Header Ads

ad

SOMA MAKALA NZITO KUTOKA KWA YERICKO NYERERE YENYE UJUMBE KWENDA RAIS MAGUFULI

Imeandikwa  na  Yericko Nyerere
Image may contain: 1 person, closeup
ZAWADI YA JUMAPILI KWA MH. RAIS JOHN POMBE MAGUFULI
Mh Rais, kwanza kabisa naomba nikusalimie SHIKAMOO... Mh rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pili naomba utambue Mh Rais mimi Yericko Nyerere mkulima wa Bamia Mbutu Kigamboni ninavichukia vitu viwili tu duniani, cha kwanza ni Shetani yule afahamikae na wakristu na waislamu, na cha pili naichukia CCM yani hicho chama ambacho kimekupa dhamana ya urais na ambacho wewe ni mwenyekiti wake. Hili nakuomba utambue wazi misimamo yangu kwa kuwa ni haki yangu inayolindwa kwa katiba ya nchi yangu na katiba ya ulimwengu.
Leo jumapili nataka nikupe zawadi yangu maalumu kwako Mh rais wangu kipenzi, ninatumia mitandao ya kijamii kama ukurasa wangu wa facebook, JamiiForums na twita kufikisha zawadi yangu ya jumapili kwako kwakuwa naamini wewe ni mmoja ya wasomaji wazuri wa habari za mitandaoni na ninahakika wewe ni mmoja ya "mashabiki wangu" katika kurasa zangu za mitandao kama JamiiForums, Instagram na Twita. Nilifurahi juzi uliposema unasoma haya tunayotaandika...
Naam, Mh Rais, tunapingana kwa mengi, tunakosoana kwa mengi japo wewe hupendi kupingwa wala kukosolewa, Lakini leo nakuomba ukubali kupingwa, kukosolewa na kusifiwa, yote hii nikwakuwa wote mimi na wewe na wale tunalipenda taifa na wote tunawajibika kwa taifa letu lifike kwenye ndoto ya taifa huru kiuchumi, kifikra, kisiasa na kitamaduni.
Naaam, Katika kujenga taifa letu ni lazima tuwe na kipaumbele, na katika taifa lililoparaganyika kama Tanzania linahitaji mbinu tofauti sana katika kufikia malengo ya taifa la uchumi wa kati na uchumi imara.
Hapo awali tulishauri serikali yako iwe na vipaumbele mhimu katika kujenga taifa, hili lilitokana na ukweli kwamba taifa na serikali yako Mh Rais John Pombe Magufuli haikuwa na dira wala kipaumbele kilichoonekana kwa umma, kila jambo tuliligusa kanakwamba hatuna malengo.
Baada ya hapo nilianza kusikia na kukuona mh Rais unasema Tanzania inapanga kununua ndege aina ya Boeing 787 Dash 8 Dreamliner yenye uwezo wa kuchukua abiria 262 ambayo inatarajiwa kuwasili nchini Juni 2018.
Ndege nyingine ambazo Tanzania itazinunua ni ndege moja aina Bombardier Q400 Dash 8 NextGen inayotarajiwa kuwasili Mwezi Juni 2017, ndege 2 aina ya Bombardier CS300 zenye uwezo wa kuchukua kati ya abiria 137 na 150 na zinazotarajiwa kuwasili nchini kati ya Mei na Juni, 2018. Malipo ya awali kwa ndege hizi yameshafanyika. Hii inamaana kwamba taifa litakuwa na ndege 6. Hapa nilianza kupata mwangaa wa kipaumbele chak, safi sana.
Nimefuatilia kwa miezi kadhaa tangu shirika la ndege kupitia pangaboi zake lianze kazi, nikiri kuna mabadiliko makubwa ya kimfumo, nimeona wanatumia mfumo ambao unatumiwa na Emirates, na Rwanda. Ni mfumo mzuri katika katika ulimwengu mpya wa biashara ya anga...
Pia udhibiti wa watumishi wa umma katika kusafiri kumeongeza faida kubwa kwa shirika hili, ifahamike kuwa mteja mkubwa wa biashara ya anga nchini tanzania ni serikali kupitia watumishi wake, Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2015 TASAF pekee ndio iliyovunja rekodi kwakulipa nauli ya ndege yenye thamani ya Shilingi bilioni 3 (safari za ndani).
