Header Ads

ad

MAXIMO KUSAINI MKATABA YANGA

 


Yanga, Maximo wafikia patamuKOCHA mpya wa timu ya Yanga, Mbrazil Marcio Maximo, anatarajiwa kusaini mkataba mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam.
Maximo aliwahi kuifundisha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kwa takribani miaka minne kabla ya kupokewa na Mdenish Jan Poulsen ambaye naye alimwachia mwenzake Kim Poulsen, ambaye ametupiwa virago hivi karibuni na nafasi yake kuchukuliwa na Mholanzi Mart Nooije.
Kwa mujibu wa habari za ndani kutoka uongozi wa Yanga, Maximo ameishapewa mkataba wake ili aweze kuupitia kabla ya kusaini.
“Maximo tulimpa mkataba wiki iliyoisha ili aupitie halafu atupe majibu, nina imani kubwa ndani ya wiki hii atasaini tayari kuja kuifundisha Yanga,” alisema mtoa habari huyo ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini.
Alibainisha kuwa wana imani Yanga itafanya vizuri chini ya kocha huyo ambaye hivi sasa yuko nchini Brazil, kwani ana uzoefu na soka la Tanzania na hata bara la Afrika.
Aliongeza kuwa Maximo alitarajiwa kuja nchini ili kutazama mkataba huo kabla ya kusaini, lakini ikashindikana baada ya kuwa na programu ya kuangalia Kombe la Dunia linalotarajiwa kuanza Alhamisi nchini Brazil