Header Ads

ad

SOMA UJUMBE MZITO WA BW; BEN WA SAANANE KWA MICHAEL RICHARD WAMBURA

Kama shabiki na mpenzi damu damu wa Simba Sports Club nimefurahishwa sana na uamuzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kumpitisha Rasmi Michael Richard Wambura kuwa Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Club ya Simba baada ya kusikiliza hoja zake na mapingamizi ya Club dhidi yake
Nampongeza Wambura kwa dhamira ya mapambano .Alipambana hadi dakika za Mwisho,hadi tone la Mwisho bila kuchoka.Hakuna tafsiri nyingine ya upambanaji zaidi ya hii ya kupigania haki yako hadi pumzi ya M...wisho
Sijali kama atashinda uchaguzi au hatashinda ila cha muhimu kwangu ni kupigania haki yake bila kuchoka nq kuhakikisha Demokrasia inachukua Mkondo wake.
Ifikie hatua sasa wale ma-conservative wanaogopa uchaguzi wajiandae.
Hans Pope namuheshimu sana sana kulingana na historia yake ya mapambano kisiasa,harakati na kibiashara/kiuchumi.Namshauri akae mbali na marafiki wahafidhina wasiopenda Reform na demokrasia ndani ya Club.Club ya Simba ni ya wanachama wote na sio ya wafanyabiashara wachache wenye maslahi yao
Kinachohotajika Simba ni mikakati,Sera na programe za kisayansi kabisa zitakazoleta Transformation na Club kupiga hatua na kujiendesha kisomi
Azam FC wametutia Aibu sana sana kwa kufanya football professional kabisa
Sisi tumekalia sera ya zama za mawe za kale (Stone Age) eti "Mpira Fitna bwana"! ! ! Aarghhh!
Halafu,Hii Ouster clause ya shirikisho la soka Duniani(FIFA) mimi naiona kuwa ni ya kijinga kweli kweli.Eti maswala ya Mpira hayastahili kupelekwa Mahakamani?Ina maana masuala ya Mpira ni jungle entertainment? Hawa jamaa wanalea udikteta kupitia soka maana FIFA hawajaimarisha mfumo wa Haki kupitia mifumo ya kuendesha soka lakini bado wameweka clause Katili kama Hii?
I salute You Michael Wambura...! Wewe ni mpiganaji usiyechoka unayestahili kuigwa katika Mapambano.

..