Header Ads

ad

UJUMBE!! SOMA TAARIFA MUHIMU KUTOKA KWA VIJANA HAWA AMBAO WAMEJITOLEA KUFATILIA UANZISHWAJI WA BARAZA LA VIJANA


Ndugu vijana wa Tanzania,Mara baada ya sisi kuamua kufuatilia swala la uanzishwaji wa baraza La vijana Tanzania, tumebaini kuwa bado vijana wengi hawana  elimu juu ya ujio wa baraza La vijana, na hawaelewi baraza la vijana ni nini.Na ndio sababu Leo hii vijana tumethubutu kuwa kimya kabisa katika kufuatilia jambo hili lenye maslahi mapana kwetu sisi vijana na kwa maendeleo ya taifa letu.
Hivyo sisi tumeona ni vyema tuamue kuungana ili sasa kuanzia kufuatilia juu ya mchakoto mzima wa upatikanaji na uanzishwaji wa baraza LA vijana Tanzania.Aidha tunatoa wito kwa walio guswa na jambo hili na wenye  utayari katika kuungana nasi katika hili jambo muhimu sana kwetu na taifa letu Basi piga simu namba [0719-893 765] kwa Maelezo zaidi ya kujiunga nasi,ama kutoa ushauri. 
Ndugu vijana wa kitanzania, kama kuna mahala tunapaswa kuweka pembeni itikadi zetu za kivyama,na kuwa pamoja,basi ni hapa,kama kuna mahala tunapaswa kuzumgumza lugha moja kwa maslahi mapana ya taifa letu, basi ni hapa katika swala hili.kama kuna mahala tunapaswa kushirikiana kikamilifu pasipo masihala na kupiga kazi,basi ni katika jambo hili,huku tukijua fika kuwa vijana ndio nguvu gazi ya taifa na tukiamua tunaweza.Inawezekana,wajibika katika nafasi yako.
Ila ni vyema mkajua madhumuni ya sheria ya uanzishwaji wa baraza kama .

MADHUMUNI YA SHERIA 
a) kuweka jukwaa la utekelezaji wa masuala ya vijana katika ngazi ya wilaya, mkoa,Taifa na kimataifa;
(b) kuhamasisha kujitolea na kujitegemea miongoni mwa vijana;
(c) kuishauri Serikali kuhusu masuala yanayohusiana na maendeleo ya vijana’
(d) kuwatayarisha vijana kubeba majukumu ili kuwawezesha kuwa na tabia njema, maadili na mienendo mema;
(e) kutayarisha mazingira bora kwa ajili ya ushiriki wa vijana katika masuala yanayohusiana na utoaji wa maamuzi;
(f) kujenga mtandao miongoni mwa vijana na wadau wengine;
(g) kuendeleza umoja miongoni mwa vijana mbali na tofauti zao katika rangi, kabila, siasa, uchumi, dini, utamaduni, jinsia na maeneo wanayotoka.
KAZI ZA BARAZA ZITAKUWA NI,
(a) kuhamasisha na kuendeleza ari ya kujenga umoja, utaifa, kujitolea na kujituma miongoni mwa vijana;
(b) kuendeleza tafiti, kukusanya na kuchambua data katika masuala ya vijana;
(c) kuendeleza mahusiano baina ya mashirika ya vijana na vyombo vingine ndani na nje ya nchi yenye madhumuni na maslahi yanayofanana;
(d) kuendeleza na kuitangaza Sera ya Taifa ya Vijana na sera nyingine zinazohusu vijana;
(e) kutambua shughuli na mipango inayohusu vijana, inayoendeshwa na vijana, makundi ya jumuiya zinazojihusisha na vijana, asasi zisizokuwa za serikali, makundi ya asasi za kiraia na mashirika mengine.
(f) kuendeleza na kuhamisha usawa wa jinsia miongoni mwa vijana; na
(g) kuendeleza masuala yanayohusiana na watu wenye ulemavu miongoni mwa vijana.
MAMLAKA YA BARAZA
Baraza litakuwa na mamlaka kwa ajili ya utekelezaji wa kazi zake chini ya Sheria hii, na bila kuathiri ujumla wake, itakuwa na mamlaka ya-
(a) kuingia kwenye mkataba;
(b) kusimamia, kudhibiti, kusimamia mali zake kwa utaratibu na kwa malengo ya kuendeleza madhumuni ambayo Baraza limeanzishwa;
(c) kupokea zawadi, mikopo yenye masharti nafuumisaada au mali iliyowekwa wakfu inayotolewa kwa Baraza au fedha yoyote ambayo ni kwa ajili ya Baraza na kufanya mgawanyo kwa mujibu wa masharti ya Sheria hii;
(d) kwa idhini ya Waziri, kuingia katika ushirikiano na vyombo au mashirika mengine ndani na nje ya Tanzania kama itakavyoonekana inafaa katika kuendeleza malengo ambayo ndio sababu ya Baraza kuanzishwa;
(e) kufungua akaunti za benki au akaunti ya benki kwa ajili ya fedha za Baraza ambapo fedha zote zinazopokelewa na Baraza zitalipwa na malipo yote yatakayolipwa.
(f) Kuunda kamati yoyote itakayosaidia utekelezaji wa kazi za Baraza.
Taarifa hii imeandikwa na,MASON KIMBO[0719-893 765