria mahakamani.

 Hata hivyo, hadi Nipashe inaondoka mahakamani hapo, mshtakiwa alikuwa hajatimiza masharti ya dhamana. Kesi  hiyo imepangwa kutajwa Mei 3, mwaka huu.
1:17 PM

Miaka 40 Hakuna cha Maana Kinachoendelea - Chenge


Miaka 40 Hakuna cha Maana Kinachoendelea - Chenge
Mbunge wa Bariadi na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge amefunguka na kusema kuwa zaidi ya miaka 40 ya uhuru wa nchi serikali imekuwa ikishikilia eneo lenye ukubwa wa ekari 2,472 bila kulifanyia jambo lolote lile la maana na kuomba serikali iwarudishie wananchi ili waweze kulitumia eneo.


Chenge amesema hayo leo bungeni April 19, 2018 alipokuwa akihoji kama serikali ipo tayari kurejesha maeneo hayo ambayo hayatumiki kikamilifu kwa wananchi ili wananchi waweze kufanyia shughuli zingine, lakini Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alifunguka na kusema kuwa serikali haipo tayari kurudisha maeneo hayo kwa kuwa serikali iliyachukua kwa lengo magereza kuweza kuendesha shughuli za uelimishaji wa wafungwa kwa njia ya kilimo na ufugaji kupitia maeneo hayo.

"Gereza la Matongo lililopo mkoani Simiyu katika wilaya ya Bariadi lenye ukubwa wa ekari 2472 lilianzishwa mwaka 1975, baada ya kuchukuliwa eneo hilo lililokuwa eneo la Mbunge wa enzi hizo Edward Mwani ambaye alifidiwa eneo jingine na serikali. Kwa serikali ipo kwenye mpango wa kuboresha kilimo kupitia jeshi la magereza kwa kuliwezesha kuzalisha chakula cha kutosheleza kulisha wafungwa na mahabusu hivyo eneo la Matongo lipo kwenye orodha ya maeneo yaliyopewa kipaumbele katika kilimo cha mahindi, alizeti, pamba, ufugaji wa nyuki na mifugo pamoja na upandaji wa miti na uhifadhi wa mazingira, serikali ilichukua eneo hilo ili kuwezesha magereza kuendeleza shughuli za uelimishaji wa wafungwa kwa kutumia kilimo na ufugaji kwa sasa eneo hili limepimwa na taratibu za kupatikana kwa hati zinaendelea hivyo serikali haina mpango wa kurejesha eneo hilo kwa vijiji tajwa" alisisitiza Masauni

Majibu ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni yalimuinua tena Andrew Chenge na kutaka kufahamu ni lini serikali itakuwa tayari kuanza mpango huo kwani ni miaka mingi imeshindwa kufanya hivyo. 

"Mhe. Spika gereza na Matongo ni gereza ambalo ni miongoni mwa magareza yaliyoanzishwa na serikali katikati ya miaka ya 70 kwa lengo hilo hilo ambalo waziri amelisema lakini zaidi ya miaka 40 ukifika pale Matongo hakuna cha maana kinachoendelea na Mhe. Waziri katika majibu yake anasema gereza hili lipo kwenye mpango wa kuboresha kilimo sasa ni lini mpango huu mahususi kwa gereza la Matongo utaanza kutekelezwa na serikali" alihoji Andrew Chenge 
1:11 PM

Mabishano Makali ya Kisheria Yatikisa Kesi ya Nondo Kesi Yaahirisha Hadi Jumatatu


Mabishano Makali ya Kisheria Yatikisa Kesi ya Nondo Kesi Yaahirisha Hadi Jumatatu
Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa imeipiga kalenda kesi ya mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo hadi Jumatatu kutokana na mabishano makali ya kisheria yaliyotokea kortini hapo kati ya pande mbili za utetezi na Jamhuri.

