Header Ads

ad

Ukweli Mchungu..Kwa Hili la Mchanga wa Madini..Rais Magufuli Umetuonyesha Sura Yako ya Pili Kuhusu Nafasi Yako ya Urais..!!!

Image result for magufuli
Rais John Magufuli angalau amefanya jambo la ujasiri,haya yalimshinda Rais wa awamu ya nne Mh Jakaya Kikwete ambaye pamoja na kuunda kamati mbili,ile ya Jaji Mark Bomani na ile ya Laurence Masha, baada ya kumaliza kazi ziliwekwa kabatini!.

Kuiweka wazi Ripoti ya Prof Mruma ili watanzania wajue angalau kinachoendelea kwenye mgodi wa Kahama,kumeibua angalau hasira kidogo kwa watanzania,moja ya madhaifu ya watanzania wengi huwa hawakasiriki hata pale wanaponyonywa,wanapoibiwa tena waziwazi!.

Madhaifu makubwa ya watanzania ni upole na unyonge hata pale wanapotendewa mambo ya hovyo,wanaoonyanyaswa,miaka yote wakazi wa Geita,Kahama,Nzega,Tarime,Biharamulo wameishia kitazama tu mali zao zikipanda ndege na kwenda Ulaya,Asia na Marekani!.

Angalau Mrehemu Chacha Wangwe aliyekuwa mbunge wa Tarime alivishinda kwa kiasi chake vita hivi,Wangwe alihakikisha wana wa Tarime wanapata angalau kiasi kidogo,alisimama kidete kuhakikisha kila mkazi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa North Mara wanapata karo ya shule/Chuo kama sehemu ya kufaidi utajiri wao!.

Angalau Tundu Lissu wakati hata akiwa hajawa mbunge alizunguka kuanzia Kahama mpaka Nyamongo akitoa msaada wa kisheria kwa walioitwa wavamizi wa mgodini,nakumbuka akiwa na shirika la wanasheria watetezi wa masuala ya mazingira walitoa masaada wa bure kwa waliokamatwa kwa kudaiwa kuvamia mgodi!.

Nakumbuka jinsi Lissu alivyokumbana na kesi ya uchochezi pale alipopaza sauti baada ya kuwepo kwa taarifa za watu kufukiwa huko kwenye mgozi wa dhahabu wa Bulyanhulu!.

Angalau wewe Lissu uliuweka uwoga pembeni ukaandika kitabu kwa kushirikiana na Mark Curtus mlichokipa jina la "The golden opportunity"kitabu mlichokiandika kwa lugha ya kiswahili na kingereza,kitabu hiki kimeleza kinagaubaga jinsi tunavyoibiwa!.Kama serikali ingeamua kukifanyia kazi kitabu hiki,tusingefika hapa leo!.

Angalau Comrade/wakunyumba Hamis Kigwangala wakati fulani alisimama kidete kupinga wana wa Nzega kuishi maisha ya ufukara wakati Mungu kawajalia dhahabu,ndugu yangu huyu nakumbuka alivyojikuta mikononi mwa polisi!.

Niliwahi msikia Augustino Mrema akizunguka nchi nzima akiwatuhumu Ashanti Gold mine kuwa walimhonga kiongozi wa juu wa serikali ya awamu ya tatu,angalau ulipaza sauti kulikemea hili!.

Angalau Zitto Kabwe ulisimama kidete kuusaka ukweli ndani ya bunge mwaka 2007,juu ya waziri wa kipindi hicho Nazir Karamagi kwenda Uingereza na kusaini mkataba kati ya Tanzania na Barrick ili wachimbe madini Buzwagi!

Angalau Marehemu Dr Sengondo Mvungi ulipinga bila woga kwenye maandiko na hata ulipoalikwa kwenye vyombo vya habari kiongozi mkuu wa nchi kujiuzia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwila tena kwa bei ya kaptula!

Angalau aliyepata kuwa mbunge Mh Kimaro yeye alipambana bungenu na Mzee Sitta kupaza sauti kupinga kiongozi wa juu kabisa kujiuzia mgodi,kelele hizi zilioazwa sana na Dr Wilbroad Slaa kila akisimama bungeni alikuwa mwiba kuhusu mgodi wa Kiwila,nakumbuka sauti zenu zilizaa matunda mpaka serikali ikatangaza kuurejesha mgodi ule serikalini!.

Angalau kamati ya viongozi wa dini ya haki na amani,mlitimiza wajibu wenu,amlizunguka nchi nzima mkiongozwa na akina Askofu Mkuu Paul Ruzoka,Shehe Fereji na maaskofu wengine na mashehe,nakumbuka jinsi mlivyozuiliwa kuingia kwenye mgodi wa Geita bila kujali nafasi zenu kwenye jamii,jinsi mlivyotafuta ukweli wa kilichoitwa sumu za mto Tigithe huko Mkoani Mara.

Ripoti yenu ambayo hata mimi mlinioatia imethibitisha kuwa majinya mto tigite yalikuwa na sumu kutoka mgodini,watu waliyatumia wakafa,wakababuka,lakini mgodi ukaishia kuwaita wavamizi,watumishi wa Mungu mmeacha alama kwenye utetezi wenu dhidi ya wizi huu!.

