Header Ads

ad

HUYU NDIYE MENGI, BILIONEA ALIYETOKEA FAMILIA MASIKINI, ALIISHI NYUMBA MOJA PAMOJA NA MBUZI NA NG’OMBE,

IMEANDIKWA  NA Respicius Francis
Image result for MENGI

DR. REGINALD  MENGI  NI BILIONEA  ALIYETOKEA  KWENYE  FAMILIA MASIKINI,
ALIISHI NYUMBA  MOJA PAMOJA  NA   MBUZI  NA NG’OMBE,
ALIKWENDA  SHULE BILA  VIATU.
 Image result for reginald mengi
Reginald   Mengi    ni  kati  ya  wafanyabiashara  maarufu  hapa Tanzania    pamoja  na  Afrika  mashariki  kwa  ujumla  ,umaarufu  wake  unatokana  na  juhudi  zake  za  kushiriki  mambo  mbaliambali ya  kijamii  hasa  kusaidia  watu    wasiojiweza mfano yatima,walemavu,wajane na  watu  wa  kipato  cha  chini , Hali  hii imesababisha  jina  la Dr. Regnald Mengi  liendelee  kuwa  maarufu  zaidi  na  kubaki  midomoni  mwa  watu  kutokana  na kugusa maisha ya watu  wengi hasa  wale  wenye  kipato cha  chini.Licha  ya hivyo Dr. Reginald  Mengi  ni  kati ya  wafanyabiashara  wenye  ushawishi  mkubwa  sana hapa Tanzania kutokana  kuwa  mstari wa  mbele  kukemea  maovu  ndani  ya  jamii 

   Tanzania  Classic tumejitahidi  kufanya  uchambunzi   juu ya Dr. Reginald  mengi  kuhusiana na   historia ya maisha   yake  kwa  ujumla hapa  Tanzania  ili  kuwapa  mwanga vijana  kufahamu  kuwa siku  zote mafanikio  huanzia mbali, Dr. Reginald  Mengi  amezaliwa  mkoani  Kilimanjaro wilaya  ya  machame katika familia  ya  kipato  cha  chini  sana maana   wakati  akisoma  shule   alikuwa  anafikia   hatua  ya  kwenda  shule  bila  viatu huku yeye na    wazazi  wake  walikuwa  wanaishi  nyumba  moja  na  mbuzi  pamoja  na  Ng’Ombe  hii  ilitokana  na familia  yao  kuwa  na uwezo  mdogo sana  kifedha maana   wakati  mwingine  chakula  kwao  kilikuwa  ni  tabu  kidogo  kutokana  na  ugumu  wa  maisha  katika  familia  yao enzi  hizo  kabla  Dr.Regnld Mengi  hajawa  bilionea,    wakati  akisoma  shule  alikuwa  na sare  moja  ya  shule  tu  maana uwezo  wa  kuwa  na sare  nyingi  wakati  huo  haukuwepo ,Hii  ndio hali halisi  ambayo Dr. Reginald  Mengi  alikuwa  nayo  hapo  Mwanzo.
         Image result for reginald mengi

Wakati  tukiendelea  kufanya  uchambuzi  ili  kujua  maisha  ya  awali   ya Dr. Reginadl  Mengi  tulijaribu  kuwahoji baadhi  ya  wananchi  kutoka mkoani  kirimanjaro  ambao  wanamfahamu  vizuri Dr. Reginald  Mengi  tokea  alivyoanza  mpaka  kufikia  hatua  ya  Kuwa  Bilionea  mkubwa  hapa  Tanzania. Bi swai kutoka  wilaya ya  Hai ambaye ana  umri  wa  miaka  87  anasema  familia  ya Dr. Reginald  Mengi  ilikuwa  ni  familia  ya  kipato  cha  chini sana ndiyo  maana Dr. Regnald Mengi  alikuwa  anafikia  hatua  ya  kwenda  shule  bila  viatu  kutokana  na wazazi wake  kutokuwa  na  uwezo  wa  kumnunulia  viatu  wakati  huo, Ila  Anasema Dr. Reginal  Mengi  ni  kati  ya  vijana  ambao walikuwa  na  uwezo  mkubwa  sana darasani  licha  ya  wakati huo  kukabiliwa  na changamoto  nyingi  za  kimaisha , Bi  SWai  anaendelea  kusema Dr. Reginald  Mengi  ni  kijana   ambaye   alikuwa na   heshima  na Ukarimu   kwa  jamiii  nzima  enzi za  udogo  wake ndiyo  maana  ata  walimu  wake  walikuwa  wakimpenda  sana.
Katika  maelezo  yake  Bi swai  anasema Dr. Regnald  Mengi  alikuwa  ni  mchapakazi  sana kwa sababu  alikuwa   akiwahi  shuleni  kila  siku  na  baada  ya  kutoka  shuleni  anarudi  nyumbani  na kuwasaidia wazazi  wake  haraka ndiyo  maana  amefanikiwa  kwenye  maisha  yake.
Tanzania  classic  tulijaribu  kumuuliza  Bi Swai  juu   ya  tabia  ya Dr. Regnald  Mengi  enzi  za  ujana  wake, anasema Dr. Regnald Mengi alikuwa na tabia nzuri sana kwasababu  likuwa  ni  vigumu  sana kusikia  ana kesi  zozote  shuleni  au  mtaani maana  wazazi  wake  walimlea  kwenye  maadili  ya dini sana   kwahiyo  hali  hiyo  ilimsaidia  Mengi  kuwa  na  tabia  njema  mbele  ya  Jamii, Dr. Regnald Mengi  alikuwa  akikutana  na mtu  njia anasimama  anasalimia  au  kama  ana  mzingo  wowote  anamsaidia. Bi Swai aliongeza Kusema,  kweli Dr. Reginald  mengi  ni  kati  ya  watu  ambao  wametoka  mbali  sana kimaisha  ndio  maana  unaona  yupo  mstari  wa  mbele  kusaidia  masikini  kwasababu anatambua  shida  wanazozipata masikini  kutokana  na  yeye  kapitia  huko,  Bi Swai aliongea  kwa  kujiamini.  Tanzania classic  tulitaka  kujua  historia  ya  elimu  ya Dr. Regnald Mengi kiufupi. Dr. Regnald Mengi  alipata  elimu ya  sekondari katika  shule  ya Moshi  sekondari  au  zamani  OLD  MOSHI  baada  kumaliza  shule  ya  sekondari alipata  sponsorship  kwahiyo  alikwenda  uingereza kuchukua  masomo  ya  uhasibu, Mwaka  1971  reginald  mengi  alirudi  Tanzania  na  kuajiriwa  kwenye  kampuni  ya  Cooper  and  Lybrand  Tanzania  ambayo  kwasasa  inajulikana  kama  prince  water  house  cooper, Baada  ya  kufanya  kazi  muda  mrefu  kwenye  kampuni  hiyo  akiwa  Kama chairman and partner mwaka 1989  aliondoka  kwenye  kampuni  hiyo  na kwenda  kuanzisha  kampuni  yake  ya  IPP MEDIA GROUP.
Image result for reginald mengi
Dr. Reginald  Mengi  wakati  akianzisha  IPP MEDIA GROUP  ilikuwa  ni kampuni  ndogo  sana ambayo   alianza  kwa  kutengeneza  kalamu  za  wino lakini  IPP MEDIA GROUP  iliendelea  kupanuka  na  kwasasa  ni  kati  ya  makampuni  makubwa  hapa  Afrika  mashariki  kwa  ujumla,
                          