Akiahirisha kesi hiyo, Hakimu Mkazi John Mpitanjia alisema anajipa muda kwa lengo la kupitia sheria kuhusiana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na shahidi wa pili; kwamba kielelezo chake kipokelewe na mahakama ama la.

Upande wa uetetezi ukiongozwa na wakili Jebra Kambole akisaidiwa na Chance Luwoga, uliomba mahakama kutopokea hati ya upekuzi kwa madai ina mkanganyiko wa majina na kwamba ni watu wawili tofauti.

Aidha, utetezi ulipinga hati ya uchunguzi kuwa imekosewa jina la mshitakiwa kwani badala ya kuandika Abdul Mahamud Omary Nondo imesajiliwa kwa jina la Mahmud Omary Nondo.

Upande huo uliomba kutupiliwa mbali kwa nyaraka hiyo ambayo upande wa Jamhuri ukiongozwa na wakili wa serikali, Alex Mwita akisaidiwa na Pianzia Nchemba umesema cha muhimu ni ujumbe uliopo ndani.

Mwita alisema huenda nondo alitoa majina mawili tofauli kwa sababu alihojiwa na watu wawili tofauti.

Hoja ya tatu iliyotolewa na upande wa utetezi ni kwamba ilikuwaje Koplo John kutumia kifungu cha 10 (3) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA)Sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kuthibitisha waraka huo ili hali kabla alisajili kwa kutumia kifungu cha 34 (b) cha Sheria ya Ushahidi.

Awali, shahidi wa kwanza ambaye ni E.32328 Koplo Salim aliiambia mahakama kwamba Nondo aliwasili kituo cha polisi majira ya moja usiku na kuchukuliwa maelezo ya awali.

Alidai Nondo alisema amefika kituoni kutoa malalamiko ya kutekwa na watu wasiojulika na kutelekezwa katika Kiwanda cha Pareto Pct Mafinga.

Kolpo Salim aliiambia mahakama kuwa Nondo aliiambia Polisi kwamba alitekwa jijini Dar es Salaam na kusafirishwa hadi Mafinga Iringa na ndipo alimkabidhi kwa mpelelezi Koplo John mwenye namba E.7665 ambaye ni shahidi wa pili katika kesi hiyo, ili aweze kumchukua maelezo kwa kina kuhusiana na malalamiko yake.

Hata hivyo, mahakama ilipokea vielelezo ambavyo Nondo alivikabidhi Kituo cha Polisi Mafinga ambavyo ni kompyuta mpakato aina ya Dell, kadi ya mawasiliano (bussness card), kadi ya benki, simu ya kiganjani aina ya Itel na kitambulisho cha chuo.

Awali, Hakimu Mpitanjia alisema kabla ya mashahidi kutoa ushahidi wao inabidi mtuhumiwa kusomewa mashataka yake yanayomkabili na Nondo alikana mashtaka hayo.

Jamhuri imekusudia kuleta mashahidi watano zaidi ambapo jana ni mashahidi wawili tu waliopanda kizimbani kutokana na kutofikia muafaka baada ya pande mbili hizo kunyukana kwa kutumia vifungu vya sheria.

Jamhuri imekusudia kuwaleta pia kutoa ushahidi Koplo Salum, Veronica Fredy ambaye ni mpenzi wake Nondo, Alphonce Mwamule, Koplo Abdulkadir na mtu kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Tigo.

Nondo ameshitakiwa kwa makosa mawili ya kuchapisha taarifa za uongo kwa njia ya kompyuta na kutoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma ambaye ni askari polisi Koplo Salim wa Kituo cha Polisi Mafinga wilayani Mufindi.

Ilidaiwa kwamba Machi 7, mwaka huu akiwa Ubungo jijini Dar es Salaam, mshitakiwa alitenda kosa la kuchapisha taarifa za uongo kwa njia ya kompyuta akitumia simu ya kiganjani yenye No. 0659366125 kinyume cha Sheria ya Makosa ya Mtandao na kusambaza katika mitandao ya kijamii. 

