Header Ads

ad

HUYU MAMA NI MFANO WA KUIGWA KATIKA JAMII; UJASIARIMALI WAKE WAMPA MAFANIKIO

MAMA   GODELIVA    AKIHUDUMIA     MIFUGOUJASIRIAMALI KWA AKINA MAMA NA AKINA DADA
Kwa majina halisi ninaitwa Godeliva Simon, Ninafanya shughuli ya ujasiriamali kwa lengo la kujipatia mahitaji yangu mwenyewe pamoja na familia yangu .Ujasiriamali niufanyao ni wa ufugaji wa Mifugo mbalimbali,mifugo ninayofuga ni kuku wa kienyeji [Kiswahili],kanga,batamzinga,bata wa kawaida,bata bukini {bata maji},mbuzi wa kawaida,mbuzi wa maziwa pamoja na sungura. Mifugo hii hunisaidia sana katika kuongeza kipato badala ya kutegemea mshahara wa mwajiri pekee kwani hali ya maisha ni ngumu na kila mmoja anaelewa.Nimeanza ujasiriamali huu tangu mwaka 2012 hadi leo hii ninaendelea na ujasiriamali huu wa ufugaji.
Kwa upande wa akina mama pamoja na vijana ninawaomba mjiajiri kwa upande wa kufuga kwani faida yake ni kubwa, kwa mfano huwezi kukosa pesa ya matumizi kwa kutumia jasho lako na mikono yako,pia utakuwa na afya njema kwani hutohangaika kununua yai,nyama na maziwa hususani maziwa ya mbuzi kama nifaidikavyo mimi,pia utaweza kuepukana na umbea ambao huletwa na ukosefu wa shughuli za kufanya,
       Mafanikio,  kupitia    ujasiriamali   huu  umenisaidia    kuwasomesha     watoto   wangu   wote,    hakika   kwangu      ni    mafanikio    kwasababu   zawadi   pekee   kwa  mtoto    ni   elimu   tu,   pia  umeniwezesha    kunipatia   makazi   ya   kuishi
Ujasiriamali huu kwa njia ya ufugaji una changamoto mbalimbali ambazo ni
1.      Chakula cha mifugo, hii ni changamoto kubwa kwani ili mifugo ikue na iishi inahitaji chakula ambacho upatikanaji wake ni mgumu kwani lazima uwe na pesa kwaajili ya kuwezesha hili, pia chakula cha baadhi ya mifugo kama mbuzi na sungura upatikanaji wake ni mgumu kutokana na jiografia ya eneo letu hili la dar es salaam ambalo ni kavu hivyo upatikanaji wa nyasi huwa ni wa tabu sana.
2.      Mabanda(makazi) kwaajili ya kuhifadhi wanyama hawa,  Wanyama hawa wanatakiwa kuhifadhiwa katika mabanda yaliyojengwa vizuri na imara ili kuwalinda na hali zote pamoja na maadui wa aina mbalimbali, hivyo pesa nyingi huhitajika ili kukamilisha makazi yao.
3.      Soko la mifugo, inahitajika kama mfugaji uwe na soko la uhakika na si kubangaiza wateja mitaani kwani hii hupoteza muda na nguvu nyingi.
4.      Afya ya mifugo, mifugo hii huhitaji chanjo ya mara kwa mara ili kuikinga na magonjwa mbalimbali,mfano batamzinga huhitaji kupatiwa chanjo wiki mbili mara tu baada ya kutotolewa ili kuwakinga na ndui.
5.      Ufadhili, uanzishwaji wa biashara hii huwa ni mgumu kutokana na ukosefu wa ufadhili ambapo hukosekana fungu la kutosha kuendeshea biashara hii,ni vyema kabla ya kuanzisha biashara hii uwe na kianzio(mtaji) wa kutosha,kwa akina mama tulio wengi tunashindwa kukopa kwani kurudisha pesa hiyo inakuwa ni vigumu kutokana na ufinyu wa vipato vyetu.


OMBI
Ninaomba akina mama pamoja na mabinti tuwe tayari kuingia  katika ujasiriamali ili kupunguza utegemezi na pia ukali wa maisha unaotukabili,pia kwa yeyote anayetaka kujifunza jinsi ya kufuga na kuendesha ujasiriamali huu ninamkaribisha sana kwa moyo mkunjufu na dhati na kuhusu gharama za mafunzo haya tutaelewana maana bila kujifunza si rahisi kupata mwamko na kuingia katika ujasiriamali wa aina hii, pia tuzingatie na kuelewa kuwa hakuna lisilowezekana ni vizuri ukawa na nia utafanikiwa.


Kwa mawasiliano:
Jina       : Bi Godeliva Simon
Na.simu: 0784708726

                     
Kauli mbiu
“Mwanamke anaweza ujasiriamali”


 MAMA    GODELIVA    AKIWA    KAZINI