Utaratibu mpya wa serikali hivi sasa watumishi wote wanaosafiri nchini (safari za ndani) wanatumia ATCL, na malipo ya nauli zao yanalipya kupitia bajeti ya wizara husika yaani mfano wizara ya Nishati Na Madini katika bajeti yao wameainisha kwamba watatumia 59 bilioni katika safari za ndani, basi upembuzi yakinifu unafanywa kuhusu safari zote zitakazotumia ndege, pesa inapelekwa kabisa ATCL...
Kinachofuata ni wizara muda wa watumishi wao kusafiri ukifika wanapeleka majina mapema wakahakikiwe na wakatiwe tiketi tu.
Kiongozi wa Ethiopia alipoamua kujenge shirika la ndege la Ethiopia aliamua kwa dhati kusimamisha baadhi ya mambo katika taifa kwa mwaka mzima ili ajenge shirika hilo bora barani Afrika, moja ya mambo yaliyosimamishwa ni Elumu na Afya,
Yaani wizara hizo hazikupewa pesa ya bajeti kwa mwaka huo na badala yake pesa ikanunulia ndege... Huko ni Ethiopia na tuombe kiongozi yeyote nchini asije kuiga staili hii kwani Ethiopia walikufa watu wengi kwakukosa huduma za Afya.
Msimamo wangu toka awali ni kwamba, ili taifa liendelee ni lazima tuwe na vipaumbele na kila kipaumbele tuhakikishe kinafika mwisho katika utekelezwaji, na hili bado naendelea kusimamia na kuamini kwamba hii ndio njia maridhawa ya kuongoza nchi duniani kote.
Tanzania ina vitu vitatu ambavyo vikipangwa kwenye vipaumbele vya taifa kimoja baada ya kingine taifa litapona na kuwa la mfano barani Afrika.
1. Nishati na Madini
2. Bandari/Maji
3. Anga
Nimefurahi zaidi kuona sasa "inawezekana" unaingia kwenye kipaumbele cha pili ambacho ni sekta ya madini. Kati ya hivi vipaumbele naamini taifa likiamua kutekeleza kimoja kimoja mpaka mwisho taifa litafanikiwa na kuwa taifa la mfano barani Afrika. Hoja ni namna ya kuvitekeleza vipaumbele hivi huku siasa za vyama zikilitafuna taifa bila ganzi wala lepe.
Leo nasimama wima KUKUPONGEZA kwa hatua yako ya kuthubutukuzuia makontena yaliyo na mchanga wa madini ambayo yanasafirishwa kwenda Ulaya kwa uchakataji zaidi.
Ninazo sababu nyingi za kukupongeza kwa hatua hii, Naomba ifahamike kwamba, Tangu mwanzoni mwa miaka ya 1998 taifa ndipo lilipoanza kuumizwa na mikataba ya kilaghai katika sekta hii ya madini, mikataba hii mingi wewe Rais wangu ulishiriki ukiwa ndani ya baraza la mawaziri wakati ikiingiwa, hivyo wewe ni mmoja ya wanaolitweza taifa hili leo kwa mikataba hii inayompa haki mwekezaji kubeba ule mchanga uliouzuia juzi. Nilitaraji uanze na mikataba yenyewe, vile viwanja vya ndege vilivyomigoni vinavyotumika kutoroshea madini bila kulipa kodi.
Migodi ya Buzwagi na Bulyankulu, inaelezwa kwamba 70% ya tani za mawe ya mchanga wa dhahabu unaku katika mwitikio sawa na mchakato wa mgodi wa geita. Hivyo taarifa za kuaminikazinasema 70% ya tani za mawe/mchanga ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyankulu wanapata dhahabu halisi 97% hapo hapo mgodini.
Kwahiyo hicho kinachosafirishwa kwa makontena kinachoitwa mchanga ni 30% ya tani za mawe/mchanga wa madini. Maana imechanganyikana na copper na silver. Kwa hiyo wanachofanya wanafanya nikusafirisha kwenda kuchakata ili kupata gold, copper na silver.