Wednesday, April 18, 2018

3:58 PM

sh. Bilioni 1.9 zatengwa kwa ajili ya mikopo Manispaa ya Ubungo
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es salaam imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 1.9 kwa ajili ya mkopo kwa kina mama na vijana.

Hayo yamesemwa leo, April 18, 2018 na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Mhe Boniface Jacob wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano na benki ya CRDB ambapo mikopo hiyo itatolewa kupitia benki hiyo.
Meya Jacob ametoa wito kwa vijana kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo kwani idadi yao imeonekana kuwa ndogo kwani mfuko huu ni nusu kwa vijana na nusu kwa kina mama na asilimia 20 inakwenda kwa walemavu.
“Nikiwa Manispaa ya Kinondoni tuliweza kutenga 800M kwa ajili ya mikopo kama hii, lakini Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ina muda wa mwaka mmoja na nusu tu lakini unaweza kuona kiasi tulichotenga kwa ajili ya mikopo kwa vijana na kinamama, ni kwa sababu tuko commited kuwasaidia wananchi wa Manispaa ya Kinondoni” amesema Meya Boniface Jacob.
Manispaa ya Ubungo itakuwa ya kwanza kwa utekelezaji wa agizo kwamba asilimia 20 ya fedha ni kwa ajili ya walemavu. Kwa taarifa ya mratibu wa zoezi hilo, Wanawake waliojitokeza ni 11,321, vijana idadi yake ikiwa ni 1124.
3:49 PM

VIDEO: MCT kutoa tuzo za umahiri kwa wanahabari

Baraza la Habari Tanzania wametaja idadi ya wateule ambao wameshiriki katika ushindani wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi  wa Habari Tanzania (EJAT) 2017. Jopo la majaji nane wakiongozwa na mwenyekiti wake Ndimara Tegambwage, wameteua jumla ya waandishi 49 ambao wataingia katika kinyang'anyiro cha mashindano ya EJAT 2017 kati ya wateule hao 49 wateule 30 wanatoka kwenye katika magazeti, 10 wanatoka redio na 9 Televisheni, Tuzo hizo za umahiri wa Uandishi wa Habari Zitatolewa tarehe 12/may mwaka huu katika ukumbi wa Golden Tulip.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI................ 


2:06 PM

Ofisa wa Chuo Anaswa Live Akimnyonya Sehemu za Siri Mwanafunzi


UGANDA: Afisa Utawala Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Makerere, Bwana Kisuze Edward asimamishwa kazi baada ya picha yake akimnyonya mwanafunzi Racheal Njorogi sehemu za siri kusambaa mitandaoni

Racheal anadai aliwasili chuoni hapo kufuatilia taarifa zake za usajili ambapo alikutana na usumbufu mkubwa na baadaye alipopata nafasi ya kuingia ofisini kwa Msajili, alishangaa ghafla Afisa huyo akimvamia na kuanza kumnyonya matiti kisha sehemu zake za siri na alishindwa kumdhibiti kutokana na kumzidi nguvu

Kwa mujibu wa maelezo ya Racheal, anasema alilazimika kupiga picha (selfie) wakati tukio hilo likiendelea ili picha hiyo itumike kama ushahidi pindi atakapoenda kuripoti polisi

Tukio hilo limejiri ikiwa ni siku chache baada ya Rais Yoweri Kaguta Museveni kukemea vitendo vya ngono kwa njia ya mdomo

1:58 PM

Rais Trump afanya mazungumzo ya siri na hasimu wake Kim Jong Un


baada ya kutumiana vijembe na maneno ya kashfa kwa muda mrefu kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, hatimaye wawili hao wafanya mazungumzo mafupi kwa siri wiki mbili zilizopita.