Mh Rais Magufuli akiongea kwa uchungu mara baada ya kukabidhiwa ripoti na Prof Mruma,na alichukua hatua pale pale!.

Mh Rais geukia sasa upande wa sheria zako,hawa wakezaji muda wote huo wamekuwa wanafanya biashara halali ya kinyonyaji,serikali ya awamu ya tatu iliasisi huu ukwapuaji wa madini yetu!.

Tarehe 26.3.1997,serikali ilipeleka mapendekezo ya miswada miwili ya sheria,ile ya kodi na ile ya uwekezaji,ikiwa ni kipindi kifupi toka sera ya madini itungwe mwaka 1997.

Serikali ya Mkapa ilikuja na sera za kuwakaribisha wawekezaji na kuvutia mitaji kutoka nje(FDI),ikatunga sheria laini kwa wawekezaji,ikiwapa kipindi kirefu cha kuchota bila kulipa kodi,na hata walipoanza kulipa kodi walilipa kiduchu!.

Haya unayoyalilia Mhe Rais Magufuli ni matokeo ya watanzania kuwa na tabia za kutokasirika hata wanaponyonywa,haya ni matokeo ya wataalamu wa serikali ya awamu ya tatu ya mzee mkala,wabunge wa bunge ya Mzee Msekwa,baraza ka mawaziri la Mzee Mkapa kutuletea na kupitisha kwa hati ya dharua sheria mbili za kodi na ile ya uwekezaji!.

Mh Rais sasa badili sheria,waandae wataalamu wako wa sheria,zungumza nao ujue katika hili taifa litanasuka vipi na unyonyaji huu uliotengenezwa na sheria zetu wenyewe!.

Mh Rais bunge ambalo na wewe ulikuwa sehemu yake,miaka kumi iliyopita liliitaka serikali iipeleke bungeni ripoti ya ukaguzi kwenye sekta ya madini kutoka kutoka kampuni kutoka Marekani ya Alex Stewart Assayers(ASA report).

Nakumbuka ASA baada ya kukamilisha ukaguzi wao,walizungukza na waandishi wa habari,mbaya zaidi hawakusema jambo,walipoambiwa waseme wamebaini nini?jibu likawa,"Kazi tukiyotumwa na serikali imekamilika,hatuwezi sema chochote kwa sababu tunafungwa na sheria za ukaguzi za kimataifa",alisema Alex mbele ya waandishi wa habari jijiji Dsm!

Mh Rais mwaka 2007,Kuliibuka sakata la mkataba wa serikali na kampuni ya madini ya Barrick kutoka Canada juu ya uchimbaji wa madini huko Buzwagi,nakumbuka wewe ulikuwa naibu waziri,waziri wa nishati na madini Ndugu Nazir Karamagi alituhumiwa kusaini mkataba mbovu tena hotelini,bunge lilipoudai mkataba huo,liliambiwa mkataba ni siri,si media wala wabunge wamewahi uona mkataba huo,ni mkataba wa Buzwagi pekee ndiyo baadhi nasikia waliwahi uona baada ya kuvuja!.

Mh Rais badili sheria,ondoa kipengere cha usiri kwenye mikataba hii ya madini na maeneo mengine,ruhusi wananchi kupitia bunge wajadili mikataba hii inayowahusu!.

Na ndiyo maana ya utawala bora wenye dhana kama,uwajibikaji,utawala wa sheria,uwazi,haki za binadamu,n.k.

Ripoti ya Prof Mruma imetupa picha kiduchu cha tatizo kwenye sekta ya madini,hatujajua tunachopoteza Geita,kwenye mgodi mkubwa barabj Afrika,ripoti ya Prof Mruma haijagusa Geita,ripoti hii imepapasa tu kuhusu uhalisia kwenye sekta ya madini!.

Rais badili sheria ili unasuke katika mapambano haya,tunapambana na wizi ,kilio cha muda mrefu,ni sisi hawa hawa tuliojigunga kupitia sheria ya kodi na na ile ya uwekezaji zilizopitishwa kwa mbwembwe kwa hati ya dharura na kutusababishia umasikini,badili sheria Mh Rais tuwabane wawekezaji,ruhusu uwazi,hii ni biashara halali ya kinyama,iliyoruhusiwa na serikali na bunge letu huko nyuma!.

Katika vita hii dhidi ya mali zetu wenyewe,tujilaumu wenyewe,tulitunga sheria mbovu wenyewe,tukazipigia debe wenyewe,zimetifanya masikini,ni wakati wa wanasheria wetu kutuonesha tunapita wapi ili tutoke salama!.

Kumbuka hii ni vita na mabeberu,ukitaka kujua nguvu ya hawa mabwana,fanya utafiti juunya akina nani wanaunda Geopolitics department ya kampuni la GGM!.

Tuwaruhusu wanasheria waoneshe njia,wataalam wa miamba wameshaonesha udhaifu,wasikilizeni sasa magwiji wa sheria,tupo katika kipindi kigumu!.

Wasalaaam!.