Header Ads

ad

.Mama Salma Kikwete Aaanza Bunge kwa Kumtandika Swali Zito Waziri wa Ofisi ya Magufuli


Mbunge mpya wa kuteuliwa na Rais ambaye pia Mke wa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete hii leo katika siku yake ya kwanza Bungeni baada ya kula kiapo na kuwa mbunge rasmi ameanza kazi hiyo kwa kuuliza swali.

Katika swali lake Mama Salma Kikwete amehoji kuhusu mpango wa serikali kuongezea huduma ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) hasa watu masikini wakiwemo katika mkoa wake wa Lindi.

Akijibu hilo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki amesema kuwa serikali imepanga katika mwaka wa fedha 2017/2018 kuandikisha kaya zote zilizobakia katika mpango huo na kwamba hadi sasa mpango huo umefikia asilimia 70 kwa nchi nzima huku ikiwa imebakiza vijiji 5,690 sawa na asilimi 30 ili kuweza kukamilisha mpango huo kwa asilimia 100.

Mhe. Kairuki amesema jumla ya Kaya 355,000 zilizobakia zitaweza kutambuliwa pamoja na kuandikisha kaya masikini katika mikoa na vijiji vilivyobakia katika mpango huo.