Mazungumzo hayo yalifanyika baada ya  Mkurugenzi wa shirika la upelelezi nchini Marekani (CIA), Mike Pompeo wikiendi ya pasaka kuzuru mjini Pyongyang na kufanya mkutano wa siri na kiongozi wa taifa hilo, Kim Jong Un,  hii ni kwa mujibu wa duru za vyombo vya habari nchini Marekani.

Mkutano huo ulifanyika kwa lengo la maandalizi ya mkutano mwengine mkubwa kati ya Rais Donald Trump na Kim Jong Un ambapo hadi sasa bado haijajulikana ni wapi utafanyika.

Hata hivyo, Rais Trump amekiri kufanyika kwa mazungumzo na kiongozi huyo wa Korea Kaskazini kwa njia ya simu, wakati wa sherehe za kumpokea Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe zilizofanyika mjini Florida juzi Jumatatu.

Mkutano huo wa siri ambao haukutarajiwa ndio utakuwa mkutano wa kwanza mkubwa  kati ya Marekani na Korea Kaskazini tangu 2000, wakati Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani kipindi hicho, Madeleine Albright alipokutana na Kim Jong-il, babake kiongozi wa sasa wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un.
9:50 AM

Ndalichako Aijibu Ripoti ya CAGWaziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako, amesema anaitumia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kama changamoto na chachu ya kuendelea kufanya kazi nzuri.

 Ndalicho ameyasema hayo leo Aprili 17 wakati akijibu hoja za ripoti ya CAG iliyosomwa wiki iliyopita bungeni.

 Wiki iliyopita mawaziri wanane walifanya mkutano na waandishi wa habari wakijibu hoja za ripoti ya CAG.

“Serikali ya awamu ya tano kwenye suala la udhibiti haina utani kila mtu ameona kazi ambayo imefanyika, tunapopata ripoti ya CAG, inatupa chachu ya kuendeleza na kazi nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya tano,” amesema

Amesema kama CAG alivyoshauri, watafanyia kazi mapendekezo ya CAG na pia watawachukulia hatua watendaji wanaotumia vibaya fedha za umma.

Ndalichako alizungumzia hoja ya CAG kuhusu ukusanyaji hafifu wa fedha za mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na akasema, tangu serikali ya awamo ya tano iingie madarakani, kumekuwa na ongezeko la ukusanyaji wa madeni hayo.

“Taarifa ya CAG 2015/16 hadi 2016/17    inaionyesha kuwa makusanyo yameongezeka kutoka Sh28bilioni hadi Sh 116bilioni. Hilo ni ongezeko la asilimia 300. Takwimu hazidanganyi,” amesema

Hata hivyo amesema bado makusanyo hayo hayatoshelezi na ameitaka  Menejimenti ya Bodi ya Mikopo kuhakikisha ukusanyaji wa mikopo unaimarishwa. 

Tuesday, April 17, 2018

9:42 PM

Huyu ndiye aliyefanyiwa upasuaji kupandikizwa uso UfaransaBaada ya kuishi kwa miezi miwili bila uso, mwanaume mmoja raia wa Ufaransa, Jérôme Hamon amefanyiwa upasuaji kwa mara ya pili wa kupandikizwa uso.

Inaelezwa kuwa mwaka 2010 Jerome alifanyiwa upasuaji na kupandikizwa uso na kufikia mwaka 2016 aliumwa kifua na kunywa dawa za antibiotic ambazo zilipelekea uso wake huo wa kupandikizwa kuharibika hivyo alitakiwa kufanyiwa upandikizaji wa uso mwingine.

Hadi kufikia mwezi November 2017, uso wake ulikuwa umeharibika na ilibidi wautoe na kuanza kutafuta atakaye kuwa ‘donor’ wa sura yake kwa ajili ya Jerome ili upasuaji huo ufanywe.

Kwa miezi hii yote Jerome aliishi hospitali jijini Paris, nchini Ufaransa akiwa hana uso, jambo lililofanya asiweze kusikia, kuzungumza wala kuona hadi alipopata sura mpya siku za hivi karibuni.

