Header Ads

ad

Raila akutana na Ruto kwa mara ya kwanza tangu walipoafikiana na Uhuru kufanya kazi kwa pamoja

Mwandishi: Lauryn Kusimba  
Raila akutana na Ruto kwa mara ya kwanza tangu walipoafikiana na Uhuru kufanya kazi kwa pamoja.Picha:  


Raila Odinga na naibu rais William Ruto walikutana kwa mara ya kwanza tangu Raila alipoamua kufanya kazi kwa pamoja na serikali ya Jubilee - Wawili hao walikuwa wameenda nyumbani kwa marehemu Kenneth Matiba kufariji familia yake -Raila aliiomba serikali kufidia familia ya Matiba kwa majukumu aliyoyatekeleza katika kupigania 
Image may contain: 9 people, people smiling, people standing and suit

demokrasia ya nchi ya  Kenya -Matiba alifariki akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kuugua kwa muda mrefu katika hospitali ya Karen jijini Nairobi 
Kinara wa muungano wa NASA, Raila Odinga na naibu rais William Ruto walikutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza tangu Raila alipoamua kuungana na serikali ya Jubilee ili wafanye kazi kwa pamoja. 
Vigogo hao wawili walikutana nyumbani kwa marehemu Matiba ambapo walikuwa wameenda kufariji familia yake.  
Akiwahutubia waombolezaji, Raila aliitaka serikali kuifidia familia ya marehemu kwa kazi aliyoifanyia nchi hasa ya kupigania demokrasia. Raila aliongezea kwamba biashara nyingi za Matiba zilianguka kwa ajili ya kupigania demokrasia ya nchi hii 
Image may contain: 3 people, people smiling, people sitting, table and indoor
" Serikali inapaswa kuifidia familia ya Marehemu kwa masaibu yote aliyoyapitia kwa niaba ya Wakenya," Raila alisema Akiomboleza kifo cha Matiba, Ruto alimtaja kuwa kiongozi shupavu na shujaa atakaye kumbukwa zaidi kwa kupigania demokrasia. 
Matiba atakumbukwa kwa kupinga vikali utawala wa chama kimoja ambapo alizuiliwa mwaka wa 1990 bila ya kufunguliwa mashtaka. Afya ya Matiba ilianza kudhoofika akiwa kuzuizini na amekuwa akiugua ugonjwa wa 'Stroke' tangu mwaka wa 1990. Matiba aliaga dunia Jumapilia Aprili 15 akiwa na umri wa miaka 85 katika hospitali ya Karen jijini Nairobi.