                            [ITV NI KATI  YA  TV  VIKUBWA ZINAZOMILIKIWA NA BW: MENGI] 
Kupitia  kampuni  yake  hiyo  Dr. Reginald  Mengi  ameweza  kumiliki  vyombo  mbalimbali vya  habari  mfano  kwa  upande  wa  TV  anamiliki  ITV, EATV & Capital Tv  na kwa  upande  wa  Radio anamiliki  Radio  one, capital radio & EATV radio. Licha  ya  hivyo Dr. Reginald  Mengi anamiliki  magazeti kadhaa mfano  wa  magazeti  hayo  ni   Nipashe, kulikoni, Taifa  letu , The  Guardian , Financial  time,    Sunday observer.
Dr. Reginald  Mengi  anamiliki  viwanda  baadhi  ambavyo  vinazalisha  vinywaji  mbalimbali  hapa  Tanzania  mfano  wa  vinywaji  hivyo  ni maji  ya  Kilimanjaro ambayo  yanasemekana  ndio  maji yenye  ubora  Zaidi, Pia  viwanda  hivyo  vinazalisha soda mfano cocacola, Fanta & Tangawizi. Licha ya hivyo Dr. Regnald  Mengi  kawekeza  kwenye  vinywaji  na  kwenye  vyombo vya  habari  pia  amewekeza  kwenye  madini Kupitia  biashara  hii  ndizo  zinamfanya  Reginald  Mengi awe  bilionea hapa  Tanzania licha ya  kuwa  alianzia mbali  sana mpaka  kuja  kupata utajiri huu.
Kupitia  historia ya  Dr. Reginald  Mengi tunapata  ujumbe  kuwa  juhudi  ndizo  zinaweza  kubadilisha  maisha  yetu  kwasababu  tumeona Dr. Reginald  Mengi  anatoka  kwenye  hali  ya  chini  ya kwenda  shuleni  bila viatu  mpaka  kufikia  hatua  ya kuwa  billionea mkubwa Tanzania na  Afrika nzima. Ukweli  ni  kwamba kilichomfikisha hapa Dr. Reginald Mengi ni juhudi, maarifa na kutokata tamaa pamoja na  kumtegema  Mungu  Kwahiyo  huu  ni ujumbe  kwa vijana ambao  kwasasa  wanaamini  kuwa  maisha yao  hayawezi  kubadilika  kutokana na kukabiliwa  na changamoto  kibao  za  maisha. Dr. Reginald  mengi  anasema  ili  tufanikiwe  lazima  tuwe  ni  watu  ambao tunajiamini, tunathubutu, tunajuhudi, Tusio  kata tamaa pamoja  na  kumtegemea Mungu.

MAKALA  HII  ITAENDELEA  KESHO  KUPITIA  MTANDAO HUU.....
..

 Bw:  Respicius Francis mwaandishi   wa  makala hiii.
   Kama  wewe  una jambo lolote unahitaji litoke  kwenye  mtandao huu wasiliana  na  sisi        kupitia  namba  0755515906  
   whatsapp 0755515906 .


vigezo  na  masharti vitazingatiwa