Jerome alifanyiwa upasuaji wa kwanza kuondolewa uso wake kutokana na kuwa na ugonjwa ambao ni wa kurithi ambao ulipelekea awe na uvimbe mkubwa usoni mwake.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya upasuaji huo Jerome ameeleza furaha yake kupata sura mpya tena ya mtu mwenye miaka 22, ikiwa yeye ana miaka 41 na jinsi upasuaji mzima ulivyokuwa wa mafanikio.
9:33 PM

Mjukuu wa Malkia Elizabeth Prince William Ahaidi Kuipa Tanzania Ulinzi


Mjukuu wa Malkia Elizabeth wa Uingereza Prince William Ahaidi Kuipa Tanzania Ulinzi
Mjukuu wa Malkia Elizabeth wa Uingereza, William Arthur amemuahidi Makamu wa Rais Samia Suluhu kuwa ataisaidia Tanzania katika kuboresha ulinzi wa wanyama pori kwa kutumia teknolojia ya hali juu na kumualika Rais Magufuli katika mkutano wa masuala ya wanyapori utakaofanyika Oktoba 2018.


Prince William ameeleza hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mama Samia leo katika Jumba la Kifalme la Buckingham Palace nchini Uingereza ambapo Makamu wa Rais amekwenda kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa nchi za jumuiya ya Madola.​

Kwa upande wake Makamu wa Rais alimweleza Prince William kuwa Tanzania inatambua mchango wake katika kuzuia ujangili wa wanyama pori na serikali ya Tanzania imekuwa ikichukua hatua mbalimbali ya kupambana na kuzuia ujangili ingawa bado haijawa na teknolojia yenye uwezo wa wa kutambua na kuona wanyama wote lakini wameendelea kuimarisha ulinzi wa wanyama pori. 
9:53 AM

Safari ya Mama Samia yamkutanisha na waziri wa Maendeleo UingerezaMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan jana amkutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza  Mhe. Penny Mordaunt .

Makamu wa Rais yupo  nchini Uingereza   kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Katika mkutano wake na Waziri huyo wa Uingereza Makamu wa Rais alielezea hatua kubwa iliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika Elimu mara baada ya kuamua Elimu iwe bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne.

Pia Makamu wa Rais alishukuru mradi wa DFID unatekelezwa mkani Simiyu na kuomba mradi huo uongezewe maeneo ili uweze kuwanufanisha watoto wengi wa kike.

Makamu wa Rais pia alizungumzia namna Majukwaa ya Kuwawezesha wanawake kiuchumi yanavyofanya kazi huku taratibu mbali mbali zinafanyika ili mabenki yaweze toa mikopo kwa riba nafuu.

Mwisho Makamu wa Rais alizungumzia jitihada mbali mbali zinazofanywa na Serikali katika kuboresha Mazingira ya kufanya Biashara nchini.

Naye Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza Mhe. Penny Mordaunt ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa jitihada wanazofanya katika kuboresha huduma za kijamii, alisema nchi yake ipo tayari kusaidia katika masuala ya makusanyo ya kodi, kuboresha uwezo wa walimu kwa kuwapatia mafunzo mbali mbali.
9:47 AM

Mkuchika: Kazi ya usalama wa taifa si kufuatilia wahalifu wala Kukamata watuWaziri wa Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema kazi kubwa ya usalama wa taifa ni kukusanya habari na kuishauri serikali na wala si kukamata watu kwa mabavu.

Mkuchika ameyasema hayo jana Aprili 16 bungeni wakati akijibu hoja za wabunge waliochangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

“Naomba nichukue nafasi hii kufafanua sheria ya usalama wa taifa inasema nini, usipojua kazi za idara ya usalama wa taifa, utawapa lawama kwa kazi ambazo si zao,” alisema.

Alisema idara hii hutekeleza majukumu kulingana na sheria ya usalama wa taifa namba 15 ya mwaka 1996 na sheria hiyo katika kifungu cha nne, inasema kazi yake ni kukusanya, kuchambua na kuishauri serikali hatua za kuchukua.

