Header Ads

ad

Hii ndio sababu Rais Uhuru Kenyatta amewaomba msamaha

Mwandishi: Tina Mutinda  
 Kiongozi huyo wa Jubilee anajutia matamshi aliyotoa wakati wa kampeni 2017 -Rais aliwaomba wananchi na wanasiasa kuimarisha amani na umoja nchini Rais Uhuru Kenyatta amewaomba wananchi kumsamehe kwa matamshi yoyote aliyotoa na yaliyowaumiza wakati wa uchaguzi mkuu wa 2017. Rais Uhuru alichukua fursa ya hotuba ya kitaifa kuwaomba wananchi msamaha Jumatano, Mei 2.  
"Ikiwa kuna chochote nilichosema mwaka jana kilichowaumiza, ikiwa niliharibu umoja wa taifa hili kwa njia yoyote, ninawaomba mnisamehe na muungane nami kurekebisha hali,” alisema Uhuru 
Alisema kuwa viongozi wanafaa kuishi maisha yanayoweza kuigwa, na ndio maana aliomba msamaha.  
Aliwataka viongozi kuongoza kampeni ya kuwaleta wananchi pamoja kwa kuwakumbusha kuwa ukali haulipi lakini ukosoaji kwa njia ya kujenga ni muhimu. Kiongozi huyo aliwataka viongozi na wananchi vile vile kuheshimiana kuambatana na tofauti zao na kubuni njia za kushirikiana. Uchaguzi wa 2017 ulikumbwa na machafuko na vita ambazo zilianzishwa na uhasama kati ya Uhuru na kiongozi wa upinzani Raila Odinga. 
Kabla ya salamu kati yao ambayo imekuwa maarufu sana, Raila alimkashifu Uhuru na wenzake kwa wizi wa kura za urais wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Uhuru kwa upande wake alishambulia majaji na mahakama hasa baada ya ushindi wake kubatilishwa na Mahakama ya Juu. Wakati huo, viongozi katika pande zote mbili walionekana kushambuliana na kuchochea wananchi, hali iliyowatenganisha zaidi wananchi 
Hii ndio sababu Rais Uhuru Kenyatta amewaomba msamaha
Rais Uhuru Kenyatta amewaomba Wakenya msamaha. Picha/Kwa Hisani