Migodi ya Geita na North Mara, dhahabu inasafishwa palepale. Yaani wanachimba, inapelekwa mashine ya kuchakata pale pale mgodini hadi wanapata gold bars (dhahabu halisi 98%). Migodi ya Buzwagi na Bulyankulu, mawe yake ni tofauti kidogo na yale ya Geita na North Mara, maweyake yana dhahabu, copper na silver.
Kwa hiyo Bulyankulu wanachimba takriban tani milioni moja kwa mwaka. Wakifanya hiyo uchakataji wanaiconcentrate hadi inabaki tani elfu ishirini na tano tu. Hii ndio yale Makontena ya kusafirisha nje yakachakatwe huko kupata dhabu halisi
Kwa Buzwagi, wanachimba tani milioni nne kwa mwaka, wakifanya hio uchakataji, wanabaki na tani elfu ishiri na tano pia. Hii ndio yale Makontena ya kusafirisha nje yakachakatwe huko kupata dhabu halisi
Sasa hizo tani elfu hamsini ndizo zinazosafirishwa kwenda nje kwa mwaka (tani elfu ishirini na tano za Bulya na tani elfu ishirini na tano kutoka Buzwagi)
In summary katika mapato yote ya Bulyankulu na Buzwagi, mapato asilimia 70 yanapatikana hapo hapo mgodini bila kupeleka kuchakata nje ya nchi. Na mapato yao asilimia 30 ndio yanatokana na michanga (concentrate) inayosafirishwa nje. Kati hiyo 30%, asilimia 25 ni mapato kutoka dhahabu na asilimia tano ni copper na silver.
Asilimia 95 mauzo ya makampuni haya yanatokana na dhahabu, asilimia tano ni copper na silver. Kati ya hizo 95%, asilimia 70 ya dhahabu inasafishwa mgodini, na asilimia 25 ya dhahabu ndio inasafirishwa nje kuchakatwa, pamoja na hiyo asilimia tano nyingine ambayo ni copper na silver. Mashine bora za kuchakata hiyo michanga zipo Germany, China na Japan.
Tanzania tunaweza kujenga kiwanda cha kuchakata hapahapa bila kusafirisha mchanga tena, ili hiyo asilimia 30 ya mapato ya Bulyankulu na Buzwagi yasafishwe hapa hapa Tanzania, muda mfupu nasi kama nchi tutakuwa na uwezo wa kushindana na wachina, wajapani na wajerumani. Maana kutegemea mzigo wa Buzwagi na Bulyankulu hautatosha kuendesha hiyo mitambo. Taarifa zinasema mgodi wa Buzwagi wamebakiza miezi 12 tu kumaliza hiyo michanga inayosafirishwa, Inamaana itabakia Bulyankulu tu ndio itakayokuwa inatoa hiyo michanga....tani elfu 25 kwa mwaka.
Japo kwa haraka haijafahamika kwenye tani 50,000 zinazikwenda nje kuchakatwa maduni hupatikana kiadi gani, lakini Kwahesabu za kawaida bei ya gram 1 dhahabu bei inasimamia (50,000/=) elfu 50,000/=
Hivyo kilo1 ya dhahabu sawa na gram 1000 ni (50,000,000/=) milioni 50.
Tweke kadirilio la chini makampuni haya hupata 1/4 ya madini toka kwenye mchanga wa tani 50,000, Tani 12.5 ya dhahabu sawa na kilo ngapi ya dhahabu? Zidisha mara bei ya gramu ya dhahabu ili ujue makapuni yanatuibia shingangapi kwenye mchanga huu tu.
Kuvunja mikataba hii au kuingilia chochote katika biashara hii ni ngumu sana, Taifa lilihitaji mtu anayeweza kutumia mwanya wa amri ya kirais (presidential decree) ili kuhakikisha mikataba hii inahuishwa. Nakupongeza rais Magufuli katika hili mamlaka yako ninashauri yatumike huku kwa nguvu zote bila kusikiliza kelele za watu, badala ya mamlaka yako kutumika kwa vitu visivyo na tija katika taifa "mfano" kumkamata Malisa GJBen-Rabiu Wa Saanane na Yericko Nyerere kwakuwa tu wanakukwaza huku mitandano, hayo yatakuwa matumizi mabaya ya madaraka. Lakini katika hili la madini rais una sapoti yangu kabisa.