Alisema ameamua kulisema hilo kwa kuwa wabunge wengi wamezungumzia kuhusu watu wa idara ya usalama kukamata watu ovyo na kwa kutumia mabavu.

“Pili haitakuwa kazi ya idara ya usalama, kumfuatilia fuatilia mhalifu. Nimeona niiseme hiyo kwa sababu mazungumzo mengi yameelekeza huko, mtu ameuawa ni ‘polisi kesi’, hakuna nchi ambayo idara ya usalama ina shughuli ya kukamata watu,” alisema.

Alisema:  “Kama mnataka usalama wa taifa wafanye kazi ya kukamata watu basi walilete suala hilo bungeni.” 

Monday, April 16, 2018

8:12 PM

Huu Hapa Ujumbe wa Makonda kwa Lulu "Kumbe Wanaokuombea Mema Wako Wachache"

Huu Hapa Ujumbe wa Makonda kwa Lulu "Kumbe Wanaokuombea Mema Wako Wachache"

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemtakia heri ya siku ya mfanano wa kuzaliwa Elizabeth Michael (Lulu) huku akimwambia kuwa wanaomuombea mema wachache ila wenye nyuso za huzuni ni wengi.

Makonda ameeleza kuwa kwa kuwa Mungu ametenda basi watakuja na nyuso za furaha japo hazina mahusiano na mioyo yao.

RC Makonda ametoa ujumbe huo leo, Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

Kumbe wanaokuombea mema wako wachache ila wenyenyuso za huzuni wako wengi japo hawamaanishi. Na kwakua Mungu ametenda basi watakuja tena na nyuso za furaha japo hazina mahusiano na mioyo yao. Kwakifupi hii ndiyo dunia ambayo Mungu amekuongezea tena mwaka wa kuishi. Happy birthday mwanangu 
8:08 PM

Abdul Nondo aja kivingine, azungumzia taulo za kikeMwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Tanzania (TSNP), Abdul Nondo amefunguka na kuitaka serikali ya Tanzania kuiga serikali ya nchini Kenya ambayo imeweza kutoa taulo za kike kwa wanafunzi wote wa kike waliopo mashuleni.

Abdul Nondo amesema kuwa yeye anaamini kuwa serikali ya Tanzania pia inaweza kufanikisha jambo hilo kwa kuwa wanafunzi wengi wa kike wanakosa kufika mashuleni kipindi ambacho wapo kwenye siku zao na kuathiri masomo yao.

"Bado tunaamimi hata Serikali ya Tanzania, inao uwezo mkubwa saana wa kutoa sanitary pads (taulo) bure kwa wanafunzi wa kike dada zetu, kwani takwimu zinaonesha hedhi huchangia kiasi kikubwa wanafunzi hawa kukosa masomo. Kutokana na gharama za manunuzi hasa kijijini.Hoja hii ilipelekwa bungeni na Mbunge wa viti maalumu Upendo Peneza, ila haikujadiliwa aliambiwa kuwa hakufuata utaratibu"

Abdul Nondo aliendelea kusema atashauriana na viongozi wake wa TSNP kuangalia namna wanavyoweza kufanya ili wabunge ambao wanaguswa na jambo hilo wasichoke kuliwasilisha bungeni.

