Breaking

Monday, April 16, 2018

CHADEMA yamvaa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG)

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG
Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA kimekanusha taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inayokihusu chama hicho,

Akizungumza na Wanahabari, Mkurugenzi wa Fedha, Uwekezaji na Utawala wa chama hicho, Roderick Lutembeka, amekanusha takwimu zilizoandikwa kuhusu chama chake,

Lutembeka amesema kwenye ukurasa wa 267 wa ripoti ya CAG, kipengele (i), kinasema CHADEMA kimefanya manunuzi ya bidhaa na huduma zenye jumla ya Shilingi 24,216,625,390 (zaidi ya Bilioni 24), 

Mkurugenzi huyo alisema hesabu hizo sio za kweli kwani kwa miaka mitatu (2014/15, 2015/16, 2016/2017) chama chake kilifanikiwa kukusanya jumla ya shilingi Bilioni 14.2 tu,

Alisema fedha hizo (Bilioni 14.2) walizipata kutokana na Ruzuku na michango ya Wanachama,

Lutembeka alihoji kuwa inawezekana vipi yafanyike manunuzi makubwa kuliko fedha zilizopatikana,

“Kama tulifanya matumizi hayo aliyoyaandika CAG, basi ina maana chama kilikusanya pesa zaidi ya hizo Bilioni 24,


Mkurugenzi wa Fedha, Uwekezaji na Utawala wa CHADEMA, Roderick Lutembeka ,
“Na kwa taarifa tu ni kwamba huu ukaguzi ni wa miaka mitatu mfululizo. Na tumekuwa tunapeleka mahesabu yetu kila mwaka. Lakini CAG alikuwa haji kutukagua” alisema Lutembeka ,

Mkurugenzi huyo aliendelea kusema mwaka jana CAG alipeleka wakaguzi 15 kutoka kwenye ofisi yake kwa ajili ya kukagua hesabu za CHADEMA,

Aliongeza kusema kuwa baada ya kukamilisha ukaguzi, Wakaguzi hao pamoja na chama chake kilikaa pamoja kupitia ripoti hiyo kabla hawajaondoka nayo,

“Tulipoipitia pamoja nao, haikuwepo hiyo namba (Bilioni 24). Sasa tunashangaa kwenye ripoti yao tunakuta namba nyingine kabisa. Hii si sawa,” alilalamika Lutembeka 
Post a Comment