Mh Rais, Mwaka majuzi nilifika katikmiji ya Berlin na Bremen nchini Ujerumani, nikapata fursa ya kuzuru sehemu ya uhifadhi wa kumbukumbu za makoloni ya ujerumani, moja ya makoloni hayo ni Tanganyika. Katika kumbukumbu zile ipo michoro ya madini ya Tanganyika ambapo inaonyesha kuna AINA 360 za madini katika ardhi ya Tanganyika ikiwa ni nchi ya kwanza barani Afrika kuwa na aina nyingi za madini.
Mtazamo wangu Rais Magufuli huhitaji kutumia amana ya pesa ya nchi taslimu katika kutekeleza vipaumbele vyaka vya taifa, bali tumia raslimali hizi katika kulijenga taifa, dunia imebadilika, ipo katika uhitaji, wewe unayo unahitaji kiwanda cha kuchakata mchanga wa madini hapahapa, ACCIA, Bulyankulu, Buzwagi na GGM wanahitaji madini, wambie wajenge hapa huo mtambo tutakatana kwenye mirahaba ya madini, Wewe una gesi, yule anao utalaamu, wewe unayo uranium, yule anavyo vinu vya nyuklia, wewe unayo Tanzania, yule ana kiwanda cha vito, wewe unacho chuma, yule ana kiwanda cha chuma anahitaji chuma,
Mfano, katika mazingira haya unatoaje pesa taslimu kununua ndege ikiwa wenye kiwanda cha ndege wanahitaji madini ya Zinki na wanaagiza Uchina ilihali Uchina hawa wanayapata Tanzania madini hayo? Kwanini usimwambie Boing alete ndege 40 kisha aje achukue mdini hayo Tanzania kwa miaka10.
Unatoaje pesa taslimu kujenga Reli ilihali wachina hawa wanahitaji madini ya safaya? Kwanini usimwambie mchina ajenge reli kisha avune madini ya safaya kwa miaka 10.
Unatoaje pesa kununua ndege za kivita ilihali Warusi wanahitaji Uranium kwaajili ya viwanda vyao vya kurutubishia silaha za kikemia? Kwanini usimwambie Mrusi aje avune madini ya uranium kwa miaka kumi?
Kwanini hatujifunzi kutoka kwa nchi zilizofanikiwa mfano Singapore, Malaysia, China nk?
Nchi zenye raslimali nyingi kama Tanzania haiwezi kutumia mfumo wa nchi zisizo na raslimali kama Kenya, Rwanda nk katika kufikia uchumi wa kisasa. Lazima tutumie raslimali zetu kujenga taifa lakini tukumbuke njia ya kuzitumia raslimal hizi sio lazima ziwe zile zinazopendekezwa na wazungu...
Tuamue sasa mfano Zambia, Uganda na nchi nyingine zikihitaji gas tutumie negotiator wazuri, Kenya wakihitaji Gesi tunapima kiasi cha gesi wanayohitaji kisha kinathaminishwa na kuwapa kazi ya kujenga mji wa Dodoma wenye thamani ya trilioni 12. Zambia wakihitaji vilevile tunawapa kazi ya kusambaza maji nchi nzima kulingana na mahitaji yao...
China vilevile wakihitaji makaa ya Mawe, tunawambia tunahitaji Reli ya kisasa kutoka Tanzania hadi Rwanda, hakuna kutumia pesa ya umma kufanya jambo ambalo lingefanywa na raslimali tulizozikalia.. Urais hauna chuo.
Dubai, China, Malaysia S.Korea, N.Korea, Singapore nk walifanikiwa kwakutumia mfumo huu, tun kila sababu ya kuchagua nani tushirikiane na nani tusishirikiane kwa maslahi ya Taifa...
Pamoja na kwamba kuna masharti na mikataba ya kimataifa inayoweza kutuzuia kufanya biashara ya namna hii, lakini lazima tujifunze kwa waliofanikiwa kupitia njia hii...
Katika hili la kuchagua kipaumbele na sasa kuingia kwenye sekta ya madini nakupongeza sana, mengine yaache yajiendee kama yayalivyo lakini tekeleza moja kwa vitendo na lifike mwisho kabisa, hakika matokeo chanya yatapatikana...ijapokuwa unaathiriwa na siasa za vyama.
Na Yericko Nyerere