"Nitashauriana na viongozi wenzangu wa TSNP kuangalia namna tunavyoweza kufanya suala hili kama Agenda kubwa zaidi, na kuendelea kufanya ushawishi kwa wabunge ambao wanaguswa na jambo hili ili wasichoke kuliwasilisha bungeni kwa Mara nyingine. Ili serikali ijumuishe mpango huu wa kutoa pads bure katika Sera yake ya elimu bure. Ili wanafunzi hawa wapate haki yao kikamilifu ya kupata elimu kama Kenya imeweza hata Tanzania, tunaweza fanya hivi pia kwa manufaa ya dada zetu hawa" Abdul Nondo
11:19 AM

CHADEMA yamvaa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG)

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG
Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA kimekanusha taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inayokihusu chama hicho,

Akizungumza na Wanahabari, Mkurugenzi wa Fedha, Uwekezaji na Utawala wa chama hicho, Roderick Lutembeka, amekanusha takwimu zilizoandikwa kuhusu chama chake,

Lutembeka amesema kwenye ukurasa wa 267 wa ripoti ya CAG, kipengele (i), kinasema CHADEMA kimefanya manunuzi ya bidhaa na huduma zenye jumla ya Shilingi 24,216,625,390 (zaidi ya Bilioni 24), 

Mkurugenzi huyo alisema hesabu hizo sio za kweli kwani kwa miaka mitatu (2014/15, 2015/16, 2016/2017) chama chake kilifanikiwa kukusanya jumla ya shilingi Bilioni 14.2 tu,

Alisema fedha hizo (Bilioni 14.2) walizipata kutokana na Ruzuku na michango ya Wanachama,

Lutembeka alihoji kuwa inawezekana vipi yafanyike manunuzi makubwa kuliko fedha zilizopatikana,

“Kama tulifanya matumizi hayo aliyoyaandika CAG, basi ina maana chama kilikusanya pesa zaidi ya hizo Bilioni 24,


Mkurugenzi wa Fedha, Uwekezaji na Utawala wa CHADEMA, Roderick Lutembeka ,
“Na kwa taarifa tu ni kwamba huu ukaguzi ni wa miaka mitatu mfululizo. Na tumekuwa tunapeleka mahesabu yetu kila mwaka. Lakini CAG alikuwa haji kutukagua” alisema Lutembeka ,

Mkurugenzi huyo aliendelea kusema mwaka jana CAG alipeleka wakaguzi 15 kutoka kwenye ofisi yake kwa ajili ya kukagua hesabu za CHADEMA,

Aliongeza kusema kuwa baada ya kukamilisha ukaguzi, Wakaguzi hao pamoja na chama chake kilikaa pamoja kupitia ripoti hiyo kabla hawajaondoka nayo,

“Tulipoipitia pamoja nao, haikuwepo hiyo namba (Bilioni 24). Sasa tunashangaa kwenye ripoti yao tunakuta namba nyingine kabisa. Hii si sawa,” alilalamika Lutembeka 
11:06 AM

Kauli ya Tundu Lissu Baada ya Bi. Fatma Karume Kutangazwa Mshindi wa Urais wa TLSKauli ya Tundu Lissu baada ya Bi. Fatma Karume kutangazwa mshindi wa urais wa TLS

Tarehe Aprili 14, 2018 Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilipata Rais mpya mteule Bi. Fatma Karume, Hatimaye Mhe. Tundu Lissu ambaye ndiye aliyemuachia kiti hicho ametoa pongezi kwa wana


Mhe. Lissu ambaye yupo hospitalini nchini Ubelgiji tangu mwezi Januari mwaka huu, amesema kuwa uchaguzi huo umethibitisha kuwa TLS ni chama ambacho kinaweza kujisimamia na kujiendesha bila kuingiliwa na mtu.
“Napenda kuwapongeza wanachama wote wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kwa kumchagua Bi. Fatma Karume kuwa Rais mpya wa TLS. Uchaguzi huu umethibitisha, kwa mara nyingine tena, umuhimu wa Chama cha kitaaluma cha mawakili kujisimamia na kujiendesha bila kuingiliwa,“ameeleza Tundu Lissu na kutoa pongezi kwa Bi. Fatma .
“Namtakia Rais Mteule Fatma Karume kila kheri katika kutelekeza majukumu yake mapya na muhimu katika kipindi hiki cha historia ya nchi yetu.“ameandika Mhe. Lissu kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Wakili Fatma Karume amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)      kwa ushindi wa kura 820 akiwamwaga Godwin Ngwilimi kura 363, Godwin Mwapongo 12 na Godfrey Wasonga kura 6. 
10:58 AM

Watu saba wafariki kutokana na Mvua Dar


watu saba wamefariki dunia kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam.

