Header Ads

ad

ELIMU#### Hatua 4 zitakazomaliza changamoto zako zote za kimaisha


Je, ni mara ngapi umewahi kusikia ule usemi usemao 'kisicho kuua kitakuimarisha kiaskari' je wewe unaamini vipi katika usemi huu? Sasa leo naomba nikwambie kuhusu changamoto zinavyoweza kukuimarisha katika maisha yako.

Kwenye hatua za maisha kuna changamoto nyingi sana na kama hauna msimamo unaweza kujikuta unakata tamaa kabisa kutokana na magumu unayopitia.

Tambua kuwa kila mtu katika maisha yake huwa na changamoto zake hivyo zinazokukuta wewe usidhani kuwa umeonewa kumbuka kuwa kila mtu anachangamoto zake na huenda nyingine ni kubwa kuliko zako.

Tofauti ya kupambana na changamoto mara nyingi hutofautiana kwenye jinsi gani wanakabiliana na yale yanayowatokea na ndio maana tatizo moja linaweza kuwatokea watu wawili, lakini wakapata matokeo tofauti.

Hizi hapa njia za kushinda changamoto zako katika maisha yako.

1. Siku zote unapaswa kuamini kuwa kila changamoto unayopitia  iko ndani ya uwezo wako na unauwezo wa kuishinda.

2. Tambua kuwa kila changamoto unazozipitia katika maisha yako sasa huweza kubadilika kuwa fursa endapo utakabiliana nayo vizuri.

3. Kumbuka kuwa hakuna tatizo jipya maishani kila unachopitia kuna mtu au watu waliwahi kupitia au wanapitia pia kwa sasa na bado walishinda. Hivyo na wewe unaweza kushinda.

4. Pamoja na changamoto ambazo unapitia sasa, lakini kumbuka kuwa hakuna changamoto ya milele kwani changamoto zote huwa ni za muda mfupi tu na zitapita.

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi