Header Ads

ad

Miguna afukuzwa nchini Kenya kwa mara ya pili,Apandishwa Kwenye ndege kwa nguvuMiguna Miguna amefukuzwa nchini  Kenya  kwa mara ya pili
 Miguna anasemekana kupandishwa ndege yenye nambari ya usajili EK 722 iliyokuwa ikielekea Dubai - Haya yamejiri hata baada ya korti kutoa amri ya kumuachilia huru na kumruhusu aingie nchini  lakini  serikali  ya  Kenya  imekataa  kutii  na  kuheshimu  amri  ya  mahakama .

Mwanaharakati wa kundi la vugu vugu la NRM, Miguna Miguna ameripotiwa kufukuzwa  nchini  Kenya   i baada ya kuzuiliwa katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta kwa siku tatu tangu aliporejea nchini kutoka Canada. 

Taarifa  zinaema   kuwa Miguna Miguna alipandishwa ndege yenye nambari ya usajili ya EK 722 iliyokuwa ikielekea Dubai Jumatano Machi 28 licha ya korti kutoa amri ya kumuachilia huru.  
Mawakili wake wakiongozwa na James Orengo, Nelson Havi na Cliff Ombeta walifika katika uwanja huo wakitaka Miguna aachiliwe huru lakini walifurushwa na maafisa wa polisi. Kupitia ukurasa wake wa Twitter wakili na mbunge wa Rarieda Amollo Otieno alionyesha kughadhabishwa na serikali baada ya Miguna kufurushwa nchini kwa mara ya pili. 
Inasemekana Miguna alisindikishwa na maafisa wawili wa polisi. 

Image may contain: 4 people, including Mollel Hillary Mollel, people smiling, text