Header Ads

ad

MAKONDA: Sitta Alinisomesha na Kuniozesha, Aliniombea Kila Siku


Siku zote umeniambia nianze na mambo magumu kwanza ndiyo nifanye mambo mepesi.

Niwe na ngozi ngumu na wala nisikate tamaa. Hukuacha kuniombea na kunitia moyo hata wakati unaumwa, hakika wewe ni mwalimu mwema ambae alama zako hazitafutika kamwe maishani mwangu.

Umenisomesha na hata kuniozesha, niseme nini ili dunia ielewe kuwa kwangu ulikuwa zawadi kutoka kwa Mungu?

Unyenyekevu, upole, na ujasiri wako ni dira tosha ya kuwatumikia Watanzania ambao mpaka sasa nina uhakika unawaombea.
Nenda Mzee Sitta acha niendeleze VIWANGO na KASI kwani ndiyo urithi ulioniachia.

Mwanao Mpendwa,

Paul Makonda