Kamanda wa polisi kanda maalum jiini Dar es salaam Lazaro Mambosasa amethibitisha vifo hivyo, na kueleza kwamba mwili mmoja umekutwa ukielea kuelekea maeneo ya Jangwani jijini Dar es salaam.

Sambamba na hilo Kamanda Mambosasa amesema maeneo mengi jijini Dar es salaam yamejaa maji, na kuwataka watu kuwa makini wanapotumia barabara hasa sehemu zenye makorongo, na kuwaangalia zaidi watoto ambao wanapita mara kwa mara wakienda shule au wakiwa wanarudi kutoka shule.


“Watu wasijaribu maji, ukijaribu maji ujue utaondoka nayo, kwa hiyo watoto wetu wanapokwenda shuleni tuwasindikize, sehemu nyingi zenye makorongo kwa mfano kule Kinyerezi, kule Goba kule Makongo, zile shortcut zote maji yamejaa, watu wajiepushe kutumia njia hizo, watapoteza watoto wakiwa wanaenda au kutoka shule”, amesema Kamanda Mambosasa.

Jeshi la Polisi limesema litaendelea kutoa taarifa za sehemu mbali mbali kuhusu hali ya mvua, ambayo inaendelea kuathiri sehemu kubwa ya nchi.

Saturday, April 14, 2018

10:24 PM

Makonda: Sina mpango wa Kugombea Urais...Lengo Langu ni Kumsaidia Magufuli


mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema hana mpango wa kuwa Rais ila anapenda kumsaidia Rais John Magufuli katika utekelezaji wa shughuli zake.


Makonda ameyasema hayo leo alipoulizwa na mwandishi wa Azam TV Baruan Muhuza wakati wa mahojiano yake akielezea tathmini ya siku tano za kusikiliza malalamiko ya wanawake waliotelekezwa na wenza wao.


Muhuza aliuliza: “Hao wote uliowasaidia wanakuona shujaa na mtu wao wa muhimu sana, unatamani kuwa rais wa nchi hii siku moja."


Makonda amejibu,“Hapana ila natamani kumsaidia Rais Magufuli atimize azma yake kwa wananchi hasa kwa malengo aliyonipa kwa mkoa wa Dar, hiyo ndiyo shauku yangu."


Kuhusu madai ya kuwachafua watu maarufu kupitia zoezi hilo amesema, "Huchafuliwi kwa kuwa una mtoto, matendo yako uliyoyafanya ndiyo yanayokuchafua,"


"Si kweli kwamba eti nililenga kuwachafua wanasiasa ndiyo sababu kuna DNA. Kama kuna mtu anafikiri ni zoezi la mtu fulani anakosea, namna pekee ya kuepuka kuitwa kwa RC mtafute mtoto wako umlee,"


Amesema shauku yetu kubwa ni kuona kila mtoto anapata haki yake.
5:23 PM

Zitto Kabwe Amlilia Mama Mzazi wa Mrisho Gambo

Zitto Kabwe Amlilia Mama Mzazi wa Mrisho Gambo

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ametoa salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo baada ya kufiwa ya mama yake mzazi usiku wa kuamkia jana.Zitto amesema kuwa anajua uchungu wa kupotelewa na mama huku akieleza kuwa hakuna faraja kama kumuuguza na kumsitiri mzazi.

Pole sana kwa Msiba huu mkubwa ndugu Mrisho Gambo. Najua uchungu wa kupotelewa na mama. Hakuna faraja kama kumuuguza na kumsitiri mzazi. Mola akupe subira wewe na ndugu zako. Inna lilah waina ilaih raajiun ameandika Zitto kwenye mitandao yake ya kijamii.